Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, kwa kutujalia afya na uhai na kutupa kibali kilichotuwezesha kukutana hapa siku ya leo. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Nina furaha kubwa leo hii, kupata nafasi ya kuhutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Taifa na Kikao na Bunge la Seneti ya Jamhuri ya Kenya. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kabla sijaendelea, niruhusu nitangulize shukrani zangu kwako Mheshimiwa @SpeakerKLusaka, Spika wa Bunge la Seneti na Mheshimiwa @SpeakerJBMuturi, Spika wa Bunge la Taifa kwa kuitisha kikao hichi cha pamoja cha Bunge na kunialika mimi kuhutubia- President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kupitia kwenu niwashukuru waheshimiwa wabunge na waheshimiwa maseneta kwa kuridhia kwa kauli moja kufanyika kwa kikao hiki. Asanteni sana. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Najiona mwenye bahati kubwa kupewa heshimwa hii adhimu na ya kipekee. Kama alivyosema mheshimiwa Spika kwamba aliyewahi kuhutubia hapa ni Mheshimiwa Kikwete kutoka Tanzania, na mimi ni wa pili. Ni bahati kubwa. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Natambua fika kuwa huu si utaratibu wa kawaida wa Kenya, si kila Rais anayefanya ziara rasmi hupewa heshima hii ya kuhutubia Bunge. Ten kikao cha pamoja. Wenzetu mna bunge lenye chemba mbili, sisi wenzenu tuna bunge moja tu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kwangu ndio itakuwa mara ya kwanza kuhutubia chemba mbili za bunge kwa pamoja. Si jambo dogo na ni heshima kuba iliyoje. Mmenipa heshima kubwa sana. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Nimefarijika kuwa nimepata nafasi hii mwanzoni mwa uongozi wangu. Kumbu kumbu hii haitofutika kwa maisha yangu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Uamuzi wenu wa kunipa nafasi hii ni kielelezo cha thamani na uzito ambao mnaoupa uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi zetu mbili. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Niwahakikishieni kuwa nasi tumeguswa sana na heshima, upendo na ukarimu mkubwa ambao mmetuonyesha. Wema huacha deni na deni lake ni kulipwa kwa wema, na sisi Tanzania tutalipa wema huu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Sitatenda haki nisipomshukuru kipekee kaka yangu, ndugu yangu, Rais wa Jamhuri wa Kenya, Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Rais Kenyatta ni miongoni mwa viongozi wa mwanzo kabisa aliyenipigia simu kunifariji mara tu baada ya kusikia taarifa ya kifo cha aliyekuwa Rais wetu mpendwa Hayati Mheshimiwa Dr Magufuli. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kama haikutosha, hakusita kukatisha ratiba yake na kuweza kufika yeye binafsi kushiriki nasi katika msiba wa kitaifa kule Dodoma. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Siku ile alitufariji sana kwa maneno yake na salamu zake za buriani kutoka kwa wananchi wa Kenya. Hatutasahau kitendo chake cha kutukumbusha umuhimu wa kuheshimu dini na imani za wengine.n- President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mheshimiwa Kenyatta alisitisha kuhutubia akiwa jukwaani ili kupisha adhana iliyokuwa ikisomwa msikitini imalizike, na ndio aliendelea. Alituachia gumzo kubwa na funzo kubwa sana kwetu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Alitumia jukwaa lile kunipongeza kwa kushika dhamana hii ya Urais ya awamu ya sita ya Tanzania. Na aliahidi kunialika nchini Kenya mara baada ya kipindi cha maombolezo kumalizika. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Rais Kenyatta ni mtu wa kutimiza ahadi, mara baada ya kipindi cha maombolezo alinitumia ujumbe maalum kuniona ambao pia uliambatana na mualiko wa kutembelea nchini Kenya. Nami nimekuja Kenya kuitikiwa wito wake. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mimi na ujumbe wangu tumepata mapokezi mazuri sana toka tumewasili jijini Nairobi. Tumejisikia tuko nyumbani haswa. Tumepokewa na ukarimu mkubwa, na hiyo ni hulka, desturi na asili ya watu wa Kenya. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Siku ya jana nimefanya kikao na Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta na ujumbe wake wa viongozi wa serikali. Tumekuwa na mazungumzo mazuri na yenye ya kuamsha matumaini makubwa sana kwa mashirikiano kati ya nchi zetu mbili. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
