Madinidotcom Profile picture
Jul 10, 2022 25 tweets 10 min read Read on X
Nini kinaendelea SRILANKA..?

Uzi🧵

#Trustory labda umeshaona story nyingi kuhusu SRI LANKA na labda hujui tumefikaje hapa na ndiyo sababu unasoma hapa,au unajiuliza hivi nchi inawezaje ku collapse kiasi cha kukosa hela?kwanza nchi inakosaje hela?inamaana noti zimepotea? Image
Mwingine hata huelewi SRI LANKA yenyewe ndo wapi. So twende nikupe historia simpo yenye MASUALA Mazima ya uchumi ndani yake. Sri lanka ni kisiwa kipo kusini mwa INDIA zamani sana inasemekana kulikuwa na barabara kabisa kutoka INDIA hadi SRI LANKA ya sasa Image
lakini #Trustory maji yalifukia hilo eneo na sasa wana mpaka wa kwenye maji,ni sawa na kusema SRI LANKA zamani ilikuwa #peninsula na sasa ni kisiwa, ukiangalia watu wake wanafanana na jamii ya wahindi.Ushaskiaga wahuni wanaitwa Tamil Tigers? ImageImage
Yes hawa waasi waliotaka kujitenga walihit sana miaka ya nyuma,kutokea jamii ya wa TAMIL ambao walikua wanaonewa sana na serikali so wakakinukisha kutaka kujitenga waunde taifa lao. Image
Ni nchi ambayo mwenzi march mwaka huu ilifikia kuahirisha mitihani ya taifa kwenye shule za miji kadhaa kwasababu serikali ilikosa karatasi na wino wa kuchapisha mitihani,so wanafunzi wakala bata.Kama ulikuwa hependi mitihani labda utatamani enzi zako yangetokea ya SRI LANKA Image
lakini ni zaidi ya uwazavyo ,kila kitu kilipanda bei mara dufu,(unajua maraDufu wewe?) kuanzia mafuta, mchele,dawa za binadamu na Umeme unakata kwa saa 15 kwa siku, kudadadeki(in haji manara’s voice)
Hali ya maisha imekuwa ngumu kiasi cha kuwaleta pamoja watu wa dini zote Image
wakristo,waislam,wahindu,Budha na wasio na dini ambao miaka 10 nyuma walikuwa wanapigana wenyewe kwa wenyewe,leo wameungana kuingia mitaani kukinukisha dhidi ya serikali. Wahuni wameandamana hadi kwenye makazi ya rais na wanapiga mbizi kwenye swimming pool la rais Image
na rais ameamua kusarenda na kusema anaachia ngazi.
Shida ya SRI LANKA inazunguka ndani ya familia 1 ama ukoo wa mzee RAJAPAKSA ,hii ni familia ambayo imekuwa ikiongoza sri lanka kwa miaka 20 sasa,undugu-naization wao ndo unadaiwa chanzo cha kuiingiza nchi kwenye madeni Image
yasiyolipika na uchumi wake umecolapse kwenye kiwango cha kushindwa kununua karatasi za mitihani.Serikali imejaa ndugu ambao wanalaumiwa kwa upendeleo a.k.a undugu-naizesheni ,rushwa na matumizi mabaya ya ofisi. Image
Mahinda Rajapaksa ndiye aliyeanzisha safari ya undugulaizesheni aliingia kwenye urais 2005-2015 na wakati huu alihakikisha kila ndugu yake ambaye alikuwa na ‘potensho’ ya uongozi alipata nafasi nyeti serikalini,wakatafuna nchi na mwaka 2015 ndo wananchi wakaamua kuchagua Image
‘PIPOZ PAWA’ YAO akaingia madarakani kiongozi wa chama pinzani
MAITHRIPALA SIRISENA akaingia white house.Hata hivyo hakuna maajabu, miaka 4 mbele 2019 ukafanyika uchaguzi akapigwa chini, na aliyeshinda ni GOTABAYA RAJAPAKSA ,ambaye ni mdogo wake na Mahendra RAJAPAKSA Image
aliyekuwa rais before,so familia ikarudi madarakani.GOTABAYA alipoingia ofisini akafanya uteuzi, jopo lake la mawaziri likiongozwa na waziri mkuu na gues what,akamteua MAHINDA kuwa waziri mkuu wake,yaani aliyekuwa rais kwa miaka kibao amerudi kuwa waziri mkuu Image
