Kuduishe Kisowile Profile picture
Aug 27, 2020 24 tweets 5 min read Read on X
Nimeketi kitandani, nikatazama picha hii, nikatabasamu.
Hakika ni sanaa iliyofana.
Kwanini picha hii? tena ambayo bado haijakamilika?
Hayumkini ni kwasababu imeakisi utu wangu, ya kwamba mimi si mkamilifu.
Natazama nilipotoka. Nashusha pumzi. Natabasamu. #UZI
#DaktariMwandishi Image
Kwa sababu fulani, machozi yananilenga.
Nafumba macho. Taa zimezimwa. Chumba kipo kimya. Wenzangu wawili wametoka, mmoja amelala, siku yake haikuwa njema.
Sauti ya pekee ni ya feni inayozunguka kutupunguzia joto la jiji hili.
Navuta hisia. Mawazo yanarudi nyuma. Kumbukumbu
za tangu nikiwa mdogo. Nikiwa nisiyejua ya dunia. Nakumbuka kisiwani Mafia, rafiki yangu mzungu Samantha, na mdogo wake, Christopher. Najiuliza, wako wapi? Nawakumbuka Dorothea, Geo, Mselo, Mlekwa na Waziri. Namkumbuka Mama Mchungaji, alikuwa mwalimu mkuu wangu chekechea, alikuwa
wa kwanza kuniamini. Na kunionyesha kuwa, wanawake wanaweza.
Naikumbuka siku tuliyoenda mnarani na Marehemu mamamdogo Stella, ilikuwa mara ya mwisho kumuona hai. Nayahisi machozi yakitiririka mashavuni mwangu. Namkumbuka sana.
Naikumbuka siku ile tuliyohama, tulipoiaga Mafia.
Giza limetanda machoni mwangu. Nimezama kwenye mawazo. Nakumbuka Lushoto, kama mkanda wa video, nakumbuka nikiwa na binamu yangu Mamy, tumebeba viroba vya majni ya ng'ombe, mifagio, vidumu na mabegi yetu tukielekea shuleni asubuhi. Baridi ikitupiga, tunakaza mwendo kuwahi namba.
Nawakumbuka Zuhura, Frank Yuda, Elieza(Mungu ailaze roho yale mahali pema peponi) na Abubakari. Hawa tulicheza nao sana harusi. Nanong'ona, "Eeh Mungu, walinde huko walipo."
Naikumbuka siku tuliyohama Lushoto. Nilivyolia kumuacha binamu yangu kipenzi, Mamy. Safari ya Namtumbo.
Nakumbuka siku mama aliyonichapa kwasababu nilienda kuangalia mpira hadi saa moja usiku. Shule yetu ilikuwa inacheza na shule ya Rwinga. Nilirudi sauti imekauka kwa kushangilia. Vumbi jekundu la Namtumbo limejaa hadi kichwani. Nacheka ninapokumbuka hasira za kuchapwa.
Namkumbuka rafiki yangu Mabaga, Kasimu Rehani, Mwajuma, Shufaa, Nasorro Kipa, Yasini, Zuberi, Rama Madevu, Issa Kiduchu, Jafari, Mabula, Maisha, Shamira na wengine wengi. Eeh Mola, walinde, watimizie haja za mioyo yao.
Nakumbuka siku tulizocheza rede, kipindi cha mfungo wa
Ramadhani. Na siku zile za kutisha. Nyakati ambazo wavulana walipewa jukumu la kutusindikiza kuhakikisha kila msichana amefika kwao, kwasababu kulikuwa na watu wanakata matiti na sehemu za siri za watoto wa kike. Akili inaganda kidogo, nawaza namna gani ule upepo ulipita ukapotea
Alhamdulillah, hilo liliisha.