kwa siku zijazo mbele yetu. Hapakuwa na ugumu wala ukakasi wowote katika kufikia mwafaka wa mambo tuliyokuwa tukijadiliana. Tumezungumza kwa kindugu sana. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kilichojitokeza uwazi kwa mazungumzo yale, ni namna ambavyo nchi zetu mbili zinakubaliana katika mambo mengi kuliko yale machache sana tunayotofautiana. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Hata hayo machache tunayotofautiana yenyewe haikuwa na misingi imara ya tofauti. Ila ni mitazamo ya watu. Ambayo mitazamo mingi inayoleta ukakasi huchangiwa kutokana na kukatika kwa mawasiliano kati ya nchi zetu mbili. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Sasa ili kuondoa mitazamo hasi kati yetu tumekubaliana kujenga na kuendeleza utamaduni wa kukutana mara kwa mara katika ngazi zetu mbali mbali. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Ndugu na jirani wanaotembeleana hujenga ukaribu kuliko wale wasiotembeleana. Umbali hujenga mashaka na ukaribu huondosha mashaka hayo.- President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kama nilivyosema hii ni ziara yangu ya kwanza rasmi nchini Kenya tangu kushika wadhifa wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, tarehe 19 Machi mwaka huu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Ipendeze kusema kuwa itaingia katika kumbu kumbu za kihistoria kuwa Kenya ndio nchi ya kwanza kwa Rais wa awamu ya Sita ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kufanya ziara rasmi. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kwa lugha nyingine, mguu wangu wa kwanza kutoka nje kwa ziara rasmi umeanza Kenya. Nataka niwaambie, jana nlikaribishwa Iftar na Mheshimiwa Rais lakini wakati tuko kwenye Iftar na baadaye chakula cha usiku kulikuwa kuna Dua nyingi sana - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
zimesomwa na baada ya kumalizika Dua, mvua ikanyesha. Ilikuwa baraka kubwa. Mungu ameweka baraka kwenye ziara yangu na yale yote tumezungumza. Kwa hiyo tumshukuru Mungu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Uamuzi wangu huu wa kuja Kenya kuwa nchi ya kwanza si wa bahati mbaya bali ni wa makusudi. Busara inaelekeza kuwa, ukiwa mpangaji mpya lazima ujitambulishe kwa majirani. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Nimeanza Kenya si kwa sababu ni karibu kijiografia bali kwa sababu ya umuhimu na nafasi ya Kenya kwa Tanzania. Uhusiano ya Kenya na Tanzania ni wa kipekee sana. Ni uhusiano uliofungwa katika mafundo matatu. -President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Fundo la kwanza, ni undungu wa damu kati ya wananchi wetu wa pande mbili ambao hauwezi kutenganishwa na mipaka ya kuchorwa kwenye ramani. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Makabila ya pande mbili za mpaka yanaingiliana na watu wake ni wale wale wamoja. Tanzania inapakana na nchi nane lakini ni nchi ya Kenya pekee ndio ambayo tuna jamii nyingi zaidi zilizoko katika pande mbili za nchi zetu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Fundo la pili ni historia. Kabla hata ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1967, nchi zetu mbili hizi tayari zilishakuwa chini ya East African Common Service Organization zikiwa chini ya utawala ya kikoloni wa waingereza. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Huduma zetu muhimu, miundo mbinu yetu na chumi zetu zilifumwa pamoja kabla hata nchi zetu hazijapata uhuru. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Fundo la tatu ni jiografia. Mwenyezi Mungu amejalia nchi zetu hizi kuwa majirani. Tuna mipaka ya baharini na mipaka ya ardhini. Na hata ikolojia yetu ni moja. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kutokana na ukweli huu, ushirikiano wetu si wa hiari bali ni wa lazima kutoka na kanuni ya uasili, wa undugu ambao Mwenyezi Mungu ameumba. Ushirika na ujirani, yote yanatufanya tuwe pamoja. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Hili hatuna uwezo nalo la kubadilisha, hili la maumbile. Liliobaki; ama tupendane au tuchukiane. Tuzungumze ama tununiane. Hatuwezi kukwepa kutokana na mafundo haya matatu tuliyowekwa nayo pamoja. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tunategemeana kwa kila hali. Iwe heri ama shari. Iwe neema au iwe dhiki, tunategemeana. Panapotokea ukame Tanzania, njaa inabisha hodi Kenya. Uzalishaji wa viwanda ukisimama Kenya, bidhaa zinakosekana Tanzania. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kwa hiyo tunategemeana. Hivyo hapana budi ila tupatane na tuelewane ili tuishi kwa pamoja kwa neema na furaha. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Binafsi huwa nashangazwa sana na wale ambao wanadhani kuwa eti Kenya na Tanzania ni washindani na hivyo uhusiano unapaswa kuwa wa kuhasimiana. Nawashangaa wanaodhani kuwa Kenya pekee ama Tanzania pekee inaweza kuendelea bila mwenzake. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mbaya zaidi ni kule kuamini kwao kwamba hilo linawezekana tu mmoja wetu kumuangusha mwenzake. Hawa ni watu wenye mioyo ya choyo, maono mafupi na akili mbovu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Ni bahati mbaya kuwa watu hawa wapo katika pande zote mbili; Kenya na Tanzania. Hutokea pia wachache wao sana wakawa ni watumishi wa serikali zetu na hata wanasiasa wa pande mbili za nchi zetu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Bahati nzuri ni kuwa si wengi na ndio maana uhusiano wa nchi zetu mbili unatimiza miaka 56 sasa. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kwangu mimi na katika awamu ya uongozi, nitahakikisha kuwa Kenya inabaki kuwa ndugu, jirani, mshirika wa mkakati. Kenya ni nchi ya tano kwa nchi zinazoongoza kwa uwekezaji, nchini Tanzania. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Na ndio nchi ya kwanza ndani ya Afrika inayoongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania. Nyuma ya mataifa makubwa kama Uingereza, Marekani, China na India, inakuja Kenya. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Takwimu za kituo chetu cha uwekezaji zinaonyesha kuwa hadi kufikia March 2021 kuna miradi mingi tu ya Kenya inatekelezwa Tanzania, kama 513 na kutoa ajira kwa waTanzania 51,087 na kuchangia mapato ya kiasi cha $1.7 billion. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Sekta zinazoongoza kwa uwekezaji kutoka Kenya ni uzalishaji viwandani, usafirishaji, kilimo, benki, huduma, ujenzi, rasilimali watu, madini, utalii na mali asili. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kutokana na uhusiano wetu mzuri, kampuni za Tanzania zimewekeza nchini Kenya lakini tumekuja kwa uchache sana. Tuko kama 25-30 zilizosajiliwa na mamlaka ya uwekezaji ya Kenya. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Miradi hiyo ina thamani ya Ksh 19 billion na kutoa ajira kwa raia kama 2641. So Tanzania tuna deni kubwa Kenya. Lakini na mapungufu hayo tuliyonayo, bado tunaawalika wakenya wengi zaidi waje Tanzania kuwekeza. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Dhamira yangu ya kuja nchini Kenya ni kuzungumza nanyi na kuona ni kwa namna gani watanzania wataweza kufanya vizuri zaidi nchini Kenya. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mbali na uwekezaji, ushirikiano wetu kwenye sekta ya biashara ni mkubwa na umeendelea kushamiri siku hadi siku. Usafirishaji wa bidhaa za Tanzania kuenda umeongezeka kwa tukoka Tsh390.6 bilion mwaka 2017 hadi - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tsh 526.3 bilioni mwaka 2020. Kwa upande wa Kenya, nayo iliongeza kiwango cha kuuza bidhaa zake nchini Tanzania kutoka Tsh420 bilioni mwaka 2017 hadi Tsh571 bilioni mwaka 2020. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Takwimu hizi zinatusuta sisi viongozi na wanasiasa. Zinatuonyesha kuwa wananchi wa nchi zetu mbili, daima wako hatua mbele, mbele yetu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Wanafanya biashara zao kwa ubunifu mkubwa lakini sisi tunang'ang'ana na sheria na vikwazo na mambo kama hayo na tunawavuta nyuma kidogo. Ni wakati sasa sisi viongozi kubadilika. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tuwe daraja la kuwaangunisha watu wetu na sio tuwe vikwazo kwao. Mimi na ndugu yangu Rais Kenyatta tumekubaliana kuweka utaratibu madhubuti wa kuzuia na kukabiliana na zile pilka pilka pale zinazotokea katika mipaka yetu - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
