Msichana aitwae Aida, mwanafunzi wa darasa la tano shule moja ya msingi ilioko huko Ludewa Njombe alikuwa akichukiwa sana na mwalimu wake wa darasa. Aida alikuwa akijitahidi kufanya kila jambo kumfurahisha mwalimu wake lakini mwalimu alizidi kumchukia kuliko wanafunzi wake wote..
Siku moja wamisionari tokea Marekani walitembelea shule ya wakina Akida na wakataka kuwachukua watoto watatu waliopo darasa la tano ili waende nao Marekani wakasome huko na kuwafadhili masomo yao mpaka chuo kikuu....
Kwa kujua hili mwalimu wa darasa la wakina Aida alimweka Aida mwishoni kabisa mwa darasa akae huko ili watakapoingia wale wafadhili wasipate kumchagua.
Wamisionari walipoingia darasani, waliongea na wanafunzi na mmoja wao akaenda nyuma ya darasa.
Kutoka kule alimteua Aida kuwa mmoja wa wanafunzi watakaonufaika na ofa ile ya kwenda Marekani kusoma. Hivyo basi ingawa Aida aliwekwa mwisho kabisa mwa darasa lakini akawa wa kwanza kupata ofa ile ya kwenda kusoma.
Alisoma na kumaliza masomo yake ya chuo kikuu, na mpaka hivi sasa ni mwanasheria katika kampuni moja ya uwakili huko New Jersey Marekani.
HAKUNA ANAYEMTEGEMEA MUNGU AKAACHWA YATIMA ,UKIONA UNAATABIKA JUA NJIA YAKO INASAFISHWA!
HATA katika changamoto za maisha,bado Mungu yupo na Wewe....
Usikubali kumwacha Mungu eti kwa sababu majaribu yamezidi...
Usikubali hali unayopitia inyong'onyeze Imani yako kwa Mungu...
Muhimu:
Hakuna binadamu atakaetibua Mipango ambayo Mwenyezi Mungu amekupangia. Mipango ya adui zako kuzuia baraka zako haitafanikiwa kamwe. Siku zote utakuwa wa kwanza na sio wa mwisho.
Wewe endelea kumwomba bila kukoma...
Endelea kumtumikia Mungu bila kuacha. Endelea kumwamini Mungu kuwa hata katikati ya dhoruba unayopitia atafanya njia.
Kumbuka, kama vile hakuna Kufuli linalotengenezwa bila ufunguo wake; hakuna tatizo lisilokuwa na ufumbuzi kwa Mungu..
Nakutakieni heri ya mafanikio na fanaka katika shughuli zenu halali zinazowaingizieni kipato.
Nakutakieni heri ya mafanikio na fanaka katika shughuli zenu halali zinazowaingizieni kipato KILA SIKU USIKU MWEMA•
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Laki tano, Mshahara wa Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya IPHONE 6 ya kujishebedulia Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pomb HELA FLANI YA MBOGA TU• .... @nyuki_malkia ANAANDIKA✍🏼
Lakini ,Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.
Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambazo zinaweza....
kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.
Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6..
Mwenye degree asiye na ajira kuna wakati huwa anaona bora angeishia form four na angefanya shughuli nyingine... Na aliyeishia darasa la saba kutokana na hali ya maisha aliyonayo kuna wakati anaona alipaswa kufika chuo kikuu ili awe na maisha mazuri...
...HUO NDIYO UTAMU WA MAISHA... Uzuri ni kwamba maisha huwa hayana formula maalum...aliyesoma maskini, wakati asiyesoma ni tajiri, na kuna asiyesoma maskini wakati aliyesoma ni tajiri... Mwenye pesa anaumizwa na mapenzi mpaka anatamani kuwa Single....
na asiye na pesa anaachwa kwa sababu hana kipato cha kumudu gharama za mwenzi wake... Unawaza kuacha shule ili ufanye biashara kwa sababu watu wengi wanafanikiwa na kuna mwenzako anawaza kuacha biashara kwa sababu biashara hailipi ili arudi shule akimaliza akaajiriwe.....