Siku zote SILAHA kubwa katika biashara na MAARIFA!
Maarifa ndio silaha yako kubwa, ndio maana leo unapaswa kunisikiliza kwa makini kwa sababu ninaenda kukupa MAARIFA (Mbinu) takazokusaidia kufufua tena matumaini yako.
"Asilimia 80 ya mafanikio yako, yatatokana na asilimia 20 ya juhudi zako katika kujitangaza."
Kwa watengeneza Maudhui kama @fotty__ kanuni hii inasema,
"Hakikisha 80% ya maudhui yako yanatoa VALUE kwa Audience wako, na 20% kufanya promotion ya biashara yako."
Wafundishe watu kuhusu huduma au bidhaa yako;
Kama unauza saa, wafundishe faida zake, jinsi ya kutofautisha saa original na fake, nk. Chochote unachouza, unaweza kukitengenezea maudhui yenye kuongeza VALUE kwa wafuasi/wateja wako watarajiwa.
Halafu tumia 20% zilizobaki kulipia Ads na kufanya promotion ya bidhaa zako bora na zenye demand kubwa kwa wateja wako.
4. Fanya Matangazo.
Nimegusia kidogo hapo juu.
Waswahili wanakuambia "Biashara, Matangazo"
Sasa kuna kitu natamani kukuambia....
Kabla ya kufanya Tangazo lolote, hakikisha unatengeneza FUNNEL.
Funnel ni mfumo unaweza kukusaidia kumvutia mtu asiyekufahamu kabisa, kushawishika kununua bidhaa yako.
Brother @GillsaInt ni mtaalamu sana wa kutengeneza funnels. Ongea nae vizuri.
Unapotangaza, maana yake unataka watu wengi (wasiokufahamu) waone na kununua bidhaa yako.
Kumbuka, HAWAKUFAHAMU!
Sasa kosa kubwa la wafanyabiashara wengi ni kujaribu kuuza kwa siku moja.
Ni sawa na kukutana na binti mrembo kwa mara ya kwanza, halafu ukataka ufunge nae ndoa. ATAKUKIMBIA tu!🙊
Ili tangazo lako livutie, hakikisha unaanza kutoa kitu flani BURE.
Mfano; Ushauri, Darasa online au short Ebook.
Ndani yake, sasa ndio unaweza kuweka ofa ya kile unachotaka kuuza.
Hapo unakuwa umetumia 80% Maudhui, halafu unamalizia 20% kuuza bidhaa yako.
5. Kuwa na Muendelezo (CONSISTENCY)
Kuna wakati utapata like 2, wakati mwingine 0 kabisa.
Kuna wakati utalipia matangazo, na kuishi kupata likes tu. Hupati simu wala DMs.
Haya yote ni kawaida huku mtandaoni.
Kikubwa ni kujitahidi kufanya Improvements kila wakati.
Always weka room ya kufanya Improvements. As you improve l, ndivyo utakavyozidi kukua.
Changamoto zisikufanye uishie njiani.
Endelea kutoa VALUE, endelea kupost, endelea kujitangaza, endelea kubadili strategies zako, mpaka pale utakapoona umeanza kupata matokeo mazuri.
Mbinu ya Nyongeza,
6. RETWEET Post hii.
Mafanikio yapo katika kusaidia watu wengine pia.
Hebu Retweet Post hii ili tuwasaidie watu wengine kupata Maarifa haya.
JINSI YA KUTENGENEZA MAUDHUI (CONTENTS) YENYE KUONGEZA USHAWISHI KWA MTEJA.
Mara nyingi katika kutengeneza Maudhui, tunatumia mawazo, Ideas na ushawishi wetu binafsi...
..lakini, kuzingatia muonekano na aina ya Maudhui yanayoandikwa ni jambo muhimu mno.
Ni rahisi sana kutengeneza mawazo na topic mbalimbali kwa ajili ya wateja wako...
..Lakini, kama muuzaji, ni lazima uwe na uelewa mkubwa wa namna ya kuwasilisha mawazo hayo kwa mteja wako.
Ndio maana ni muhimu sana kufahamu namna mbalimbali ya kuandika maudhui yanayokidhi mahitaji ya mteja wako.
Kupitia mchanganyiko huu wa maudhui, itakusaidia kuongeza wafuasi wako zaidi, kufikia wateja wapya, na kutengeneza mazingira rafiki ya kuuza Bidhaa au huduma yako.