JAPHET MATARRA Profile picture
Father l Husband | Human Right Activist | Mineral Processing Engineer @JSPLcorporate |#Paralegal | Member @ChademaTz | #ManUTD |~Boss Himself | 💨StoryTeller💣

Sep 26, 2021, 17 tweets

PUTIN ANAVYOPINDUA VIONGOZI WA AFRIKA KUJIIMARISHA

#UZI:

💨Rais Alpha Conde (Guinea) alipinduliwa kwa msaada wa USA & Ufaransa, lkn kwa ASSIMI GOÏTA (Mali) alisaidiwa na Urusi.Pia mauaji ya IDRIS DÉBY (Chad) yalifanywa na URUSI
👩‍💻𝐌𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐌𝐚𝐳𝐢𝐭𝐨 𝐓𝐮𝐬𝐢𝐲𝐨𝐲𝐚𝐣𝐮𝐚👇

Mnamo Aprili 20, 2021 majira ya jioni zilianza sherehe huko La Brasserie Kiss, umbali wa 100M kutoka ktkt ya mji wa Bangui (Afrika ya Kati). Kila aliyepita huo mtaa aliona magari kadhaa yamepaki mbele ya nyumba moja ya Ghorofa 3, jumba ambalo ni kivutio kikubwa sana ktk jiji hilo

Jengo hili lipo nje kidogo ya mtaa maarufu wa DU COLONEL CONUS na ikifika usiku hupendeza sana kutokana na mng'ao wa taa ulioizunguka. Kulingana na saa kule ilikuwa mida ya saa 2 usiku hivi na kwa wenyeji wa mji huo, ni muda ambao amri ya kutotembea usiku huanza kutumika.

Siku hiyo watu fulani hawakutaka kuondoka ili wahudumu wafunge.

#Naam...!!!

Siku hiyo watu fulani hawakutaka kuondoka ili wahudumu wafunge.

Kanali VASSILI, mutu ya pamba kali, Mzee wa kuwaka na mvuvi wa watoto wazuri mjini kama @BarakaSaimon3, basi naye alialikwa ktk sherehe hiyo na alikuwa ametupia nguo za kiraia ukimuona huwezi kumjua.

KANALI VASSILI NI NANI?

#Inshort:Ni kijana mdogo raia wa Urusi, anapenda sana raha, pombe kwake ni kama maji tu.Unaambiwa pia mara nyingi akiwa na gari lake la kivita ndani ya mitaa ya jiji hilo, hujiona km yupo Moscow

Yaani huwa hajali sana vizuizi vya traffic akiwa barabarani

Akiwa na wine yake aligonga glasi kadhaa kufurahia kifo cha Rais IDRISS DÉBY ITNO wa Chad, ambaye alikuwa amefariki siku 02 zilizopita. Wenzake hawakufurahia hali hiyo ingawa hawakuhusika na mauaji yake. Walifadhaika sana na ilionekana ni kukosa heshima kusherehekea kifo chake.

Licha ya kuwa Kanali huyu alikuwa akifurahia hafla hiyo akiwa na marafiki zake, Lkn alikuwa kazini na simu yake ilimkumbusha km mara 02 hivi

Mtu wa kwanza aliyewasiliana naye usiku huo alikuwa Rais FAUSTIN-ARCHANGE TOUADÉRA wa Afrika ya Kati na alitaka kufahamishwa habari fulani

Rais TOUADÉRA alitaka kujua vikosi vya Urusi vilikuwa vimefikia hatua gani kwenye operation zao dhidi ya kikundi cha Coalition of Patriots for Change/Coalition des Patriotes pour le Changement (CPC).

Kikundi hiki cha CPC ni muungano wa vikundi kadhaa vinavyojiita vya wazalendo!!

#CPC ni kikundi cha waasi na kinaongozwa na FRANÇOIS BOZIZÉ YANGOUVONDA, aliyekuwa rais wa nchi hiyo miaka 10 iliyopita (2003/2013).

#BOZIZÉ alimpindua rais wa zamani ANGE-FÉLIX PATASSÉ akiwa ameenda Niger. Mnamo 2013, naye alipinduliwa na waziri mkuu TOUADÉRA aliye madarakani.

Kikundi cha CPC kiliundwa mwaka jana 2020 na kuvuruga uchaguzi mkuu wa 2020/21 nchini humo.

Kanali Vassili ambaye jina lake kamili halijulikani kabisa, ndiye amepewa kazi ya kupambana na CPC na ni mmoja wa viongozi wa kampuni ya WAGNER yenye Mercenaries na makomando wa kivita.

Kikundi cha CPC nitakielezea baadae kuanzia
📡Kuanzishwa
📡Uongozi
📡Operation n.k

Pia kampuni ya #Wagner nitaichambua kwa undani zaidi kadri tunavyoenda na huu Uzi, #muhimu ni kufahamu kuwa inaendeshwa na Tajiri wa Urusi rafiki na swahiba #01 wa Rais VLADIMIR PUTIN wa URUSI

Kanali VASSILI alikuwa amezoea kuzungumza na TOUADÉRA na haraka alimjibu na kumhakikishia kuwa kikosi chake bado kina nguvu

Aliongezea kuwa, Jeshi la nchi hiyo ambalo mara nyingi ndio huwekwa mbele karibun litasonga zaidi na punde litadhibiti maeneo yanayoshikiliwa na waasi hao

Kisha baada ya mazungumzo hayo alikata simu na kurudi kunywa wine 🍷 yake

🎼Sherehe ziliendelea ingawa kulikuwa na amri ya kutotoka nje usiku. Yote kwasababu kiongozi huyo wa kijeshi toka Urusi alikuwa maarufu sana kiasi kwamba uwepo wake tu Club hiyo iliruhusiwa kuvunja sheria.

Lkn unaweza ukajiuliza KIJANA huyu ni nani?🤔

💨MTU ambaye anaogopeka kwa karibu watu wote Jijini Bangui mpk sheria zinavunjwa!!

📡Kijana ambaye ana mawasiliano ya moja kwa moja na rais, na ni kiongozi wa ngazi ya juu wa Kampuni ya WAGNER huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.!!

📡Je, ndiye BOSS wa WAGNER huko Afrika ya Kati? kampuni ambayo kwa mujibu wa vielelezo inaonekana haina LEGAL STATUS huko Urusi!

💨#Wagner ni nani?

💨#Kanali VASSILI ni nani?

💨#Wagner imefikaje nchini humo, kufanya nn?

Maswali yote hayo + mengine tutapata majibu hapa chini👇

#Inshort:WAGNER iliingia nchini humo miaka 03 iliyopita

Kwann ina nguvu sana serikalini?
Ni Kwa7bu ilipenyeza watu wake ktk nafasi za uongozi ndani ya nchi hiyo

Sasa kabla hatujaenda huko...

📡Tuingalie kwanza mauaji ya Rais IDRISS DÉBY (Chad) & connection na #Wagner (Putin)👇

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling