My Authors
Read all threads
ISHI NA WATU KWA KUFUATA TARATIBU HIZI.

1. Usimpigie mtu simu kwa zaidi ya mara mbili mfululizo. Ukishaona simu yako haipokelewi basi elewa kuna sababu ya msingi acha subiri akupigie pindi atakapoona ulimtafuta. Image
2. Rejesha pesa ulizokopa bila kusubiri kukumbushwa na aliyekukopesha. Hiyo inaonesha uadilifu wako na tabia yako. Vivyo hivyo rejesha mwamvuri, peni, kitabu au chochote ulichoazima hata kama kidogo usisubiri kukumbushwa
3. Usiagize chakula cha gharama kubwa pale unapotolewa out na mtu. Ikiwezekana mwombe akuagizie mwenyewe au shauriana naye chakula gani unaweza kuagiza
4. Usiulize maswali yenye ukakasi kama "Hee bado hujaolewa/hujaoa tu? Au " he! Hujapata mtoto tu?", "he! Hamjajenga tu? " Mwee bado tu hamjanunua gari?" Kwa kifupi ni kwamba hayakuhusu mhusika akipenda mjadili hilo ataanzisha mwenyewe.
5. Ikitokea unaingia mahali na kuna mtu anakuja nyuma yako ni vizuri ukamshikia mlango bila kujali umri au jinsia yake. Haikugharimu lolote kuonesha unajali.
6. Mkienda mahali na rafiki yako na akalipia usafiri au chakula basi jitahidi nawe kulipia zamu inayofuata usipende kupokea tu.

7. Kubaliana na mitazamo tofauti kumbuka 6 kwako inaweza kuwa 9 kwa aliyekaa upande mwingine. Mawazo ya ziada ni mbadala mzuri.
8. Usiwakatishe watu wanapokuwa kwenye mazungumzo yao mfano kwenye kundi kubwa la watu wao wamejitenga pembeni wawili wanaongea jambo fulani wewe unajiingiza kwenye mazungumzo bila samahani na bila kukaribishwa
9. Ukimtania mtu akaonesha kutofurahia acha mara moja na usirudie tena kumtania.

10. Sema Asante mtu anapokusaidia jambo lolote.

11.Msifie Mtu hadharani, mpinge faraghani
Mpe mtu heshima yake mbele za watu na umseme baadae
12. Unapokutana na mtu huna sababu ya kukosoa uzito wake "hee mbona umenenepa hivyo?" Au "Mbona umekonda sana?" Hayakuhusu akitaka kukueleza mwenyewe atakueleza wewe unatakiwa kusema tu "Umependeza.
13. Mtu anapokuonesha picha kwenye simu yake usianze kwenda kushoto au kulia ili kutazama picha zingine ishia hiyohiyo anayokuonesha huwezi jua picha gani inafuata
14. Mtu anapokuambia anakwenda hospitali usianze kumuuliza " una tatizo gani?" Haikuhusu akitaka atakuambia mwenyewe
15. Mheshimu mfagizi kama unavyomheshimu boss maana heshima ni kitu cha bure.

16. Ongea na mtu huku unamtazama machoni sio kuwa bize na simu yako au kutazama pembeni.

17. Usitoe ushauri wowote kama hujaombwa kufanya hivyo.
Asante
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Sultan M N Y A L U 🇹🇿🇹🇿🧚‍♀️🧚‍♀️

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!