UZI: HUWA SIPIGI WEZI KWASABABU HII...👇
😥Wakati nimefika AYA Sec 2007 Kondoa kuanza form 1 (boarding), niliibiwa suruali 3, mashuka 2, viatu, nk. Ilikuwa ndio 'Welcome Party' pale kila mwaka. Kuhamishiana vitu ilikuwa ni kawaida sana bwenini kwetu.
#TravStories #Testimony
Nilipofika Form 2 nikaanza kujifunza hizo mishe na mimi. Nakumbuka nilijifunza kutekenya KILA KUFULI unayoijua wewe. Enzi hizo SOLEX zinasifiwa balaa, ila kwangu hazikuwa shida kabisa😁. Nilikuwa na bunda la funguo natembea nalo. Nikitaka chochote napata fasta kwenye matranka😆
Sabuni zangu hazikuwahi kuisha. Ilikuwa raha sana kupata chochote nilichokitaka. Baada ya hapo nikatamani kuiba VIKUBWA zaidi. Na hapa ndipo nilipobugi mpenzi msomaji😁. Endelea 👇
Basi kuna mabroo ambao walikuwa wanamiliki simu bwenini ingawa shule hairuhusu. Walikuwa wanazichaji usiku kwenye makenchi karibu na ninapolala. Nikaanza kuzipigia hesabu za kupita nazo. Na kweli nikafanya siku moja usiku wa manane. Nikaibeba Nokia 2310 na kwenda kuificha porini.
Then nikarudi bwenini kuendelea kulala na hakuna aliyeniona. Asubuhi jamaa (wa form 4) alianza kuiulizia. Nikapiga kimya. Kwasababu jamaa kwao mambo safi sana (kiuchumi) nikajua tu hawezi kumaindi sana au kuniendea kwa mganga😂. It was a smart move kwa wakati ule.
Baada ya siku kadhaa nikamtonya mshkaji wangu kuhusu huo mchongo na tukawa tunaenda wote kule porini kuicheki na kucheza game sometimes😁. Baada ya muda tukaamua kwenda mjini kuibadilisha muonekano wa nje (housing) ili tuwe na uhuru wa kuitumia bwenini. This was very stupid of me
Baada ya kwenda Town na kurudi shule, tulianza kuitumia bwenini usiku huku tukiweka laini zetu (mimi na mshkaji wangu). Sasa siku moja usiku katikati ya 'prep time' badala ya kuiacha bwenini, nikaibeba mfukoni. Wakati nakaribia darasani ticha mmoja alitokea akiwakimbiza wazururaj
Alitutaitisha na akawa anatuhoji. Muda huohuo simu ilijibonyeza mfukoni so akaona mwanga unatokea kwenye suruali yangu. "Akaniuliza nini hicho?" Daah! Nikaishiwa pozi kabisa yaani. Sema kwasababu ticha mwenyewe alikuja kijana, na aliipenda simu, ikabidi aichukue bila kunishtaki
Dili letu ilikuwa ni kwamba nimwachie awe anaitumia mpaka muda wa likizo utakapofika ndipo anirudishie au lasivyo anichome kwa Head Master. So nikakubali awe anaitumia😒.
