JAPHET MATARRA Profile picture
Father | Human Right Activist | Mineral Processing Engineer | Paralegal | Member @ChademaTz | @ManUtd | @YoungafricansSC | Boss Himself | StoryTeller | 430'2023

Sep 9, 2021, 211 tweets

MAPINDUZI YA GUINEA TZ🇹🇿 YA SAMIA INACHAKUJIFUNZA

#UZI

Ilianza kama utani Mzee Condé hakuamini kijana wake mwenyewe aliyemlea, mwenye masters ya vita na cheo akampatia alipomwambia "simama juu hlf ukae chini" Unadhani ilikuwa rahisi kumpindua? Naam It's #Guinea:1958-Present👇

Sikuweza kuandika Uzi yalipotokea mapinduzi ktk nchi nyingine mbalimbali, lkn kwa yaliyotokea jumapili nchini Guinea nimeona niandike ili Watanzania tuone km kuna lolote la kujifunza. Nitaangazia upande wa kisiasa tu. Nitachambua kila kitu kuanzia uhuru hadi kutokea mapinduzi.

Maswali nayotaka kukujibu km ulijiuliza ni haya:👇

💨Historia ya Guinea ikoje?

💨Kwnn mpk mapinduzi?

💨Col. Doumbouya ana nguvu gani

💨Kwann wananchi wamefurahia?

History repeats itself, 1st as Tragedy, second as Farce.
Just retweet 🔄 huenda siku
Uzi huu ukakukumbusha kitu

Mapinduzi dhidi serikali zilizo madarakani ktk miaka ya hivi karibuni yametokea mara kwa mara barani Afrika. Mengi yaliyofanikiwa yametokea nchini Burkina Faso, ambapo kati ya majaribio 07 ni moja lililoshindwa. Inayoongoza ni Sudan, ambapo 15 yalifanyika na 05 yalifanikiwa.

Utafiti uliofanywa na watafiti wawili kutoka nchini Marekani, Bw JONATHAN POWELL na CLAYTON THYNE, ulibainisha kuwa zaidi ya majaribio 200 yamefanyika Afrika kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1950 na ktk majaribio hayo nusu yalifanikiwa lkn hayakudumu kwa zaidi ya siku Saba.

Tangu 2015, kati ya mapinduzi 11 yaliyoripotiwa kote ulimwenguni, Nane yalifanyika Afrika na 03 yalitokea:Uturuki (2016), Myanmar (2021) na Afghanistan (2021). Kwa ujumla, Afrika imepata mapinduzi mengi kuliko bara lolote na inafuatwa na Amerika ambapo kati 95 ni 40 yalifanikiwa.

Lkn kwa miongo 2 iliyopita majaribio ya kupindua serikali yamepunguua sana Amerika ya Kusini. Mapinduzi ya mwisho yalikuwa Venezuela (2002) ambapo walitaka kumtoa madarakani HUGO CHAVEZ, lakini jaribio lilishindwa. Bara Asia pia limepungua majaribio ya mapinduzi ya kijeshi.

Barani ulaya mapinduzi ya kijeshi yamesahaulika kabisa ILA huku kwetu Afrika yamekuwa mambo yaliyozoeleka.

Chanzo cha mapinduzi mengi ni kutokana na kuyumba kwa serikali zilizo madarakani.Ukiangalia nchi zilizo nyingi zimekuwa na mazingira ya kufanana yanayosababisha mapinduzi.

Hali ya umaskini, ubadhirifu wa rasilimali za nchi, utawala wa kimabavu pamoja na ufisadi, uminywaji wa haki za kiraia hizo ni moja ya sababu zinazochangia kushuhudiwa mapinduzi mengi Afrika. Maandamano ya wananchi dhidi ya madikteta waliohudumu kwa muda mrefu yamechangia pia..

Miaka ya karibuni mapinduzi yaliyoshuhudiwa Afrika ni pamoja na mapinduzi ya nchini Zimbabwe kwa ROBERT MUGABE aliyetawala miaka 37, Sudan kwa OMAR BASHIR aliyetawala zaidi ya miaka 20 pamoja na nchi za Mali kwa BAH NDAW ijapo hakumaliza mwaka na hivi majuzi nchini Guinea.

Nchi ya Guinea ipo Magharibi mwa bara la Afrika na ina wakazi takribani milioni 13.5. Makao Makuu yake yapo Mji wa Conakry unaokadiriwa kuwa na wakazi milioni 02. Kabla kuwa Jamhuri inayojitawala ilijulikana km "French Guinea" kuanzia mwaka 1891 ilipokuwa koloni la Ufaransa.

Nchi hii inafahamika zaidi km GUINEA-CONAKRY kuitofautisha nchi nyingine zinazotumia jina la "Guinea" mfn Papua New Guinea, Guinea-Bissau na Equatorial Guinea. Asili ya Guinea ni neno la kireno 𝐆𝐮𝐢𝐧𝐞`=watu weusi waoishio kusini mwa mto Zenega (Senegal) milima FOUTA JALLON.

Mnamo 28/09/1958 ilishiriki kura ya maoni ktk mabadiliko ya katiba ya Ufaransa. Mabadiliko ambayo yalipelekea kupata uhuru wake mnamo Oktoba 2, 1958 na kijana AHMED SÉKOU TOURÉ kutoka kabila la Malinke au Mandika akateuliwa na Bunge Maalum la Katiba kuwa kiongozi wa nchi hiyo.

SÉKOU TOURÉ NI NANI?

Bila shaka ukiwa umetokea kanda ya Ziwa especially Mwanza jina 𝐒𝐄́𝐊𝐎𝐔 𝐓𝐎𝐔𝐑𝐄́ ambayo ni Hospitali Rufaa ya mkoa Mwanza haliwezi kuwa geni masikioni mwako.Jina hilo limetokana na aliyekuwa Rais wa kwanza mwafrika wa nchi ya Guinea AHMED SÉKOU TOURÉ.

SÉKOU TOURÉ ni mjukuu wa ALMAMY SAMORE LAFIYA TOURÉ, mwanzilishi na Mfalme wa "Wassoulou Empire", milki ya Kiislam iliyokuwa Pwani ya Afrika Magharibi.Mfalme TOURÉ ndiye aliyepigana na Wafaransa baada ya kuvamiwa kabla ya kukamatwa mnamo 1898 na kufungwa uhamishoni nchini Gaboni.

Historia ya SÉKOU TOURÉ kuwa kiongozi wa Guinea inaanzia akiwa na miaka 15 mnamo 1937, alipofukuzwa chuo cha GEORGES POIRET alichojiunga kusomea ufundi. Alifukuzwa kwa7bu aliongoza maandamano ya wanafunzi kudai kupatiwa chakula, akawa maarufu na kujiunga na vyama vya wafanyakazi.

Kufukuzwa kwake kulichukua sura mpya ya kisiasa nchini na wengi walimuona shujaa.Baadae aliruhusiwa kufanya mtihani wa mwisho.Mwaka 1940 alipata kibarua kampuni ya Compagnie du Niger Français. Alipohitimu mwaka 1941 aliajiriwa kama karani Postes, télégraphes et téléphones (PTT).

SÉKOU TOURÉ alianza kujihusisha na siasa kwa mara kwanza wkt alipokuwa akifanya kazi PTT. Mnamo 1945, alianzisha Chama cha Wafanyakazi cha Post and Telecommunications Workers' Union (SPTT), na kilikuwa chama cha kwanza cha wafanyakazi kwenye makoloni yote ya Ufaransa.

Mnamo 1946 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi (SPTT) na mwaka huo huo Muungano umoja wa vyama vya kidemokrasia uliofahamika kama Afrika Rassemblement Démocratique Africain (RDA) ulianzishwa na FÉLIX HOUPHOUËT-BOIGNY aliyekuwa Rais wa kwanza wa Ivory Coast

Mkutano wa kwanza wa RDA ulifanyika mnamo Oktoba 18, 1946 Mjini Bamako nchini Mali, ambapo viongozi kutoka Ivory Coast, Equatorial Guinea, Benin , Congo Brazzaville pamoja na Sudan walihudhuria. SÉKOU TOURÉ alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa RDA waliohudhuria.

Mnamo 1947, alianzisha chama cha Parti démocratique de Guinée (PDG) tawi la RDA kikaungwa mkono sana na 1952 akachaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa PDG. Umaarufu wake ulipelekea akachaguliwa Katibu Mkuu wa Territorial Union of the Confédération Générale du Travail (CGT)

Miaka 2 baadae aliteuliwa kuwa Mkuu wa CGT ukanda wa Africa Magharibi. Mafanikio yake makubwa yalikuja 1953, baada ya kuanzisha mgomo kushinikiza serikali ya kikoloni kutoa haki kwa wafanyakazi, ambapo wafanyikazi kote nchini waligoma kufanya kazi kwa kipindi cha muda wa siku 71.

Ulikuwa mgomo wa muda mrefu na mwaka huo huo alichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Guinea.

SÉKOU TOURÉ alipata nguvu na vijana walimuunga mkono ikapelekea 1954, akachaguliwa km mmoja wa makatibu wakuu 03 chama cha Kikomunisti cha Kifaransa cha Confédération Générale du Travail.

Mnamo 1956 alichaguliwa kuwa Meya wa Conakry nafasi iliyomfanya kuchaguliwa kuwa Naibu Spika ktk Bunge nchi hiyo.

Mnamo 1957 ulifanyika Uchaguzi Mkuu na chama chake cha Parti Démocratique de Guinée (PDG) kilishinda uchaguzi kwa kupata viti 56 kati ya 60 Bungeni.

Alitumia nafasi hiyo kukosoa vikali utawala wa Ufaransa na nchi nyingi za nje zilimpatia support kubwa na mnamo Oktoba 02, 1958 Guinea ilijitangazia Uhuru kutoka kwa Mfaransa.

