Mwaka 2013 Club Billicanas ilifunguliwa baada ya ukarabati wa gharama kufanyika. Ilikuwa ni uwezo wako wa kunywa/kula siku hiyo. Freeman Mbowe alilipa bili zote. 2015 anaingia mwendazake madarakani, anaanza vibweka, 2017 BILLZ inavunjwa kwa unyama. Mwendazake alikuwa katili sana.
Picha ya kwanza Club BILLZ ikiwa na uhai wake. Show kubwa za wasanii wa ‘bongo fleva’ zilifanyika hapo. Frame ya pili ni baada ya Club Billicanas kubomolewa kwa hila tu, sababu nyingi zikiwa za kisiasa. Watu wengi wakakosa ajira. Eneo hilo sasa ni parking tu ya magari. Roho mbaya
Mbowe Hotels ambao walikuwa wapangaji wa muda mrefu kwenye jengo hilo ambapo mbali ya kuendesha Club Bilicanas pia kulikuwa na ofisi za gazeti la Tanzania Daima. Mwendazake alibomoa na hakujali mali na samani zilizokuwa ndani. Ilikuwa ni mbaya sana. Uharibifu ulikuwa mkubwa.
Watu wakajiokotea mali na vitu vingi, ilikuwa ni kubeba unavyoweza na kutokomea na NHC wakatangaza mbada wa mali zilizokamatwa kwamba Mbowe alikwepa kodi ya Shs. 1.2 bilioni kwa miaka 20, jengo la NHC makutano ya mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi, katikati ya jiji Dar es Salaam
Magari yalishuhudiwa yakisomba mali mbalimbali ambapo mmoja wa maafisa wa NHC ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema wanachukua mali ambazo zinaweza kupigwa mnada tu. Lakini mali nyingi hazikuwahi kuonekana tena hata katika mnada Julai 6, 2019. Ulifanyika wizi wa mali tu.
Vyombo hivyo vilikamatwa na kampuni ‘HEWA’ ya udalali ya Fosters Auctioneers & General Traders iliyopewa kazi ya kuondoa vifaa hivyo baada ya Freeman Mbowe kudaiwa kushindwa kulipa deni hilo ndani ya miezi 2 ya notisi ambayo shirika hilo lilikuwa limempatia. Ukatili wa mwendazake
6 Jul 2019, Dalali wa mahakama Joshua Mwaituka, kwenye ghala la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo maeneo ya Bandari alivitaja vifaa vilivyonunuliwa ikiwa ni pamoja na taa, jukwaa, viti, kreti za bia, jenereta, Mashine za kupozea na samani mbalimbali kasoro makochi.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC wakati huo, Nehemia Mchechu alisema pamoja na Bilicanas, shirika linazidai taasisi za umma, binafsi na watu binafsi jumla ya Sh. bilioni 15 akasisitiza Notisi ya siku 60 ya kuondoka Bilicanas pamoja na majengo ya wadaiwa wengine ilishatolewa.
Mchechu alisema ukusanyaji wa madeni hayo kwa nguvu ni mkakati wa shirika hilo kukusanya fedha ili kusaidia ujenzi wa nyumba za watumishi wanaohamia Dodoma. “Mwaka huu ujenzi unaanza Dodoma,” alisema Mchechu, hivyo “fedha tunazodai zitatusaidia kukamilisha uwekezaji mjini humo.”
Mungu siyo Athumani, 16 Dec 2017 — Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akaagiza kusimamishwa kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu na June 21, 2018 uteuzi wake ukatenguliwa.
JPM pamoja na uharibifu na ukatili wake alikuwa ni fursa. Wakati wote nasema, JPM alichelewa kutawala ardhi yetu. Nimeeleza. Alitusaidia mambo mengi kwa kutumia udikteta wake. Tulishughulikiwa na kuimarika sana. Tukashikamana na kuwa imara. Tuliwafahamu hadi matapeli ndani yetu.
Ni ukweli dhahiri. Ni tabia za binadamu wote. Kadiri anapoumizwa ndivyo anavyochukizwa. Ni kama alivyo mnyama Paka. Ni kiumbe mpole sana. Huwezi kumuona akigombana na wenzake hovyo. Lakini ukimfungia chumbani, ukampiga, utaona upande wake wa pili. Wataalam wanaita “Apathy spirit”
Wakati wa SSH, tunacheka pamoja ikulu, tunakutana Serena, wakati huo CHADEMA hawaruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara, CCM wanakusanya wanachama mikoani viongozi wake wakuu wanazunguka. Utashiriki vipi uchaguzi wakati ulikuwa likizo miaka 5 yote ukicheka na mwenyekiti wa CCM?
Nimekumbuka makala ya “Collective Imbecilization” Profesa Chachage imeandikwa na Jenerali Twaha Ulimwengu….
Neno “Imbecilization” usilitafute katika kamusi ya kiingereza kwa kuwa hilo ni neno alilotengeneza Profesa Seithy Chachage mwenyewe. Alikuwa binadamu akili nyingi.