Kumbe yule ticha alikuwa ni mshkaji sana wa wale mabroo wa form 4. So huwa anawaazima simu yake wakimuomba, na sometimes wanaenda ghetto kwake (nyumba za walimu) na kuangalia movie au mpira. So, kuna siku yule bro alimuomba simu ticha awapigie home kwao. Picha linaanzia hapa...😭
Jamaa kaandika namba akashangaa zinaleta na jina kabisa. Akashangaa sana. Ikabidi acheki kwenye contacts za simu (saved on SIM Card). Si akakuta namba zake...(za ndugu na washkaji zake hadi wa home). Ikabidi amuulize ticha simu kaitoa wapi. Ticha akamwambia ameitoa kwangu...😥
Kesho nilishangaa kumuona jamaa kaniita kistaarabu tu na kuniuliza kuhusu simu. Nikamwambia kuwa simu ni yangu na nikakana kuiba ile simu. Jamaa ndipo alipoenda kwenye contacts na kunionyesha, pia meseji kadhaa zilikuwepo ambazo TULISAHAU KUFUTA🤦‍♂️. Pamoja na evidence, nikakataa😁
Kesho yake usiku akaniita tena kistaarabu na kuniambia nisiogope kumwambia ukweli kwani yeye anachohitaji ni laini yake tu ambayo ilikuwa na contacts za muhimu sana kwake. Daah! hofu iliniingia na kuona kuwa kama jamaa ni muelewa basi bora nimwambie ukweli. So,nikafunguka bwana🤣
Ila nilipompa jamaa hasira ni pale nilipomwambia kuwa laini niliivunja. Jamaa alikasirika sana na akaichukua simu. Akaniambia yameisha, nisirudie WIZI. Na mimi nilivyo FALA nikajua yameisha kweli. Weeeeeee "Cha mtu mavi" guys😂. Kumbe mwana akawaambia form 4 wenzake bwana...
Nikashangaa kesho yake form 4 wachache bwenini wanaongea "Huyo dogo lazima awe mfano", "Tupige huyo mwizi, tumechoka kuibiwa humu". Hofu ikaanza kuniingia zaidi. Jioni nikaitwa na mwalimu wa bweni. ALikuwa ni kijana pia. Nikamkuta yupo na jamaa. Nikajua ohooo, jamaa kesharipoti🤦‍♂️
Basi kwenye hicho kikao wakawa wananiambia kuwa wenzake (form 4) wanataka kunipiga ila hajawatajia jina langu. So, akapendekeza kuwa ili kuwatuliza itabidi niombe msamaha PUBLICLY na nichapwe fimbo 6 na mwalimu wa bweni. So, sikuwa na options. Nikakubali.
Kesho yake mchana nikiwa nimetoroka class, nimelala bwenini peke yangu kwenye godoro ambalo huwezi jua kama kuna mtu kalala, nikashtushwa na kelele za waliokuwa wanaingia bwenini kupitia mlango wa nyuma. Walibeba magongo&fimbo nyingi wakiziweka kwenye makenchi na chini ya vitanda
Maongezi yao yalikuwa
Wa kwanza: "Leo lazima nipige sana huyo dogo". Wa pili: "Hatuwezi kuacha wizi uendelee humu. Lazima asulubiwe leo"
Mwingine: "Ticha kasema tumshughulikie, yeye hatakuja. Leo nitaua huyo ms*nge"
Mwingine:"Nimeibiwa sana humu ndani,lazima alipe huyo fala leo"
Mpenzi msomaji, USINGIZI ULIKATA GHAFLA😂. Nikahisi kutaka kukojoa na kukata gogo hapo hapo. Bahati nzuri wakaweka na wakaondoka. Walikuwa kama 6 hivi. Wote form 4. Walipotoka tu nikarudi class nikiwa na hofu sana kumshtua mshkaji wangu kuwa leo usiku kinanuka. NASULUBIWA MIE!😭
So, jamaa akanituliza na tukapanga kuwa inabidi nisirudi bwenini baada ya 'Prep Time'. Lilikuwa ni wazo zuri na lenye matumaini.

Kumbe wkt sisi tunapanga, na wale mabroo nao wanapanga namna nzuri ya kunitaitisha.Ukisikia "siku ya kufa nyani miti yote huteleza" ndio ilifika sasa
Tumeingia Prepo vizuri tu. Saa 4:00 usiku ndio kengele ya kwenda kulala hugongwa. Na ndio tukapanga nisirudi bwenini.