Miongoni mwa nchi zilizompa support baada Uhuru ni Ghana, nchi za kiarabu na za kijamaa ikiwemo China. Marekani pia ilitambua uongozi wa SÉKOU TOURÉ Novemba 01, mwaka 1958. Mwaka huo mnamo Novemba 12 Bunge la Katiba lilipitisha Katiba ya nchi hiyo ambayo inatumika hadi Leo hii.

Mwezi mmoja baadae yaani Desemba 12, 1958 Jamhuri ya Guinea ilijiunga na Umoja wa Mataifa ikiwa nchi ya 82 kujiunga Jumuiya hiyo na Ufaransa ilitangaza rasmi kuondoa majeshi yake Guinea Trh 16/01/1959 kwa kuitambua nchi hiyo kuwa Taifa huru na linalijiongoza kikatiba.

Baada ya Uhuru Umoja wa Kisovieti (USSR) ziliamua kuisupport kiuchumi kwa kuipatia mkopo wa
US$ 35M mnamo Agosti 26, 1959. Czechoslovakia iliyokuwa moja ya nchi za Umoja wa Kisovieti pia ilitoa msaada wa ulinzi kwa kuipatia magari (vifaru) 03 ya kivita, silaha pamoja na mabomu.

Czechoslovakia ilitoa wakufunzi wa kijeshi 25 pamoja na washauri wa masuala ya ulinzi na usalama na kuwapeleka Guinea kwa ajili ya kutoa mafunzo ktk nchi hiyo iliyokuwa changa. Ujerumani Magharibi nayo ni miongoni mwa nchi zilizotoa misaada ya kiuchumi na kijeshi kuanzia 1959

Nchi jirani zilikuwa hazijapata Uhuru. Mwaka 1960 alimkaribisha AMÍLCAR CABRAL kiongozi wa chama cha PAIGC kilichopambania Uhuru wa Guinea-Bissau na Cape Verde kutoka kwa Wareno. PAIGC iliweka kambi Conakry mnamo 1963 na vita dhidi ya Wareno
(Guinea-Bissau War of Indep) ilianza

Huyu AMÍLCAR CABRAL ni kaka yake mkubwa LUIS CABRAL Rais wa kwanza wa Guinea-Bissau.
#Inshort: AMÍLCAR CABRAL aliuawa na majasusi wa kireno mwaka 1973 mjini Conakry na Guinea-Bissau ilipata Uhuru mwaka 1974 ambapo LUIS CABRAL alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo.

Tuendeleee na SÉKOU TOURÉ...

Kama ilivyokuwa nchi nyingi za Afrika baada ya kupata uhuru, zilijikuta kuwa ktk MFUMO wa chama kimoja. Utakumbuka hata huku kwetu tulikuwa na TANU kabla ya CCM. Hivyo na Guinea ilikuwa na mfumo huo kuanzia mwaka 1960 na kwa takribani miaka 24 hv

Mnamo 15/01/1961 alichaguliwa tena kwa muhula wa miaka 7, akiwa mgombea pekee.Aliendelea kuchaguliwa bila kupingwa ktk miaka ya 1968, 1974 na 1982. Mnamo Machi 26, 1984, SÉKOU TOURÉ alifariki ktk Hospitali ya Cleveland Marekani kutokana na maradhi ya Moyo aliyougua kwa muda mrefu

Hebu tuangalie UTAWALA wake (1958-1984) kabla ya kufariki.

Novemba 1961, DANIEL SEMYONOVICH SOLOD, aliyekuwa Balozi wa Umoja wa Kisovieti (USSR), alifukuzwa na SÉKOU TOURÉ kwa kesi za kujimilikisha eneo la walimu.

Licha ya Balozi mwingine DMITRY DEGTYAR, kutumwa Guinea lkn sakata SOLOD lilipunguza mahusiano baina ya nchi hizo. Mnamo Januari 01, 1963 kulifanyika uchaguzi wa wabunge Chama chake Parti Démocratique de Guinée-Rassemblement Démocratique Africain (PDG-RDA) kilishinda viti vyote.

Mnamo 09/11/1965, Serikali ilitangaza kuwepo kwa ukandamiza uliofanywa na wafanyabiashara ukioongozwa na MAMADOU (Mohamed) TOURÉ.
Meja KEITA MAMOUDOU alihukumiwa kunyongwa kwa kuhusika na sakata hilo.Mwezi huo huo Guinea ilikata uhusiano wa kidiplomasia na Ufaransa na Ivory Coast

Mnamo Agosti 1966, Cuba iliipatia Guinea washauri wa kijeshi (Military Advisors) na Januari 01, 1968 kulifanyika tena uchaguzi mkuu ambapo PDG-RDA kilishinda na yeye kuchaguliwa kwa muhula mwingine wa miaka 7 ya uongozi. Kumbuka hakukuwa na vyama vya upinzani kipindi hicho

SÉKOU TOURÉ alianza kukumbana na changamoto ktk uongozi wake kuanzia 1969 yalipoibuka majaribio ya kumuua. Mojawapo, lilikuwa Februari 1969 watu takribani 1000 wenye silaha walitokea Labé....

💨Ilikuwaje?

💨Easy Do It

RT🔄 Follow me @Eng_Matarra

#EngineerOnKeyboard👩‍💻

#Muendelezo

💨SÉKOU TOURÉ (1958-1984)

Mnamo Februari 1969 kulitokea kundi la watu takribani 1000 wenye silaha kutokea Labé wakimpinga.Wote walikamatwa wakafungwa gerezani. LABÉ ni mkoa kati ya mikoa 8 nchini humo na upo kaskazini ktk milima ya FOUTA JALLON yenye misitu mikubwa

LABÉ ni moja ya mikoa yenye madini mengi ya Bauxite.

Kufuatia uasi huo...

Mei 14, 1969, watu 12 akiwemo Waziri wa ulinzi wa zamani FODÉBA KEÏTA na Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo Kanali KAMAN DIABY walihukumiwa kifo kwa kuhusika ktk njama za kutaka kupindua serikali.

Hukumu yao ilitekelezwa mnamo Mei 27, 1969, isipokuwa FODÉBA KEÏTA na Kanali KAMAN DIABY waliendelea kushikiliwa ktk Gereza la Camayenne, kwa ajili ya Upelelezi ili kuwapata wahusika waliokuwa wanapanga kumuua rais SÉKOU TOURÉ.

Hali iliendelea kuwa mbaya ktk utawala wake na..

Mnamo Juni 24, 1969 Rais SÉKOU TOURÉ alinusurika tena jaribio la mauaji akiwa mjini Conakry lililosemekana kwamba lilipangwa kutekelezwa na huyo Kanali FODÉBA TIDJIANE KEÏTA.

Kilikuwa kipindi ambacho Rais KENNETH KAUNDA wa Zambia alipokuwa ameitembea nchi Guinea.

Kwa mara nyingine tena, mnamo 21-23/11/1970, watu takribani 420 wakisaidiwa na wanajeshi kutoka nchi jirani Guinea-Bissau, walivamia mji wa Conakry. Waasi hao walitumwa na serikali ya kikoloni ya Kireno iliyokuwa inatawala Bissau kwa lengo la kuwaua SÉKOU TOURÉ na AMÍLCAR CABRAL

Waliingia Conakry saa8 mchana wakiwa na meli za kivita 6 na ndege 2 wakauteka mji huo. Jaribio la kuwaua lilishindikana baada ya wawili hao kufanikiwa kutoroka na kujificha mahali pa siri. Wafungwa 26 (wareno) ktk Gereza la BOIRO walichukuliwa na watu 300 waliuawa ktk majibizano

#Turudi nyuma kidogo:

Ktk tukio hilo, baada ya SÉKOU TOURÉ kujificha aliomba kutoka Umoja wa Mataifa. Mnamo Novemba 22, 1970 Baraza la Usalama la @UN liliitisha kikao cha dharula na kulaani tukio hilo. Baraza la UN Lilisema itafanya uchunguzi kuwabaini wahusika wa tukio hilo.

Mwl. Nyerere alikuwa rais wa kwanza (Afrika) kupinga tukio hilo. Mnamo 23/11/1970 alitangaza kumsaidia SÉKOU TOURÉ.

Kipindi hicho Mwalimu alikuwa mstari wa mbele kusaidia nchi za Afrika kupambana na Wareno waliokuwa ving'ang'anizi sana ktk kuachia makoloni yake barani Afrika.

Nyingine zilizotangaza kutoa msaada baada ya Uvamizi wa Portuguese Guinea (Guinea-Bissau)
ni nchi ya Mali, Nigeria, Sierra Leone na Misri.

Umoja wa Kisovieti (USSR) haikuwa nyuma nayo ililaani tukio hilo na China pia ilitangaza kutoa msaada wa kijeshi kuisaidia Guinea.

Nchi ya Kenya ilikuwa nchi ya kwanza kwa Afrika kutuma majeshi yake nchini Guinea mnamo 24/11/1970 ikifuatiwa na Misri iliyotuma vikosi vyake mnamo Novemba 26.

Mnamo 26 & 27, 1970 nchi nyingine za Algeria, Libya na Nigeria nazo pia zilituma wanajeshi kulinda amani nchini humo.

Mnamo Novemba 24, 1970, Baraza la @UN liliunda wajumbe 05 kufanya uchunguzi kutoka nchi za Colombia, Finland, Nepal, Poland, Zambia wakiongozwa na Meja Jenerali PADMA RAHADUR KHATRI wa Nepal. UN ilitarajia kutoa ripoti mnamo 4/12/1970 na Marekani ilikubali kutoa msaada kwa Guinea

Desemba 08/11, UN na OAU zilitangaza kuiwekea vikwazo Portuguese Guinea (Guinea-Bissau) kufuatia tukio hilo. Waziri wa Fedha wa Guinea OUSMANE BALDE na IBRAHIMA BARRY kiongozi wa chama cha DSG, walikamatwa wakafungwa Gereza la BOIRO

Tukio hilo hufahamika km "Operation Green Sea"

Watu wengine 68 waliopatikana na makosa ya kuhusika na njama hizo walihukumiwa kifungo cha maisha jela ambapo wengi wao walifariki kwa sababu ya njaa huko gerezani.