Unaweza kushangazwa na hili ukiwa Africa au pengine, lakini kumbuka SRI LANKA ina historia ya kuongozwa na KILE WANAITA Dynasty(Familia inaongoza nchi) km unavyoona korea, Japan na bara la ASIA kiujumla.Uarabuni wanaita Emirates. Image
Akamteua mwanaye wa kiume kuwa waziri wa michezo,na kifupi uwe shemeji,binamu nyama ya hamu au yeyote unayehusiana na familia ya RAJAPAKSA ujue mashavu yapo nje nje.Ukumbuke miaka yote wanachaguliwa kwa kura na mifumo ya kiserikali lakini undugulaizesheni umefanya imeonekana Image
kama SRI LANKA ni serikali ya familia. Both GOTABAYA na MAHINDA wanalaumiwa kwa hapa tulipofikia kwasababu mbalimbali.Kuelewa kilichotokea SRI LANKA, kiliwahi kutokea UGIRIK. Ni kitu real kwamba uchumi wa nchi unaweza kucolapse ndiyo maana kila nchi ina watalam wa uchumi Image
na taasisi zinazodeal na mambo hayo.Hii itakupa kuelewa uchumi wa nchi yyte unavyofanya kazi.Mzunguko wa uchumi wa nchi yoyote una sura au makundi 2.Nchi inapokuwa ina IMPORT zaidi, yaani inanunua VITU nje kuliko inavyotoa ndani kupeleka nje (export) wanaita TRADE DEFICIT. Image
Nchi ambayo wana EXPORT vitu kuliko wanavyo IMPORT inaitwa TRADE SURPLUS .Kwa harakaharaka tumezoea hutakiwi kutumia kuliko unachoingiza, lakini kwenye uchumi ni complicated kidogo.Mfan MAREKANI wana DEFICIT kubwa kinoma,yaani wanaingiza bidhaa nyingi kuliko wanazouza nje, Image
Lakini JAPAN wana SURPLUS KUBWA yaani wanauza nje kuliko wanavyoingiza ndani, Sri Lanka ni nchi iliyokuwa kwenye kundi la TRADE DEFICIT yaani wanaagiza vitu vingi kutoka nje.Nchi za aina hii zipo nyingi duniani sio kitu kigeni wala kibaya kivile,shida ni kinapokosa balancing Image
so pesa ya kigeni ilihitajika kwenye mzunguko muda wote.Kwa kesi ya Marekani wao ndo Center ya pesa ya kigeni yenyewe na wana sera zinazoilinda Dola na mzunguko wake unafanya dola kuwa pesa inayoaminika msimamo wake sokoni.Ndio maana USD ni SI UNIT ya pesa nyingi duniani. Image
Kifupi Biashara duniani inafanyika kwa DOLA ya kimarekani (USD).Na haijatokea bahati mbaya,niliwahi kukwambia KIHISTORIA kwanini USD ndo pesa inayotumika zaidi duniani.
Kwahiyo tunaposema pesa za kigeni mara nyingi ni ile ambayo inapokelewa sehemu kubwa duniani ambayo nchi husika Image
inategemea kupata bidhaa hizo. So ni dola ya kimarekani.Sri lanka wanaimport dawa,mafuta yote,vyakula na mambo kibao.Kinachofanyika kwenye nchi za aina hii ya uchumi ambao unahitaji PESA nyingi za kigeni, hukopa pesa za kigeni ili ziwepo kwenye hazina kuu. Image
Wakati waziri mkuu MAHINDA alikuwa rais alianzishaga miradi mingi ya miundombinu ambayo iliishia kufeli so hela zilizotumika hazijawahi kurudi kwenye mzunguko.Mbali na hilo rushwa ilikuwa nyingi serikalini.Alijenga majengo makubwa kwa nia ya uwekezaji na biashara lakini Image
hawakupata walichotarajia,akajenga kiwanja cha cricket ,akatanua bandari na kote alipowekeza return ilikuwa ndogo,ana skendo ya kupoteza zaidi ya BILIO 87 za kitanzania kwenye ujenzi wa barabara na hazikuonekana zimepitia chocho gani. Image
Hiyo skendo ilikuja kuwekwa wazi baadaye kwamba alikua ameandaa hadi majeshi kufanya mapinduzi,jamaa anapenda madaraka kuliko kula, alipomaliza urais akagombea ubunge wa eneo linaitwa KURUNEGALA na akarudi bungeni kama mbunge. Ni rais wa kwanza kufanya hivyo. Image
Hopefully umepata mwanga, hii kama intro tu #PichaLINAENDELEA madudu mengi sana kutoka kwenye hii familia.

