UTT-Amis ni nini? kampuni binafsi au ya Umma? Naanzaje kuwekeza kupitia kwa UTT? kuna usalama kiasi gani ndani ya UTT? Haya ni baadhi ya maswali unayoenda kupata majibu ndani ya #UZI huu. Soma uzi huu hadi na mwisho uwe miongoni mwa 6% ya watanzania wanaoijua UTT
SHUKA NAO🧵👇
UTT-Amis ni kampuni inayohusika na uanzishaji na uendeshaji wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja (CIS) yaan Collective Investment Schem. UTT AMIS kwa lugha ya malkia Unit Trust of Tanzania (UTT)- Asset Management and Investors Service (AMIS). Taasisi hii ipo chini ya wizara ya fedha
UTT inatoa huduma ya usimamiz wa mitaji binafsi, inatekeleza majukumu yake kulingana na sheria ya masoko ya mitaji na dhamana ya mwaka 1994 na marekebisho yake, pamoja na kanuni za mifuko ya uwekezaji wa pamoja ya mwaka 1997. Kwa sasa UTT inasimamia jumla ya Mifuko 6 ya uwekezaji
Mifuko iliyo chini ya UTT ni Umoja Fund,Wekeza maisha, Watoto Fund, Jikimu Fund, Liquid Fund na Bond Fund. Mifuko hii ina malengo,masharti na vigezo mbali mbali kukidhi matakwa yako mwekezaji. Hakuna mfuko bora wala mbaya zaidi ya mwingine sababu kila mfuko upo kwa lengo tofauti
NIPANUE🫡 kidogo hapa kwenye mifuko, Tunajua kwamba kila mwekezaji anayo malengo ya uwekezaji wake. Wapo wanaozichanga ili wapate mitaji,mahari,kujenga,watoto,kustaafu nk. Hii ndo sababu kuna mfuko zaidi ya mmoja. Ikiwa unajikusanya upate mtaji upo mfuko unaokidhi hitaji lako.
kama wewe ni mzazi na unajichanga mwanao akasomee urubani👩✈️upo mfuko sahihi kwa kazi hiyo. Ikiwa wew ni mstaafu na hutaki presha za kumiliki 🚐 uzeeni basi upo mfuko sahihi kwako ambao utakupa faida kila mwezi na bila stress yeyote. Ewe mstaafu epuka Presha, Wekeza UTT.💪🤑
Kama kuna mambo rahisi duniani bas ni utaratibu wa kujiunga na UTT, unatakiwa kufika Ofisi za UTT zilizo karibu nawe ili kukamilisha kujaza fom ya maomb ya kujiunga na mfuko ulochagua. Ni vizur kufika ofsini ujue ni wapi unawekeza pesa zako. Ofisi zipo Dar,Arusha, Mwanza na Mbeya
Ukija Ofisini hakikisha una kitambulisho kimojawapo kati ya Leseni ya udereva (sio ya duka)😌Kura, Nida au pasi ya kusafiria.Hakikisha unamjua mrith wako ikitokea wamekuloga ukafa mapema kuwe na mrith wa uwekezaji wako. Watahitaji majina,# ya sim na DOB. Epuka kumjaza mchepuko😁
Taratibu zikikamilika unanza kuwekeza papo hapo. Kima cha chini kwa uwekezaji wa kwanza kinatofautiana kutoka mfuko mmoja na mwingine. Mojawapo ya njia unazoweza kuzitumia kununua vipande ni Bank,dalali wa hisa (DSE), Mobile money zote Voda,Tigo,Airtel,Halotel,TTCL na EZYPESA
UTT hawakuishia hapo, wametuletea mfumo utakaotuwezesha kufurahia huduma za uwekezaji kwa kutumia simu. Siminvest inakupa taarifa mbali mbali za uwekezaji wako kama vile, Thamani ya vipande,Kununua vipande, Kufungua account mpya, Taarifa fupi na kuangalia uwekezaji wako.
Pia UTT wamekutengenezea APP ambayo unaweza kupata huduma zote tajwa hapo juu na nyongeza ya kuona salio na uwekezaji wako unavyoongezeka kila siku. App inapatikana App store na sisi wa Play Store hatujaachwa nyuma. Ipo simu ya bure ukitulia sehem umeboeka jipe ubize
Emb wapigie waulize maswali watakusaidia. Jiamini, hata kama huna kitu leo kesho utapata.MANDONGA kafosi mpaka tumemuelewa leo yeye anatajwa kuliko ata Samatta. Kumbuka ile room kila mtu anakwambia haustahili kuwa hapo ndo sehem sahihi kwako. 0754800455
RT & Share na wengine wapate jambo jipya mwaka ukiwa bado mchanga. Zikifika RT 10 tu ntakuandalieni uzi wa kuelezea kila mfuko masharti na malengo ya kila mfuko na ROI ya kila mfuko kwa mwaka 2022. Note: Sifanyi kazi UTT, mim n mwekezaji tu kama wewe.
Nimepokea maswali mengi kwenye DM na comment kuhusu jinsi ya kuanza safari hii
⚡ Katika thread hii, nitakuelekeza hatua kwa hatua jinsi ya kuanza leo!
⏳ Dakika 2 zijazo zitakua za thamani sana kwako
👇 Karibu kwenye safari ya uwekezaji! 👇
1/ Elimu ya Msingi
Kuwekeza katika hisa kunamaanisha kununua sehemu ya umiliki wa kampuni kwa matumain ya ukuaji wa thaman na kupata sehemu ya faida kupitia gawio
Hili linaambatana na hatari/risk,ni muhimu kujielimisha kujua basics za uwekezaji na hatari kabla ya kuanza kuwekeza
2/ Weka Malengo Bayana
Jiulize, unataka kuwekeza kwa ajili ya nini?
Kustaafu, kununua nyumba, au kulipia elimu?
Malengo yako yataamua mpango mkakati wako, kiwango cha risk unachoweza kuchukua, na muda wa uwekezaji wako
Kumbuka mwenye umri mdogo anamuda mrefu zaid wa kuwekeza