Upelelezi uliendelea ambapo watu wengine 91 walikamatwa na 33 walikuhukumiwa kunyongwa mnamo Januari 23, 1971.

Waziri OUSMANE BALDE, KARA SOUFIANA na IBRAHIMA BARRY pamoja wengine 70 walinyongwa mnamo Januari 25, 1971.

Hata hivyo, USSR ilituma msaada wa kijeshi nchini Guinea kwa kuipatia meli za kufanya Patroli baharini na wataalamu 100 wa mafunzo ya ulinzi kati ya miaka 1971/1978.

Mnamo Aprili 26, 1972, Rais AHMED SEKOU TOURE alimteua Bw. LOUIS LANSANA BEAVOQUI aliyekuwa Waziri wa Fedha kuwa Waziri Mkuu lakini kilikuwa cheo ambacho hakipo kwenye katiba ya Guinea.

Mnamo Desemba 27, 1974 uchaguzi mkuu mwingine ulifanyika na chama chake Rais SÉKOU TOURÉ cha PDG-RDA kilishinda viti vyote 150 vya Bunge la Guinea akiwa hana mpinzani na Julai 1975 serikali ya Guinea ilitangaza kufufua upya uhusiano wake na Serikali la Ufaransa.

Mnamo Julai 18, 1976 Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (OAU) na waziri wa sheria kwa kipindi hicho DIALLO TELLI, alikamatwa nyumbani kwake na kufungwa kGereza la BOIRO. DIALLO alishtakiwa kutaka kupindua serikali. Pamoja na wengine 4 walinyongwa Februari 1977.

Kuanzia Agosti 25, 1977 Conakry na maeneo mengine kulianza maandamano nchini humo. Vikosi vya usalama vilitumia nguvu ambapo viliwakamata baadhi ya waandamanaji na kuwaweka vizuizini. Mnamo Januari 27, 1980 kulifanyika Uchaguzi wa Wabunge na PDG-RDA kilishinda viti vyote 210.

Utawala wa AHMED SEKOU TOURE ulianza kutiwa dosari mnamo Mei 14, 1980 ambapo raia 1 aliuawa ktk machafuko ya kisiasa mjini Conakry.

Mei 09, 1982 uchaguzi wa Rais ulifanyika na SÉKOU TOURÉ alichaguliwa kwa mara nyingine bila upinzani na Mei 14 aliapa kwa muhula wa miaka 5.

Kipindi hiki ndicho alichokuwa alisumbuliwa na maradhi ya moyo.

Ht hivyo siku za SÉKOU TOURÉ hazikuwa nyingi kwani mnamo Machi 26, 1984 alifariki dunia ktk Hospitali ya Cleveland Ohio nchini Marekani wkt akifanyiwa operesheni na LOUIS BEAVOQUI akakaimu urais wa mpito wa Guinea.

Kifo cha SÉKOU TOURÉ mnamo 1984 kiliacha viongozi wa chama chake cha PDG-RDA wakiwa na uungwaji mkono mdogo sana. Mapinduzi ya kijeshi dhidi ya utawala yalianza kufuata kwa msaada wa nguvu kutoka kwa wananchi. Wiki 03 baada ya kifo cha SÉKOU TOURÉ kulifanyika mapinduzi ya kijeshi

Ilikuwa Aprili 3, 1984 na LOUIS LANSANA BEAVOQUI akapinduliwa.

Waziri Mkuu LOUIS BEAVOQUI alikamatwa na kufungwa ktk gereza moja mkoa wa Kindia, ambapo alianza kusumbuliwa na maradhi ya kisukari akarudishwa mjini Conakry kupatiwa matibabu na alifariki mwezi Agosti mwaka huo huo

Mapinduzi hayo yaliongozwa na Kanali LANSANA CONTÉ na Lt. Col. DIARRA TRAORÉ. Siku moja baada ya mapinduzi Kanali CONTÉ aliunda Baraza la kijeshi lililoitwa Military Committee for National Recovery (MCNR) lenye na wajumbe 25 kuongoza akajitangaza mkuu wao nchi hiyo.

Baraza la MCNR lilichukuwa uongozi wa nchi ikiwa ni siku chache ambapo chama tawala cha PDG-RDA kilikuwa kinajiandaa kufanya uchaguzi wa kiongozi mkuu wa chama, atakayeiongoza Guinea mpk uchaguzi, lkn MCNR ilipiga marufuku kufanyika kwa shughuli zozote za kisiasa nchini humo.

Baraza la MCRN lilitangaza kuwa rais atatoka kabila lenye watu wengi, pia sera ya umiliki wa mali na uwekezaji kutoka nje walinaungwa mkono na utawala wao.

Ingawa MCRN haikuzingatia suala la uchumi wa nchi hiyo kukua, wao walijitizama kibinafsi na kujipatia utajiri.

Nchi iliendeshwa kikabila na kupelekea mpasuko mkubwa ktk taifa.

Mwaka mmoja baada ya MCRN kushika madaraka ya nchini hiyo, mnamo Julai 4-5, 1985, wanajeshi watiifu wa ile serikali iliyoondolewa madarakani waliibuka kupambana na vikosi vya wanamapinduzi hao.

Bahati mbaya Juhudi zao ziligonga mwamba baada ya kuzidiwa na majeshi yaliongozwa na Lt. Col DIARRA TRAORÉ na watu 18 waliuawa.

Kufuatia tukio hilo wanajeshi 160 walikamatwa wakanyongwa mwezi Mei 1987 kwa kutaka kupindua serikali.

Mnano Desemba 23, 1990, Luteni Kanali DIARA TRAORE alianza mchakato wa kufanya mabadiliko ya Katiba lkn hali haikutulia.

Katiba mpya ilipitishwa kibabe mnamo 1991 na kuandaliwa uchaguzi ulioshirikisha vyama vingi na ilikuwa kwa mara ya kwanza upinzani kushiriki Uchaguzi wa rais

Mwenendo wa serikali ya Kanali LANSANA CONTÉ kuelekea ukombozi wa kiuchumi ulififia sana. Maandamano na vita ya wenyewe kwa wenyewe vikaendelea na mnamo 28-29- 09-1993 watu 63 waliuawa ktk machafuko mjini Conakry.

Desemba 19,1993 kulifanyika uchaguzi mkuu na vyama vya upinzani vilishiriki kwa mara ya kwanza.

LANSANA CONTÉ aliyekuwa akitokea kabila kubwa la SOUSSOU alishinda Urais kwa 51% kupitia chama chake cha Parti de l’Unité et du Progrès (PUP) au The Unity and Progress Party.

Vyama vya upinzani vilipinga matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na wizi wa kura kasoro kadhaa siku ya kupiga na kuhesabu kura. Uchaguzi wa Wabunge ulifuatia Juni 11, 1995, chama cha PUP kilipata viti 71 kati ya 114 na Upinzani Rassemblement du Peuple Guinéen (RPG) kikipata 19.

Hata hivyo upinzani bado ulilalamikia dosari kadhaa ktk uchaguzi huo mpk shirika la The International Commission of Jurists (ICJ) likatuma wachunguzi kufuatilia madai hayo.

Mnamo Julai 05, 1995 chama cha upinzani vya The Party for Renewal and Progress (PRP) na vingine viliunda muungano ulioitwa "The Coordination of the Democratic Opposition (CODEM)".

Aidha, mnamo Februari 2-9,1996 kulifanyika tena jaribio la mapinduzi ambapo raia 50 waliuawa.

Ktk jaribio hilo LANSANA CONTÉ alinusurika kuuawa na ni mwaka huo huo Guinea iliingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoenda mpk katika nchi za jirani za Sierra Leone na Liberia. Kufuatia tukio hilo Waziri Mkuu SATURNINO da CASTRO alitiliwa mashaka kutomuunga Rais Conte

Mnamo Julai 09 CONTÉ alimteua SIDYA TOURÉ kuwa Waziri Mkuu mpya.

Na hiki ndicho kipindi ambacho makundi mengi ya wapiganaji yaliibuka na mwishoni mwa 1998 kuelekea uchaguzi mkuu mwingine wa Rais, kulizuka machafuko ya kisiasa mjini Conakry na raia wapatao 6 walipoteza maisha.

Ktk Uchaguzi wa Desemba 14, 1998, LANSANA CONTÉ kwa mara nyingine tena alishinda kwa 54%.

Na uchaguzi huu ndio ALPHA KONDE aliyepinduliwa juzi aliwania Urais kwa mara ya kwanza kupitia chama cha Rally of the Guinean People (RGP).

#Inshort:Uchaguzi ulighubikwa na rafu za kutosha

Mnamo Desemba 20, 1998 ALPHA CONDE alikamatwa na polisi na kesho yake kukazuka machafuko baina ya wafuasi wa CONTE na Serikali na baadhi waliuawa.

Serikali Guinea na Liberia ziliendelea kutupiana lawama kwamba Liberia ilikuwa ikiwapa silaha wapinzani na kuunga mkono uasi wao.

Mnamo Juni 25, 2000 kulifanyika uchaguzi wa serikali za mitaa (Madiwani na Meya) na ulighubikwa pia na machafuko, ambapo watu 03 waliuawa kufuatia mapigano mjini Conakry

Vyama vya upinzani viliendelea kuilalamikia serikali kwa kuhusika na kushindwa kuandaa uchaguzi huru na wa haki. Mwaka huo huo upinzani wakisaidiwa na wapiganaji wa kikundi cha Revolutionary United Front (RUF) kutoka Sierra Leone, walianza uvamizi ktk kambi za Majeshi ya Guinea.

