Kati ya mwanaume na mwanamke nani huwa wa kwanza kupenda?
Wanaume wanaweza wasiwe tayari kukubali uhalisia lakini mara nyingi mwanaume huwa wa kwanza kupenda. Mwanamke huwa makini sana ni mtu gani aweze kumpenda, hivyo huonyesha hisia zao taratibu Hadi pale atakapo weza kumuamin
yule mtu.
Sababu zinazopelekea mwanamke awe makini juu ya mtu gani aneeweza kumpenda:
1. Wanawake wamejifunza kuweza kuunganisha upendo na sex
Jamii kiujumla kwa asilimia kubwa imefundisha wanawake kwamba usifanye sex kama haupo katika mahusiano.
Hivyo mwanamke huwa makini
nani aweze kumpenda kwani kumpenda mtu inamaana kumruhusu aweze fanya nae sex
2. Kwa mwanamke mahusiano na sex huwa na athali zake.
Mwanamke huchagua mtu gani ampende kwani ndie anaebeba mimba. Kulala na mtu usiku moja huweza kupelekea miezi 9 ya mimba. Mwanamke anakuwa makini
kuweza chagua mwanaume ambae huenda akawa na mchango bora katika uzao wake. Mfano, kifedha, na kiafya.
Moja ya tafiti iliyofanyika nchini Australia ilionesha wanawake walivutiwa zaidi na wanaume wenye magari ya kifahari sababu yaliashiria uwezo wa wanaume hao kuweza kutunza
familia.
3. Mitazamo hasi juu ya wanawake.
Mwanamke hata akipenda mtu kufunguka kihisia lazima ichukue muda sababu ndani yake kuna sex Linapokuja swala la sex, jamii inamtazamo tofauti juu ya tendo hilo hasa upande wa mwanamke.
Mwanamke anaefanya sex mapema tu baada ya
kuingia kwenye mahusiano hutazamwa vibaya na jamii yake kuliko mwanaume aliefanya nae hilo tendo. Hali inayofanya wanawake wajaribu kuwa na subira linapokuja swala la sex katika mahusiano. #NyumaYaPazia
Mwanasaikolojia;
Daniel Adam Kidingija.
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh