~Kijana mmoja alikua mtu wa hasira sana na ugomvi hata kwa jambo dogo. Baba yake alijaribu kumwelimisha madhara ya ugomvi na majibu mabaya kwa watu lakini hakuelewa.
~Siku moja baba yake alimuita na kumkabidhi Nyundo.๐๐พ
Ubao na misumari. Akamwambia "ukigombana na mtu yoyote chukua msumari mmoja njoo gongelea hapa kwenye ubao."
~Siku ya kwanza yule kijana aligongelea misumari kumi, na baada ya mwezi mmoja ubao wote ulijaa misumari.
~Baba yake akamwambia, "fikiria huu ubao ni mioyo ya watu..๐๐พ
Je ni watu wangapi umewajeruhi mioyo yao kwasababu ya maneno yako?" Basi sasa fanya hivi, mfuate kila mmoja uliyemkosea umuombe msamaha, na akikusamehe njoo ng'oa msumari wake.
~Ulikua ni mtihani mgumu lakini mwisho alifanikiwa, basi baba yake akamuambia "Ni sawa watu...๐๐พ
wamekusamehe, lakini tazama ubao, umetoka misumari yote lakini umebaki na matundu. Fikiria ni watu wangapi wamekusamehe lakini wamebaki na majeraha au vinyongo mioyoni mwao kwaajili yako."
~Yule kijana alisikitika sana na kumuomba baba yake msamaha na kumshukuru kwa ushauri...๐๐พ
Mzuri aliompatia.
~Baba yake akamwambia, hakuna asiyekosea sababu sote ni binadamu, ukikosea omba msamaha. Lakini vyema zaidi kutofanya kosa ambalo unaweza kuliepuka.
Siyo pesa tu inayohamisha milima bali hata wewe unaweza kuhamisha mlima kama ukiamua.
Jifunze kitu ktk uzi huu wa Kapuku aliyehamsha mlima na kuitwa "The Mountain Man"
Anaitwa Dashrath Manjhi ni mzaliwa wa kijiji cha Gehlaur nchini India. Kisa cha ๐๐พ
yeye kuhamisha mlima kilizuka baada ya mkewe aliyekuwa anampelekea chakula Manjhi kuanguka mlimani na kufariki, walishindwa hata kumpeleka hospitali sababu kulikua ni mbali.
~Hali hii ilimuhuzunisha sana Manjhi akaona ipo haja ya kufanya kitu kwaajili ya jamii yake. Ndipo ๐๐พ
akaamua kuchonga njia ktk mlima Gehlaur kwa "Nyundo na Patasi tu" ili kurahisisha mawasiliano kati ya kijiji chake na kijiji kingine na kituo cha afya pia endapo kutatokea tatizo kama lililompata mkewe.
~Alipoanza hiyo kazi wengi walimcheka maana mlima wenyewe ulikua wa mawe.๐๐พ