Usikose kutuskiliza kila jumamosi kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 10 jioni kupitia @earadiofm

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Madinidotcom

Madinidotcom Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @madinidotcom

Dec 22, 2022
MAFUTA YANATOKA-GA WAPI?🤔
#PICHALINAANZA...
Mpaka sasa jibu la kisayansi juu ya chanzo cha uwepo wa mafuta, hata mimi sipendagi sana kumuaminisha mtu😅,Tho nitakuelewesha wanasega nini ,ukiona haikuingii basi tuishie kukubali tu MUNGU FUNDI.Lakini wanasema...
ni matokeo ya mgandamizo(presha) wa mimea,viumbe waliowahi kuishi duniani na mazagazaga kibao yaliyovunda-ga ardhini ambapo vilitengeneza hewa ya HYDROCARBON.
Hii HAIDRO-KABONI wala isikuogopeshe,hili jina ni kitu kinachotokeaga pale...
Kemikali za asili wanaita Organic chemical yaani unajua kuna zile kemikali za maabara za mikonoYaWatu na hizi za Asili zinaweza kujiumba zenyewe tu labda umetupa takataka na vyakula sehemu moja,then zinajimix zikivunda huenda kuna chemical zinajitengeneza.
Read 25 tweets
Aug 25, 2022
SAKATA LA MAUAJI YA RAIS WA CONGO.
🧵🔥

#PichaLinaanza Hili ni picha kuhusu tukio la kuuawa kwa rais wa Congo Laurent-Désiré Kabila,ni kama movie la kutisha lakini BASED ON TRU EVENT. Mwamba ambaye ni Stelingi wetu anaitwa RASHIDI MIZELE,baadaye mastelingi watabadilika. Image
hii ndio story,ambayo tulikugusia episode zilizopita za rais aliyeingia mkataba maarufu wa kuigawa Congo MKABA WA LEMERA.HADI leo Congo juzi kati imekubaliwa kuwa sehemu ya africa mashariki,ni nchi yenye historia nyeusi.Licha ya kwamba imebarikiwa madini... Image
ANZIA HAPA......agiza popcorn kabisa

Acha turewind mkanda ,Lets go back hadi siku ya TUKIO lenyewe la mwamba aliyempiga risasi kadhaa Rais wa nchini na akatoka zake mbio akitarajia kutoroka.Huyu ndo mwenye siri hii nzito ya KWANINI alimuua rais wa Congo Laurent-Désiré Kabila Image
Read 20 tweets
Aug 23, 2022
SAKATA LA BILIONEA JEFF BEZOS NA KING SALMAN WA SAUDIA.

Did you know unaweza kuhack an Iphones? Unafahamu ndicho chanzo cha tajiri namb 1 duniani Jeff Bezos kuachwa na mkewe?unafahamu aliyefanya hilo tukio ni King Salman kiongozi wa Saudi Arabia? #PICHALINAANZA Image
Kuna imani kwamba iphones zina strong security ni ngumu kuichezea,yes inawezekena bhanaa lakini kudakwa ni njenje.Sasa hacking inahitaji vitu flani ambavyo sometimes ni teknolojia ghali au lazima uwe na connections kali .
Juzi kati ikatangazwa BREKING NYIUZ Image
WhatsApp imeishtaki kampuni flani inayodevelp computer programs kutoka Israel. Sababu inashtumiwa kumpa Paul Kagame wa Rwanda program ya computer iliyowezesha kudukua "WhatsApp conversation” za wapinzani wa serikali ya Rwanda wanaoishi uhamishoni wanaojiita 'wanaharakati' Image
Read 37 tweets
Jul 13, 2022
MAUAJI YA Mohsen Fakhrizadeh KAMA MOVIE.

