My Authors
Read all threads
SIKUMPENDA NILIMTAMANI TU ILA ALIKUFA KWAAJILI YANGU
—————————————
PART 2 👇
Tulipoishia ni pale nilimpo mpgia Irene simu na ikawa inaita
“Tiii tii tiii#
Nilijikuta natabasamu kwa kitendo cha simu kuita! Iliita na hatimaye ikapokelewa
“ Helo, habari za kwako Irene”
Nikachombeza
“Salama tu! Mimi wa afya sijui naongea na nani!” akajibu Irene huku akiuliza
“Naitwa Franco, unakumbuka tulikutana kwenye interview!”
nikajibu kwa sauti ya kiume
“Ohh nimekumbuka! Franco jina lako zuri sana! Vip interview imeendaje!?” Irene akanijibu kwa madaha
@mpambazi_
“Imeenda vizuri japo nahisi nimevurunda! Najua Irene ndio utapita bila shaka” nikasema.
“Hahaa! Hapana bwana we ndio itakuwa umefanya vizuri zaidi yangu! Actually mimi nimeenda tu kujifunza interview ikoje ila nikipata sawa na nisipopata pia hakuna shida kabisa” akajiibu Irene
Jibu lake lilifanya nijione mimi ninashida sana! Wakati mimi nikitia mkazo kwenye kupata kazi Irene yeye anaenjoy tu kujifunza interview! The world is not fair and won’t be fair, nikajikuta nawaza sana! Tukaongea mengi huku kila mtu akisema mwenzake ndio atashinda interview!
Story zikahama mpka tukajikuta tunaambizana habari za vyuo na mambo mengi ya maisha! Story zikawa tamu mfanowe hakuna! Wivu tu wa mtandao wa simu ukakatisha mazungumzo yetu eti kwa kisingizio cha kuisha kwa dakika! Simu ikawa imekatika na tukahamia kwenye kuchati sana
Katka kuzoeana kule ikabidi nimweleze kibano na kifinyo nilichapata kutoka kwa wahuni! Akanambia nisikae tu bila kwenda hospital labda huenda nimeumia majeraha ya ndani kwa ndani! Licha ya kukukataa kutoumia bado alisisitiza ni lazima niende hospital! Lait angejua kuwa sikuwa
na hiyo fedha ya hospital wala asingesumbuka kunilazimisha vile! Baada ya kuona juhudi za kunishawishi niende hospital hazizai matunda akasema jioni ile ile nijiandae twende hospital! Nilikataa mno ila akasisitiza kuwa ni lazima twende na kunipa dakika 30 tukutane sehemu!
Sikuwa na namna zaidi ya kukubali! Kwanza nauli naitoa wapi!? Gharama je itakuwaje!? Mwisho ikabidi niombe nauli kwa majirani na kuwahi chap nikiwa na nia tu ya kumuoa Irene kisha nimpige chenga wala nisiende hospital maana sina pesa! Nikajiandaa na kwenda sehemu ya makutano yetu
Kufika nikabaki kuangaza huku na kule! Sikumuona mtu! Muda nao uliyoyoma kweli kweli! Nikiwa katika kuzubaa, si ghafla bin vuu Irene huyu hapa! Alivaa kwa heshima kweli! Alipendeza mno! Akanisogelea hapo ndio pua zangu zikapata harufu ya marshi na unyunyu murua aliojipulizia
Baada ya salamu fupi, huku nikimshangaa kwa kupendeza sana akaniambia twende! Kwa jinsi nlivyokuwa nimevaa sikuona km nafaa kuongozana nae! Naenda wapi!? Mbona sina hela!? Kwanini nisimwambie sina hela ikajulikana moja!? Halmashauri ya kichwa changu ikawaza huku nikipiga hatua
“Una mawazo sana Franco! Pole sana usiogope nitakusaidia” Irene akavunja ukimya
“ Asante Irene! Nisiposema ukweli nitaonekana sifai! Irene tunaenda hospital ila mimi sina pesa kabisa” ili bidi niseme tu ukweli! Mficha uchi hazai na mficha maradhi kifo humuumbua! Sikutaka kuumbuka
huko mbeleni nikasema ukweli
Jibu lake likawa rahisi “we twende tutajua mbele ya Safari” Hatua zetu zikatufikisha sehemu ambapo taksi zilipark! Akaongea na dereva! Tukaingia na safari ikaanza kwa kukatiza mitaa kadhaa. Safari yetu ikaishia kwenye hospital nzuri na maridhawa kabis
“Orbit Hospital, your health is our concern” yalisomeka hivyo maandishi ya kibao cha hosptal! Tulishuka baada ya dereva kulipwa ujira wake tukaongoza moja kwa moja ndani! Irene alikuwa connected kwani nilipokelewa kifalme na bila kupoteza muda jopo la madkatri wakawa mbele yangu
Vipimo vilifanyika kwa ustadi mno! Ikabainika sikuwa nimeumizwa sehemu yeyote labda tu michubuko iliyokuwa kwenye mikono na magoti kutokana na kupigwa mitama mchna ule!
Hatukukaa sana tukaruhusiwa! Sikujua hata bei ilikuwa shingapi! Yote aliyafanya yeye Irene! Hakika nilikuwa
nimebarikiwa kukutana na Irene!
Lakini kwanini nilimfanya mpka akajiua licha huu wema wote! Najuta kweli wakati nikiandika hapa! Nina dhambi kubwa mno, moyo wangu una huzuni kuu, sisitahili msamaha
Tulitoka hospital na jua lilikuwa likizma! Irene alinisihi niende home nipumzike
akiahidi kama atapata nafasi basi kesho atakuja kuniona! Hakuishia hapo akaniachia kiasi kadhaa cha fedha! Nilimshukuru mno, kwakeli nilimuona Irene kama ni malaika aliyekuja kwa Wakati sahihi maishani mwangu!

