Dr. Badi 👴🏽 Profile picture
Jun 6 24 tweets 4 min read
Kama huna mpango wa kufanya biashara au hutaki kufika mbali kibiashara Usisome #Thread itakuboa

Utasikia watu wakisema "dah huyo jamaa ana akili ya biashara sana" au "yule dada ana akili ya kibiashara sana". Au "huyu jamaa hana kabisa akili ya kibiashara....
Hii AKILI YA KIBIASHARA ni nini hasa? Well, Business Acumen ni uwezo wa mtu kufanya maamuzi ya HARAKA na YALIYO SAHIHI kibiashara Yaani maamuzi yake yanakuwa ya haraka (not slow) na wakati huo huo yanakuwa maamuzi sahihi. Mpaka hapa utagundua ni watu wachache wana uwezo huo. ..
Kumbuka nimesema maamuzi ya HARAKA... sijasema maamuzi ya PUPA ya KUKURUPUKA. Kuna tofauti kubwa sana.

Kama huna utashindwa tu biashara hata kama unaiombea biashara yako kwa Mungu kutwa mara tatu kama dozi. Mungu hafanyagi mazingaombwe. Mungu anaoperate kwa KANUNI.....
Sasa unaweza kuniuliza swali: Dr Badi nitajuaje kama nina Business Acumen au la?"

Well njia rahisi ni kuangalia namna unavyofanya maamuzi yanayohusu jinsi unavyotaka kuingiza pesa maishani mwako iwe kupitia biashara au ajira.....
Ngoja nikupe Mfano

Mwaka 2016 nilikutana na vijana wawili waliokuja kwa ajili ya kupata mafunzo ya biashara. Ni vijana wa Chuo Cha Kamapala University (KIU) Baada ya kuongea nao Nikaamua kuwapa test ya swali. Wote niliwapa test ya swali linalofanana..
SWALI:

Chukulia kama umeitwa kwenye usaili wa kazi (ajira) na kampuni mbili tofauti kwa wakati mmoja. Kampuni A na kampuni B. Ukaamua ukafanye usaili kote ili kujaribu bahati yako. Na bahati nzuri kote ukafanya vizuri hiyo interview lakini tofauti ikawa kwenye offer zao.....
KAMPUNI A*
Kwenye hii kampuni ukapewa offer ifuatayo.

1. Mwaka wa kwanza utalipwa shilingi 300,000/ (laki tatu kwa mwezi) kwa mwaka mzima kwa kuwa huna experience yoyote na ndo utaratibu wao kwa mtu yeyote mpya asiye na uzoefu wa kazi....
2. Mwaka wa pili utalipwa shilingi 400,000/- (laki nne) kwa mwezi mwaka mzima kwa kuwa umeanza kupata experience kidogo

3. Mwaka wa tatu utalipwa shilingi 600,000/ (laki sita) kwa mwezi maana wanaamini sasa uko vizuri zaidi ....
4. Na mwaka wa nne mshahara wako utaongezeka na kuwa shilingi 1,200,000/- (milioni moja na laki mbili)

Then baada ya hapo mta-discuss upya kulingana na performance yako na kuona miaka inayofuata

*KAMPUNI B*
Kwenye hii kampuni ukapewa offer ifuatayo.....
1. Mwaka wa kwanza hutapata mshahara kabisa bali utapewa posho tu ya nauli shilingi 50,000/ (elfu hamsini kwa mwezi) kwa mwaka mzima kwa kuwa huna experience yoyote na ndo utaratibu wao kwa mtu yeyote mpya asiye na uzoefu wa kazi pia....
2. Mwaka wa pili pia hutopata mshahara bali posho yako itaongezwa mara dufu itakuwa shilingi 100,000/- (laki moja kwa mwezi) mwaka mzima kwa kuwa umeanza kupata experience kidogo na bidii yako imeonekana...
3. Mwaka wa tatu utaanza kulipwa mshahara wa shilingi 300,000/ (laki tatu kwa mwezi) mwaka mzima maana wanaamini pia sasa uko vizuri zaidi na unastahili mshahara rasmi sasa.

4. Na mwaka wa nne mshahara wako utaongezeka na kuwa shilingi 900,000/- (laki tisa)...
Mmoja Akasema ndani ya miaka minne kwenye kampuni A nitakuwa nimeshatengeneza jumla tsh2,500,000 wakati kwenye kampuni B ndani ya miaka minne nitatengeneza juma tsh1,300,000/ so hapo nitachagua kampuni A maana naweza kujibana nikaanzisha muradi pembeni.ukiangalia yuko sahihi..
Swali hilo niliendelea kuwapa watu mbali mbali kwenye talks zangu za biashara kuanzia mwaka huo 2016 hadi sasa na kuuliza sababu zao na katika kila watu takribani 10 basi watu 8 au 9 huchagua kampuni A ni mmoja tu au wawili ambao wao huchagua kampuni B...
nilipowauliza kwa nini wanachagua B mmoja akasema ukiangalia jinsi kipato kinavyoanza unaweza kuchagua A lakini ukiangalia jinsi kinavyoongezeka ukiwa na akili utachagua B.

