NJIA 6 BORA ZA KUZUIA MIKOROMO UNAPOLALA

Watu wengi wanapolala huwa wanakoroma na tatizo hilo huwakera wengi wasiokoroma ambao labda hulala chumba kimoja na mtu mwenye hali hiyo. Lakini ni kwa nini watu hukoroma? Image
✔Mirija ya hewa iliyoziba kwa kitaalamu obstructive sleep apnea (blocked airways)

✔Unene kupita kiasi.

✔Tatizo la mfumo wa mdomo wako, pua, ama koo

✔kukosa kulala kimakusudi (sleep deprivation).

✔ kulala chali

✔ kunywa pombe muda mfupi kabla ya kwenda kulala.
NJIA ZA KUZUIA KUKOROMA

1. Punguza unene na kuzingatia mlo bora.

Kuwa na uzito mkubwa (unene) kunaweza kusababisha mtu kukoroma. Mafuta yaliyozunguka shingo hubana mirija ya hewa na kuzuia hewa kupita kiurahisi kutoka nje au kuingia ndani
2. Jaribu kulala kwa ubavu badala ya kulala chali.

Wakati wa kulala kwa mgongo, ulimi wako au tishu yoyote ya mafuta huweza kulalia ama kukandamiza na kuziba njia ya hewa. Kulala kwa ubavu huzuia hii.
3. Acha kunywa pombe kabla ya kwenda kulala.

Pombe hufanya misuli ya koo kulegea zaidi kuliko kawaida wakati unapolala na hivyo huchangia kutetemeka kwa misuli hiyo na hatimaye kutoa sauti ya mikoromo ya kuchukiza.
4. Acha ama punguza uvutaji wa sigara.

Moshi wa sigara huathiri sana njia ya hewa katika pua na koo kuingia na kutoka kwenye mapafu, na husababisha uvimbe. Hali hii husababisha kupungua kwa upana katika njia ya hewa na hivyo kusababisha mikoromo.
5. Hakikisha pua zako zipo wazi.

Ikiwa kuna vikwazo vinavyozuia pua yako ni vizuri kumuona daktari kwa ushauri kwa kuwa, vikwazo hivyo huenda vinaletwa na 'allergy' au matatizo mengine yanayojirudia mara kwa mara kama vile mafua
6. Tumia mto wakati wa kulala.

Kuhakikisha kichwa unakilaza sehemu iliyoinuka kiasi wakati wa kulala kutakusaidia kupunguza tatizo la kukoroma kwani itasaidia kuhakikisha njia ya kupenyeza hewa zipo wazi.

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Dr.Socy²³ (HS)

Dr.Socy²³ (HS) Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @biturojr

15 Nov
JINSI WATOTO WANAVYO SABABISHA BABA ZAO KUFA MAPEMA!!

Baba anapokuwa bado ana nguvu, yuko kazini, ni mkulima, au anafanya biashara; huwa anakua na nguvu na ushawishi mkubwa sana kwenye familia yake: Familia humsikiliza, humjali humpenda, na huzingatia na kutambua uwepo wake.! Image
Tatizo huanza pale baba anapozeeka, nguvu za uzalishaji mali zimekwisha, au amestaafu.! Na pale watoto wanapokua wamekua watu wazima wameanza maisha yao.! Hapo ndipo mambo kwa baba huanza kuharibika na kupewa kisogo na wanae.!!
Mkewe huanza kumchukulia poa! Ile heshima aliyokuwa akipewa huanza kupungua taratiibu.. Baba hasikilizwi tena Kama zamani, isitoshe anakua hahusishwi sana tena kwenye mambo ya mkewe sababu hata akiambiwa atasaidia nini na pesa hana?
Read 12 tweets
12 Nov
JE, NI KIPI HUMFANYA MWANAUME KUINGIA RASMI KWENYE NDOA?

👇👇

Wanaume huwafuata Wanawake kwa mambo mawili, ambayo ni MAPENZI na SEX. Lakini inapofika hatua ya Kuoa, Wanaume hawaoi kwa sababu ya SEX au MAPENZI, wanaoa kwa sababu ya kutafuta AMANI NA UTULIVU WA NAFSI (STABILITY).
Mwanaume anaweza kukupenda na asikuoe,
Mwanaume anaweza kuwa anafanya mapenzi na wewe tena mkadumu kwa muda mrefu lakini asikuoe.