Hiki kikundi cha RUF kiliundwa na vijana wadogo umri 14-26 na walipata silaha na magari kutoka nchi jirani. Waliungwa mkono na Upinzani na kilipata nguvu kikawa tishio.

Mnamo Sept2-3, 2000, RUF wakisaidiwa na Serikali ya Liberia walivamia kijiji cha MASSADOU na kuua watu 40

Mashambulizi yaliendelea na mnamo Sept 04,2000 Mji wa MADINA WOULA ulivamiwa watu 43 waliuawa.

Mnamo Sept 06, 2000 walivamia pia kijiji cha PAMELAP na kuua watu 27. Nchi ikawa imechafuka, wanajeshi wakatumwa maeneo kusini kupambana na waasi na siku hiyo pekee watu 125 waliuawa.

Mnamo Sept 13, 2000, Ufaransa ikangilia kati mgogoro na kuwaomba waasi (RUF) kufanya mazungumzo ya kitaifa ili kurejesha amani nchini Guinea. RUF hawakujibu kitu na siku 4 baadae mfanyakazi mmoja wa shirika la Umoja wa Mataifa (UNHCR) aliuawa tena ktk Mji wa Macenta.

Mashambulizi mengine yalifanyika Sept 28, ambapo miji ya BAYARO na SOKOLALU na kambi moja ya kijeshi iliyokuwa ktk vijiji vya Macenta na Farmoreya zilivamia na watu 81 waliuawa. Aidha, Dec 4 waasi walivamia pia vijiji vya Kotizu na Gbayaro ambapo watu 12 waliuawa.

Mnamo Desemba 7-8, 2000 Jeshi lilivamia maeneo ya GUÉKÉDOU ilipohisiwa kambi ya waaasi na ktk mapambano baina ya vikosi vya RUF, raia zaidi 100 walipoteza maisha.

Siku mbili baadae jeshi lilivamia Mji wa Kissidougou uliopo mpakani na waasi 30 waliuawa wakarudi Siera Leone.

Kilikuwa kipindi kigumu sana kwa Guinea, wengi waliuawa ktk mapigano hayo.

Ktk matukio hayo Waguinea zaidi 1,000 waliuawa kwa uvamizi huo, na maelfu zaidi ktk maeneo ya kusini walikimbia makazi yao.

Wkt vita vya wenyewe kwa wenyewe vikiendelea, wakimbizi zaidi ya 400,000 kutoka nchi za Liberia na Sierra Leone walikimbilia Guinea na hivyo kuongeza uhasama kati ya Guinea na majirani zake.

Mnamo Desemba 12, 2000, KOFI ANNAN, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wkt huo alilaani vitendo hivyo na shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa @Refugees lilianza kutoa misaada kwa wakimbizi nchini Guinea na watu wengi zaidi ya 1.5M walikimbia kutoka Sierra Leone na Liberia.

Ukiangalia matukio yote yalitokea mfululizo, inaonyesha waasi walijipanga kabla kuanza uhalifu huo.

Desemba 21, 2000 Baraza la Usalama la @UN lilikaa kikao kujadili hali ya Usalama wa Guinea-Conakry na lililaani vikali kikundi hicho cha RUF kutoka nchi jirani ya Sierra Leone.

Kati ya Jan 01 & April 15 , 2001, shirika la kimaitafa la @RedCross lilituma watu zaidi ya 83,000 nchini hulo kusaidia huduma mbalimbali za kibinadamu.

Vita ni mbaya sana ndg waTz🇹🇿

UKIONA haki inaminywa mahala paze sauti yako kupinga kuliko kusubili vita itokee uanze kulaumu.

Hii yote ulisababishwa na uminywaji wa #HAKI na uchafuzi ktk uchaguzi nchini humo. Watawala hawakujali kuhusu hilo.

Na sio kwamba vita iliishia hapo, HAPANA!! Vita vya wenyewe kwa wenyewe viliendelea nchini humo #MFANO; Januari 04/06, 2001 kulizuka mapigano na raia 350 waliuawa.

Mauaji makubwa ya raia yalifanyika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka 2001, ambapo waasi walivamia vijiji kadhaa na kufanya mauaji na ktk mwezi huu pekee, watu 1500 waliuawa na zaidi ya 250,000 walikimbia makazi yao maeneo ya kusini mwa nchi ya Guinea kwenda nchi jirani.

Ukiona serikali anashadadia mambo haya uminywaji uhuru kundi fulani lenye haki kikatiba, Pinga sana hizo ni dalili za kuchochea uasi na Uasi ni mbaya sana.

Tizama jinsi raia wasio na hatia ktk mapigano hayo walivyosababishiwa kisasi kwa7bu ya madaraka. Inaumiza sana !!!

#INAUMIZA SANA!!!

Na nikuombe ukiona viashiria vya hali hii ombea nchi yetu.

Vuta picha uko Dodoma bungeni waasi wanavamia pale kijijini kwenu TENA kwa wananchi wasio na silaha wanaua na kuondoka!!!

Inaumiza sana bt anyways..😭😭

Tuendelee!!!!👇

Baada ya vikosi vya kimataifa kutumwa Guinea makundi hayo ya waasi yalikimbia na amani ikarejea nchini humo japo kidogo.

Jumuiya za Kimataifa zililaani vikali mauaji yale ikiwemo Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) lilitangaza kuitizama upya serikali ya Guinea.

Kipindi vita inaendelea hakuna aliyekwenda shambani wala ktk biashara hasa maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.

Hivyo, serikali kwa kusaidiana mashirika ya kimataifa ilianzisha mpango wa kutoa msaada wa chakula kwa kaya zilizoathirika zaidi na watoa misaada 25,000 walipelekwa Guinea.

Mnamo 11/11/2001 kulifanyika zoezi la kupiga kura ili kupitisha marekebisho ya Katiba.

Marekebisho hayo hayakupokewa vizuri na wengi hususani asasi za kiraia pamoja na vyama vya upinzani. #Sababu ilikuwa kumuongezea rais muda wa kutawala kutoka muhula wa miaka 5 awali na kuwa 7

Mapingamizi mengine kuhusiana na marekebisho, ni kuhusu Rais LANSANA CONTÉ kugombea urais tena kwa muhula wa TATU.
Vyama vya upinzani vilisusia mchakato wa kupigia kura marekebisho ya katiba. Waliopiga ni wafuasi wake pekee na ilitangaza kuwa mapendekezo yaliungwa mkono kwa 98%.

Baada ya marekebisho hayo kupitishwa mukwamo wa kisiasa na hali ya amani ilitishia kuibuka migogoro mingine nchini.

Hali hiyo ilipekea mnamo Desemba 01, 2001, kutangaza kusogezwa mbele kwa uchaguzi mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika baada sikukuu za Krismas mnamo Desemba 27, 2001

Vuta ni kuvute zilikuwepo hapa na pale baina ya serikali na upinzani na asasi za kiraia, lkn baadae mnamo June 30, 2002 uchaguzi wa wabunge ulifanyika na chama tawala (PUP) kilipata viti 85 kati ya 114 huku UPR cha upinzani kikipata viti 20 na ikabua mvutano wa kisiasa TENA!!

Mnamo Machi 04, MAMADOU BA, Kiongozi wa Upinzani aliomba jeshi kuchukua madaraka kunusuru nchi kutoingia machafuko mengine. Hakuna aliyemsikiliza ikapelekea kuibuka kwa maandamano, ambapo Juni 11, 2003 watu 02 waliuawa wilaya ya KOYA na upinzani ukatangaza kususia Uchaguzi ujao.

Mnamo Desemba 21, 2003 kulifanyika Uchaguzi na Rais CONTE na kushinda, ukawa muhula wake watatu na Upinzani haukushiriki kabisa.

Hatua hiyo ilipelekea Waziri Mkuu FRANÇOIS LOUNSENY FALL kujiuzulu mnamo April 30, 2004 na Desemba 09 aliteuliwa CELLOU DALEIN DIALLO kuwa Waziri Mkuu

Mnamo Januari 19, 2005 Rais CONTÉ alinusurika kifo ktk jaribio la mauaji Mjini Conakry.

Upelelezi ulifanyika ikapelekea kuondolewa DALEIN DIALLO uwaziri mkuu mnamo April 05, 2006.

Mdogo mdogo tena, walimu nao wakaanzisha mgomo nchini wa kutoingia kazini mnamo Juni 08, 2006.

Mgomo wa walimu ulihusisha pia wanafunzi na ulifanyika kote nchini wakidai hali ngumu ya maisha na kuongezewa mishahara.

Kufuatia mgomo huo mnamo June 12, 2006 vikosi vya serikali vilitelekeza mauaji ya wanafunzi 10 ambao walikuwa miongoni mwa wanaandamanaji Mjini Conakry.

#Ikapelekea kuibuka kwa maandamano makubwa.

Aidha, Januari 10-26, 2007 vyama vya wafanyakazi, vikundi vya jamii, Asasi za kiraia pamoja na vyama vya Siasa viliungana kwa pamoja na kufanya maandamano kupinga gharama kubwa za maisha na ufisadi serikalini na kumtaka CONTÉ ajiuzulu

Waandamanaji 60 waliuawa na vikosi vya usalama nchini humo.
Baada ya mauaji hayo, serikali ilitangaza "Hali ya hatari" mnamo Februari 12, 2007.

Rais CONTÉ alipoona amani inatoweka nchini, akakubali kupunguza mamlaka kwa waziri mkuu akamteua EUGENE CAMARA kushika nafasi hiyo.

Uteuzi huo haukupokelewa vizuri na ulipingwa na vyama vya wafanyakazi nchini humo na maandamano yaliendelea siku iliyofuata, ambapo kuanzia Februari 12-15, 2007 watu takribani 23 waliuawa pia.

