KILA SIKU UNAJIULIZA MBONA NDUGU HAWANITEMEBELEI KAMA zamani😟
Umeenda semina Dodoma, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Chamwino shukia St.Gaspar……
Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!"……
Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.
Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Baada ya muda mke wa mdogo wako anakuja kupiga magoti……
kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani, anakuja kukunawisha mikono huku akisema "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo.." Unakula unashiba.

Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry na Irene…..
Ukija tena uje nao" Unaondoka kwa heshima zote.

Siku ya siku nduguyo naye kapata kitrip cha Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu Mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye……
Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha Mbezi, lina waya za umeme juu".

Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti" Housegirl anaenda kufungua……..
Ndugu yako anaingia sebleni anawakuta. Anawasalimu unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia yake.

Wanao wanacheza game kwenye computer hata hawajashituka kuna mtu kaingia
Unawaambia, nyie msalimieni baba yenu mdogo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!

Mnazungumza kigogo, unamuuliza habari ya Dodoma. Kabla hajakujibu unashika simu unaanza kuchat, mke wako naye anachat! Sitting room imejaa watu,
lakini kila mtu kama hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula.
Kwa kua upo busy na simu
Hujali na huku njaa mgeni inamtafuna, Baada ya siku mbili anaaga unamuitia dreva wako wa toyo eeh! Haloo kuna mtu hapa njoo umkimbize Magufuli stand anafika anamchukua anaondoka zake
Anafika kwake anakujuza amefika salama then kimya week, mwezi miaka unaanza kutafuta mchawi eti kwanini ndugu zangu hawaji kwako kwakua ndio malezi ya familia yako hadi marafiki zako unawafanyia hivyo hivyo wakija kwako hata haujali…
Katika Duniaa ya sayansi na teknolojia tambua kwamba heshima inatafutwa, lakini katika kutafuta heshima kuna watu hawatakuheshimu vilevile, hata uwe mwema kiasi gani katika jamii yako lazima kuna watu hawatakutambua wala kuyaona mema yako,
unaweza ukawajali na kutoa misaada kiasi gani kuna watu hawatatambua misaada yako, kuishi na watu ni kazi ngumu kuliko kazi zote hapa duniani, na ukianza kudili na watu na kutaka watu wakuelewe au watambue msaada awu mchango unaotoa katika jamii yako lazima utagombana nao,
hakika naaamini umenielewa embu chukua na hii hapa, kuna watu watapenda jinsi ulivyo lakini hawatapenda vitu unavyovifanya, kuna watu watakpenda wewe Kama wewe lakini hawatapenda kazi yako, hawatampenda mke wako hawatapenda mafanikio yako😒
Ishi na watu wote kwa makini na kwa wema wakumpendeza Mungu @DrBadiBoy tunawatakieni jioni njema …. Group la #Telegram liko tayari kwa mafundisho muda sio mrefu Tutashare link hapa lakini pia msisahau kutembelea na kupakua APP YA @Clubzila_ KUNAKO Mkala zangu bora kasome🙏

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Dr. Badi 👴🏽

Dr. Badi 👴🏽 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @DrBadiBoy

Jul 26
Wengi itakuwa bado miaka miwili, mitatu au minne kabla ya kutimiza miaka 30. Natambua kuwa kuna waliokwisha fikisha na kuna uwezekano kuna walio nyuma kidogo.
Kama katika umri ulionao sasa kuna mtu anakuambia wewe bado ni mdogo/, basi huyo mtu hakupendi na anakulemaza kiakili…
Kua! Acha utoto! Mambo yafuatayo kwa vigezo vya kibinadamu mwenye akili timamu, mtu mwerevu lazima uwe ushayatimiza.