Ghafla ilipofika saa 3 na nusu mabro wa form 4 wakaja class na kuamuru BOYS wote wabebe vitu vyao waelekee bwenini huku kukiwa na usimamizi mkali balaa. Mamae😁
Nikajua nimekwisha. Escape Plan yangu imekuwa compromised. Jamaa walikuwa '2 steps ahead of us'. Tulipangwa 'single profile' (Waliopita jeshi wanajua) kuelekea bwenini. Hakukuwa na namna nyingine ya kutoroka. Nilianza kuomba Mungu aninusuru na hilo balaa huku nikitetemeka sana😱
Bwenini mlango wa kuingilia ukabakishwa mmoja tu, jamaa wapo kila mahali na 'mikanda ya ngozi' wakiwa na hasira sana. Makelele yalisikika ndani ya bweni "Yukwapi huyo?", "Apigwe, Apigwe", "Tum*ire kabisa huyo, wamezidi". Nilianza kutoa machozi😭 huku nguvu zikiniishia miguuni🥺
Tulipoingizwa ndani tukaambiwa tutulie na hakuna kutoka nje. Mshkaji wangu akawa ananionea huruma sana nikiwa sina matumaini kabisa. Nikicheki mlangoni jamaa wamejaa na hawaruhusu mtu kutoka. Nilikuwa simjui MUNGU ila siku hiyo nilimuomba kama yupo basi anisaidie n sitarudia tena
Baada ya kuvaa koti langu (jioni ni baridi sana kule) nikaamua nisogee mpaka pale mlangoni huku nikiendelea kushuhudia na kusikia makelele ya hasira za wananchi kama mizimu iliyokosa damu kwa miaka mingi sana. Nilijiona nakufa siku hiyo. Nilijua nitafanywa hata visivyoongeleka😭
Sijui hata ishu gani ilitokea, wale mabroo wakatoka pale mlangoni. Labda kuna madogo walikuwa wanazingua kuingia. Basi nilipoona wametoka tu mlangoni, nikapita pale kwa spidi moja ya FLASH⚡️😁. Nikatokea upande wa pembeni wa bweni kwenye giza nikatokomea porini.
Baada ya kama dakika 10 nikawa nipo kwenye mlima mmoja wa karibu na bweni. Nikawa nasikiliza wakiulizana "yukwapi uyo?" "yukwapi?". Na baada ya muda nikaanza kuona tochi nyingi zikiwa zinakuja porini. Nikajua wameshtuka kuwa nimekimbia so wananifuata. Ikabidi nikimbie zaidi
Nikafika kwenye mlima wa pili nikawaona bado wanakuja. Nikasogea kwenye mlima wa 3 mbali zaidi kutokea bwenini. Hapo ndio nikawaona wamekata tamaa, wakaamua kurudi. Hapo nipo pekua, nimepita kwenye changarawe, katani kibao na maumivu siyasikii. Nilipoona wamerudi ndipo nikatulia
Palikuwa ni porini sana, baridi kama yote. Sauti za fisi zikisikika kwa mbali. Nilijificha chini ya mti fulani mkubwa na nilikuja kushtuka saa 11 asubuhi niliposikia kengele ya 'mchakamchaka'. Niliamka nikiwa siamini kama nimelala pale na nipo salama. Nilijawa na hofu kubwa sana
Ilibidi siku hiyo nishinde siku nzima porini nikila zambarau,maembe na mapera. Mida ya jioni mshkaji wangu alikuja mpaka mahali ambapo huwa tunakaaga tukitoroka fimbo au msala. Ni kabla ya ule mlima wa kwanza. Akanielezea namna ambavyo walitaka wampige yeye baada ya kunikosa mimi
Ila aliambia "Bora umekimbia bro, wangekuua." Walikuwa na hasira sana na hata mwalimu hakuwepo kama alivyosema." Nilimshukuru sana MUNGU ingawa nilijua kuwa ishu bado ni mbichi sana. So siku hiyo ikabidi nikalale tena pale mlima wa tatu chini ya mti
Kesho yake ndio nikawa narudi bwenini mida ambayo watu wapo darasani kwani mshkaji aliniambia kuwa atakuwa ananiachia msosi chini ya kitanda chetu. So nilikuwa naenda kula na kurudi porini. Siku hiyo hiyo walimu walianza kunitafuta. Ikabidi mwalimu wa bweni anitafute
Akamtuma mshkaji wangu aje aniambie nirudi na ishu zitakaa sawa. Nikasema "Weeeeeeeeeee, huyu si ndio mshenzi aliyeniahidi kuwa atakuwepo kunilinda na ni yeye pekee ndiye atakayenichapa bwenini halafu akatokomea pasipojulikana?". Nikamwambia jamaa, mwambie ticha sirudi
Maticha wote wawili (aliyeichukua simu na kuitumia, pamoja na wa bweni) walijua vibarua vyao vitaota nyasi iwapo ishu itafika uongozi wa juu so wakabidi watafute kila namna ya kunirudisha. Siku ya tatu mshkaji wangu akaja na msosi akaniambia kuwa maticha wamemruhusu aniletee
Then akaniambia saa 9 usiku nije bwenini watakuwepo tuyamalize. Nikamwambia labda tukutanie huku porini na sio shule. Basi alienda na akarudi kuthibitisha kuwa wamekubali.

