Unamjua #MGANGA_PAZI Wewee...😂🤣😂????
#UZI
Wakati ule wa enzi za usultani na ufalme, kulikuwa na nchi moja iliyoitwa Mkira.
Katika nchi hiyo, aliishi mtu mmoja aliyeitwa #Pazi. Mtu huyu alikuwa fukara sana lakini hakuridhika na hali hiyo.
Katika kufikiria mbinu itakayomfanya awe tajiri, aliamua ajifanye mgangd. Baada ya uamuzi huo, alipita kila sehemu akijitangaza.
Alitangaza kwehye masoko, mashamba, mdchungoni mpaka visiwani kuwa yeye ni mganga hodari, asiyeshindwa na lolote.
Wakati huo hakukuwa na hospitali wala madokta,shughuli zote za tiba zilifanywa na waganga.Ukunga ulifanywa na wakunga ambao siku hizi tunawaita waganga wa kienyeji
Habari za mtu aliyekuwa akijitangaza kuwa mganga hodari asiyeshindwa lolote, zilimfikia Mfalme wa nchi ya Mkira.
Kwa bahati mbaya, habari hizo zikamfikia Malkia mke wa Mfalme,wakati akiwa katika majonzi makuu. Kwa siku mbili zilizopita,alikuwa akiitafuta pete yake ya dhahabu
Pete hiyo alivishwa na mumewe siku ya harusi yao miaka kadhaa iliyopita. Alipokata tamaa, aliamua amweleze Mfalme.
Mfalme alimwamuru Pazi aitafute pete hiyo. Kama angeikosa angeuawa kwa kuwadanganya raia wema wa Mkira. Mfalme alimpa Pazi siku moja tu kuifanya kazi hiyo.
Maskini Pazi alipopewa amri hiyo, alipata homa ya ghafla. Alilala kitandani taabani akijua kuwa kifo chake kimewadia.
Akajilaumu kwa kujifanya mganga wakati hata dawa moja hakuijua.🤣Hata hivyo mkewe alimfarij
Jion mfalme alienda kwa Pazi akiwa na mkewe,..Wacha Pazi Ajae.🤣😂🤣cndo akajua nimesha Kufwaa mimii..ikabidii...
Waongozane kwenda jumba la kifalme alipo karibia jumba,Pazi siakaona kuku aki tembea kwa uchovu akajua huyu kesha karibia kufa.
Uchu uka mjaa Mganga Bana😂akaona bora nikafe huku nimetia kitu tumboni akaagiza yule kuku achinje apatiwe firigisi😅ana balaa nakwambia....
Kuku akachinjwa na kupasuliwa tumboni. Firigisi lilipopasuliwa ile pete ya dhahabu ya Malkia si ikadondoka chini bhana😂
Ilikuwa furaha kubwa nyumbani kwa Mfalme. Malkia alichangamka tena na kumpa Pazi zawadi nyingi mnoo..
Mfalme nae akatoa amri kuanzia sasa bwana Pazi Ndio Mganga Mkuu Wa familia yangu jamaa kala shavu Bana😅😅
Pazi alipewa Nyumba nzur karib na jumba la Kifalme akiwa na familia yake wakaanza enjoy life kiutan utani tuu...aisee let goo...
Katikati ya mwezi wa sita lilitokea tatizo. Ulitokea wizi mkubwa ambao ulikuwa haujawahi kutokea katika nchi ya Mkira.
Masanduku makubwa saba yakiwa na dhahabu na almasi za Mfalme yaliibiwa! Nchi nzima ilipatwa na mshangao na woga mkubwa. Nani huyo aliyediriki kumwibia Mfalme.?
Mfalme ali kasirika sanaa akaamuru ufanyike uchunguz wa maana,ila mkewe alikia aki muamin sana bwana Pazi🤓akamshaur Mfalme basii...
Mfalme alimuita Bwana Pazi Na Kumpa Siku 3 awe amepata wez wa masanduku yake oyaa muongo kapewa kazi sasaa...enheee ....
Kumbuka Jamaa Hana Uganga wowote ile pete ilikua bahati nasibu tuu sasaaa
Wengi walisema kuwa wezi wamepatikana maana Mganga Pazi alikuwa hashindwi kitu.
Wengine ambao hawakumwamini Pazi walidai sasa amepatikana maana asingeweza kuwapata wezi hao.
Huku watu waki muwaza Mganga Pazi yeye akiwa kwake viti havikaliki..maana alidanganya kua ni mgana ali muita mkewe...
Nakumuomba amuandalie maandaz 7 ili ale anapo kua safarini Pazi akiwaza kutoroka mji bhana wewe huku nako....
Wezi, kumbe walikuwa na wasiwasi kuhusu Pazi.😂😂 Walihofu kuwa Mganga yule hodari angewatambua na kuwasemea kwa Mfalme....Pazi ana Bahati Sana Uyu Boya ila hana Degree kama @kipepe123 (jokes)😁
Wez siunajua wana Tabia ya kusikilizia kama jee kweli tuta rogwaa..
Wakaona hapana ebu tuka chunguze nyumba kwa Mganga sasa hivi ana mpango gani,wakafika adi kwa mganga..,kumbuka Mke wa pazi nae wakati huo anaandaa maandaz ya mumewe akiwa safarini.