Wow!

And very much so. Nikaona kijana anawaza tofauti sana na watu wengi sana....
Hebu tutazame tena zile offer.. Ukitazama kampuni A kutoka mshahara wa laki 3 hadi laki 4 kwa mwaka ni ongezeko la 33% tu japo pesa inaonekana nyingi lakini kampuni B kutoka posho ya elfu 50 hadi laki 1 kwa mwaka ni ongezeko la 100% japo pesa inaonekana ndogo mkononi...
Hapa ndipo ilipo tofauti ya namba tu na hesabu. Ndipo ilipo tofauti ya mtu mwenye pesa na TAJIRI.

Kwenye ulimwengu wa kibiashara usiangalie namba tu angalia mahesabu yamekaaje. Usiende tu kufuga kuku kisa umeambiwa inalipa. Do the maths!..
Sasa tuwaze mbele zaidi. Kama kampuni hizi zikiendelea increment (ongezeko) la asilimia hizo hizo za hapo mwishoni miaka minne mbele then kwenye kampuni B utakuwa unalipwa mara nyingi zaidi ya kampuni A.

Wanasema if all factors remain constant.....
Listen to me. Maamuzi ya kufanya biashara hayaangalii UHAKIKA wa chochote.. Wewe siyo Mungu. Ndo maana tunasema TAKE THE RISK. Hakuna anayeweza kukuhakikishia chochote. Mtu atakupa potential ya biashara husika tu. Lakini siyo UHAKIKA. Piga mahesabu tu vizuri....
Ndo maana nazungumzia BUSINESS ACUMEN.

Kitu muhimu katika biashara siyo pesa utakayoingiza mwezi huu huu na ujao. Ukiona unawaza kuanza biashara halafu unawaza mwezi ujao mtaji wako urudi (break even) basi hujawa tayari kuwa mfanyabiashara. Bado una mawazo ya kiAJIRA. ...
Sasa wewe unataka eti ufundishwe biashara ambayo utapiga hela leo leo. Kabet Liverpool kumfunga Real fainali my friend. Maana Betting siyo ya wafanyabiashara ni ya wanaobahatisha zali la mentali kama wewe ulivyo in your mind....
Listen to me closely my friend. Pesa hupenda kuja taratibu ikukute uko tayari kuihandle kiusahihi. Unspaswa kuwa tayari kuvumilia huo mchakato. Hujiulizi kwa nini hakuna mtu amewahi kutajirika ndani ya mwaka mmoja wa biashara? Yani miezi 12 toka ameanza?...
Ni kwa sababu pesa inahitaji uwe na uzoefu wa kuihandle. Sasa unaweza kujua matumizi sahihi ya milioni kumi na ya bilioni moja ndani ya miezi 12 kwa mara yako ya kwanza?

Develop your business acumen first.....
Nakutakia mafanikio kibiashara; amani malangoni mwako na salama ndani ya nyumba yako. Kama una nia ya kujifunza biashara karibu DM IKO WAZI . (Serious people only). Kama una biashara na unataka iende kwenye next stage na unahitaji kujua nini cha kufanya karibu•

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Dr. Badi 👴🏽

Dr. Badi 👴🏽 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @DrBadiBoy

Jun 4
Ukitaka kujenga maisha mazuri ya #baadaye halafu unataka uyajenge ukiwa umerelax na ukiwa "comfortable" basi unachojenga siyo maisha ya baadaye. (Kama hunielewi ngoja hiyo baadaye ikifika utaelewa tu) Jitie kichwa Ngumu eti hujitambui….
Business Empires na lasting success katika field yoyote iwe siasa au diplomasia, ministry, biashara au uwekezaji, michezo na burudani, mahusiano na familia nk haijengeki mpaka ukubali kwanza maisha yako yawe UNCOMFORTABLE a lot!…….
Chunguza wote waliofanikiwa katika jambo lolote utaona hakuna aliyekuwa anaamka saa moja asubuhi mara saa mbili. Ni saa kumi au kumi na moja alfajiri. Au hata saa tisa kabisa mtu yuko macho tayari…..
Read 7 tweets
Jun 2
#UZI SOMA ITAKUSAIDIA ✍️

