Mwezi Machi 2023, zilisikika tetesi kuwa timu ya wataalam huru na wachambuzi toka fitch wa masuala ya ufafanuzi kwenye uwezo wa nchi hizi wa soko la kifedha na kukopa, kukopesheka kwa nchi yetu.
Lakini Tarehe 9 june 2023 Basi taarifa rasmi ya fitch inayoipa tanzania B+ imetoka.
JOPO HILI LA WATAALAMU LILIJUMUISHA AKINA NANI HASA.
Timu ya wataalamu zaidi ya 100 waliokuja nchini na ambao hawakuja ndio waliokuja na huu utafiti wakiongozwa na Bw. Garreau, Thomas ( Associate director EMEI sovereign ratings) , Dr. Friedrich Jan. ( Assistant prof EACP biz sc)
Lakini pia Bw. Iles Toby (Head of middle east and Africa. Fitch ratings) kwa pamoja na washiriki wengine basi ndio wamekuja na utafiti ulioipa tanzania B+ yenye mtazamo imara (stable outlook)
JE NCHI GANI NYINGINE ZIMEPIGA HATUA KAMA HII.
Hii ikiwa ni hatua kubwa sana kwa Taifa letu na baadhi ya nchi ambazo zimewahi au zimefikia hadhi hii (ratings) ni kama vile: Kenya ambao kwa sasa walishuka na wanasoma negative na nchi nyingine ni kama zinavoonekana 👇🏿
FITCH RATINGS NI NINI HASA.
Hii ni taasisi ya wataalamu inayokadiria viwango vya Nchi fulani kwenye soko la kifedha kwa kutazama mawazo endelevu (Foward looking opinions) na uhusiano wake na uwezo wa nchi hizi kufikia malengo yake ya kifedha (financial commitment)
Hawa Fitch ratings hutumia kitu kinaitwa Issuer default ratings (IDRs). Ambapo hutazama zaidi Mashirika, Taasisis huru za kifedha lakini pia taasisi fedha kama vile Benki na wadau wa masuala yote ya kifedha nchini. Sasa kupitia hii ndipo wameweza kuirate Tanzania kuwa na IDR B+
WAMETAZAMA VITU GANI HASA.
Ili kutoa hii B+ kwa Tanzania hawajakisia tu bali wametazama mambo kadhaa.
1. CREDIT FUNDAMENTAL(Misingi ya mikopo)
B+ rating inaashiria kuwa Tanzania kuna maendeleo imara ya uchumi (strong microeconomics performance) hasa kwenye real GDP.
2. UKUAJI WA UCHUMI CHANYA.
(Strong growth)
Kwa mujibu wa fitch wanategemea uchumi wa Tanzania kukua kutoka 5.2% 2023 hadi 6.0 mwaka 2024 toka 4.7 ya mwaka 2022. Hii inaashiria uchumi wa nchi unapanda (postively) Kutokana na kukua kwa sekta za utalii, madini na miundombinu
3.LOW INFLATION (Mfumko finyu wa bei.)
Kwa mujibu wa wataalam hawa wanasema licha ya kuwepo kwa sera dhaifu lakini bado mfumko wa bei nchini upo chini ya wastani mbaya wa 5% Ambapo sasa ni 4.6% na inakadiriwa kuwa 4.0% mwaka 2024 huku mwaka 2022 ilikuwa 4.2%
4. IMPROVING FINANCIAL MANAGEMENT. (Udhibiti wa fedha unaoendelea)
Kwa mujibu wa wataalam hawa wa fitch wanasema licha ya kuwepo udhaifu mkubwa uliopo sasa nchini juu ya udhibiti wa fedha lakini serikali inaonesha nia ya dhati ya kudhibiti fedha za ndani na zile zinazoingia.
5. LOW BUT RISING REVENUE.
Wataalamu hawa wanasema Tanzania licha ya kuwa na mapato kidogo lakini yanaongezeka na kuboreshwa kila siku. Kwamba uwezo wa kukunya na kusamehe kodi kwenye sekta muhimu unaongezeka na kuboreshwa. Pia utegemezi unapungua na inategemea kupungua zaidi.
Hii inamaanisha sasa Tanzania inatambulika kama nchi ambayo inaendelea vema katika masuala ya soko la kifedha (Financial market) na uwezo wake wa kukopesheka unakua na ina maendeleo endelevu chanya kila uchao.
Licha ya changamoto za kiuchumi za kidunia zinazotokana na mtikisiko uliosababishwa na covid lakini pia UKRAINE- RUSSIAN Conflicts bado taifa letu linangaa. Hapa akina Dkt Mwigulu Nchemba PhD na wenzao Wanaupiga mwingi sana.
ANGALIZO.
Kuna vitu ambavyo vinaweza kuendelea kutupaisha kwenye hizi ratings na vile vinavyoweza kutushusha pia.
VITU VINAVYOWEZA KUTUSHUSHA.
1. Kama sera zetu za fedha na Maendeleo zitakuwa dhaifu. (Weakened trend of Macroeconomic Performance, Policies.)
Lakini pia 👇🏿
2. Mtikikisiko ya kifedha ya ndani na ya nje ikizidi na kuweza kudhuru uchumi wa ndani.
INGAWA.
Uwepo wa wataalamu ndani ya nchi kuanzia waziri @mwigulunchemba1 ambae ni daktari wa uchumi, katibu wa wizara Dkt Natu Mwamba PhD ambae pia ni daktari wa uchumi. magavana wa BOT pia
Hawa wote ni wataalamu hivyo sidhani kama wataweza ruhusu hii itokee na tunaimani bado nchi yetu itazidi kupaa zaidi na wataendeleza
VITU VINAVYOWEZA KUTUPAISHA ZAIDI.
1. Public finance imrovement:
Kuongezeka kwa mapato ya ndani na uthubutu katika kufanya miradi ya maendeleo
Hii itapunguza Utegemezi na itaongeza maendeleo ya sekta zalishi nchini.
2. Uwazi katika soko la nje la fedha. (Greater transparency and confidence in the exchange-rate regime and foreign exchange interventions sustainability) hii itasaidia kuweza kupata mikopo lakini pia FDI
3.Kuwa na sera imara za kiuchumi kwa maendeleo endelevu ( Macroeconomic Performance, Policies and Prospect)
Wataalam wamesema kuna improvement kwenye sera na maendeleo ya uchumi hivyo tukiweza kumantain ama kujitahidi zaidi basi tutasonga mbele zaidi.
IMEHUSISHWA PIA MOODYs
Kwa kawaida Fitch na Moody's huendana ingawa wakati Fitch imejikita kwenye IDRs Moody's yenyewe imejikita kweye Short term na long term categories Inayohusisha uwezo wa sekta binafsi na zile za umma katika kupokea mikopo na kuweza kuihimili.
Na ndio maana taarifa imekuja na Kwa kusema kuwa.
"Fitch has assigned Tanzania as a Long term Foreign Currecy Issuer default ratings ya B+" hii ina maana imehusisha pia Moody's rating.
Hii inatoa picha njema sana kwa nchi yetu na uchumi wake kote duniani.
KISHIRIKISHO.
Nimejitahidi kuandika kwa lugha nyepesi ili hata mtu ambae hana ujuzi na masuala ya fedha au uchumi (Economics and Finance)
Aweze kuelewa. Kwa upana Fitch and Moody's ratings hutazama vitu vingi sana na wao hawapindishi. Ukiambiwa umepanda basi umepanda kweli. 😂
MWISHO WA UZI.
Kwa wale wataalamu wa masuala ya kifedha na wachumi pia mnaruhusiwa kutoa mtazamo wenu chanya hapa chini kweye comments ili kuelewesha jamii juu ya mambo haya yenye kuipa taifa tija n.k.
Sitaki kunyanyuka nipige makofi peke yangu. Nimeamua kuwashirikisha wenzangu, Angalau ninyi mtaninyeshea pakavu pangu. Na hili litakaa sawia sawilia.
Tafadhari naomba urejee viambatanisho hapa chini 👇🏿viliyotolewa na Wizara ya fedha na mipango.
Kimoja cha mwaka 22 kingine 23
Kama umesoma vema kiambatanisho 👆🏿. Utaona kwenye mstari ulalo wa chini kabisa kuna kipengele kinachoelezea makadirio ya matumizi katika ofisi za mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali kiasi cha zaidi ya Bilioni 80.09 Tsh. (22/23) na kingine ni Bil 97.1 Tsh. (23/24)
Moja ya matatizo makubwa ya serikali kuendesha sekta fulani ni kutokuwepo kwa ufanisi. So mi lilitegemea na naunga mkono alichokizungumza jamaa.
Wakati Raisi analeta uhuru wa vyombo vya habari tulimpongeza. Kwa sababu lilikua ni suala la kujenga taifa bora
Sasa sahizi kwenye masuala haya ya sasa. Tunapoanza kuleta uzanzibari nk. Kidogo inafikirisha.
Kama ambavyo ipo mahala popote pale. Ili bandari yetu iwe na ufanisi na hata zile kero za wafanyabiashara zipungue basi njia pekee ni kuendeshwa na sekta binafsi na TPA wasimamie tu.
Nimekua nikisikia kuwa tunavutia wawekezaji toka nje. Na kila mtu alikua anapiga makofi. Ooh "Mama anafungua nchi na kuvutia wawekezaji." So mlitegemea wawekezaji gani.? 😂
Niwaambie kuna watu wanawajaza chuki wananchi hili suala lionekane sio na wao wanamaslahi yao mahala. 😂
Kati ya wizara ambazo zinapigwa mawe nchini basi wizara ya fedha inaongoza. Kwa sababu ndio wanasimamia sera za kodi, Wanakusanya mapato, Ndio wakopaji, Ndio walipa madeni, hivyo lawama dhidi yao haziepukiki.
Lakini. 👇🏿
Nilikua na hamu ya kusikia makadirio ya bajeti ya wizara hii kwa hamu ili nijiridhishe na hiki nachoenda kukizungumza na hatimae leo nimejiridhisha na kwa bahati nzuri nilikuepo mjengoni kabisa. 😂
Kwa ufupi sana baada ya kuwepo kwamjadala na mvutano mkubwa sana kati ya wale wanaosema bandari imeuzwa na wale wanaopigia chapuo faida za serikali kuingia makubaliano na State of Dubai ili kuendesha bandari ( Intercontinental agreement ) nimefanikiwa kupitia MOU hii 👇🏿
Hiyo kitaalamu inaitwa Memorandum of understanding na si mkataba kama inavyosemekana ingawa ndiyo unaojenga hoja za mkataba husika ambao kwa sheria zetu za nchi ili uingiwe ni lazima uhusishe Bunge na ndio Mchakato uliopo sasa na kuna Mchakato wa kutoa maoni pia.
Ulipoumbwa ulimwengu, Ikaumbwa Afrika, Ikaumbwa Tanzania ikapambwa ikapambika, ndani yake Iliumbwa Njombe. Moja ya mikoa nadhifu sana kuwahi kutokea. Je unataka kujua zaidi kuhusu mkoa huu basi shuka na uzi huu mpaka mwisho. 👇🏿