Lakini akampata mtu mwingine akamuoa hata kama mahusiano yake na mtu huyo yalikuwa ya miezi miwili.
Wanaume wengi hutizama mbali zaidi pale wanapotaka KUOA. Huwa hawafikirii habari za suti kali za harusi na sherehe ya gharama, vitu ambavyo hufikiriwa zaidi na wanawake kila wanapoiwaza ndoa.
Read 5 tweets
11 Nov
DAWA KUMI AMBAZO MAMA MJAMZITO HATAKIWI KUZITUMIA KABISA

Leo tutaangalia dawa ambazo jamii yetu hupenda sana kuzitumia lakini bahati mbaya baadhi ya dawa hizo hazitakiw kupewa kwa wajawazito kabisa kulingana na madhara makubwa yanayoambatana na dawa hizo kwa mtoto aliyepo tumbon
1.Albendazole;

hii ni dawa ya minyoo ambayo
hutumika mara kwa mara kujitibu lakini ni dawa mbaya sana kwa akina mama wajawazito kwani una uwezo wa kutoa mimba kabisa hivyo
mebendazole hutumika kama mbadala.
2.Gentamycin:
hii ni dawa ambayo iko kwenye
mfumo wa sindano tu, mara nyingi hutumika kutibu magonjwa ya mfumo wa mkojo.
Dawa hii huharibu mishipa ya fahamu (auditory nerve) ambayo hutufanya sskusikia. Hivyo matumizi ya dawa hii huweza kusababisha mototo kuzaliwa akiwa kiziwi
Read 12 tweets
11 Nov
BIASHARA YA CHAKULA (MGAHAWA)

 Kwa huzoefu wangu nahisi biashara ya mgahawa inalipa kwa wakati kuliko biashara nyingine ile.

Chakula ni hitaji muhimu kwa maisha ya kila mwanadamu, lazima watu wale.

ZINGATIA huduma bora, chakula kizuri na eneo zuri.
CHANGAMOTO ya biashara hii ni kwamba inataji lazima uwe na msaidizi mchapakazi lakini pia uwe serious na unachokifanya.

📌CHANGAMOTO nyingine ni wateja wakiume kuja kwa njia ya kutaka huduma tofauti na bidhaa husika, badala kula chakula wanataka kumla mpika chakula.
Lakini ndio wateja ambao watakuvusha na kupiga hatua ilimradi usiwe mkali kwa wateja hata wakiongea nini achana nao focus kwenye mradi wako ili na wao waendelee kuja.
Read 4 tweets
11 Nov
WACHAGA WAMEGAWANYIKA KAMA IFUATAVYO; SIO WOTE WAJANJA.
Kuna:-

1. Warombo

Wajanja sana kibiashara/wezi pia, wameajiri Wamarangu mjini ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanawake zao ni mama Huruma, wanaachia tu.. Ukioa mrombo ujue umeolea kijiji.
2. Kuna Wamarangu

Wazuri sana wa sura na umbo wanawachuna Warombo. Wanawake wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu.
3. Kuna Wakibosho

Wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchinja... Wengi wanamiliki mabucha. Wana hasira sana na ni wakatili.. Akikuchoma kisu, siku ya mazishi anakuja kudai kisu chake.
Read 8 tweets
10 Nov
VITU SITA USIVYOTAKIWA KUFANYA KABLA YA KULALA

1. USILALE UKIWA UMEVAA SAA.

Saa ya mkononi ina madhara iwapo utaivaa kwa muda mrefu, wanasayansi wanashauri sio sahihi kulala ukiwa umevaa Saa (ya mkononi). Image
2. USILALE UMEVAA SIDILIA (wanawake wanayovaa kwenye matiti ).

Wanasayansi wa America wamegundua kuwa wanaovaa sidilia zaidi ya masaa 12 Wako kwenye hatari zaidi ya kupata Kansa ya matiti.
3. USILALE NA SIMU IKIWA KARIBU.

Wanasayansi wanashauri usiweke simu pembeni kwasababu ya mionzi ya simu sio salama hasa ukiwa umelala, ni vizuri ukaizima kama ni lazima ukae nayo karibu.
Read 5 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!