1) Kuweka misingi ya kifamilia:
Katika umri huo unatakiwa uwe umeoa, umechumbia au uko katika uhusiano wenye kueleweka unaelekea kwenye kujenga familia…..
Kama katika umri huu bado unabadilisha wanawake na kudandia vicheche, basi sahau kuwa na familia imara. Mambo yafuatayo yatakuwa yanakunyemelea;
– Kuoa/kuolewa msichana/mvulana mdogo sana ambaye atakuona unamzeesha
– Kuoa /kuolewa chapchap bila kuwaza….
Read 9 tweets
Jul 24
Wale waliokuwa wakimzuia Daudi asiende kupigana na Goliath na kudharau uwezo wake ndio waliokuwa wa kwanza kumshangilia na kusema kuwa ni ndugu yao baada ya yeye kumpiga Goliath.
Wale waliokuwa wa kwanza kumzuia Bathromayo yule kipofu na kumkemea asiende kwa Yesu kwaajili ya Uponyaji wake ndio waliokuwa wa kwanza kumtia moyo kwa kusema INUKA JIPE MOYO ANAKUITA
(Marko 10:49)
Wale waliokuwa wa kwanza kuyakataa na kuyapinga maono ya Yusufu na kuamua kumuuza akawe mtumwa ndio waliokuwa wa kwanza kwenda Misri kumpigia magoti wakihitaji msaada kutoka kwake wa chakula.
Read 5 tweets
Jul 17
Unachoenda kukisoma hapa muda si mrefu kinaweza kubadilisha maisha yako milele.
Mwombe Mungu akupe akili ya kuelewa usomapo. ……#Thread
So nimekuwa nikifanya utafiti wa safari za kibiashara za makampuni makubwa duniani. Nimejifunza mengi sana. Nakutana na vijana wengi wanataka kujenga biashara ziwe kubwa na ninapojaribu kuwashauri kuwa wanahitaji kujifunza mambo kwa kina na kuwa tayari kupambana
Kwa miaka mingi wengi wanaona kama hujui unachosema. Kama unakusudia kujenga biashara kubwa pia jifunze vitu upate UKWELI wa mambo. Vitabu kama OUTLIERS kitakusaidia kujua vitu muhimu katika hilo.

Bila shaka ni watu wachache sana wanaofahamu kuwa kampuni kama SAMSUNG
Read 20 tweets
Jun 27
Nimekuwa nikikutana na vijana mbali mbali everyday kuongea nao kuhusu biashara na ujasiriamali Vijana wengi wanadhani mafanikio ni kama kutuma 'SMS'. Kwamba unatype tu kidogo kisha unabonyeza SEND afu tayari. Ndo maana wamekuwa WALEVI WA BETTING.😂 Image
Ukweli ni kwamba mafanikio hasa katika biashara na ujasiriamali yanahitaji kupata MAARIFA sahihi ya kitu unachotaka kufanya. Kujiamini ni kuzuri lakini kudhani kuwa kujiamini kwako ndo kutaleta mpenyo kibiashara bila kuwa na maarifa sahihi ni kujitengenezea kachumbari ya disaster
! Biblia inasema Watu #wanaangamizwa kwa kukosa MAARIFA! Umeona ee?

So bila msaada sahihi UTAANGAMIZWA KIBIASHARA. Utasingizia biashara yako imerogwa na shangazi au na mpemba au shetani ameiinukia kumbe shetani yuko zake Brazil huko ni wewe tu huna maarifa sahihi.
Read 17 tweets
Jun 26
Sisi watu weusi ni wavivu kwenye KUTAFITI vitu. Hivyo mtu mweusi amebaki na GENERAL KNOWLEDGE tu ya mambo yote muhimu. Mfano kuhusu uchumi, michezo, utawala, uongozi, biashara na uwekezaji, afya, hata mambo ya imani, mtu mweusi amebaki na GENERAL KNOWLEDGE tu.
Ufahamu wa jumla jumla tu. Hajui vitu in deep sababu hataki kujisumbua na kufanya utafiti. Mara nyingi general knowledge ina mchango mdogo sana kwenye mafanikio yako na wakati mwingine ina-mislead. Inapotosha.

Jiulize hivi mambo unayoyajua kuhusu maisha nani hayajui,
mfano eti kuna kupanda na kushuka. Nani hajui? Lakini hiyo knowledge imekutofautishaje na watu wengine.

But jiulize ni kitu gani HUJUI kuhusu maisha. Hicho ndo muhimu zaidi. Mambo yaliyo wazi sana kuhusu maisha yana mchango mdogo mno kwako.
Read 24 tweets
Jun 24
UNA NIDHAMU SAHIHI YA KAZI?
Ukisikiliza mtu anayetaka kuanza biashara huwa hawazi sana kuhusu kazi anawaza tu ATAFANYA hivi atafanya na hivi halafu wateja watakuja halafu atanunua gari halafu ataenda Ulaya😂.
Bila kujua utahisi wewe ni jembe kweli kweli kumbe una DELUSION. (Kama hujui maana ya hili neno Google tu utaelewa vizuri zaidi. Please do.) Yes watu wengi huanza na DELUSION. Mwisho kifo cha mende! Jichunguze kisha uone nini huwezi ili uajiri watu wanaokiweza uwalipe
UNA NIDHAMU SAHIHI YA MATUMIZI YA FEDHA?
Katika vitabu ambavyo natamani ningesoma enzi zile tunasoma THE RIVER BETWEEN basi ni RICH DAD POOR DAD! Nimekisoma baada ya kumaliza chuo na kuajiriwa. Yani wakati nimeshajenga nidhamu mbaya kabisa ya matumizi ya fedha.
Read 8 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(