My Authors
Read all threads
#UZI
💨 MWAMBA ALIYEVUJISHA SIRI ZA UDUKUZI WA MAREKANI

✴ Ni matokeo baada ya shambulizi la Osama 9/11 pale Marekani.

✴ Marekani yamfungulia kesi ambayo hataruhusiwa kuongea ni kifo tuh.

✴ Urussi ya mwambia chakula, malazi n.k sisi tutakupa.
#FLowMaTaTa shuka nayo 👇👇
✴ Twende chap chap
• Baada ya shambulizi la Osama pale Marekani 9/11. Marekani ilijilaumu sana, Kwanini nchi kubwa kama yeye ashindwe kupata taarifa mapema la hilo chambulio?

✴ Ikabidi sasa NSA na CIA wakae chini na kuja na project ya Surveillance ya kunakili data za
✴ za mawasiliano yote ulimwenguni, ili siku ukipanga njama za kuidhuru Marekani wakugundue, watajua watakavyo-kuzibiti mtoto mdogo wewe.

✴ Kuna Jamaa mmoja hivi ni bwana mdogo sana, umri wake nitakutajia ni bwana mdogo sana. Alifanikiwa kupata kazi NSA.

✴ Sio kwasababu
✴ Alifanyiwa interview akafaulu hapana. Familia yao ni kizazi cha serikali, Babu yake alikua anafanya kazi kule Pentagon, baba askari, mama secretary n.k.

✴ Jamaa jina lake ni EDWARD SNOWNDEN (39) ni kijana ambaye alikua anapenda sana mambo ya computer. Familia ikampa shavu
✴ Akapata kitengo NSA (Nashino Sequriti agensi). Alifanya kazi kwenye ofisi zao pale Marekani kwa muda kidogo kisha akapelekwa Uswisi kwenda ku-spy mambo ya Nchi. Alifika kule akawa anafanya kazi ya kurepea computers za CIR na UN ndio kazi yake.

✴ 2009 akaacha kazi NSA.
✴ Dell wakampa shavu. Kumbuka NSA inatumia computers za kampuni ya Dell. Kwaiyo aliacha kazi @bajabiri alafu @JustFittz wakampa kazi. Kwaiyo kisu ni kile kile.

✴ Bwana mdogo akapelekwa kwenye ofisi za NSA huko Japan kwenda kuwafundisha wanajeshi
✴ jinsi ya kujikinga na ma-hacker kutoka kwa maadui zao.

✴ Kwenye ofisi za NSA Hakuna mtu anayeeuhusiwa kuingia na flash labda yeye tuh. Mambo aliyokua anayaona yakifanyika nafsi inamsuta anajiuliza kwanini nisiwazamishie tuh utambi? Hii kufuatilia nchi za watu imekithiri sasa
✴ 2012 akakopy documents kama million 1.7 hivi alafu akaacha kazi. EDWARD huyo na anajua ni kosa ataweza kupelekwa mahakama ya kijeshi we muache tuh.

✴ Mwaka huo akamtafuta mwandishi wa The Guardian Bw. Gleen 😂, akamtumia program yake spesho ya kujiepusha na ma-hacker
✴ Akamwambia ai- install kwenye computer yake kuna kataarifa kazito anataka kumpenyezea. Mwandishi Gleen akampotezea akamuona hii nyau tuh haina jipya.

✴ Stellingi wetu ikabidi hamtafute rafiki yake na Gleen huyu ni Laura wa New York times kumbuka The Guardian ipo Uingereza.
✴ New York times ipo Marekani. Jamaa akafanikiwa kumpata akawa anamuomba amshawishi bw. Gleen amwambie kua ana taarifa za siri. Gleen akashawishika akakubali.

✴ Wakaanza kuwasiliana kwa kutumia Verax ambayo ni ngumu ku-hack wakatumiana email
✴ kibao wakakubaliana na siku ya kukutana.

✴ Stellingi wetu Edward Snowden akaomba likizo kwamba yeye ni mgonjwa akapanda ndege akaenda Hong Kong ilikua May 2013. Akaenda kwenye hotel moja hapa Hong Kong The Mira Hotel.

✴ Akiwa na documents kama million 1.7 mkononi
✴ Za Serikali ya Australia 15,000 za Serikali ya Uingereza 58,000 na Nchi nyingine kubwa kubwa naona na za kwangu alikua anazo aishi miaka mingi.

✴ Bw. Gleen wa The Guardian pale Uingereza naye akapanda ndege moja kwa moja Hong Kong kubeba secret data
✴ alikua ameambatana na yule mwandishi wa New York times na mtu mwingine tena.

