Mwaka 1993 tajiri namba moja duniani alikuwa m-Japan mmoja wakuitwa Yoshiaki Tsutsumi
Huyu somo mwaka huo alikuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni 9
Mwaka 1993 pia ndio mwaka aliokufa mbabe wa cocaine kutoka pande za Medellin Columbia kwa jina Pablo Escobar Gaviria (don Pablo)
Data zinaonesha kwamba wakati somo wetu huyu anaaga dunia alikuwa na mkwanja unaokadiriwa kuwa dola za kimarekani bilioni 30
Sasa ukiangalia hizo namba unaona kabisa kwamba somo wetu Pablo alikuwa na mkwanja mnene kuliko bwana Yoshiaki mara tatu na ushee
Kwa hiyo kimsingi don Pablo ndiye alikuwa Elon Musk wa zama hizo ila kwa sababu chanzo cha hela zake ni ngada, forbes wakawa wanamvungia
Katika historia ya biashara ya madawa ya kulevya, Pablo Escobar Gaviria anatajwa km binadamu wa kwanza kuifanya kwa ufanisi mkubwa sana..
Hii ilimpelekea kufikia kiwango cha juu cha utajiri duniani wakati wa kifo chake
Pablo baada ya kudrop chuo miaka ya 60 mwishoni, alianza kufanya biashara za magendo na wizi wa pikipiki.
Alianza biashara ya dawa mwaka 1970 akifanya kazi na makundi mengine. Huu muda alifanya sana mishe za kuteka watu na kudai fidia kabla ya kuwaachia, akafanikiwa sana
Mwaka 1976 Pablo akaanzisha genge lake kwa jina Medellin Cartel
Baadaye Pablo akaanzisha njia ya kwanza kabisa ya kuingiza cocaine US, akipitia jimbo la Miami..
1976 baada ya kuanzisha Medellin Cartel, Pablo akaanza kutafuta namna ya kupanua empire yake ya kuuza ngada
Ndipo hapo akapata wazo la kutengeneza kikosi cha kusafisha njia kabla hajaanza kuingiza mzigo kwenye empire alizokuwa anafikiria
Yaani iko hivi, wauza madawa wakipata eneo zuri la ku-push-ia bizinea yao, ni lazima walisafishe kwanza
Kusafisha eneo ni kuondoa watu wote wanaoweza kuwavutia askari kwenye hilo eneo
Empire ya cartel haitakiwi kuwa na vibaka, machangudoa, wauza ngada wengine wadogo wadogo n.k
Hawa watu hawahamishwi km wamasai wanavyohamishwa Ngorongoro
Hawa wanauawa.
Pablo akaanzisha kikosi cha mauaji, kikiwa na lengo la kuwaua watu wote walioonekana kuwa kikwazo kwenye maeneo waliyotaka kuweka mzigo wa kutosha
Pablo alitumia baadhi ya walinzi wake aliowaamini sana kufanya recruitment ya vijana wadogo (miaka 13-17) kwenye mitaa maskini mjini Medellin..
Vijana waliopewa kipaumbele ni wale waliokuwa na record za uhalifu, wavuta bangi, walioacha shule na wenye vipaji maalum
Walipopatikana walipelekwa kwa Pablo kuapishwa kiapo cha utii, wakishaapa wanaenda kambini sasa kwenye mafunzo
Kambi za mafunzo ya sicarios ni milimani, mbali na makazi ya watu. Kwenye misitu minene
Interview zinagawanyika kutokana na rekodi za uhalifu wako
Kwa kijana aliyewahi kuua mtu kabla (intentionally) anaweza kupewa bunduki akaambiwa amuue mwenzake waliyekuja naye.. akishindwa anauawa yeye
Kwa wale ambao hawajawahi kuua kabla wanaanza na brainwashing kwanza
Wanafundishwa kuwa kuua ni kazi km kazi zingine, wanafundishwa kuwa hata hivyo sio wao wanaoua ila yule anayetoa order - boss wao
Wale wanaofuzu kwenye hizi interview za kwanza wanaanza mafunzo sasa
Wale wanaofeli wanauawa afu wanatundikwa mtini wanatumika km target kwenye kujifunza kulenga shabaha
Kuna sicario mmoja alihojiwa na gazeti la NYT akasema kwenye hii interview ya pili kwa sababu yeye alikuwa ameshaua mtu kabla, basi alipewa kisu afu akaoneshwa mwili wa mtu aliyeuawa. Akaambiwa aukate vipande vipande.. anasema ukionesha kusita au kuogopa unakula bullet ya kichwa
Mafunzo yanaendelea sasa, mnakuwa na mafunzo ya shabaha, kukimbia, kujificha, kutambua target, kusoma mazingira iliyoko target yako n.k
Inasemekana kuwa kwenye haya mafunzo kosa dogo sana linakupatia adhabu ya kifo..
Kuna hatua mkifika mnaenda field, mara nyingi field zao huwa ni kuwawinda maafisa wa polisi na kuwachalisha
Anayeshindwa kutii order ya mkufunzi hufanywa target pia. Yaani mnaweza kuamka asubuhi mwenzako akapewa mission ya kukuua, au wawili mkapewa mission moja - kuuana
Atakayemuwahi mwenzake ndo anakuwa amesave
Mnaweza kwenda 20 kwenye mafunzo, mkahitimu 6
Baada ya kuhitimu mnarudi kwa boss, mnasaini mkataba wa kazi afu mnarudi mtaani kwenye maisha yenu ya kawaida. Ikitokea mission unaitwa chap unapiga unapata bonus unaendelea na maisha
Sicario akishapewa oda huua yeyote anayeonekana kikwazo kwenye biashara..
Kuanzia polisi, wanasiasa, wanaharakati, waandishi wa habari, wanachama na viongozi wa cartels nyingine, viongozi au wanachama wa cartel yenu wanaokaidi amri au wanaoanza kuwa na ushawishi kupitiliza n.k
Pia sicario anaweza kupewa mission ya kumuua sicario mwenzake ambaye haonekani kueleweka kwa wakuu
Baada ya Pablo kuanzisha matumizi ya Sicarios 1970's na kuonekana ni idea nzuri, baadaye cartels nyingine zikaanza kutumia sicarios pia.
Wakapanda bei
Kwenye late 1980's sicario mbali na mshahara wake alikuwa anapata hadi US $2000 km bonus akiua mtu mmoja
Kuna sicarios wana rekodi za kuua mpaka watu 300 na kuendelea
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
April 30, 2021 mwanetu DJ Khaled aliachia album yake ya 12..
Ndani ya ile album kuna ngoma inaitwa 'SORRY NOT SORRY'
Ndani ya hiyo ngoma kuna ma-legendary wawili wa Rap, wazaliwa wa New York. Wana wanachana ki-boss sana kuelezea mafanikio yao mle
Hapa kuna Nasir Jones aka Nas, kule kuna Sean Carter au Jay Z.. kiitikio kimegongwa na James Fauntleroy
Ni ngoma ya kitajiri sana. Wana hawajatumia nguvu nyingi, wanatiririka tu ki-boss sana na wanaeleweka (si unajua tena tajiri hata akikohoa kuna kitu anakuwa anamaanisha😁😁)
Sasa ule wimbo ni sehemu ya udhihirisho wa mapatano kati ya Nas na Jay Z kufuatia beef yao nzito sana miaka ya mwishoni ya 90 na 2000 mwanzoni
Shuka na huu uzi upate ABC za hii beef iliotikisa muziki wa Hip Hop miaka ya 90 mpaka 2000 mpaka mama mzazi wa Jay Z akaingilia Kati👇