Akasogea mwiz mmoja kibarazani..akasikia mke wa paz asema "Bwana Pazi Lakwanza iloo"(Aipua andaz)
alimweleza mumewe ambaye alikuwa chumbani akifungasha nguo zake tayari kwa kutoroka.
“Haya mama, mimi nashughulikia huku!” Pazi alijibu kutokea chumbani.
Yule mwizi pale, dirishani alishikwa na woga mkuu. Alidhani Mganga huyu maarufu alishamgundua kuwa yupo pale nje.😂😂
Akatoka mbio kwa wenzake aka waeleza aliyo skia Mmoja wao akasema ww muoga sana boya ww😁ngoja niende mimii...
Jamaa akasogea kibarazan paaaap....maraa akaskiaa...(......)
Itaendeleaa...............
Kaa tayar kwa Sehem ya 2
#RETWEET
follow @iam_mobam
UNAMJUA MGANGA #PAZI WEWEE ...!?!😂😂
PART 2
Jamaa aka sogea kibarazan mara paaap akaskia Mume wangu la pili hilo.,..Pazi akajib tokea chumban ndio ndioo mke wangu mm naendelea kuweka mambo vizur uku.😂(anapanga nguo za kubeba safarini)
Mwiz akaona mbona kisangaa hiv tenaaa..
Akaenda wapanga wenzake aliyo skia bas walifanga ivo mpaka alipo fika mwiz wa saba Mama Mpishi akasema Bwana paz la saba ilo😂🤣jamaa wakajua awa wana tuona hawa.
Wakajadiliana ikabid waende kumuomba msamaha Mganga Pazi kwa kujua labda alikua ana waroga.😂
Mke wa pazi ali wakaribisha Wezi waliongea kwa huruma huku wana lia ,..na kumba msamaha
Pazi akaona apaa apaa sindo akaanza kua mkali sasaa🤣😂🤣pumbav munaiba mkajua sita wajua ninge wafanya vichaa mna bahati
Jamaa wakalia sanaa na kuomba Pazi asi wataje kwa Mfalme.
Wezi hao wakamwongoza mpaka kwenye bonde la mto. Huko ndiko walikokuwa wameficha hazina hiyo ya Mfalme.
Pazi alipaangalia vizuri na kuweka alama zake za siri. Baada ya hapo walirudi nyumbani. Pazi aliwaambia wamsubiri aende kwa Mfalme.
Alipo fika kwa mfalme kwa heshima kabsa aliongea na mfalme na kuhitaj vitu vi wili ili afanikishe mfalme akasema ucwe na shakaa ww sema wataka nini Pazii..
Jamaa akataja vile alivyo ombwa na wale wezi kwanza..Wasiuliwe lakin pilii wapate pesa kidogo awana ata ya kula.😂
Mfalme alikubali na kumfanyia Pazi kama alivo taka...Paz akasema Usik mzigo una tua apaa mm ndo kiboko ya weziii.😂😂
Aliporudi nyumbani, Pazi aliwagawia wale wezi fedha walizohitaji na kuwaamuru waondoke upesi.
Usiku Paz alikwenda kwa Mfalme na kuomba waende akaoneshe hazina ilipo...Pazi aliongoza msafara huku akishikashika shanga zake😂Boya ana mikwara nakwambia..🙌🏾😂
Baada ya muda, masanduku yote saba yakiwa na hazina yote ya Mfalme yalifukuliwa.
Ilikuwa shangwe na cherekochereko
Pazi akawa na Jinna kubwa Mjin apo.😅baada ga muda Mke wa mfalme alishaur wafanye sherehe ya ndoa yao ilio na miaka 10 hivi na mfalme.
Walialika wafalme wengine kuja shirik sherehe iyo watu wali ruka sana Majokaaa...eeeh banaa mguu juu singel sanaa tuu😂😂😂
Siku ya sherehe hii pazi aka kutana na Mtiti mwengine mfalme mmoja alikuja na kasha lime fungwa aliuliza mgangaa mnae msfi yuko wap aje aseme humu ndan kuna nini😅😅😅
Bwana pazi Mkojo wataka mtoka kwa woga na kuwaza kuumbuka leo aka kaza uku akisema umo ndan kuna PANZI
Yule mfalme aliruka ruka na kusema amepataa..mfalme mwengine ajaamin akasimama na kumuuliza tena Pazi Unasema kuna nn ndan ya kashaa..
Pazi akarudia kwa msisitizo yaani Kunaa Panzi..😅😅 mfalme aka fungua kasha paaap maraaa Panzi akaruka🤣🤣watu wali gonga cheaz za kutoshaa
Bwana Pazi alipoona mbona itakua msala hii alipo rudi nyumban aka mwambia mkewe ujue pale nusu nigundulike..!?
Sasaa hapa mke wangu hakuna kukaa tumesha pata pesa na jina tutafute pa kukimbilia hawa watakuja jua mm sio mganga wani ue😂Usiku haoo waka toroka zao
Oyaaa thanks much kua pamoja toka mwanzo wa li Uzi letu la Mganga Pazi😅👊🏽
Chuma ingjne itakuja jion kama ya Jana ile ila usije lia ukiwa una isoma😨
#RETWEET
#like
Follow @iam_mobam
Uweke Notification On tuu usiko Nyuzi zetu.✨🤳
@danitykuyi apaa tumeanza nao 🤳
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.