✴ Jamaa alikua ashakaa wiki mbili pale hotelini akawapa wakina Gleen location ya sehemu alipo, kumbuka hata sura yake hawaijui akawaambia watamuona ameshika kidude flani hivi vile vya kupanga rangi
✴ Wakamuona akawapeleka chumbani kwake, alivyoanza kuwasimulia walistaajabu sana bwana mdogo hivi ametoa wapi akili zote hizo?

✴ Aliwaonyesha program zinazotumiwa na Marekani kudukua taarifa za nchi kubwa na za kwetu sisi wa kilosa.
• Black peark- inadukua mawasiliano ya
✴ Viongozi wakubwa wa nchi kama 120+ duniani.
• GCHO- Hii ina-spy taarifa za siri za Uingereza.
• Love int- inakusanya taarifa ya vile unavyokipenda ili siku wakikutaka wavitatumia vile vitu kukukamata. We kama unakesha huku mtandaoni kuangalia ushetani shauri yako.
✴ Zote hizo zipo chini ya PRISM ya NSA.

✴ Mwandishi Gleen akareport kama Mtu wako wa nguvu anavyoreportigi habari zake. Bahari zikaenea duniani kote. Marekani ikachafuliwa ikachafuka sana sana sana sana. Hawakudeal na mtoa habari wakadeal na chanzo cha habari.
✴ Yaani mpaka Angel Mark chancellor wa Ujerumani akasema urafiki ni urafiki ila sio huu wa kufuatiliana.

✴ Marekani ikagundua source ni nani, Stellingi akajulikana yule mwandishi Gleen alikua anajua Jamaa anajiingiza kwenye matatizo ila Jamaa yeye hakutilia maanani sana.
✴ Marekani ikajua yeye Ndio kavujisha siri za kambi ila hawakujua yupo nchi gani.

✴ Polisi mmoja ndio aligundua Jamaa yupo Hong Kong kutokana na taa ambazo zilikua nyuma yake wakati anafanyiwa interview
✴ Kikosi kazi kikatumwa Hong Kong kwenda kumchukua raia wa Marekani anayetakiwa na nchi yake.

✴ Bw. Gleen akamtoa Jamaa kwenye ile hoteli, Jamaa akapelekwa mtaani akawa anaamishwa nyumba moja moja Marekani wakashindwa kumpata.

✴ Master mmoja mmiliki wa website ya
wikileaks.com website inayovujishaga siri nyingi za dunia. Akamtuma presenter wake wa Hong Kong amtafute Stellingi dakika 0 Jamaa akapatikana.

✴ Assange alikua anataka apenyezewe taarifa zaidi.
✴ Snowden akatafutiwa nchi ya kukaa kama Mkimbizi maana kurudi Marekani ishakua msala. Maombi yalitumwa nchi kama 20 hivi Ecuador ndio ilimkubalia nyingine zikakataa si mnaujua mziki wa Marekani??.

✴ Airport akapitishwa kiwizi wizi ikabidi apande ndege ila lazima apitie Urussi
✴ Maana hamna root ya kutoka Hong Kong kwenda Ecuador moja kwa moja.

✴ Alivyofika Urussi ile anataka apande ndege nyingine aende Ecuador akaambiwa hana passport, Marekani ishaidelete 😂 sasa jiulize pale Hong Kong ilikua bado haijadeletewa?.
✴ Marekani akasema China akailalamikia China kwamba imempitisha kimakosa kwani passport yake ilikua ishazuiliwa.

✴ China ikasema nyie mmezuia passport ya EDWARD J SNOWDEN na sio ya EDWARD JAMES SNOWDEN.

✴ Urussi akamkaribisha mgeni kutoka kwa rafiki yake Marekani.
✴ Urussi amempa Nyumba nzuri, chakula kizuri, kiyoyozi fulu aisii na kashalika kijana wa watu amekosa nini mpaka akimbilie Marekani ambapo amefunguliwa keshi ambayo hataruhusiwa kuongea ni hukumu tuh.

✴ Kesi za kiivyo sio nzuri rafiki 😁. Waziri wa mambo ya nje wa Urussi
✴ alipost Facebook kwamba SNOWDEN aishi miaka mingi Urussi maana aliifadhiwa kwa muda tuh.

✴ Marekani anahofia kwamba Jamaa alisema na siri za jeshi lake. Putin naye anasema hajawai ona kijana smart kama huyu😂.

MWISHO
Written by @njiwaflow
Naomba RT yako rafiki.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Njiwa FLow

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!