Naikumbuka siku ya kwanza sekondari, nikiwa nimetoka shule ya serikali, kijijini. Namna nilivyokuwa nikiwashangaa wale wa St.Mary's. Nakumbuka nilivyoumwa. Pumu ya ngozi. Najihisi nimeketi kitandani kwangu, bweni la Bibi Titi, nikitazama vidonda
vyangu, nikikumbuka maneno ya mwenzangu aliyenikataza nisiguse kitu chake, nitamuambukiza. Nakumbuka nilivyokuwa nikijitenga na kuketi nje ya darasa. Nakumbuka siku nyingi nilizolia. Nilizomuuliza Mungu, kama kuna kitu nimemkosea akanipa ugonjwa huo. Nakumbuka nilivyojishuhudia
nikipoteza kujiamini. Nikiuchukia mwili wangu. Kila nilipoamka na kuona vidonda baada ya kujikuna usiku kucha. Siamini kama sasa, ni miaka imepita tangu kupatwa na attack ya pumu ya ngozi.
Machozi yanatiririka mashavuni mwangu. Ni machozi ya maumivu na furaha. Makovu ya kihisia
bado mabichi. Bado najifunza kujipenda upya. Kujiamini. Kuyakubali makovu yangu kama sehemu ya maisha yangu.
Namkumbuka rafiki yangu mpenzi, Liz-Mindy, tumekuwa marafiki miaka 11 sasa. Naye ameyapitia hayo ya pumu ya ngozi.
Nakumbuka nilipomwambia, "mbona yako ina afadhali?
mwenzio nipo kama chui"
Nafuta machozi mashavuni. Natabasamu. Macho yangali yamefumbwa.
Kumbukumbu zinanipeleka Mazinde. Siku za kusimamia usafi, kwa nguruwe, siku za kuandaa mahafali na siku zote nilizoshinda nikisubiri kwa hamu kuona basi la Shambalai ili nilishangilie.
Ni kama filamu, nipo Maramba. Churwa, shambani na ndoo yangu navuna mahindi. Napeleka, annaisimamisha CO Meja Ngairo, ananiambia nirudi kujaza ndoo mahindi. Naondoka, nazama shambani, sirudi. Nalala kusubiri filimbi ya chakula.
Nakumbuka usiku wa madoso na chenja. Walionishika
mkono kwenye mabio. Nawakumbuka maST wenzangu. MaMTM nilipokuwa nawaoshea vyombo na kuwapigia kiwi. Nakumbuka namna ule wimbo wa, "Zaina Zaina (Zaina), Zaina mtoto (Zaina), mtoto wa kidigo (Zaina), lete raha (Zaina)", ulivyokuwa unaisuuza roho yangu na kunipa morali kukimbia.
Naikumbuka siku ya kwanza Kairuki, nikimbembeleza Hostel meneja anipe chumba. Nakumbuka mama alivyonisindikiza hadi chumbani na kunitandikia kitanda. Tukakaa. Moyoni siamini kuwa ndio safari ya udaktari imeanza.
Nayasikia machozi ya furaha yakinilenga. Ni miaka minne iliyopita.
Nakumbuka siku ya kwanza wodini. Sikujua niongee nini na mgonjwa. Nakumbuka siku ya kwanza mtoto alipofariki. Nililia usiku kucha. Nakumbuka nikiwafuata nyuma interns wanifundishe. Nikiwasumbua hadi wanakubali niende nao. Nacheka. Natabasamu
Nashtuka, mkanda wa kumbukumbu umeisha
nipo wakati uliopo.
Nafikiria research, mitihani na mipango yangu ijayo.
Naifikiria biashara yangu changa.
Nawaza kama nitaendelea kuandika makala magazetini. Je, nitakuwa daktari mzuri? Lakini, yafaa nini kuhofu kuhusu yajayo?
Septemba 11, 2016 asubuhi nalikuwa nikiwaza matokeo
yangu ya mwaka wa kwanza. Jioni yake, nilikuwa nimelazwa Bochi, nikipigania maisha yangu baada ya kunywa dawa ambayo bahati mbaya ime-expire. Naikumbuka vema siku hii. Namna nilivyokosa pumzi. Nilivyolia sababu kifua hakikuweza kuingiza wala kutoa hewa. Nilionja kifo. SITASAHAU
Ya nini kuhofu kuhusu yajayo sasa? Mwenyezi Mungu afahamu hayo.