wakati wa kuvusha biashara kuenda na kurudi katika nchi zetu mbili. Mashirikiano ya uwekezaji na biashara ni sehemu tu ya mashirikiano mazuri kati ya nchi zetu. Utalii ni eneo jingine ambalo tunafaa kushirikiana sana. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kama nlivoygusia, ikolojia zetu zinaingiliana. Hivyo hivyo ukaribu wa vivutio vyetu vya utalii na vyenyewe vinaingiliana. Tunayo nafasi ya kuneemeka pamoja ikiwa tutashirikiana katika sekta hii kuliko kushindana. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Badala ya kunyang'ang'ana idadi ya watalii, busara inatutaka tuelekeze nguvu zetu kuhamasisha mtalii aongeze idadi ya siku ambazo atazitumia nchini Kenya na nchini Tanzania. Kwa kufanya hivyo, sote tutafaidika. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Rais baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema na nanukuu, "tukipoteza muda mwingi kugawana kibaba, tutapoteza mdua mzuri sana wa kuvuna kipimo kikubwa zaidi." - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mashirikiano yetu yanashamirishwa na jitihada kubwa tunazochukua vita dhidi ya uhalifu, ujangili, ugaidi, madawa ya kulevya na uharamia bahari ya Hindi na katika Ziwa Victoria. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mashirikiano haya mazuri baina ya vyombo vyetu yamechangia na yatachangia sana kuwepo kwa utulivu na kutoa fursa kwa shughuli za kibiashara na uwekezaji kushamiri. Kenya ikiwa salama na sisi Tanzania tuko salama. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Hali kadhalika Tanzania ikiwa salama Kenya nayo inakuwa salama. Ujenzi wa miundo mbinu ya pamoja ni sehemu ya jitihada zetu za kuimarisha za mashirikiano yetu ya kiuchumi na kimikakati. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Miradi hii inajumuisha kwa uchache miradi ifuatayo. Kwanza ni ujenzi wa barabara wa lami kutoka Lamu, Mombasa, kupitia Tanga, Bagamoyo, hadi Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 454 chini ya programu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
ya kuendeleza ya miundo mbinu ya barabara kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Katika ushoroba wa pwani. Kwa upande wetu tuko karibu kukamilisha tuko mbioni kukamilisha ujenzi wa kipande cha pangani Bagamoyo na barabara za lami zenye urefu wa 124.5km na tayari tumekwisha pata fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Jana nlikuwa na mazungumzo na kakangu Uhuru, naye anamalizia mazungumzo ya kupata fedha ili kazi hii ianze kwa upande wa Kenya na tukutane pale kwenye mpaka. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mradi wa pili ni barabara ya Arusha-Holili-Taveta-Voi yenye urefu wa kilomita 260. Mradi huu ni sehemu wa mradi wa maendeleo ya barabara ya Arusha-Namanga-Athi River iliyofunguliwa rasmi mwaka 2012. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mradi huu unatekelezwa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza imeshakimilika, sasa tunajipanga kuendelea na awamu ya pili wa mradi huu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mradi wa tatu, tunavyo vituo vya huduma za pamoja mpakani vya Namanga na Holili -Taveta. Vitu hivi vimerahisisha shughuli za biashari mpakani na uvukaji wa watu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tunaendelea na mchakato wa kukamilisha mifumo ya vituo vya Horo Horo, Lunga Lunga, Sirari, Isibani ili navyo viweze kutoa huduma kwa wepesi na kwa ufanisi. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mradi wa nne ni wa kusafirisha umeme mkubwa wa 400kW. Kwa pande wa Tanzania mradi unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme kutoka Singida hadi Namanga. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Ujenzi wa kituo kipya cha kupozea umeme na eneo la Legumor na upanuzi wa kituo cha kupozea umeme cha Singida. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kwa upande wa Kenya mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya umeme msongo wa 400kW inayojengwa kutoka kituo cha kupozea umeme cha Isinya hadi Namanga yenye urefu wa 94km inayounganishwa na njia ya umeme inayojengwa upande wa Tanzania. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na Shirika la Maendeleo la Japani zimekubali kugharamia miradi hiyo. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mradi mwingine, serikali zetu mbili zitaanza kutekeleza mradi wa bomba la gesi. Kutoa gesi Dar es Salaam hadi Mombasa. Mazungumzo ya kutafuta fedha kwa ajili ya mradi huyo yanaendelea na tunatarajia yatakamilika mapema inavyowezekana. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mtakubaliana nami kuwa kwa ukubwa wa miradi hii, gharama zake na muundo wake unalazimisha nchi zetu mbili kushirikiana kujenga miradi hiyo. Ni ishara tosha kuwa uhusiano wetu si wa kuishia kesho, wala kesho kwetu wala mtondogoo. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Hivi ndivyo majirani na ndugu walioshibana wanavyoishi. Yeyote anayefikiria au kudhamiria kuleta uhasama baina yetu, ujumbe kwao ni kuwa Tanzania na Kenya, tulikowepo, tupo na tutaendelea kuwepo. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Sote tunafahamu kwamba dunia inakabiliwa na janga kubwa la ugonjwa wa korona ambalo limeathiri kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi zetu na limepelekea kwa sehemu kubwa kutulazimisha kubadili mfumo wetu wa maisha. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tunatambua kwamba kila nchi ikiwemo Tanzania imejiwekea utaratibu wa kupambana na janga hili kulingana na mazingira yake mahususi na hali ya kusambaa kwa ugonjwa huo katika nchi hizo. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Sisi Tanzania sio kisiwa, tunaishi kama sehemu ya familia ya jumuiya ya kimataifa. Kwa maana hiyo, kupitia kamati ya wataalamu niliyoiunda tumeanza mchakato wa kutafakari mbinu zaidi za kukabiliana na janga hili. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Wakati tunaendelea kusubiri mapendekezo ya wataalamu na hatua za kuchukua, tahadhari zote, ikiwemo kusitisha baadhi ya safari kwenye maeneo ya milipuko zinachukuliwa. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kwa vyovyote vile itakavyopendekezwa, jambo ambalo nina hakika nalo ni kwamba, lazima tushirikiane na jirani zetu ikiwemo Kenya katika kupambana na janga hili. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Ni imani yangu kwamba tukiweka jitihada zetu na maarifa yetu pamoja basi tutakabiliana na janga hili bila uoga na tutashinda na maisha ya wananchi wetu yataendelea kuwa ya kawaida, huku tukichukua hadhari za kutosha. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Hatuwezi kuelezea uhusiano wetu vizuri bila kutambua uhusiano wa mabunge yetu ya nchi mbili. Umekuwa ni uhusiano mzuri wa majira yote. Nitumie fursa hii kufikisha kwenu shukrani za dhati na salamu kutoka Bunge la Tanzania na Watanzania wote. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
kwa kuungana nasi na kutufariji katika kipindi kigumu cha msiba wa Hayati Mpendwa wetu Rais Dr John Pombe Magufuli. Mlitufuta machozi na mlitufariji sana. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tuliguswa sana na uamuzi wa Bunge la Seneti kupitia kikao chake cha tarehe 24 Machi 2021, kujadili na kusajili kwenye kumbu kumbu za Bunge salamu maalum za rambi rambi kufuatia kifo cha Hayati Dr Magufuli. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Nafahamu pia viongozi wa mihimili mitatu ya serikali ya Kenya, ukiwemo wewe mheshimiwa Spika. Mlitembelea makaazi ya Balozi wetu kutoa salamu za pole. Sisi Watanzania tulifarijika sana kwa kuwa nasi wakati wa majonzi. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Hatuna la kuwalipa ndugu zetu Wakenya zaidi ya kusema, Mungu awabariki sana. Wakati wa msiba na dhiki, ndio wakati unamjua ndugu yako wa kweli na jirani zako wa majira yote. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Mlitudhihirishia bila chembe ya shaka kuwa nyinyi ni ndugu zetu wa shida na raha. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Ndugu zangu wabunge sisi ni wafuatiliaji wakubwa ya mikutano ya Bunge la Kenya. Mimi binafsi huwa napenda kusikiliza Bunge la Kenya. Tunafanya hivyo kwa kuwa, yanayojadiliwa humu nasi yanatuhusu. - President
@SuluhuSamia #BungeLiveKE
Niseme tu kuwa Bunge la Seneti la Kenya na Bunge la Taifa la Kenya linatusisimua kwa mengi. Tunafurahia upana wa demokrasia yake, uzito wa mijadala yake na hamasa ya wabunge wake. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tulifurahishwa zaidi na uamuzi wenu wa kuanza kutumia lugha ya Kiswahili ndani ya Bunge. Na ndicho kinachonifanya mimi nisikilize bunge la Kenya. Naenjoy kile kiswahili kile. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kiswahili chenu kina vionjo vingi ambavyo pekee yake ni burudani tosha kusikiliza. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Rai yangu kwenu ni kuwaomba mtusaidie kulea uhusiano wetu mzuri ndugu zangu wabunge. Nasema hivyo nikitambua kuwa nyinyi ndio wawakilishi wa wananchi na ndio sauti yao wananchi wa Kenya. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Nyinyi ndio wenye dhamana ya kutunga sheria na kushauri serikali juu ya mwelekeo wa sera na kuongoza wananchi wenu waliowachagua. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Dhima yenu katika kukuza ushirikiano baina ya nchi zetu mbili. Mna uwezo mkubwa wa kuamua kasi ya ushirikiano wetu, iwe ya haraka ama ya kusuasua kwa aina ya sheria mtakazozitunga na sera mtakazozipitisha. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Dira na mwelekeo wa serikali ya awamu ya sita ninayoiongoza ni kudumisha mazuri ya awamu zilizopita, kuyaendeleza mema yaliyopo na kuleta mazuri mengine mapya. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Hivyo nimekuja kuwaahidi kuwa chini ya uongozi wangu, mimi na wenzangu katika serikali ya Tanzania, tutafanya kila linalowezekana kuimarisha uhusiano kati ya nchi zetu mbili. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kama kuna linalolegalega au uhusiano wetu kama unasuasua basi nimekuja hapa Kenya ili kukazia yale ambayo yamelegalega. Na nimekuja kuyanyoosha yale ambayo yalikuwa yamejipindapinda. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tanzania na Kenya na wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Nchi zetu mbili ndizo zenye eneo kubwa kijiografia na idadi kubwa ya wetu na milango pekee ya bahari kwa nchi zengine za Afrika Mashariki. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Ukweli huu unakuja na wajibu na dhima kubwa kwa nchi zetu mbili. Uhusiano wa nchi zetu mbili ukishamiri, Afrika Mashariki nzima itashamiri. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Hivyo basi hatuna budi nchi zetu mbili kutambua wajibu wetu na dhima yetu hiyo kwa upande huu Mungu alikotuumbia Afrika Mashariki. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tunapaswa tutambue kuwa, kila mara panapotokea kutoelewana kati yetu, tunadhohofisha jumuiya ya Afrika Mashariki. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Bila kukusudia tunajikuta pia tunaathiri kasi ya utangamano wa Afrika Mashariki, hivyo hatuna budi kuendelea kuelewana. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Niwahakikishie kuwa, mimi na wenzangu nchini Tanzania tutafanya kila linalowezekana ili uhusiano wetu uzidi kung'aa na kwa kufanya hivyo tung'arishe ushirikiano wa Afrika Mashariki. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tanzania itaendelea kuwa jirani na rafiki mwaminifu wa Kenya na mwanachama mwadilifu na wa kutumainiwa ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Jitihada zangu na wenzangu katika serikali ninayoongoza, zitaelekezwa katika kuimarisha ushirikiano wetu ndani ya jumuiya yetu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tutaelekeza jitihada zetu katika kutafuta majawabu palipo na changamoto, kufufua fursa palipo na vikwazo na kuleta tumaini palipo na mashaka. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tutafanya hivyo kwa kuamini kwa dhati kabisa kuwa wana Afrika Mashariki hatma yetu imefungamana. Nasi hatuna budi tufungamane. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Ombi langu kwenu waheshimiwa wabunge, kama nlivyosema awali, mtusaidie kutimiza azma hiyo. Sisi tulioko serikalini mtusukume tutekeleze wajibu wetu huu adhimu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Na pale tunapozubaazubaa, msisite kutukosoa. Nanyi pia tunawaomba mtimize wajibu wenu. Mtusaidie kutunga sheria na kushawishi serikali zetu kuhusu sera zinazachochea na kuwezesha mtangamano. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tusiruhusu na tukemee misimamo, mitazamo na kauli za baadhi ya wanasiasa ndani ya mabunge yetu ya kuleta mgawanyiko na kudhohofisha jumuiya yetu. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Daima, tuwatangulie wafanyabiashara na wananchi wetu katika utangamano na kuwaongoza badala ya wao wananchi wetu kutuongoza sisi. -President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Nasema hayo kwa sababu, falsafa zinasema kuongoza ni kuonyesha njia na sio kufunga njia. Kwa hivyo sisi kama viongozi tuonyeshe wananchi wetu njia na tusiwafungie njia za maendeleo na njia za ustawi wao. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Nihitimishe hotuba yangu na niseme kwamba kama mnavyojua, moyo ukielemewa na furaha, furaha ya moyoni hutoka kwa mdomoni. Ningetamani kuendelea kuzungumza nanyi kirefu zaidi. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Kueleza furaha yangu kwa upendo mkubwa mlionionyesha, ukarimu mkubwa mliotufanyia mimi na ujumbe wangu na heshima kubwa mlionipa. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Isitoshe, tunapokutana Tanzania na Kenya tunakuwa na maneno mengi sana ya kuzungumza. Hayaishi. Na hii ni kutokana na ukubwa na uzito wa uhusiano wa nchi zetu mbili. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Nataka nisiseme yaishie hapa. Niseme mniruhusu niahirishe maneno yangu hapa kwa sababu nitakuja kusema maneno mengine mbele tukikutana. Kwa hiyo siishii hapa naahirisha maneno yangu hapa. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Nitumie fursa hii kuwashukuru waheshimiwa Maspika kwa mara nyingine tena kwa kunikaribisha lakini nimshukuru Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kwa mualiko wa kuniomba mimi kufanya ziara hii rasmi ya kiserikali nchini Kenya. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Nataka niwathibitishie kwamba ziara hii tumevuna mengi na makubwa mengi sana. Imefungua milango mingi sana, lililobaki mtusimamie kwenye utekelezaji. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Lakini nami, nimemualika Mheshimiwa Uhuru Kenyatta aje Tanzania. Tanzania mwaka huu Disemba tunatimiza miaka 60 ya uhuru. Kwa hiyo nimemualika Mheshimiwa Kenyatta aje kwenye sherehe hizo kama mgeni wetu maalum. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Tunaondoka Kenya na kumbukumbu nzuri ya ziara hii na shauku kubwa ya kurudi tena siku zijazo. Hii ni ziara yangu ya kwanza nchini ya Kenya nawaahidi haitakuwa ya mwisho. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE
Udumu undugu wa Kenya na Tanzania. Wadumu viongozi wetu. Mungu aibariki Jamhuri ya Kenya. Mungu aibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na asanteni sana kwa kunisikiliza. - President @SuluhuSamia #BungeLiveKE

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Mzalendo

Mzalendo Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @MzalendoWatch

7 May
The @Senate_KE has set in motion the trial of Wajir Governor Mohamed Abdi Mohamud who the country assembly impeached, despite a High Court order barring the proceedings.