Siku hiyo nikalala pale ambapo tutakutaniana ambapo ni mlima wa kwanza karibu na bweni/shule.
Walipofika, mshkaji wangu akanishtua. Nikaamka nikawaona maticha wote 2, yule bro mwenye simu, kiongozi wa bweni pamoja na mshkaji wangu. Tukakaa tukayajenga huku nikiwalaumu sana kwa kwenda kinyume na DILI la mwanzo. Walinionea huruma sana na mwisho tukakubaliana kesho yaishe
Kivipi?
1. Kuondoa zile fimbo na mgongo yote bwenini
2. Nitaomba msamaha na sitapigwa hata fimbo/mkanda mmoja
3. Narudi kuendelea na masomo, nikiulizwa ulikuwa wapi, natakiwa kujibu kuwa nilikuwa naumwa.
4. Jamaa mwenye simu alipaswa kuwatuliza washkaji zake na kunilinda pia😊
Ilikuwa ni kama El Chapo anajadili terms za dili lake na FBI kule Marekani ili ajisalimishe😂. So kesho yake usiku (watu wakiwa Prepo) ndipo niliporudi bwenini rasmi huku nikiwa na tahadhari kubwa sana. Lakini MUNGU mkubwa bwana. Mambo yakaenda fresh. Nikaomba msamaha na yakaisha
Ni moja ya matukio ambayo sitakuja kuyasahau maishani mwangu. Ni moja ya mambo yaliyonifanya nijifikirie sana na kuamua kutulia na kutafuta msaada. Nilijua ipo siku nitachomwa moto kipumbavu mtaani. That was my turning point. Niliacha wizi, nikamjua YESU, Nikabadilika💪😊 #Jesus
Yes, huwezi kuacha wizi kama haujafunguliwa kutoka kwenye miroho michafu uliyoibeba. Mimi nilikuwa naiba hadi nyumbani. Namuibia mama, majirani, nk. It was too much. But baada ya hapo, nilirudi form 3 nikiwa nimebadilika sana kiakili, kiroho na hata kielimu. GLORY TO GOD!
Siwezi kupiga mwizi kwasababu najua jinsi wanavyojisikia pale wanapokamatwa/kutaitishwa. Lakini kingine ni SECOND CHANCE ambayo MUNGU kupitia wanafunzi wenzangu na walimu alinipa siku ile, leo nimekuwa mtu mwema na mwenye IMPACT kwa jamii. Vipi kama ningekufa au kupata kilema?
So, ushauri wangu ni kuwa pamoja na hasira zetu nyingi za kuibiwa vitu vyetu vya thamani, tuwape SECOND CHANCE hawa jamaa. Yes, nipo serious😆. Kwa mtu anayejielewa, baada ya hiyo experience ya kutaka kuuliwa, akiachiwa atabadilika. Kama atarudia basi CHOMENI MOTO TU HUYO MBUZI😡
Naamini sana katika SECOND CHANCE. Kama ambavyo nilihurumiwa na kupewa nafasi nyingine, basi na mimi huwa natoa kwa wanaonikosea kwa namna yeyote ile. Nimetoka mbali sana.

Hii ni video ya kubadilika kwangu. Share kwa wengine #Testimony #confession

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Eagletraves🦅

Eagletraves🦅 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(