Ikabidi Rais LANSANA CONTÉ kumpiga chini EUGENE CAMARA ktk nafasi ya uwaziri mkuu.

Mnamo Februari 23, 2007, Katibu Mkuu wa UN, BAN KI-MOON alitoa tamko la kumtaka Rais CONTÉ afanye mazungumzo ya amani na vyama vya wafanyakazi pamoja upinzani nchini.

Baada ya tamko Bunge la Guinea lilipiga kura kwa kauli moja kuondoa kwanza hali ya hatari mipaka ifunguliwe

ECOWAS iliingilia kati ikamtuma IBRAHIM BABANGIDA, rais wa zamani wa Nigeria kufanya upatanishi na makubaliano kati ya serikali na upinzani. Mnamo Februari 26, 2007 Rais Conte alimteua LANSANA KOUYATE kuwa waziri mkuu, ikapelekea maandamano tena kesho yake ambapo 130 waliuawa!!

Maandamano yaliendelea bila kukoma huku viongozi wa upinzani wakiomba jeshi lisiwashambulie raia kwa sababu wanachodai ni kwa maslahi ya Wananchi wote Guinea. Na kweli hali iligeuka, polisi waliacha kabisa kuwashambulia waandamanaji.

Kwa Machi na Aprili maandamano yaliendelea lkn hakuna aliyeuawa.

Mnamo Mei 02, 2007 wanajeshi nao mjini Conakry walianza mgomo kudai nyongeza ya mishahara. Ikaambukiza kambi ktk miji mingi nchini Guinea kufanya mgomo ulioendelea mpk Mei 12, 2007 na watu 6 walipoteza maisha.

Mgomo wa Jeshi ulipelekea Rais Conte kumuondoa Waziri Mkuu KOUYATE mnamo Mei 21, 2008 akamteua Doctor AHMED TIDJIANE SOUARE kuwa waziri mkuu.

Wanajeshi hawakukubaliana na uteuzi huo waliendelea na mgomo sababu madai yao yalikuwa hayajatimizwa.

Walipoona rais hawasikilizi, wakabadili upepo na kutoka ndani ya kambi za jeshi na kuanza maandamamo ktk barabara za mji mkuu Conakry na kupelekea mapigano baina yao na polisi.

Maandamano haya yalitokea mnamo Mei 26 hadi Juni 17,2008 raia 2, polisi 4 na wanajeshi 2 waliuawa.

Maandamamo yaliendelea na mnamo Oktoba 10, 2008 yalitokea mapigano makali ktk migodi huko Miamba ambapo watu wawili walipoteza maisha.

Licha ya ghasia kuendelea na jaribio la mauaji (2005) bado Lansana Conde alishikilia madaraka ILA alikuwa haonekani kw7bu alikuwa anaumwa.

Mnamo Desemba 23, 2008 mapema Asubuhi, Bw. ABOUBACAR SOMPARÉ, Spika wa Bunge alishangaza wengi kwa kutangaza kutokea kifo cha Rais wa LANSANA CONTÉ wa Guinea.

Spika alisema CONTE alifariki saa 12:45 jioni jana yake baada ya kuugua kwa muda mrefu lkn hakueleza ugonjwa uliomua.

Kulingana na taarifa yake Lansana Conte alikuwa akiugua kwa miaka mingi, lkn alijitahidi anapokuwa hadharani aonekane mzima kuwafurahisha raia wa Guinea.
Alisafiri mara nyingi kwenda nje ya nchi kutibiwa na alifanya hivyo kwa siri.

Lkn Tetesi za kuugua kwake zilikuwa zikisikika

Kumbuka matatizo na jeshi la nchi hiyo yalikuwa hayajaisha.

#Inshort: ALIUGUA very tight kweli. Hakuoneka ktk Televisheni kwa miezi 4 mfululizo. Kiongozi wa upinzani almaarufu "TABASKI" alisema fununu za kuugua kwake mwanzoni mwa Desemba na kupelekra maandamano zaidi Jeshini

Ubaya zaidi licha ya wanajeshi kuendelea na maandamano hakuwahi kujitokeza kuongelea lolote juu ya maandamamo hayo.

Gazeti moja lilichapisha picha yake ikimuonyesha alivyokuwa amedhoofika, picha ilionyesha hata kusimama kwake ilikuwa kwa shida sana.

Mhariri wa gazeti lile alikamatwa akaamrishwa aombe radhi TENA kupitia media na aweke picha nyingine inayomuonyesha RAIS CONTE akiwa mzima wa afya.

Kulingana na katiba yao rais akifariki inatakiwa Spika kushikilia madaraka ya Rais kwa kipindi cha siku 60 ili kufanyike uchaguzi.

Jaji Mkuu wa nchi kwa kipindi hicho, LAMINE SIDIME, alihodhi nafasi hiyo kwa muda hadi Spika atakapoapishwa.

Baadae alikula kiapo cha kukaimu Urais mbele ya waziri mkuu na Mkuu wa Majeshi DIARRA CAMARA, akishika hatamu ili zoezi la kumpata mrithi wa Lansana Conte ufanyike.

SOMPARÉ aliapa kuwa kiongozi wa mpito kwa siku 40 mpk hapo nchi itakapopats rais mwingine.

Kwa kuwa Lansana Conte chama chake ndio kilikuwa madarakani na yeye ndiye alikuwa mwenyekiti wake. Ilitakiwa kikae kikao kichague Mwenyekiti mwingine ili kugombea ktk UCHAGUZI wa Rais ujao

Alitoa amri kwa majeshi kuweka ulinzi wa mipaka na kuhakikisha utulivu na amani ktk nchini kusubilia kupatikana kwa kiongozi mwingine na wakati huo taratibu za kuuzika mwili wa Rais CONTÉ zikiendelea.

#MASAA 6 baada ya SOMPARÉ kuapishwa kulitokea taarifa za kuogofya zilizotikisa nchi zikatokea.

#BreakingNewsLIVE🔴 iliyorushwa ktk kituo cha Televisheni cha Serikali kusema kwamba rais aliyeapishwa muda mfupi uliopita amepinduliwa na madaraka yapo chini jeshi.

Taarifa hiyo ilisomwa na Kapteni MOUSSA DADIS CAMARA kwa niaba ya kundi lililojiita National Council for Democracy and Development(CNDD).

Kapteni CAMARA alitangaza kuwa shughuli zote za kiserikali zipo chini ya utawala mpya wa CNDD na Vyuo, mashule vimefungwa kwa muda.

Aidha, alipiga marufuku kufanyika shughuli zozote za kisiasa ndani ya nchi mpk hapo itakapotoka taarifa nyingine. Wananchi walikuwa wanatarajia kumzika LANSANA CONTÉ mnamo Desemba 26, 2008.

Shughuli zikasimamishwa kwa muda GHAFLA na mwili wake ukawekwa mahali maalum.

TAARIFA nyingine ilitolewa kwamba mwili utapelekwa Bungeni, kisha uwanjani ambapo watu takribani 20,000 walihudhuria kumuaga. Kipindi yote yanatokea viongozi kutoka nchi jirani walikuwa wameshaingia nchini Guinea tayari kwa ajili ya mazishi, hivyo nao walimuaga pale Bungeni.

Mbele ya bunge Gen. MAMADOUBA TOTO CAMARA wa Baraza la CNDD lililofanya mapinduzi hayo, ktk msiba alitamka maneno haya:

"We pray God to give us the courage to continue (Conté's) work of tolerance and peace for the welfare of Guinea". akimaanisha nchi iko ktk utawala mpya

Baadaye mwili wake ulipumzishwa kijijini kwao LANSANAVA mbele ya nyumba yake na alizikwa kijeshi.

Ukichangia alipougua hakuonekana kwa kipindi kirefu, maandamamo ya wanajeshi na tukio la jeshi kumpindua Spika Sompare, LANSANA CONTÉ alizikwa na watu wengi sana.

BILA shaka ni kwa sababu jeshi lilichukua madaraka ghafla pengine mazishi yake yangekuwa ya kawaida tu.

EU ililaani mapinduzi hayo, ikatangaza kuwawekea vikwazo wanajeshi waliochukua madaraka na kusimamisha misaada ya kiuchumi.

Canada pia ililaani tukio hilo mnamo Desemba 24,2008.

Umoja wa Afrika (AU) na pia hawakuwa nyuma, ulitangaza kusimamisha uanachama nchi hiyo iliyokuwa chini ya CNDD mnamo 28/12/2008.

Mnamo Desemba 30, 2007 Baraza la kijeshi la CNDD lilimteua KABINE KOMARA kuwa Waziri Mkuu.

Jumuiya ya kiuchumi nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilitangaza kusimamisha uanachama wa Guinea ktk Jumuiya hiyo mnamo Januari 10, 2009.

Kilichofuata aliyekuwa Waziri Mkuu kipindi cha Rais huyo aliyefariki AHMED TIDIANE SOUARÉ alikamatwa na jeshi hilo mnamo Machi 22, 2009.

Mnamo Machi 23, 2009, Serikali ya Marekani iliongeza vikwazo kwa kuwafungia wahusika wote wa Mapinduzi kutoingia nchini mwake, wakiongozwa na Kapteni CAMARA pamoja na viongozi wengine walioshirikia nae.

Aidha, EU pia uliwafungia viongozi wa CNDD kukanyaga barani Ulaya.

Mwezi Agosti 2009, MOUSSA DADIS CAMARA alitangaza kuwa uchaguzi wa rais na wabunge utafanyika mnamo Januari na Machi 2010 na yeye akasema hatogombea ktk Uchaguzi huo. Licha ya ahadi zake za awali kwamba yeye na wanachama wengine kutokea ktk Baraza la CNDD hawatasimamisha mgombea

ktk uchaguzi huo, uliibuka uvumi kwamba CAMARA anapanga kuwania urais.