Nafumbua macho yangu na kuona namna safari ya maisha yangu imenipeleka mbali na kunifundisha mengi. Natabasamu. Hakika tunatoka mbali.
Tunavuka mabonde na milima.
Tunaanguka. Tunakata tamaa. Tunaumizwa. Tunajutia.
Tunafurahi. Tunajifunza. Tunasamehe. Tunabariki. Tunapenda. Tunapendwa. Tunalaani. Tunabeba vinyongo. Tunaendelea kutobu vidonda.
Yote ni maisha.
Kwenye chumba cha marehemu Babu yangu, Dr.Nasetsi alikuwa na kikaratasi kimeandikwa, "MAISHA NI NINI?"
Nilikuwa nimekariri yote lakini
kwasasa nakumbuka haya tu:
"Maisha ni SAFARI, JARIBU.
Maisha ni WAJIBU, TIMIZA.
Maisha ni FUMBO, FUMBUA.
Maisha ni ZAWADI, IFUMBATE.
Maisha ni MAPIGANO, PIGANA."

Tazama ulipotoka, yaelewe mazuri na mabaya, vicheko na vilio, hasira na furaha, maumivu na raha uliyopitia.
Yatumie hayo kusonga mbele.
Andaa mpango wa yajayo. Furahia wakati uliopo. Jenga yaliyopo mbele yako.
Kwasababu, hakika maisha ni FUMBO na maisha ni SAFARI.
Nimeandika mengi. Nikuage kwa maneno ya Samba Mpangala akisema, "Dunia tunapita, kila kitu kitabakia"
#DaktariMwandishi 👣 Image

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Kuduishe Kisowile

Kuduishe Kisowile Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Kudu_ze_Kudu

Jan 4
I woke up today with so much in my mind, and that Sylvia Plath quote pierced right through me and I felt every inch of it.
This made me think about the life cycle of a butterfly and how much it resonates with our lives. Female butterflies lay many eggs because not all will (1/?)
survive. Apparently, we are the eggs that survived long enough to become caterpillars. Oh the fun stage, probably the school years where we ate and ate and ate and ate again to grow and run around exploring everything. Then comes the pupa stage, the very uncomfortable (2/?)
one especially because hidden inside the coccoon is us knowing what we are cooking but outside it looks like we are stuck in a box for weeks, months and even years. This is a stage of patience and resilience. Depending on the species, the pupa may be suspended under a (3/?)
Read 9 tweets
Apr 23, 2023
A lot of people spend most of their lives away from their families and homes that they barely build a community around them. They become visitors of their own homes. Things that used to hold people who live around together don’t do that much anymore. Weddings, funerals conducted Image
far from home. Where one builds their house to call home is not where they live. So, you have this group of people who have spent most of their lives away from home for years and suddenly they have to build a home and make it work with those within it and around it.
Kids spend years in boarding schools away from home and holidays are for visiting relatives again away from home. For years & suddenly they get to university and have the new found freedom in their hostels and home becomes somewhere they visit when they can; again AWAY FROM HOME
Read 15 tweets
Mar 3, 2023
Mjadala uliofanyika leo katika mkutano mkuu wa MEWATA kuhusu afya ya akili baada ya kujifungua, umenikumbusha mbali.