Ukiwa katika changamoto nyingi na huoni wa kukusaidia kabisa... basi jua ndivyo ilivyopaswa kuwa.. yaani kuna kitu Mungu aliweka kwenye kichwa chako anataka ukitumie vizuri. Na ukitii hiyo sauti utajishangaa kuwa kumbe una solution nyingi balaa…. Image
Kwamba kumbe wewe ni creative kuliko ulivyofikiri. Kwamba kumbe wewe una mpaka majibu ya changamoto za wengine wengi tu, na kumbe wewe mshauri na mtia moyo wa wengi waliojikatia tamaa sababu ya umasikini na magonjwa makubwa kuliko wewe sema nivile umekilemeza hicho kichwa….
Je! Una changamoto na unatamani kupata mtu wa kukutia moyo? Unatamani mtu wa kuomba na wewe ili usikate tamaa?
Vizuri Unatamani jambo jema kabisa Lakini sasa unachopaswa kufanya ni kutafuta mtu wa kumtia moyo. Kama wewe unavyohitaji basi kuna wengi zaidi wanahitaji kutiwa moyo…
Read 17 tweets
May 31
Leo ukibahatika kushika baadhi ya simu za wapendwa wako utakuta wengi wao wana picha zako nyingi kwenye simu zao lakini hutawaona wakizitumia picha hizo mahali popote pa wazi kukusifu,kukupongeza wala kukutia moyo. ……
Ila wamezitunza tu ili siku moja ambayo wewe hutakuwa unaweza kuona wala kusikia waadike mengi kuhusu wewe ambayo wewe kwa wakati huo hutaweza kuyasoma wala kuyaona wakikusifu.

Kwa Jina la Yesu yeyote ambaye hatakusifia wakati ambao unaona anasubiri kukusifia wakati ambao…
utakuwa huoni asuburi sana kwa Jina la Yesu.
Lolote baya analokuombea aliye adui yako wa siri halitakupata wewe kwa Jina la Yesu.

Ni maombi yangu ya kwamba kabla ya Mwaka huu kuisha Mungu akakutendee mema hata asiyependa kusema kuwa anakufahamu ….
Read 4 tweets
May 31
#UZI SOMA UJIFUNZE👇..

Mzee Bakhressa anaishi Masaki lakini maji ya Uhai au lambalamba na chapati zake hauzii majirani zake. Au ulishaona vile vibaiskeli vya lambalamba za Azam vikizunguka Masaki nyumba kwa nyumba?...
Mzee Mengi toka akiwepo mpaka leo hakuwa akiuza maji ya Kilimanjaro kwa ndugu zake au wakwe zake au jirani zake.

Shigongo hauzi magazeti kwa majirani zake maana unaweza kukuta majirani zake wanasoma Daily News na The Citizen na wasijue hata sura ya gazeti la Shigongo ipoje...
Dewji hauzi vitu vyake kwa classmate wake wa zamani au jirani zake. Masanja anauzia mchele majirani?

Lakini wote hao niliowataja wamepiga hatua bila kujali jirani au ndugu au classmate zao wa zamani wananunua au la.
Hiyo ndo akili ya kibiashara....
Read 19 tweets
May 31
KUWA MAKINI NA WATU UNAOWASHIRIKISHA NDOTO ZAKO,MAONO YAKO

Wengi husema ili uweze kufanikisha Ndoto zako basi haina budi kuzizungumza Kwa watu ili ikupe deni la kutimiza

Mimi nasema sio wote wa kuwambia….
Daudi aliwambia Kaka zake juu ya kwenda kumuua Goliath wakamkatisha tamaa na kumwambia arudi nyumbani Kuwa yeye hawezi.

Kuna watu ukiwambia Maono yako watasema hayo Maono ni makubwa huwezi,hivyo watakukatisha tamaa…..
Yusufu mtoto wa mzee Yakobo alivyowambia Kaka zake juu ya Ndoto alizokuwa anaota walijenga chuki juu yake,wakamuita Bwana Ndoto na kumpangia njama ya kumuua hatimaye kumuuza Misri….
Read 9 tweets
May 30
Njia ya kufikia mafanikio ni nyepesi tu:

Unaanguka.
Unachubuka.
Unapata hasira zaidi.
Na kwa hasira unaamua kusonga mbele zaidi bila kugeuka nyuma.
Majanga baada ya majanga yanakukuta.
Hakuna anayekuona kwamba na wewe ni wa maana au unachofanya ni cha maana sana….
Jasho na maumivu ndo vinakuwa washirika wako wa karibu.
Ndoto zako zinaonekana kama hazitamia tena licha ya mapambano ya muda mrefu.
Unaanza kufikiria kuacha.
Wakati ndo unataka kukata tamaa tu ghafla kuna kama mafanikio kidogo yanakubeep.

Unapata moyo kidogo... unajaribu tena
Mafanikio yanaongezeka kidogo.

Ushagraduate! Akili yako ishakuwa tayari kwa mafanikio makubwa.

Then BOOM!!! Struggle zote zinakulipa pakubwa. Umefanikiwa!

Sasa rafiki...mpaka ufike hapo kwenye "BOOM!!" ujue ushapigana kwa miaka ya kutosha. ….
Read 5 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(