Baada ya fununu hizo maandamano nchi nzima kutaka jeshi kuachia madaraka yaliibuka TENA na mnamo Septemba 28, 2009 watu takribani 155 waliuawa ktk maandamano ingawa serikali ilisema ni watu 57 tu waliofariki.

Mikutano ya siasa ilipigwa marufuku na likatolewa tangazo kuwa vyama vyote vya siasa vimesimashiwa shuguli za kisiasa.

Mnamo Septemba 29, 2009 Ufaransa ilitangaza kuiwekea Baraza la CNDD vikwazo vya kiuchumi na kusitisha misaada yake ya kijeshi nchini Guinea.

Marekani na Umoja wa Ulaya (EU) nao, walilaani vitendo vya mauaji vinavyokuwa vikiendelea nchini humo ambapo wanaharakati na viongozi wa siasa walikamatwa na kuuawa kimya kimya, pamoja na mauaji ya Septemba 28, 2009.

Rais BLAISE COMPAORÉ wa Burkina Faso, akatumwa na ECOWAS kwenda Guinea kutafuta mazungumzo baina ya upinzani na serikali ya kijeshi. Rais BRAISE alifanya kazi hiyo kati ya Oktoba 05, 2009 mpk Machi 25, 2011.

Mnamo Oktoba 16, 2009 ECOWAS iilaani mauaji ya raia wasio na hatia ktk tukio lililofanyika Sept28.

Mnamo Oktoba 15 Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), ktk kikao cha shughuli zake za kawaida ilitangaza kuwa itafanya uchunguzi juu ya matukio ya vikosi vya CNDD nchini Guinea

ICC ilisema itatoa ripoti ya awali kufuatia mauaji yaliyotekelezwa mnamo Septemba 28, 2009 ambapo raia 150 waliuawa lkn taarifa iliyotoka ilisema walikuwa 57.

Mnamo Oktoba 29, 2009 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo, BAN KI-MOON, aliunda Tume kufanya uchunguzi iliyoundwa na watu kutoka nchi tatu.
WATU hao walitoka Algeria, Burundi na Mauritius, wakiongozwa na MOHAMED BEDJAOUI wa Algeria kuchunguza mauaji ya Sep 28 huko Conakry.

Mnamo Oktoba 29, 2009 Umoja wa Afrika (AU) uliongezea vikwazo vya kiuchumi kwa serikali ya kijeshi ya CNDD na vikosi vya walinda amani vilitumwa nchini Guinea.

Mnamo Desemba 03, 2009, MOUSSA DADIS CAMARA, alinusurika kuuawa ktk shambulio lililofanywa ktk kambi ya wanajeshi.

Luteni ABOUBACAR DIAKITE ndiye aliyeongoza shambulio hilo.

MOUSSA DADIS CAMARA alipasuliwa kidogo kichwani kwa risasi ikabidi asafirishwe kesho yake kwenda nchini Morocco kwa ajili ya upasuaji na matibabu.

Naibu Kiongozi wa CNDD ambaye ndiye alikuwa Waziri wa ulinzi Gen. SEKOUBA KONATE alipewa kijiti cha uongozi wa mpito kipindi Camara hayupo.

Mnamo Desemba 18, 2009, Tume ya uchunguzi ya UN ilitoa ripoti ya mauaji ya Sept28, na ilisema CNDD ilikiuka mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu na mauaji yale yalitafsiriwa kama uhalifu dhidi ya binadamu.

EU iliongeza vikwazo kwa CNDD mnamo Desemba 22, 2009

Baraza la CNDD likatisika sana.

Ikabidi Kapteni CAMARA alipotoka matibabu Morocco mnamo Januari 12, 2010 achukua ndege kwenda Burkina Faso.

Alikutana na Rais BLAISE COMPAORÉ, aliyekuwa akiwapatanishi ili kufikia makubaliano ya amani baina CNDD na wapinzani nchini Guinea

Mazungumzo yalifikiwa muafaka mnamo Januari 15, 2010, ambapo mkataba wa amani ulisainiwa kwa masharti kwamba MOUSSA DADIS CAMARA aendelea kusalia Burkina Faso na Gen. SEKOUBA KONATE pamoja na Baraza lake la CNDD wamchague kiongozi mwingine ambaye atakuwa waziri mkuu wa mpito.....

kwa ajili ya kuiongoza nchi ila KONATE abakie wasaidiane naye.

Mnamo Januari 26, 2010, Baraza la kijeshi la CNDD Lilimteua JEAN-MARIE DORÉ kuwa Waziri Mkuu wa mpito kwa kipindi cha miezi SITA.

Baada ya hayo kufikiwa serikali ya Ufaransa ililegeza vikwazo vya kiuchumi kwa Guinea trh 26-02-2010 na ikatangaza kutoa ushirikiano wa kijeshi na serikali mpya ya JEAN-MARIE DORE na alitakiwa kuandaa uchaguzi wa rais

Duru ya kwanza ya Uchaguzi ilifanyika mnamo Juni 27, 2010.

Huu ndio uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini Guinea tangia Uhuru na zaidi ya wagombea 20 waliwania kiti hicho.

Waliokuwa na ushawishi mkubwa na maarufu sana ktk kampeni ni miamba wawili, CELLOU DALEIN DIALLO waziri mkuu wa zamani na ALPHA CONDÉ (aliyepinduliwa juzi)

DIALLO aligombea kupitia chama cha The Union of Democratic Forces of Guinea/ Union des Forces Démocratiques de Guinée (UFDG) na alipata 44% dhidi ya mpinzani wake ALPHA CONDÉ aliyepata 18% kupitia The Rally of the Guinean People au Rassemblement du Peuple Guinéen (RPG) kifaransa.

Kulingana na katiba matokeo yakitangazwa mgombea mwenye kura kuanzia 50%, ndiye hutangazwa kuwa mshindi wa Urais.

Hivyo, kwa matokeo hayo hakuna ht mmoja aliyefikisha, ikabidi wagombea wawili waliopata kura nyingi zaidi ALPHA CONDÉ na DIALLO warudie duru ya pili ya Uchaguzi.

Duru ya pili ilirudiwa mnamo Novemba 07, 2010 na matokeo yalitangazwa:

Mgombea wa Rassemblement du Peuple Guinéen (RPG) kutokea kabila dogo la "Malinké" na mpinzani muda mrefu, ALPHA CONDÉ, alionyesha kuwa mshindi kwa 53% huku DIALLO kutokea kabila "Peul au Fulani" akipata 47%.

EU ilituma wataalam wa masuala ya uchaguzi 07 na Waangalizi wa uchaguzi 63,bna waliingia Guinea kuanzia Juni 01, 2010 kufuatilia uchaguzi huo.

AU ilituma waangalizi 44 wakiongozwa na EDEM KODJO, Waziri Mkuu wa Togo, ile Duru ya kwanza na waliingia Guinea kuanzia Juni 22, 2010.

ECOWAS ilituma waangalizi wa uchaguzi 200.

Shirika la International de la Francophonie (OIF), lilituma waangalizi zaidi ya 20 ktk ILE duru ya kwanza na walikuwepo nchini humo kuanzia mnamo Juni 22 hadi Juni 28, 2010.

Wengine 30 ni kutoka Shirika la Carter Center (CC), wakiongozwa na YAKUBA GOWON wa Nigeria walioingia Mei 23, 2010.

Mgombea wa chama cha UFDG na aliyewahi kuwa waziri mkuu (2004) kabla ya kuondolewa na marehemu Rais Conte wa nchini, Bw CELLOU DALEIN DIALLO, alipinga matokeo hayo

Akafungua kesi Mahakamani. Mwezi uliofuata Mahakama Kuu ilithibitisha matokeo na kutupilia mbali madai yake ya kuwepo udanganyifu na wizi wa kura.

WAFUASI wa DIALLO walianzisha vurugu ktk miji mbalimbali, wakishinikiza kufutwa kwa matokeo hayo.

Vurugu ziliendelea kote nchini hasa mjini Conakry.

Kumbuka kwa kipindi chote Waziri Mkuu wa mpito JEAN-MARIE DORÉ, ndiye alikuwa akiongoza nchi hiyo.

Ghasia ziliendelea na watu takribani 10 waliuawa kati ya Septemba 12 na Novemba 15, 2010.

Kufuatia vurugu hizo Serikali ilitangaza hali ya hatari kwa nchi nzima, na Marekani na Baraza la Usalama la UN vililaani sana vurugu hizo.

Mnamo Desemba 09, 2010, Umoja wa Afrika uliondoa vikwazo vyote vya kiuchumi, usafiri, kidiplomasia na kusimamishwa kwa uanachama wa Guinea

Mwezi Desemba 10, 2010, hali ya hatari iliyokuwa imetangazwa ilifutwa.

ALPHA CONDÉ alikula kiapo cha Urais mnamo Desemba 21, 2010 na ECOWAS iliondoa vikwazo vyake vya kijeshi, kidiplomasia na kusimamishwa kwa uanachama mnamo Machi 25, 2011.

Akaanza utawala wake, lkn nchi ikiwa imefujwa pesa hatari. Wapo waliojenga imani naye lkn ktk kipindi chake cha kwanza alikabiliwa na changamoto kibao.

Naam huyu ndio ALPHA CONDÉ Rais wa Guinea-Conakry ambaye video na picha zake zimesambaa mitandaoni akiwa AMEPINDULIWA!!

Rais ALPHA CONDÉ alilazimika kushughulikia hali mbaya ya kiuchumi ktk nchi hiyo ambayo aliipokea kutoka kwa CNDD ikiwa imefilisika na hazina iko tupu. Alianza na kupitia mikataba mbalimbali hususani ktk wizara ya madini iliyokuwa imesaniwa na watangulizi wake miaka ya nyuma.

Mikataba mingi iliyoonekana kuinyonya nchi ilibadilishwa. Baadhi ya vigogo walitumbuliwa na wengine walikabiliwa na mashtaka ya ufisadi akiwemo mke wa rais wa zamani LANSANA CONTÉ, ambaye ilionekana alikuwa amehongwa mgodi mmoja nchini humo na Baraza la kijeshi (CNDD).

Wapo waliokuwa na IMANI na ALPHA CONDE, lkn kama kawaida huwezi kupendwa na wote, wewe nani upendwe na wote, MTUME mwenyewe hakupendwa na wote.

Mnamo Julai 10, 2011, ALPHA CONDE alinusurika kuuawa ktk shambulio lililofanywa ktk Ikulu Mjini Conakry na mlinzi wake mmoja aliuawa.

Upelelezi ulifanyika na watu 17 wakiwemo wanajeshi walikamatwa kwa tuhuma hizo. Mnamo Agosti 16, 2011, ALPHA KONDE aliwasamehe watu hao, akawaachilia pamoja na viongozi waliokamatwa kwa ufisadi.

Mnamo Septemba 27, 2011, pia kulitokea maandamano ambapo watu 03 walipoteza maisha.

Baada ya hapo rais ALPHA CONDÉ akaona anaweza kupinduliwa muda wowote na saa Yeyote, akaanza kuwabana wapinzani na wakosoaji wa serikali yake vilivyo kwa historia ya Taifa hilo alikuwa anaijua.

Akazuia shughuli zote za kisiasa nchini na vyama vya upinzani vilimlalamikia sana!!!

ALPHA CONDÉ alianza kushughulikia uchumi kwa kuangalia mikopo ambayo watangulizi wake walikuwa wamekopa na kupelekea serikali kushindwa kujiendesha. Alifanya mazungumzo na wadai wake sugu wa mikopo "PARIS CLUB" na walikubali kuifutia Guinea 20% ya madeni iliyokuwa inadaiwa.

Uongozi wake ulikumbana na changamoto kutokana na kuchelewesha kwa "uchaguzi wa wabunge", ambao hapo awali ulikuwa umepangwa kufanyika mwaka 2011.

Ulicheleweshwa mara kwa mara kwasababu ya machafuko ya kisiasa nchini humo.

Viongozi wa Upinzani walianza kuitisha uchaguzi huo kufanyika.

Kwa mara nyingine dosari ktk utawala wa ALPHA CONTE zilianza kujitokeza mnamo Septemba 12, 2012, baada ya vikosi vya usalama kuzuia mkutano wa siasa uliokuwa ufanyike siku hiyo na kupelekea kifo cha mtu MMOJA.!!

MAUAJI hayo yalikuwa kama njiti ya kiberiti inayowaka hlf imerushwa ktk tanki la Petrol. Viongozi wa upinzani walishawishi wananchi kufanya maandamano nchi nzima.

Na maandamano ya kwanza yalishuhudiwa kwa siku mbili, mnamo Desemba 2-3, 2012 ambapo watu watatu waliuawa.

Upinzani uliitisha tena maandamano ya nchi nzima kuanzia Februari 19, 2013 kuelekea ktk Uchaguzi mkuu wa Wabunge.

Ilibidi ALPHA CONDÉ aandae uchaguzi wa wabunge na ulipangwa kufanyika mnamo Februari 24, 2013.

Vyama vya upinzani vilitangaza kutoshiriki UCHAGUZI ikiwa serikali haitakuwa na "Tume Huru" ya kusimamia uchaguzi.
Madai ya upinzani hayakutekelezwa na kilichofuata Rais ALPHA CONDÉ alisema ikiwa bado hawatali kushiriki basi zoezi la uchaguzi huo lisogezwe siku za mbele.!!!

Kauli hiyo ilipokewa tofauti na Upinzani na kuanzia Februari 27 hadi Machi 06, 2013, kulizuka maandamamo yaliyoambatana na vitendo vya vurugu nchi nzima na kupelekea watu 9 kupoteza maisha.

Mnamo Machi 1, 2013 Katibu Mkuu wa UN, BAN KI-MOON, alihimiza upinzani kufuata njia ya mazungumzo kushughulikia masuala ya uchaguzi ili kufikia makubaliano ya amani.

Machi 5, 2013, pia EU ilitoa wito kwa serikali kukaa meza moja ya mazungumzo na upinzani ili kumaliza tofauti zao

Chama kikuu cha upinzani kilikubali kufanya mazungumzo ya mwanzo na serikali iliahidi kufanya mabadiliko ikaomba kukutana na upinzani kujenga umoja kuelekea ktk uchaguzi.

Mnamo Aprili 07, 2013 chama kikuu cha upinzani kiliridhia kutoa ushirikiano kuelekea Uchaguzi mpya wa Bunge.

Mjumbe wa @UN, SAID DJINNIT wa Algeria ndiye aliyekuwa mtu kati kufanya upatanisho ktk mazungumzo kati ya serikali na upinzani mnamo Aprili 15, 2013.

Chama kikuu cha upinzani kiliungana na vyama vingine kadhaa ili kupata nguvu. Licha ya mazungumzo hayo kuna baadhi hayakufikiwa.

Ikapekea mkwamo wa kisiasa na kudorola kwa maelewano.

Hali hiyo iliongeza kutoelewana na kukatokea kwa mgogoro na baadhi ya maeneo kulishuhudiwa maandamamo kati ya April 18/25 na Mei 21,23 na 27, 2013 ambapo watu takribani 17 walipoteza maisha TENA!!!

Mnamo Juni 20, 2013, DALEIN DIALLO alitangaza kutofuata mapendekezo ya Julai 02, yaliyofikiwa ktk makubaliano na serikali na mjumbe wa UN.

#Moja ya makubaliano ilikuwa uchaguzi wa wabunge ufanyike Julai 03, 2013 na alijiondoa kwasababu alidai bado Tume ya uchaguzi haikuwa huru

Umoja wa Afrika (AU) ulituma waangalizi 40, wakiongozwa na MAHAMADOU DANDA, Waziri Mkuu na Rais wa zamani wa Niger, ambao waliingia nchini Guinea mnamo Agosti 24, 2013.

Wengine walitoka EU na waliingia Agosti 22, 2013.

ECOWAS pia ilituma waangalizi wake 100 wakiongozwa na Waziri Mkuu wa zamani EDEM KODJO wa Togo, na wao waliingia nchini humo Sept 16-29, 2013.

Aidha, shirika la kimaitaifa la International de la Francophonie (OIF), nao walituma watu wake kuanzia mwanzo mpk mwisho wa uchaguzi

Mnamo Nov 15, Mahakama Kuu ilitoa taarifa ya kupitisha matokeo ya uchaguzi huo, kupelekea kuibuka kwa ghasia kwa mara nyingine nchini humo.

Ghasia ziliendela mjini Conakry kati ya Novemba 17-26 na watu wawili waliuawa kufuatia maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

Kukiwa bado na mvutano juu ya matokea ya uchaguzi, kulitokea mlipuko mbaya wa UGONJWA wa EBOLA.

Ugonjwa ulienea nchi nzima Desemba mwanzoni kwa haraka mno mpk nchi jirani za Sierra Leone na Liberia zilikumbwa. Watu wakafa wengi + maandamano kuendelea ikawa shida juu ya SHIDA!!

💨Nini kilifuata?

📋Mtiririko mzima kuanzi ALPHA CONDE kumuibua mtu ambaye amekuja kumpindua. Utajiri/Ukwasi wa mabilion alionao Doumbouya ameupata wapi?
✴️Kwanini alitoka Ufaransa?
✴️Unadhani ilikuwa rahisi kumpindua ALPHA CONDE?

💨Easy Does it

📡Follow me @Eng_Matarra👩‍💻

#MORNING....!!

Hebu Tumalizie huu UZI

Kipindi outbreak ya EBOLA

Hii ilikuwa mwishoni mwa 2013. Upinzani ulitangaza kususia bunge mnamo Januari 20, 2014. Licha ya kuwepo kwa mlipuko wa EBOLA nchini humo, kuliendelea na maandamano na watu 02 walipoteza maisha mnamo Feb 18, 2014.

Kutokana na ripoti ya Waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU) juu ya uchaguzi uliofanyika Sept 28, ambayo ilitolewa Aprili 14, 2014, EU iliondoa vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi kwa serikali ya Guinea. Ugonjwa wa EBOLA uliuwa watu wengi na kupelekea maandamamo kusimama kwa muda.

kwa kiasi fulani hali ya utulivu ilipatikana mpk kwenye uchaguzi mkuu.

#Ripoti zinasema hadi kufikia kufanyika uchaguzi mwingine wa Rais, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), lilikuwa limerekodi visa vya wagonjwa 2,081 na kuthibitisha vifo 453 kutokana na Ebola nchini Guinea.

Ingawa kuenea kwa virusi vya EBOLA kulipunguza sana maandamano nchini lkn visa vya mauaji vilikuwa bado vikiripotiwa.

Kuelekea uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika Oktoba 11, 2015, upinzani ulielezea wasiwasi wao juu ya mchakato wa majumuisho ya kura dhidi ya Tume ya Uchaguzi.

Upinzani ulionya na kulalamika kuwa inahofia kwamba serikali ilikuwa imeiangilia Tume na kuwa ilijiandaa kufanya wizi wa kura.

Licha ya shutuma hizo, wagombea wa upinzani walichukua Fomu za kugombea akiwemo DALIEN DIALLO wa UFDG kutoka chama kikuu cha upinzani, kwa matumaini

kwamba uchaguzi utakuwa huru na utafanyika kwa amani na Oktoba 11, 2015 uchaguzi Mkuu wa Rais ulifanyika. Ripoti zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vya Afrika magharibi, zilisema uchaguzi huo uligubikwa na vurugu, udanganyifu wa kura.

