Hoteli tuliyofikia kulikuwa na wazungu kibao. Wengi wametoka mlimani wakipongezana kwa dinner, wines na kupeana vyeti..
Nikawa nawatizama kwamba can I do this? Unaona watu wanachechemea miguu, sura hazitamaniki wamebabuka, wengi wako hoi.
Nikaguna, mambo yenyewe ndio hivi!!!
Basi, ule usiku tukafanyiwa training na rescue team ya ile kampuni.
Tukapewa maelekezo yote muhimu yaliyohitajika. Asubuhi safari ya Mlimani.
Nilikuwa na shauku na hofu kwa wakati mmoja. Nikasali na kuamua liwalo na liwe. Kesho ndio kesho!
SAFARI YA MARANGU
Alfajiri tukaamka!
Mimi pamoja na kununua vifaa vya mlimani lakini bado nilikuwa nahitaji kukodi baadhi ya vifaa kama vile hiking boot, balaclava, walking stick, sleeping bags zile zenye joto maana huko juu tushaambiwa kuna baridi la kufa mtu..
Saa 3 asubuhi tukaanza safari ya Marangu. Si umbali mrefu.
Usajili getini tukamaliza saa 9 mchana.
Mwezi ule ulikuwa ni ile miezi ya high season, hivyo kuna watu kutoka nchi mbalimbali walikuwa wamekuja kupanda mlima. Yaani kulikuwa na nyomi la kufa mtu!
Jambo nililopenda Marangu getini kuna ramani ya njia unayotumia kufika kileleni.
Pia kuna picha za kumbukumbu za watu waliofanikiwa kupanda mlima kwa muda mchache. Kuna mmoja alipanda kwa 5hrs tu. Huyu hadi leo najiuliza aliwezaje? Masaa 5 hadi kileleni is not a joke!
๐ธGetini
Leo naomba niweke kituo hapa. Kesho nitaelezea kwa kirefu yaliyojiri kuanzia hapo getini hadi Mandara huko na ugumu wake.
Nitamtambulisha na personal guide wangu Freddy๐๐
Hii ndio ilikuwa point yangu ya kwanza baada ya kutoka getini. Nilikuwa na personal porter anaitwa Fredy. Mwenyewe alinipokea bag (back pack) na kujitambulisha kwangu.
Ukiwa na personal guide ina maana yeye atakua na wewe bega kwa bega, achana na wale guide wa group..
Leo tunaendelea na experience yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro ambapo machozi, jasho na damu ni sehemu ya safari hii inayohitaji ujasiri na moyo wa chuma kweli kweli..
Mfululizo wa matukio niliyopitia unaweza kukufundisha na kukuandaa vyema ewe Mtalii mtarajiwa ๐ ๐
UZI ๐๐พ
Kituo 1: MLIMA URUGURU
Urefu wa Mlima Uluguru ni kama 8600ft. Na huu ulikuwa ni moja ya mlima wa majaribio kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Kiukweli hili lilikuwa ndio jaribio rahisi kuliko yote hadi tukaona kumbe mambo ni mepesi hivi! Tungejua ๐๐
Nakumbuka tulienda siku ya Ijumaa. Jumamosi tukapanda Mlima. Jumapili tukarudi Dar.
Mandhari ya Uluguru ni bomba sana. Kuna memories nyingi nzuri ila mojawapo ni kuoga alfajiri katika water falls ๐คฉ๐คฉ
Waluguru mmebarikiwa ndugu zetu. Hii ni moja ya kumbukumbu yangu bora pale!
Miaka kadhaa iliyopita nilipata mzuka wa kwenda kutimiza moja ya ndoto zangu kubwa - kupanda Mlima Kilimanjaro.
Siku zote nilitamani kufika juu kabisa ya "Paa la Afrika". Nikasema ipo siku tu!
Hatimaye siku zikawadia za kuitimiza ndoto yangu hii kongwe.
Ilikuwaje?
THREAD๐๐พ
Kampuni niliyotumia inaitwa Origin Trails. Sikusafiri peke yangu, kundi letu tulikua 21. Njia tuliyotumia ni Marangu.
Gharama ilikuwa ni USD 560 kwa kila mmoja na hii ilihusisha kila kitu kuanzia usafiri Dar-Moshi, chakula, hoteli, vifaa, ada za getini, personal guides n.k.
MAANDALIZI YA SAFARI
Baada ya kuthibitisha ushiriki wangu kupanda Mlima Kilimanjaro, jambo la kwanza nilifanya medical checkup. Nikawa 100% fit kupanda mlima na hadi kufika kileleni.
Basi, nikaanza mazoezi. Nakimbia uwanja huki nazunguka mara 7-10 kila siku kuuandaa mwili..