Alinijali ndani ya muda mfupi niliokutana nae! Japo hatukuwa marafiki
ila km angetokea mtu kwa ule muda akaona jinsi ninavyojaliwa basi angejua sisi ni marafiki wa enzi na enzi

Kunijali kwake kukafanya nizidi kuwaza mbali! Kichwa kile cha pili kule chini ya miguu kikawa kinavimba kila nilipochat ama kuongea na Irene! Tamaa ikanikamata! Ama kweli
tamaa ni ujinga! Muda wote nikajikuta nawaza kama nitapata nafasi nimfunue Irene! Umbo lake la kuvutia, miguu yake ya kujaa, kiuno kilichokaa vema kwenye bambata la tumbo lake! Usisahu macho yake makubwa na ngozi yake yenye mvuto! Hivi vyote vilifanya nizidi kumtamani mno Irene
Nilifika nyumbani na muda wote tukawa tunachati! Si unaujua sisi wanaume wazee wa mipango! Kila chat yangu ilikusudia kumuweka karibu Irene! Ni kweli ilikuwa hivyo! Alionesha kunielewa nikiingia kwa gia ya kutaka urafiki wetu ufike mbali
Zaidi nikamuomba kesho anitembelee na aka
niahidi kuja ikiwa tu angepata upenyo! Ina maana kwao ni geti kali!? Ina maana analindwa!? Mbona simuelewi! Nililala huku nikitamani kukuche ili tu Irene aje!

Kokorikoooo! Ewaaa asubuhi hii hapa kumekucha! Cha kwanza kabisa ilikuwa kumtext Irene na baada ya salamu akiniambia
saa 7 mchana atakuja hivyo niwe tayari kwenda kumpokea!
Ohh huyo nampata kilaini! Nikajipongeza kwa kujipiga ngumi kifuani! Ugumu wa maisha nikausahau kabisa! Tamaa ikaniteka nikawa namwaza tu Irene
Unaambiwa nilifanya usafi kila mahali, uvunguni mwa kitanda mpka juu ya dari!
Chumba kilidekiwa, vyomba vikaoshwa, sufuria zikasuguliwa! Vitu vikapangwa kwa ustadi sana!
Mpaka majirani walishangaa heka heka zangu! Chezea ujio wa Irene wewe!?
Masaa yaliyoyoma kweli! Saa 5 hii hapa! Nikapata breakfast na kuoga kisha nikajipendezesha kwa kuvaa vizuri sana
Nikatoka na kununua juice fulani amzing ili mtoto akifika ajipoze koo! Si unajua sio mtoto anafika ndio unaanza kuhaha!
Ila mimi mjinga kweli! Maandalizi yote haya ya nini wakati hatujakubaliana kama kuna kamchezo!? Ona nilivyo mpuuzi! Akikataa je!? Noo! nitafanya lolote lile
nitulize rungu, nilijiwazia kwa kubishana mwenyewe ! Muda haugandi!
“Tiiiiii tii tiiiiii” kiswaswadu changu kikaita! Kucheki mpigaji ni yeye yule Irene! Ewaa
“Helo Irene” nikasema
“Abee Franco! Unahamu nije ila mwenzio nimeshindwa kuja”
“What the F***k” nikaropoka
“Am joking,
Qam on my way, plz come to pick me up where we meet yesterday” akaongea kimombo fulani, mtoto alijua kunirusha roho huyu! Sauti yake sasa, mashetani yote yalinisisimka mwilini
Huyo fasta kwenda kumpokea Irene
***
Part 3
Usipange kukosa
Retweet
Comment
Folow 🔔 @IamFranco92
Njoo msome part 2 wakati tukisubiri part 3 na 4 zenye uchungu Mwingi mno

Tamaa mbaya sana
Usisahau kuretweet na ku nifolow @IamFranco92
@IamFranco92
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Sultan M N Y A L U 🇹🇿🇹🇿🧚‍♀️🧚‍♀️

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!