Via/Daily Nation
On Wednesday, Justice Edward Muriithi had stopped the Senate from debating the motion of removal from office of Mr Mohamud until a case challenging the impeachment is heard and determined.
The judge also ordered the petitioners to serve the House and @SpeakerKLusaka copies of the suit and directing the parties to appear before him on May 20.
Read 7 tweets
6 May
Voting is as follows:
Hon. Yussuf Hassan - YES
Hon. Abdullahi Bashir - YES
Hon. Abuor Paul - YES
Hon. Beatrice Adagala - YES
Hon. Adan Safia Sheilh - YES
Hon. Shakeel Shabbir - YES
Hon. Alpha Miruka - YES
Hon. Adan Haji Ali - YES
#BungeLiveNA Image
Hon. Fatuma Gedi - YES
Hon. Ali Amin Deddy - YES
Hon. Olago Aluoch - YES
Hon. Rashid Amin - YES
Hon. Otiende Amollo - YES
Hon. Ayub Savula - YES
Hon. Angwenyi Jimmy - YES
Hon. Samuel Arama - YES
Hon. Malimo Arbelle - YES
Hon. Janet Teiyaa - YES
#BungeLiveNA
Hon. David Ole Sankok - YES
Hon. Dennitah Ghati - YES
Hon. Simba Arati - YES
Hon. Samuel Atandi - YES
Hon. Babu Owino - YES
Hon. Badi Twalib - YES
Hon. Owen Baya - YES
Hon. Florence Koskey - NO
Hon. Sakwa Bunyasi - YES
Hon. Rosa Buyu - YES
#BungeLiveNA
Read 32 tweets
6 May
My view and my view now is that unlike what Sen. Linturi has said, if the plenary decides it's a committee, both sides will sit and pick the names as opposed to the whips going to sit in a corner. - @SenMutula #BungeLiveSEN Image
We've done plenary committees here and I sit here during the last one and there were heaps and heaps of paper here. I can bet, most of you never opened even one file. - @SenMutula #BungeLiveSEN
Every accused person wants to feel innocent. We must make every accused person feel innocent. The only problem about committees, because I want to disclose these things, is that if a committee acquits they don't bring the committee report for a vote. - @SenMutula #BungeLiveSEN
Read 4 tweets
6 May
Communication from the chair on the proposed removal from office by impeachment of Hon. Mohamed Abdi Mohamud, Governor of Wajir County. #BungeLiveSEN Image
I hereby proceed to read the charges against the governor:
1. Gross violation of the Constitution, County Governments Act, 2012, the Public Procurement and Disposal Act 2015, and the Public Finance Management Act, 2012. - @SpeakerKLusaka #BungeLiveSEN
a) Failure to account for the financial resources allocated to the county in disregard to Article 201(a), 183(3) of the Constitution and Sections 149 and 166 of the PFM Act. -@SpeakerKLusaka #BungeLiveSEN
Read 14 tweets
6 May
I think this is a very democratic process for us to make that decision. Finally, I want to say that in my many years in Parliament, I would encourage that each Senator has got their own self worth. - @orengo_james #BungeLiveSEN Image
When we sit or camp before the Senate as a parliamentarian, you have your own self worth. And me, I can never be intimidated in my political life. Because I've seen many people come and go. I've seen many powerful people come and go. - @orengo_james #BungeLiveSEN
I have seen presidents come here and go. I have seen people who on their word, you'd leave this house and be locked in the same day, they've come and gone. - @orengo_james #BungeLiveSEN
Read 7 tweets
6 May
PAPERS:
@HonAmosKimunya, Leader of the Majority Party, is currently laying the following papers on the table of the House Today Thursday, 6th May 2021 for the afternoon session.
#BungeLiveNA Image
1.The statutory 6 month preference and resolution report for the Public Procurement Regulation Authority

2. Report of the Auditor General on Financial statements in respect to the following institutions for the year ended 30th of June 2020 and certificates therein..
#BungeLiveNA
-The state department for agricultural research.
-The National Environmental Complaints Committee.
-The Numerical Machining Complex Limited.
-The state department for the East African Community.
#BungeLiveNA
Read 22 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(