Mambo muhimu 3 ili kupata ushindi kabla ya kuanzisha mchakato wowote kisiasa.
1. Jua wakati sahihi wa kupigana na ni lini usipigane.
2. Jiandae, toa elimu kwa umma kujenga uelewa wa kile unataka kupigania.
3. Chukua maoni juu ya utayari wa umma kwa kile unachotaka kupigania.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hawakufuata mambo hayo muhimu kabla ya kuanzisha mchakato wa kudai #KatibaMpya
Ukweli usiofichika Katiba Mpya ni muhimu sana lakini ni lazima kuwe na ushirikishwaji wa wadau wote wa siasa na wananchi katika mchakato wa kuidai.
Hatua ya kwanza muhimu ambayo CHADEMA walipaswa kuanzia ni kujiuliza swali kwamba huu ni wakati sahihi wa kupigania Katiba Mpya au kuanza kutoa Elimu ya Katiba Mpya kwa umma ili kujenga uelewa?
Kisha wangeanza ‘inter-parties dialogue’ shirikisha wadau wengine na wananchi.
Hatupingani kwenye maswala ya #KatibaMpya hata kidogo, tunapingana kwenye njia zinazotumika kuidai. Njia ambazo hazishirikishi wadau wote wa siasa, taasisi za kiraia na wananchi. Tatizo letu ni mchakato wa #KatibaMpya kugeuzwa Ajenda ya chama au kikundi cha watu wachache.
Tangu awali tumekuwa tukishauri CHADEMA kufanya majadiliano na vyama vingine vya siasa nchini ‘inter-parties dialogue’ ili upinzani uwe na sauti moja, kisha waanze kutoa elimu ya Katiba kwa umma ili kujenga uelewa kabla ya kuanzisha mchakato wa kudai Katiba Mpya.
There are four different roles activists and social movements need to play in order to successfully create social change.
Social movement activists need first to be seen by the public as responsible citizens. They must win the respect and, ultimately, the acceptance of the majority of ordinary citizens in order for their movements to succeed.
Consequently, effective citizen activists need to say “Yes!” to those fundamental principles, values, and symbols of a good society that are also accepted by the general public.
Je, Kuna uwezekano kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA @freemanmbowetz kuoneshwa Mubashara kwenye vituo vya TV?
Mhe. Rais @SuluhuSamia katika mahojiano na @BBCNews umesema kesi ya Bw. Mbowe ni nafasi nzuri kwa mahakama zetu, kuionyesha dunia kuwa haki inatendeka kwa usawa na uwazi.
Kutokana na ukweli kwamba tangu mwalimu Julius Nyerere apewe kesi ya aina hiyo ‘UGAIDI’ na wakoloni wa Uingereza hakuna kiongozi wa kisiasa amshafunguliwa mashtaka ya aina hiyo tangu Uhuru. Basi itakuwa vema @judiciarytz ikimpa Bw. Mbowe ‘open, fair and transparent trial’
Kesi ya Bw. @freemanmbowetz ina ‘public interest’ kubwa sana. Ili kujenga imani na @judiciarytz uendeshaji mzima wa jaribio ‘trial’ ufanyike mubashara. Watanzania na dunia iweze kufuatia shauri hili lenye maslahi makubwa kwa demokrasia, haki na utawala wa Sheria. Ni ushauri wetu.
Ni maajabu kuona CHADEMA wanamjibu Rais @SuluhuSamia katika masuala mbalimbali ambayo ametoa maoni yake Kikatiba.
Swala la @freemanmbowetz Rais SSH amesema wazi tuache @judiciarytz wafanye kazi yao na kuhakikisha Haki inatendeka.
UKWELI MCHUNGU, hakuna utulivu ndani ya CHADEMA, tulitegemea wachukue MUDA kutafakari na kuyafanyia kazi yale aliyosema Rais @SuluhuSamia sio kukurupuka kuita ’Press’ eti wanamjibu. Watakuwa wanamjibu kila akifanya mazungumzo?
KWAMBA RAIS KAINGILIA UHURU WA MAHAKAMA
Ni dai lenye akili ambalo halijazingatia ’logic na facts’. Rais @SuluhuSamia amejibu swali la @Salym na kupitiliza kidogo kuzungumzia kesi ya Mbowe kitendo ambacho hata Chadema wamekuwa wakisema kuwa Mbowe kafunguliwa mashtaka ya kisiasa.
CHADEMA wanakutana kujadili mahojiano ya Rais @SuluhuSamia na @bbcswahili ili kujibu nini?
Tumeona mahali @godbless_lema ameandika kwamba @ChademaTz kitakutana kujibu mahojiano ya Rais SSH na @Salym, wanataka kukutana kujibu nini?
Chama kinaendeshwa kwa matukio? 🧐
Tunashauri CHADEMA waache kukurupuka na kuparamia kila jambo. Tunashauri kwa mapenzi yetu kwa CHADEMA, Rais Samia kasema kuna Uhuru wa Habari, Baada ya Uchaguzi tujenge Nchi, Kesi ya Mbowe ilikuwepo lakini upelelezi haukuwa umekamilika, tuache Mahakama itafsiri sheria.
Ukweli Mchungu, wote humu tunajua kwamba ni kweli kesi ya @freemanmbowetz ilikuwepo, sio ya sasa, Rais amesema uongo? Kuhusu swala la kujenga CHADEMA wanatakiwa kujitathimini, kuanzisha na kuendeleza migogoro isiyoisha hakutatupa mwanya kushiriki katika Ujenzi wa nchi.
Mahojiano Maalum ya Rais @SuluhuSamia aliyofanya na @bbcswahili na mwandishi nguli @Salym yamegusa mambo mengi kwa mfano;
• Demokrasia
• Uhuru wa Habari na Vyombo vya Habari
• Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni
• Siasa bbc.com/swahili/habari…
• Uhuru wa vyama vya siasa kufanya siasa
• Uchumi
• Hali ya maisha ya watanzania
• Tozo Mpya za Miamala
• Kesi ya UGAIDI inayomkabili Bw. @freemanmbowetz
• Uhuru wa Mahakama @judiciarytz kutoa Haki.
Mwandishi @Salym ameuliza maswali mazuri ambayo yana tija kwa sasa.
Mwandishi @Salym amegusa kila eneo ambalo alipaswa kugusa kwa weledi kabisa. Kwa wale waliotazama mahojiano hayo watagundua kuwa Rais @SuluhuSamia amejitahidi kujibu kila swali aliloulizwa. Mwandishi amefanya kazi yake vema sana na amegusa maeneo yote muhimu aliyopaswa kugusa.
Tofauti ya uwekezaji wa hati fungani na masoko mengine ya mitaji kama Hisa
Hatifungani ni tofauti kabisa na masoko mengine ya mitaji kwa mfumo wake na hata faida zake.
Kwenye hatifungani unapata faida bila ya kujali uchumi unakwendaje. Kwa sababu unaponunua hati fungani unajua kabisa ni riba kiasi gani unapata kwa mwaka. Lakini kwenye hisa hujui ni faida kiasi gani unapata kwenye uwekezaji wako.
Faida inategemea na hali ya uchumi, uimara wa Soko.
Kwenye hisa unapata faida pale hisa zinapofanya vizuri na unapata hasara pale hisa zinapofanya vizuri. Kwenye hatifungani unapewa riba uliyoambiwa bila ya kujali fedha ulizowekeza zimezalisha au la.