, 14 tweets, 4 min read
My Authors
Read all threads
THREAD | MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO

KWANZA : Vidonda vya tumbo hutokea pale mfumo unaolinda kuta za tumbo unaposhindwa kazi hivyo asidi ya tumbo kuchoma kuta na kuleta kidonda/mchubuko.

🔵 Sababu kuu huwa ni maambukizi ya H. Pyroli na Dawa kundi la aspirin
Mtu mwenye vidonda vya tumbo hupata shida kama:
1️⃣Maumivu makali ya tumbo yanayochoma mara nyingi eneo la chini ya chemba ya moyo
2️⃣Tumbo kujaa gesi
3️⃣Kiungulia
4️⃣Uchovu huweza kutokea kama kuna upungufu wa damu kutokana na vidonda
5️⃣Kinyesi cheusi humaanisha vidonda vinatoa damu
Vidonda huweza kutokea tumboni au kipande cha kwanza cha utumbo

✍️Kidonda kilicho tumboni husababisha maumivu makali mara tu mtu anapokula;

✍️Kidonda kikiwa kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo husababisha maumivu mtu anakuwa na njaa, maumivu huisha mtu akila
Bakteria aina ya H. Pylori ndio chanzo kikuu cha vidonda vya tumbo

🔵Bakteria huyu ana uwezo wa kuishi kwenye kuta za tumbo na kuharibu mfumo wa tumbo kujilinda na asidi hivyo asidi huchimba kuta za tumbo na kuleta kidonda

🔵Watu hupata maambukizi haya kupitia maji na vyakula
Watu wengine hupata vidonda vya tumbo kutokana na matumizi ya dawa za maumivu kundi la aspirin, ibuprofen, naproxen nk dawa hizi zinaitwa NSAIDS.

🔴Dawa hizi huzuia tumbo kutengeneza UTE mzito ambao hutoa kinga kwenye kuta za tumbo dhidi ya asidi
VIDONDA VISIPOTIBIWA VYEMA HUJA NA KULETA MADHARA MAKUBWA

👉Kidonda kuvuja damu - mtu hupata choo rangi nyeusi, kutapika damu au kupungukiwa damu

👉Kidonda kutoboa tumbo

👉Kovu la kidonda kufunga tumbo/utumbo

👉Kuongezeka hatari ya saratani ya tumbo
MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO AKIANZA KUONA DALILI HIZI HUWA N RED FLAG AONANE NA DAKTARI WA MFUMO WA CHAKULA

1️⃣Choo cheusi
2️⃣Kushiba haraka
3️⃣Maumivu ya tumbo kuchoma mgongoni
4️⃣Kupoteza uzito bila sababu
5️⃣Kushindwa kumeza chakula
6️⃣Historia ya saratani ya tumbo katika familia
OGD ni kipimo muhimu sana kwenye vidonda vya tumbo; hii ni kamera ambayo Daktari huangalia njia ya chakula hadi kwenye utumbo

🔵Kupitia OGD utafahamu mahali kidonda kilipo, ukubwa wake , idadi yake

🔵Pia OGD huweza kusaidia Daktari kuchukua kinyama kupima kama sio saratani
SIGARA huchangia kuchochea vidonda vya tumbo kuchimbika zaidi

🔵Watu wanaovuta sigara zaidi ya 15 kwa siku huwa katika vidonda vyao hutoboa tumbo kabisa

🔵Ni vigumu sana kutibu vidonda vya tumbo kwa mvuta sigara
Tiba ya Vidonda ya tumbo uhusisha dawa za kuua bakteria (H.pylori) na kushusha kiwango cha asidi ili vidonda vipone

Kama matibabu yakienda kwa usahihi 90% ya wagonjwa hupona kabisa iwapo H.pylori wote wamekufa
Baadhi ya watu vidonda vyao hujirudia ndani ya mwaka, huwa ni 5% hadi 30% ya wagonjwa

Sababu kuu huwa ni
👉Hpylori kutoisha
👉Matumizi ya dawa aina ya aspirin
👉Vidonda vyao vinasababishwa na sababu nyingine kama asidi kuzidi tumboni, vivimbe vinavyozalisha asidi nyingi nk
Kupunguza kitambi na uzito husaidia uponaji wa vidonda vya tumbo kwa baadhi ya watu

Pia wagonjwa wa vidonda vya tumbo hufanikiwa kutibu iwapo wataacha pombe, kahawa , sigara
VIDEO CLIP FUPI IKIONYESHA KIDONDA NDANI YA TUMBO KUPITIA KAMERA YA KIPIMO CHA OGD

CHANZO: Dr Galeti
Uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo huweza kurithishwa katika familia

🔵 20% ya watu wenye vidonda vya tumbo huwa na ndugu kwenye familia wenye vidonda pia

🔵Baadhi ya Tafiti zimeonyesha watu wenye kundi ya damu O (group O) hupata vidonda vya tumbo kwa haraka.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Dr. Norman Jonas

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!