Siku moja napita round wodi ya watoto wachanga nawahimiza kina mama kunyonyesha watoto, mama mmoja aliniita “dokta ukimaliza njoo” #UZI #MEWATA2023
Nilipoenda akamchukua mwanae akanikabidhi mkononi akasema, “shogaangu hebu niangalizie mwanangu, maana mie sijielewi”
Nikamuuliza, “unajiskiaje” nikidhani labda ana shida ya mwili ili tuwaite watu wa wodi ya kina mama waje kumhudumia. Akasema, “yani nikimbeba hivi mtoto kumpa
maziwa, kuna sauti zinaniambia kabisa nimnyonge. Yani nawaza nimzibe pumzi afe. Sasa mi sitaki kumdhuru mwanangu, naomba unilelee tu”

Unajua hivi vitu ukivisoma kwenye vitabu vinaonekanaga kama utani fulani hivi hadi siku unakutana navyo. Nikawasiliana na in charge tukatoa
Read 13 tweets
Oct 3, 2022
When I saw a stream of blood down my leg, I knew right there and then; it’s happening! My worst nightmare was coming true and I couldn’t believe it because it was already days after delivery. I have NEVER been that terrified ALL MY LIFE.
This is my story: SURVIVING PPH #Thread 🧵
I tried to be calm, but I could hear my heart pounding in my ears. It felt like someone ripped out my heart and put it in speaker right next to my ears. I felt dizzy, so I sat down. I can’t tell if I was dizzy because of blood loss or the fear of becoming a statistic.
As we prepared to go back to the hospital, I tried so hard to appear calm; a big smile on my face but in my heart I was terrified. I knew it very well, PostPartum Hemorrhage is no joke. In a matter of seconds EVERYTHING COULD GO WRONG.
I asked for ONE thing: my rozary ring.
Read 24 tweets
Sep 26, 2022
Kuna safari hata ziwe fupi vipi, hazisahauliki. Hazisahauliki kwa mengi; watu uliosafiri nao, watu uliokutana nao, experience ya safari na mengine mengi.
Mimi safari hii pichani sitaisahau.
Nilipata wasaa wa kushare na @buguzi @NormanJonasMD @DrArabiFrank na @JuliethSebbaMD #UZI Image
Ilianza kama utani hivi, nikafahamishwa nimepata nafasi ya kufanya mafunzo Morogoro ambayo yaliandaliwa na @sikika1 na @tacaidsinfo
Na mimi mpenda safari na mpenda afya, naanzaje kukosa? Nikafungasha kibegi changu uelekeo mji kasoro bahari.
Moro bwana! Moro PAZURI NYIE! Basi tu. ImageImageImageImage
Katika mengi nilojifunza siku hizo mbili, kuna kitu kimoja kilichonivutia zaidi ya mandhari nzuri ya Morogoro, maana mara ya mwisho nilikuwa hapa ilikuwa ni trip ya Udzungwa na Mto Mawe.
Kitu hicho ni Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI Tanzania (ATF). Leo naomba niwashirikishe Image
Read 16 tweets
Jul 28, 2021
SEHEMU YA PILI #IjueChanjoNaDaktariMwandishi
Leo, saa 3 asubuhi, Rais SSH atazindua chanjo pale ikulu kwa kupata chanjo hiyo.
Wakati huo, tuendelee kujifunza kuhusu chanjo za COVID19 haswa aina ya Johnson&Johnson ambayo ndio imepokelewa. #UZI FUATILIA
#DaktariMwandishi
3. JE, NIKIPATA CHANJO YA COVID19 KUTANIFANYA NIWE NA SUMAKU (MAGENTIC)?

Hapana. Chanjo za COVID19 hazina uwezo wa kutengeneza "electromagnetic field" (uwezo wa wewe kuwa sumaku) na chanjo zote hazina metals.
Unaweza kuangalia nini kimo kwenye chanjo katika ukurasa wa CDC.
4. KWANINI BAADHI YA TAARIFA ZINASEMA TUMEPOKEA CHANJO YA JOHNSON&JOHNSON NA NYINGINE ZINASEMA "JANSSEN"?
Jina kamili la chanjo iliyopokelewa Tanzania kupitia mpango wa COVAX ni "Johnson&Johnson's Janssen(J&J/Janssen) COVID19 Vaccine" kwahiyo ni kitu kimoja wala si chanjo tofauti
Read 18 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(