Mwaka 2017 Rick Ross aliachia album yake ya tisa kwa jina 'Rather You Than Me'
Ndani yake kulikuwa na ngoma kali kali pamoja na diss track moja kali sana kwa jina "Idols Become Rivals"
Hii ni diss track maalum kwa ajili ya Birdman
Rosey alimdiss sana mle ndani kutokana na jinsi mwana alivyokuwa anam-treat mshkaji wake wa muda mrefu Lil Wayne
Mle ndani Ross anasema kabla hajatoka alikuwa anawaangalia Birdman na Wayne anatamani maisha yao. Hakutegemea Birdman anaweza kumtenda Wayne vibaya
Sasa kuhusu story ya Rick Ross the Boss, achana nayo!
Lil Wayne alikutana na Birdman kwa mara ya kwanza mwaka 1991 wakati huo ka-Wayne kana miaka 8 tu..
Wayne alikuwa anaishi na mama yake na baba yake wa kambo muda huo
Mama'ake na baba'ake walitengana akiwa na miaka miwili
Wayne akiwa na miaka hiyo 8 alikuwa tayari anaandika mistari na kuchana kwenye vilinge vya jiji la New Orleans Louisiana..
Ndiposa Birdman alipomuona dogo na kutambua kipaji chake...
Birdman akamuona dogo anavyoteleza na beat akamkaribisha pale studio za Cash money records (label yake Birdman na kaka yake Ron 'Slim' Williams)
Kwa sababu Cash money iko pale pale New Orleans Louisiana (nyumbani kwao Wayne), ilikuwa rahisi dogo kushinda studio akiandika mistari
Dogo akaendelea kujifua pale Cash Money japo mama'ake hakupenda kabisa mwanaye ajihusishe na hizo mbanga za muziki wala hawa majamaa 'wahuni' kina Birdman
Ni katika hiki kipindi Wayne alifanya majaribio kadhaa ya kujiua kutokana na "mental distress"
Akiwa na miaka 12 tuh, alisaini mkataba pale Cash Money records na kujiunga nao rasmi kama rapper mdogo zaidi. Hiyo ni mwaka 1995..
Mwaka 1999 Wayne akiwa na miaka 16 alitoa album yake ya kwanza kwa jina 'Tha Block is Hot'
Ikauza zaidi ya copy milioni 1
Kwa Wayne kila kitu kilianza mapema, mambo ya kujigijigi pia. Mwana akiwa high school alikuwa na pisi moja kwa jina Toya..
Mwaka 1999 pia wakapata mtoto wa kwanza. Wakamwita Reginae. Kumbuka by the time Wayne alikuwa na miaka 16 tu😊😊
Turudi nyuma kidogo
Baba'ake Wayne alimtaliki mama'ake wakati Wayne akiwa na miaka miwili tu..
Baadaye mama'ake akaolewa na jamaa mwingine kwa jina Reginald 'Rabbit' McDonald
Sasa huyu Rabbit mwaka huo huo 1999 alitekwa na watu 'wasiojulikana' na wakamuua kwa risasi
Inahisiwa kuwa Birdman na kaka'ake Slim (Ronald) baada ya kuona kipaji kikubwa ndani ya Wayne 'pengine' ndio wali-organize wasiojulikana wakamteka na kumuua Rabbit ili wao wajisogeze karibu zaidi kwa dogo Wayne..
Kweli baada ya kifo cha Rabbit, Birdman akawa sio tu boss kwa Wayne bali km baba kabisa.. (kumbuka Birdman anamzidi Wayne miaka 13)
December 2000 Wayne akaachia album yake ya pili kwa jina 'Lights Out' akiwa Cash Money records. Album imeuza zaidi ya copy Milioni 1..
July 2002 Wayne akaachia album ya tatu kwa jina '500 degrees' akiwa Cash Money
June 2004 akaachia 'Tha Carter '
Dec. 2005 akaachia 'Tha Carter 2'
Mwaka 2005 Wayne akaanzisha label yake akaiita 'Young Money Entertainment' ikiwa chini ya Cash Money. Wayne akimiliki 49%
Mwaka 2006 yeye na Birman wakaachia album ya pamoja kwa jina 'like father, like son'
Ndani yake kulikuwa na vichwa km Rick Ross, T-Pain na Fat Joe. Album kali sana ikiwa na ngoma zenye flow matata kama "Stuntin' like my father"
Wayne akawa nembo ya Cash money
Wayne akaendelea kupiga kazi akiwa 'loyal' sana kwa Birdman na Cash Money
Mwaka 2008 akaachia 'Tha Carter 4' - moja ya album bora zaidi za Lil Wayne..