Mnamo Oktoba 14, 2015 Upinzani...

ulitangaza kutotambua matokeo ya uchaguzi huo.

Waangalizi wa kimataifa (International Observers) walikuwepo tangia mwanzo wa mchakato wa kupitisha wagombea mpk kwenye siku ya kupiga kura. Walipohojiwa awali baada ya zoezi la kupiga kura kuisha walisema kulikuwa na kasoro kadhaa.

Waangalizi waliotumwa kufuatilia uchaguzi huo ilikuwa km ifuatavyo:

📋Umoja wa Ulaya (EU) ulituma waangalizi 73, Umoja wa Afrika (AU) ilituma waangalizi 30 kutoka nchi wanachama 18 wakiongozwa na DILEITA MOHAMED DILEITA, Waziri Mkuu mstaafu wa Djibouti

📋ECOWAS nayo ilituma waangalizi takribani 67 wakiongozwa na AMOS SAWYER kutokea Liberia.

#Turudi nyuma: Matokeo yalipotangazwa, Rais ALPHA CONDÉ alionekana kushinda kwa 58% ya kura zote, huku mpinzani wake DALIEN DIALLO akipata 31%.

Ktk uchaguzi huo watu 13 walipoteza maisha.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha UFDG, Dalien Diallo, alipinga matokeo hayo akilalamikia kasoro mbalimbali hasa ktk zoezi la kuhesabu kura.

ALPHA CONDÉ alikula kiapo Desemba 14, 2015 na baada ya kama wiki na siku kadhaa alimteua MAMADY YOULA kuwa Waziri Mkuu wa Guinea.

Awamu ya pili ya utawala wa ALPHA CONDÉ aliangazia zaidi uimarishwaji wa sekta ya madini nchini humo.

#ForYou:Nchi ya Guinea-Conakry ndio ya pili duniani kwa uzalishaji wa madini aina ya BAUXITE, kuna kampuni kubwa kutoka Urusi zimewekeza nchini humo na imeinua uchumi wa Guinea

Miradi ya kufua umeme ktk maporomoko ya maji (Hydro-electricity) ilianzishwa na kusambaza umeme viwandani, ikapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa umeme. Licha ya yote, BADO alikosolewa vikali kwa kutawala kimabavu (authoritarian) huku akishughulikia wapinzani.

Mnamo Machi 17, 2016, Serikali ya China ilitoa msaada wa vifaa vya kijeshi kwa Guinea.

Mwezi Juni Serikali ilitangaza hakuna tena maambukizi ya virusi vya Ebola. Mwaka 2017 walimu walianzisha mgomo uliodumu kwa muda mrefu (Feb19-Sept 15) na iliripotiwa watu 6 kufariki mjini Boke

Mnamo Feb 04, 2018, kulifanyika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo CELLOU DALEIN DIALLO, alilalamikia uchaguzi huo kugubikwa na vitendo vya uchafuzi.

Kati ya mwezi Februari 05 mpaka Machi 14 pia kulitokea ghasia mji mkuu wa Conakry na watu kadhaa waliripotiwa kupoteza maisha.

Kufuatia kuendelea kwa ghasia nchini humo, mnamo Mei 17, 2018, waziri mkuu, MAMADY YOULA alijiuzulu ktk nafasi hiyo na siku tano baadae IBRAHIMA KASSORY FOFANA aliteuliwa kushika nafasi hiyo.

Kutokana na kujiuzulu kwa waziri mkuu, serikali ilikuwa imeanguka kwa mujibu wa katiba

Hivyo, mnamo Mei 27, 2018, ALPHA CONDE aliteua Baraza jipya la Mawaziri, lililokuwa na watu 33, ambapo mawaziri wa fedha, ulinzi na wengine 13 walikuwa wapya.

Hata Tz🇹🇿 ipo hivyo PM MAJALIWA akijiuzulu automatically serikali ya @SuluhuSamia imeanguka, inabidi baraza liundwe upya

Mwaka 2019 ALPHA CONDE alianza mchakato wa kubadili katiba ili kujipa madaraka zaidi na kupelekea upinzani na asasi za kiraia kutengeneza muungano wa "Front National pour la Défense de la Constitution (FNDC)", wakaratibu maandamano nchi nzima kuanzia Okt 14 ili kupinga mpango huo

Mnamo Novemba 08, 2019, mwakilishi wa @UN kwa Afrika Magharibi MOHAMED IBN CHAMBAS alisisitiza kufanyike mazungumzo baina ya serikali na upinzani kumaliza mzozo wa kisiasa.ALPHA CONDÉ aliendelea na mpango wake na Dec 20 alitangaza rasimu ya #KatibaMpya itakayotumika uchaguzi ujao

Rasimu ya Katiba ilimuongezea Rais muda wa kukaa madarakani kwa kipindi cha miaka 6 badala ya MITANO iliyokuwepo zamani.

#Kingine, aliongeza mihula miwili ya utawala ndipo Rais anatoka madarakani, marufuku ya ukeketaji kwa wanawake na ndoa za utotoni ambayo yalipokelewa vizuri.

Zoezi la kupiga kura ya maoni kupitisha Katiba Mpya lilipangwa kufanyika Machi 01, 2020, lkn baada ya waangalizi wa kimataifa kubaini kutokuwepo kwa baadhi ya majina ktk Daftari la orodha ya wapiga kura, zoezi lilisogezwa mbele ili Tume ya uchaguzi ishughulikie changamoto hizo.

Kutokana na sababu zile zile za mwaka 2018, ambapo baadhi ya vyama vya upinzani walisusia kushiriki ktk uchaguzi wa wabunge, hii ilichangia pakubwa serikali kuamua kufanya hivyo hivyo uchaguzi huo, halafu baadae zoezi la kupiga kura Katiba Mpya ndio lifuate.

Maamuzi hayo yalifikiwa kwa kuwa upinzani hawakukubali ile Rasimu ya Katiba.

Mnamo Machi 22, 2020, Uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na wabunge ulifanyika na chama tawala cha (RPG) kilishinda kwa kipata viti 79 kati ya viti 114 bungeni, na watu takribani 10 walipoteza maisha.

Rasimu ya Katiba mpya ilikuja kupitishwa mnamo Aprili 6, 2020.

#KWANINI AMEPINDULIWA?

Chanzo cha ALPHA CONDÉ kupinduliwa kilianzia mnamo Agosti 30, 2020, ambapo chama chake ch RPG kilipotangaza kuwa Rais Conde atawania tena muhula wa 03 uchaguzi mkuu wa rais ujao.

Muungano wa @FNDC_Gn, ulishawishi vyama vyote kususia uchaguzi huo, lkn vyama vyote vilikubaliana na msimamo huo. Wengine walichagua kushiriki akiwemo kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, DIALLO, ambaye toka mwaka 2010 alikuwa akipambana na Rais ALPHA CONTÉ kuwania kiti hicho.

Wafuasi wa baadhi ya vyama vya upinzani, walianza maandamano na watu zaidi ya 50 waliuawa ktk maandamano hayo.

Mauaji hayo yalipelekea kuwepo kwa visasi ndani ya nchi, ikapelekea kuuawa kanali MAMADY CONDÉ aliyekuwa mkuu wa kikosi cha jeshi cha Special Force Group (SFG).

Kiongozi huyo aliuawa mnamo Oktoba 16, 2O20, baada ya watu waliokuwa na silaha walipovamia kambi ya kikosi hicho iliyopo mkoani Kindia

Mnamo Okt 18, 2020 Uchaguzi ulifanyika na Rais Condé alitangazwa mshindi kwa 60% ya kura. Chama cha FNDC kilishawishi watu kususiwa matokeo hayo

Mnamo Okt 19, 2020, DIALLO alijitokeza kupinga matokeo hayo na Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuchaguliwa tena ALPHA CONDÉ na watu 21 walipoteza maisha ktk ghasia za Uchaguzi.
Ktk uchaguzi huo, AU ilituma waangalizi wakiongozwa na DILEITA M. DILEITA, waziri mkuu mstaafu wa Djibouti.

ECOWAS ilituma waangalizi 116 wa muda mrefu, wakiongozwa na JOSE MARIA NEVES, Waziri Mkuu wa zamani wa Cape Verde.

Mnamo Novemba 02, 2020, Dalein Diallo, alifungua kesi mahakamani kupinga matokeo, na wiki moja baadae Mahakama ya Katiba ilimpatia ushindi wa Rais Alpha Condé.

Wafuasi wa upinzani walianza maandamano kupinga uamuzi wa mahakama kuhusiana na kutupiliwa mbali kwa madai ya kiongozi wao na mnamo Novemba 12, 2020, polisi nchini humo iliwakamata viongozi wa vyama, akiwemo makamu mwenyekiti wa chama cha UFDG.

Rais ALPHA CONDÉ aliapishwa kwa muhula wa mwingine wa TATU mnamo Desemba 15, 2020.

Kilikuwa kipindi cha #Corona, hivyo waliohudhuria uapishwaje wake ni watu wachache tu kama mia mbili.

Mnamo Januari 13, 2021, Mahakama Kuu nchini humo iliwahukumu SOULEYMANE CONDE na YOUSSOUF DIOUBATE, wote wanachama na viongozi wa Baraza la Vijana la FNDC, kifungo cha mwaka mmoja mmoja gerezani kwa kosa la kuchochea ghasia zilizohatarisha amani ya nchi.

Rais Conde hakutaka kupingwa, mwaka huu pekee amewafunga viongozi 17 kutoka upinzani. Idadi ya vifo toka mwaka 2020 uanze mpk kupinduliwa kwake juzi ni 43.

Huyo ndiye ALPHA CONDÉ, mwenye miaka 83 na aliyeanza kuongoza Guinea kwa matumaini lkn baadae akageuka na kutawala mabavu!!

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling