#CORONA --- #UVIKO19 UZI 👉 Je dalili kwa sasa ni zipi? Zimebadirika ? Picha ya ugonjwa ukiambukizwa ni ipi kwa sasa?
DALILI HUTOFAUTIANA KULINGANA UKALI WA UGONJWA?
✍️Tafiti kuhusu makali ya ugonjwa wa Korona-19 (UVIKO-19) yameonyesha makundi 3 ya wagonjwa

1. Ugonjwa usio mkali (81 kati ya 100)

2. Ugonjwa mkali maana mtu anahitaji oksijeni au 50% limeshambuliwa na ugonjwa (14 kati ya 100)
3. Ugonjwa mahututi maana mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi au ogani muhimu kama moyo, figo , ini kufeli

✍️HATARI YA KIFO: Kwa wastani vifo hutokea kwa asilimia 2.3 ya watu waliopata maambukizi kumaanisha asilimia wanopata maambukizi ya Corona 97.7 hupona
Kama ilivyo juu, ripoti ya kituo cha kudhibiti magonjwa CDC kilionesha kwa marekani wa kila watu 100 wenye maambukizi
- 14 walilazwa
- 2 walilazwa ICU
- 5 walifariki

Kwa Tanzania hamna taarifa kuhusu uwezekano wa kufariki au kulazwa ukipata maambukizi
Uwezekano wa kufariki kutokana na kupata maambukizi ya Corona huongezeka kulingana na umri
- 0.002% kufikika umri wa miaka 10
- 0.01% kufikika miaka 25
- 0.4% kwa miaka 55
- 1.4 kwa miaka 65
- 4.6% kwa miaka 75
- 15 kwa miaka 85
- Zaidi ya >25% kwa miaka zaidi ya ≥90
MUDA WA UGONJWA KUCHEPUA
- Kwa kawaida huchukua siku 14 tangu uambukizwe Corona hadi ugonjwa uchepue na kuanza kuonyesha dalili

- Watu wengi huanza kuonyesha dalili siku 4 hadi 5 baada ya kupata maambukizi ya virusi vya Corona.
✍️Kwa wagonjwa wanaokuja kupata dalili za Corona, wengi hupata kikohozi, misuli kuuma , uchovu na kichwa kuuma.

✍️Baadhi huarisha, koo kuuma , kupoteza uwezo wa kunusa au ladha
✍️Nimonia ni moja ya hatua kali ya ugonjwa ambayo hutokea wa wagonjwa wa Corona -- mtu huwa na homa, kikohozi na kushindwa kupumua

✍️ Kwa hali ya sasa kushindwa kupumua kwa wastani wiki moja baada ya dalili nyingine ni kiashiria cha Corona
✍️Dalili za Corona kati ya watu 100 wenye maambukizi

Kikohozi hutokea kwa 50
Homa kwa 43
Misuli kuuma kwa 36
Kichwa kuuma kwa 34
Kupata shida ya kupuma kwa 29
Koo kuuma kwa 20
Kuharisha - 19
Kutapika - 12
Kushindwa kunusa, kuonja , tumbo kuuma , mafua kuchuluzika - chini ya 10
✍️Baadhi ya watu wenye maambukizi ya Corona hupata dalili kama za red eyes - macho kuwasha na kuwa mekundu ila ni kwa kiasi kidogo
✍️Mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi – Hutokea kutokana na ugonjwa mkali wa upumuaji (ARDS)

✍️Ni madhara yanayoonekana zaidi kwa wagonjwa wenye ugonjwa mkali wa Corona

✍️ARDS kwa wastani inahusisha 20% ya wagonjwa na hutokea kwa wastani wiki baada ya dalili kuanza
✍️CORONA huathiri pia mfumo wa moyo na mishipa ya damu
✍️ Madhara hutokea zaidi kwa wenye ugonjwa mkali na mahututi
✍️Madhara ni pamoja na:
- Moyo kushidwa kufanya kazi
- Mapigo ya moyo yasiyo na mpangilio
- Mabonge ya damu mishipani kuleta shambulio la moyo
✍️Corona huweza kuathiri pia mfumo mkuu wa fahamu na kusababisha maumivu ya kichwa , kizunguzungu , kupoteza uelewa na kuchanganyikiwa kwa baadhi
✍️Baadhi hupata tatizo linaloitwa ukungu wa COVID maana yake hupoteza kwa kiasi uwezo wa kumbukumbu, uwezo wa kufikiri vyema na kukazia fikra
✍️Kuna changamoto ya wagonjwa wa COVID-19 wenye ugonjwa mkali kutengeneza mabonge ya damu mishipani

✍️Athari za damu kuganda mishipani ni kama kupata stroke/kiharusi ambazo zimeripotiwa zaidi kwa watu wenye umri mdogo chini ya miaka 50 bila ya kuwa na visababishi vingine.
✍️ #UPONAJI--- Muda wa kupona kabisa dalili za Corona hutofautiana sana kutegemea umri na magonjwa mengine

✍️Watu wenye ugonjwa usio mkali hupona haraka wastani wa wiki 2

✍️Wenye ugonjwa mkali huchukua muda mrefu kupona wastani hadi miezi 2
MWISHO: Ni muhimu kuendelea kuchukua taadhari kujikinga na maambukizi ya Corona maana inazuilika>

Jikinge, Wakinge Wengine

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Dr. Norman Jonas

Dr. Norman Jonas Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @NormanJonasMD

25 Feb 20
Inaweza tokea katikati ya usingizi mtu hasa mtoto akawa na tabia ya kutembea,kuongea au kufanya vitendo vingin akiwa usingizini

Hii ni SLEEPWALKING

Hutokea zaid kwa watoto hasa wavulana,inahisiwa hutokea kwa sababu mfumo wa ubongo kudhibiti msawaziko wa kulala/kuamka haujakomaa
Tabia ya kutembea au kuongea usingizini ikianza kwa mtu mzima inahusishwa na msongo mkubwa wa mawazo muda mwingine aina ya kifafa

🔵Tatizo la kutembea usingizini hutembea katika familia; 45% ya watoto wanaotembea usingizini pia na wazazi wao walitembea usingizini
Inaweza tokea katikati ya usingizi mtoto akaamka anapiga kelele,akazubaa kama Dakika 10 bila kujua nini kinaendelea akarudi usingizini kama hakijatokea kitu. Kesho akiamka hajui nini kilitokea.

🔵Hii ni SLEEP TERROR ni tatizo ambalo  huambatana tatizo la kutembea usingizini
Read 9 tweets
28 Jan 20
THREAD | MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO

KWANZA : Vidonda vya tumbo hutokea pale mfumo unaolinda kuta za tumbo unaposhindwa kazi hivyo asidi ya tumbo kuchoma kuta na kuleta kidonda/mchubuko.

🔵 Sababu kuu huwa ni maambukizi ya H. Pyroli na Dawa kundi la aspirin
Mtu mwenye vidonda vya tumbo hupata shida kama:
1️⃣Maumivu makali ya tumbo yanayochoma mara nyingi eneo la chini ya chemba ya moyo
2️⃣Tumbo kujaa gesi
3️⃣Kiungulia
4️⃣Uchovu huweza kutokea kama kuna upungufu wa damu kutokana na vidonda
5️⃣Kinyesi cheusi humaanisha vidonda vinatoa damu
Vidonda huweza kutokea tumboni au kipande cha kwanza cha utumbo

✍️Kidonda kilicho tumboni husababisha maumivu makali mara tu mtu anapokula;

✍️Kidonda kikiwa kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo husababisha maumivu mtu anakuwa na njaa, maumivu huisha mtu akila
Read 14 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(