Leo tunaendelea na experience yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro ambapo machozi, jasho na damu ni sehemu ya safari hii inayohitaji ujasiri na moyo wa chuma kweli kweli..
Mfululizo wa matukio niliyopitia unaweza kukufundisha na kukuandaa vyema ewe Mtalii mtarajiwa 😅😅
UZI 👇🏾
Kituo 1: MLIMA URUGURU
Urefu wa Mlima Uluguru ni kama 8600ft. Na huu ulikuwa ni moja ya mlima wa majaribio kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Kiukweli hili lilikuwa ndio jaribio rahisi kuliko yote hadi tukaona kumbe mambo ni mepesi hivi! Tungejua 😃😃
Nakumbuka tulienda siku ya Ijumaa. Jumamosi tukapanda Mlima. Jumapili tukarudi Dar.
Mandhari ya Uluguru ni bomba sana. Kuna memories nyingi nzuri ila mojawapo ni kuoga alfajiri katika water falls 🤩🤩
Waluguru mmebarikiwa ndugu zetu. Hii ni moja ya kumbukumbu yangu bora pale!
Jambo ambalo sikupenda Uluguru ni hali ya choo pale. Nakumbuka nilibanwa haja kubwa ila mzigo wangu niliubana hadi nilivyorudi town maana kushusha gogo porini nilikuwa siwezi. Sijui kwanini SUA hawarekebishi 😬
Hiz ni tents tulizotumia kulala muda wote tukiwa pale. Usalama 100%.
Na hapa ni camp tulikofikia. Panaitwa Morning Site. Jengo fulani amazing sana!
Humo ndani kuna machata ya watu wengi sana. Panavutia mno kusema ukweli.
Palinikumbusha yale machata tuliyokuwa tunayaona shuleni enzi hizo tunasoma!
Tunaingia Moshi usiku saa 2 na kupokelewa na wenyeji wetu wakarimu kishenzi. Wale ma-guide sijui walidhani tumetoka nchi gani hatujui Kiswahili, kumbe ni wabongo tu😅😅
Nadhani walishazoea wanaoenda kupanda Mlima ni foreigners tu. Hii kidogo ilinisikitisha..
Miaka kadhaa iliyopita nilipata mzuka wa kwenda kutimiza moja ya ndoto zangu kubwa - kupanda Mlima Kilimanjaro.
Siku zote nilitamani kufika juu kabisa ya "Paa la Afrika". Nikasema ipo siku tu!
Hatimaye siku zikawadia za kuitimiza ndoto yangu hii kongwe.
Ilikuwaje?
THREAD👇🏾
Kampuni niliyotumia inaitwa Origin Trails. Sikusafiri peke yangu, kundi letu tulikua 21. Njia tuliyotumia ni Marangu.
Gharama ilikuwa ni USD 560 kwa kila mmoja na hii ilihusisha kila kitu kuanzia usafiri Dar-Moshi, chakula, hoteli, vifaa, ada za getini, personal guides n.k.
MAANDALIZI YA SAFARI
Baada ya kuthibitisha ushiriki wangu kupanda Mlima Kilimanjaro, jambo la kwanza nilifanya medical checkup. Nikawa 100% fit kupanda mlima na hadi kufika kileleni.
Basi, nikaanza mazoezi. Nakimbia uwanja huki nazunguka mara 7-10 kila siku kuuandaa mwili..