Ikiwa na ngoma kali km Lollipop, Amilli na Get Money aliyofanya na T-Pain.. akachukua Grammy na Lollipop
2008 akam-sign Tyga ndani ya Young Money, 2009 akam-sign Drake na Nikki Minaj
Label ikawa kubwa kuliko Cash Money... Balaa la hawa watoto lilikuwa kubwa miaka ya 2009 kuja 2016 hapo
Ngoma km Bedrock, Roger That, Tapout, No New Friend na Every Girl in the World haikuwa poa
2009 pia Wayne alikuwa ndani kwenye ngoma ya Birdman kwa jina "Always Strapped" - mara ya kwanza naiona Hummer ilikuwa mle😃😃😀
2011 Wayne akaachia 'Tha Carter 4' - Humu ndani ndo kulikuwa na 6 foot 7 foot, How to Love, John, she will na Mirror - another Classic from Weezy F
Baada ya mafanikio makubwa ya Tha Carter 4, Wayne akaanza maandalizi ya 'Tha Carter 5'.. wakakubaliana na label itoke 2014
Hapo katikati kukawa na kutokuelewana kati ya Birdman na Wayne kutokana na malipo ya kazi zake pamoja na mgawanyo wa pesa zinazotoka UMG
Kutokana na situation ilivyokuwa, Wayne akatangaza kuwa atastaafu muziki baada ya kutoa Tha Carter 5
Birdman hakumwelewa Wayne, akatoa amri Tha Carter 5 isitoke mpaka waelewane
2015 Wayne akapeleka kesi mahakamani akiidai Cash Money USD 51M km fidia ya kuchelewesha project yake
Wayne akasema hawezi kuongea na boss na baba'ake mpaka waachie album yake na wavunje mkataba ule alouita wa kinyonyaji sana.. akasema ubunifu wake umefungwa sana.. akatamka mara kadhaa 'f**k cash money' akiwa jukwaani
Akaanzisha project inaitwa "Free Weezy"
2015 akatia mkataba na Tidal ya Jay-Z, akatoa mixtape 'Free Weezy', ndani yake diss kadhaa kwa Birman
Birdman akamshtaki Jay-Z na Tidal kwa kufanya kazi na Weezy bila kupitia Cash Money
July 2015 Wayne akiwa stejini huko Miami, akapigwa na drink kutoka eneo laVIP la ukumbi
Inasemekana Kinywaji kilitokea eneo alilokaa Birdman na watu wake
July hiyo hiyo bus la Tour la Wayne likashambuliwa kwa risasi likitokea Compound Nightclub huko Atlanta.. Inasemekana ulikuwa mchongo wa Birdman akishirikiana na Young Thug kumdhuru Weezy... tho hamna aliyeumia
July 2016 Wayne akafungua kesi nyingine dhidi ya UMG na Cash money kwa kushindwa kumlipa fidia ya Tha Carter 5 na sehemu ya faida ya kazi za Drake na Nikki Minaj..
Mambo yakawa mengi kati ya Birdman na Lil Wayne (A son Vs a Father)
Nov. 2016 Birdman akamfuata Wayne nyumbani kwake akamuuliza 'mwanangu unataka kiasi gani tumalize hii issue?'
Wayne akasema anataka $ 30M, Birdman anasema alimsainia Cheque ya $ 50M pale pale.. then wakaanza mazungumzo ya yeye kujitoa Cash Money
March 11 2018 wakaonekana pamoja waki-hug na kupiga story
March 31 2018 Wayne akaonekana kwenye release party ya soundtrack ya Birdman
June 2018 akajitoa rasmi Cash Money
September 2018 Wayne akaiachia Tha Carter 5 akiwa huru..
Katika kipindi chote cha kuelewana na kupishana, Birdman ali-act fatherly akisema mara zote kuwa 'that is my son, i love him, i can even kill for him'
Anasema kila kilichotokea ni masuala ya biashara, nothing more..
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh