Je, una mpango wa kufungua famasi? Tafadhali fuatilia #uzi ufuatao kupata maelezo ya taratibu za kufuata pale utakapotaka kuanzisha biashara hii ya kifamasia.
Famasi ni eneo lililosajiliwa maalum kwa shughuli za kifamasia.Hurusiwa kutunza, kuchanganya, kuuza au kununua dawa kwa matumizi ya binadamu. Eneo hili huwa chini ya uangalizi wa mfamasia kwa mujibu wa sheria.
May 18, 2020 • 9 tweets • 3 min read
Wakati fulani ulipokwenda famasi kununua dawa, inawezekana ulipewa brand tofauti ya ile uliokua unahitaji. Swali ni je, dawa hizo ziko sawa na zinafanya kazi sawa? Fuatilia #Uzi kwa majibu na ushauri.
Kwa kuwa zoezi la kutengeneza dawa ni zoezi lefu linalotumia gharama nyingi kwenye utafiti, Kampuni mgunduzi( innovator ) hupewa "patent" yaani kuwa wauzaji pekee wa dawa husika ili kurudisha gharama zilizotumika wakati wa utafiti.
Apr 29, 2020 • 11 tweets • 3 min read
Hivi karibuni Madagascar walitangaza kupata dawa ya #COVID19 huku @WHO wakisema bado hakuna ushahidi kama dawa hiyo ni sahihi.#Uzi huu inaonesha hatua za kupitia hadi dawa kutangazwa inatibu ugonjwa fulani.
Dawa hadi inathibitishwa kutibu ugonjwa fulani wa binadamu ni zoefu lefu ambalo linaloweza kuchukua kadri ya miaka 7 hadi 12.