Uzi 🧵

Kuiadhibu Iran kama taifa kwa adhabu za vikwazo vya kiuchumi hakujaweza
kuzuia hatari inayosemwa na mataifa makubwa, na 'NEXT' mbinu ni kudeal namtu mmoja kwasababu kuivamia kijeshi pia ni jambo linalowezekana lakini... Image
unahitaji kujipanga sawa sawa kama asemavyo Rose mhando.Kuna mauaji ya wanasayansi wa nyuklia yameshafanyika lakini huyu aliyeuawa Mohsen Fakhrizadeh,tunasema wahuni wamegonga ikulu. Iran sio mgeni wa hiki kinachowakuta kwasababu kilianzia IRAQ Image
aliyekuwa rais wa marekani George W bush sababu KUU aliyotoa ya kuanzisha vita na Iraq 2003, alisema Iraq ilikua inarutubisha na kununua kiwango kikubwa cha Uranium inayochimbwa Africa.Haya madini tuseme ni kama ndizi ambazo unaweza kuMIX ndizi moja na maziwa ukasaga kwenye Image
Read 25 tweets
Jul 11, 2022
Nni kinaendelea SRILANKA? Sehemu 2

Uzi🧵🙌

#PichaLINAENDELEA anzia post ya jana.

Ankali GOTABAYA alipoingia madarakani 2019 aliahidi kodi za kibwege atazifutilia mbali,wananchi wakaona “eheee,huyu ndo mwaisa mtu mbadi wetu”km ujuavyo ujuavyo kila mtazamo hujengwa na historia Image
so shida ya wana SRI LANKA ilikuwa kuona nchi inarudi kusimama kwa miguu yake,mambo ya wewe ni nduguyakeNani wala hawajali sana. Alipoingia ankali GOTABAYA alionekana ni mtu wa kusimamia maneno yake, akapitisha panga la kupunguza kodi kwa wananchi ,kampeni ambayo ilipunguza 25% Image
yaani robo ya pato la taifa ili wananchi wafurahi.Wakati anafanya hili ni wakati ambao alikuwa akijiandaa na uchaguzi mkuu.Watalamu wa kiuchumi hawakushauri hili lakini yeye alisema anataka biashara ndogondogo za wananchi wanyonge wa hali ya chini zichipue,so wasilipe kodi . Image
Read 25 tweets
Jun 23, 2022
UMESIKIA MENGI KUHUSU MGOGORO WA #RWANDA NA #DRC LAKINI PENGINE UNASHINDWA KUELEWA WTF IZ GOING ON?🧐🤭
Kuna njia mbili za kuelewa,ya kwanza ni usome Uzi ufuatao.
Pili usikose show'Jmosi hii eastafricaradio.com
History iliyorahisishwa na #SabulaMaarifa wa #MadiniDigital.
Iko hivi!! Kitambo hicho Rwanda iliwahi ku-operate chini ya mwamvuli wa KIFALME uliokuwa ukiongozwa na mwamba wa kuitwa KIGELI IV RWABUGIRI.
Rwabugiri alikuwa ni jamaa fulani hivi kutokea Kabila la walio wachache (TUTSI) kule Rwanda.
na aliingia kwenye vitabu vya kihistoria kama kiongozi pekee wa taifa hilo aliyeamua kufanya mashirikiano na Serikali za KIKOLONI. By the way kama tunavyojua kuwa RWANDA kuna Makabila makuu mawili, na la 3 ni nyongeza, kuna walio wengi ambao tunawatambua kama Wa-HUTU
Read 23 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(