Hili jaribio la kuwapumbaza watu mamilioni kwa mpigo. Ni kama vile ingewezekana kuwakusanya watu milioni 50, ukawaweka ndani ya ukumbi mmoja kwa ukubwa huo, ukafunga madirisha na milango, kisha ukawanyunyizia dawa ya uzuzu, ubwege na ufala, ikawakolea sawasawa,
kabla hujawaachia waende Duniani waendelee shughuli zao. Hiyo ndiyo Chachage aliita “collective imbecilization”
Dhahiri hiyo haiwezekani katika mazingira ya kawaida. Isipokuwa inawezekana watu wakapumbazwa kwa pamoja, wakafanywa mazuzu kwa pamoja, wakageuzwa mabwege kwa pamoja
SINOHYDRO Corporation LTD wamepewa zabuni kujenga mradi wa mwendokadi BRT-3 Gongo la Mboto-Kariakoo (23.6km) kwa $148.1M na wamepewa zabuni hiyo bila ushindani (single source), wakati ujenzi wa BRT 2 (Gerezani -Mbagala) 20.3km wamejenga chini ya kiwango. Hawa wachina wameturoga?
Zingatia, huo ni mkopo kutoka benki ya Dunia (WB). Na serikali ya Tanzania imekopeshwa $246.7 million kwa ajili ya ujenzi wa BRT-3 ($148.1 million) na BRT-4 ($99.9 million). Wanazo. Wakati huo DART wametumia $2.46 million to 77 kulipa wakazi kupisha ujenzi wa 23.6km kwa BRT-3
BRT-1 ni 21km ilijengwa na STRABAG international GmbH, Kimara kwenda Kivukoni, Morocco, Gerezani kupitia Ubungo, ulikuwa mkopo wa AfDB na WB na $154M. Lakini sasa BRT-2 na BRT-3 wamepewa SINOHYDRO ambao BRT-2 wamejenga chini ya kiwango na baadhi ya sehemu barabara imeharibika.
Riwaya iliandikwa na Euphrase Kezilahabi na kuchapishwa January 1, 1971, ni kitabu SERIKALI ya Nyerere ilikipiga marufuku sababu zikitajwa maudhui yake yalikuwa ni yenye kudhalilisha (haikuthibitishwa) ukatoliki. Dhehebu ambalo Mwalimu Nyerere alikuwa muumini huko
Watu wanajiuliza, endapo katika riwaya hiyo lingetumika jina la "MwanaAsha" kubeba taswira ya binti Rosa, wakatoliki akiwepo Mwalimu Nyerere wangelikasirika na kuzuia uchapishwaji wa riwaya hiyo ya Euphrase Kezilahabi? Maswali tu, tunajiuliza!
Kanisa katoliki pia likalalamika kwamba Mistika ni moja wapo kati ya sifa za Bikira Maria Mtakatifu (mama wa Yesu). Hivyo ni udhalilishaji kumpa Rosa jina hilo katika riwaya hiyo kwa sababu ni mchafu wa matendo kiwango cha juu katika riwaya hiyo.
Katiba yetu hakuna cheo cha “baba wa taifa”. Hakuna kanuni/sheria yeyote imetungwa wananchi kutambua cheo hicho. Sifikirii kama mtakuwa sahihi mkitaka Mwl. Julius Nyerere atambuliwe na wote kwa jina la ‘baba wa Taifa’. Ni Rais wa 1 wa TZ. Historia ya taifa letu ipo kabla yake!
Ni kizazi dhalimu tu ndiyo kinaweza kupewa kila kitu na kukubali bila kuhoji. Neno “kwanini” linaonyesha ustawi wa ubongo. Hili siyo dola la kijeshi, kifalme au kisultani. Hatupokei kila neno na kumeza. Ndiyo, hakuna sheria inayotutaka tumtambue kwa cheo cha “baba wa taifa”. Ipo?
Mwl, kaikuta TAA chini ya Abdulwahid Sykes. AA ineundwa 1929. Nyerere amezaliwa 1922. Anawezaje kuwa baba wa taifa? AA imebadilika kuwa TAA mwaka 1948 na kuwa TANU 1954. Historia ya kudai uhuru wa Tanganyika ineanza miaka mingi kabla ya Nyerere. Katikati ya miaka ya 1920.
Ukumbi wa Msekwa imefanyika semina, wabunge wamelipwa Shs. 440,000 (Shs. 172.9M). Kuipitisha bajeti ya miundombinu (ujenzi wa lot Na. 6 ya Tabora - Kigoma (411km). Na gharama za ujenzi ni (Sh.11.1bn) kwa kila 1km. 411km mkandarasi atatumia Shs. 4.6T. Kapewa tender bila ushindani.
Mnakumbuka niliwapa simulizi, wizara ya fedha wameingia makubaliano na China Civil Engineering construction corporation kwa utaratibu wa single source (tenda bila ushindani) thamani ya Shs. 6.7 trilioni kwa utaratibu wa manunuzi wa moja kwa moja ‘single source’ bila ushindani?
Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation alipewa ujenzi wa lot Na. 5, Isaka – Mwanza (249 km). Miezi 16 amejenga 4.4% pekee na HAKUNA hata kipande kimoja cha reli ameweka katika miezi 16. Mwigulu anasema bungeni kwamba haukuwepo ufadhili wa kifedha. Ni mzaha.