JAPHET MATARRA Profile picture
Sep 13, 2021 147 tweets 82 min read Read on X
FULL OPERATION MAPINDUZI YA RAIS (GUINEA)

#Thread

Baada ya TALIBAN nchin Afghanistan, habari sasa ni MAMADY DOUMBOUYA kiongozi wa kijeshi huko Guinea, kumpindua rais na kuchukua madaraka #Unadhani kikosi kidogo cha SFG kiliwezaje kudhibiti kambi za kijeshi na kumkamata rais?👇
Yes, mwanajeshi wa zamani wa Ufaransa (French Legionnaire) aliyerudi nyumbani miaka 03 iliyopita na kuaminiwa na Rais ALPHA CONDÉ, ndiye aliyemsaliti na kumuondoa madarakani baada ya kutaka kuongoza nchi kwa muhula wa 03

MAMADY DOUMBOUYA ambaye ana cheo cha Kanali alionekana..
kwenye kituo cha Radio-Télévision Guinéenne(RTG), mnamo 5 Septemba majira ya saa 2 usiku, akiwa amevalia kofia nyekundu (Red Beret) ameweka bendera ya taifa hilo begani mwake, na kuzungukwa na wanajeshi wanane, akatangaza kuwa jeshi limechukua madaraka ya nchi.
#Uzi uliopita nilielezea kwa undani zaidi historia ya Guinea tangu nchi hiyo ililopo magharibi mwa Afrika ipate uhuru 1958 hadi 2021 ktk kipindi cha utawala wa Rais ALPHA CONDÉ kabla hajapinduliwa. #Leo ninakuletea uchambuzi murua juu ya mapinduzi haya.👇

Nitagusia sehemu 03 ambazo ni:

➠ Mamady Doumbouya ni nani?

➠ Aliaminiwa vipi na Conde?

➠ Alifanikiwa vipi kuingia Ikulu na kumpindua Rais ALPHA CONDÉ ambaye aliwahi kujigamba kuwa anaweza kuuawa akiwa nje ya nchi lkn sio Ikulu (𝐅𝐮𝐥𝐥 𝐎𝐩𝐞𝐫𝐚𝐭𝐢𝐨𝐧) ilivyofanyika!!
Nachokuomba sasa sogeza kochi au kiti chako, kisha chukua Popcorn 🍿🍿 Toroli zima, weka hapo pembeni, halafu msomaji wangu uniazime macho, akili (to connect events) pamoja na muda wako na mwishoni dondosha comment yako utuambie ulichojifunza ktk mapinduzi haya

LET'S GO...
Miaka 10 sasa imepita baada ya kifo cha JOSEPH MAKAMBO LOUA, kamanda mwaminifu na hodari ktk kikosi cha usalama wa rais wa Guinea (BASP). Kamanda Makambo alikuwa ni rafiki wa karibu sana na Kapteni MOUSSA DADIS CAMARA ambaye alitawala taifa hilo mnamo 2009,
Familia yake imekuwa ikilalamikia serikali kuwasahau baada ya mzee wao kufariki.

Katika mahojiano na mwandishi mmoja huko N’zérékoré (Guinea), Binti mkubwa wa kamanda huyo, MARIE MAKAMBO LOUA, alizungumzia juu ya hali ambayo familia yake inaishi leo.
Familia ambayo, kwa maelezo yake imetengwa kinafiki sana na kila mtu, huku ikiishi kwa kuoga shida kila uchwao na serikali haina muda nayo.
"Since the death of my father, Joseph Makambo Loua, in 2009, we have been living in distress. Our family has nothing and we are living in pain. When our late father died, some of his friends came over to console us by telling us that they will take care of us,
"But it was nothing but lip service,No one thinks about our family anymore, which is in great pain. Even Toumba (presumed murderer of Commander Makambo) who is in prison lives better than us. This is why I sometimes have the impression that my father died needlessly."
Binti MARIE anailaumu serikali iliyopinduliwa na mtu mbadi DOUMBOUYA.Anasema tangia baba yao afariki wanaishi kwa tabu na shida kubwa.Marafiki wa mzee wao wamewatelekeza, maneno "tutawatunza" waliwaenjoy. Ht aliyedhaniwa kuwa muuaji ambaye yuko gerezani anaishi vizuri kuliko wao!
Siku zote ni ngumu kuponya athari zilizoachwa ktk familia ya marehemu. Rest In Peace ALPHONCE MAWAZO, BEN SAA8 DAVID MWANGOSI, AKWILINA nk siwezi kutaja wote.

Kamanda MAKAMBO alifariki mwaka 2009 ktk kambi ya kijeshi ya Koundara (Guinea), akijaribu kuokoa maisha ya mkuu wa nchi
Ikiwa umefuatilia UZI uliopita utananielewa. Kapteni MOUSSA DADIS CAMARA, alijeruhiwa vibaya kwa risasi ya kichwa na ABOUBACAR SIDIKE DIAKITÉ "𝐓𝐨𝐮𝐦𝐛𝐚" na kukimbizwa Morocco kufanyiwa upasuaji na matibabu ndipo baadae alikwenda Burkina Faso, ambapo anaishi hadi leo hii.
Maneno ya MARIE yalitrend sana ktk vyombo vya habari. Hapa ndipo tunapopatia kisa cha Rais CONDÉ kupinduliwa na DOUMBOUYA.
Rais Conde alimwamini kupita kiasi mpk kuna siku alisema haweza kupinduliwa km watangalizi wake.

Tuchukua hiyo baki na 1 kichwani
Nikirudishe nyuma kidogo.
Wakati AHMED SÉKOU TOURÉ alipofariki mnamo 1984, ilikuwa bado muhula wa kukaa madarakani haujaisha. Kumbuka alichaguliwa mwaka 1982 miaka miwili baadae akafariki kwa maradhi ya moyo. Baada ya kufariki waziri mkuu LOUIS BEAVOQUI alishika hatamu, lkn baada ya wiki moja akapinduliwa
Mapinduzi yaliongozwa na Kanali LANSANA CONTÉ na Luteni Kanali DIARRA TRAORÉ, ambapo baadae Conté alijitangaza rais wa nchi hiyo. Akaunda Baraza la kijeshi la MCNR akaongoza mpk umauti ulipomkuta mwaka 2008. Utawala wake ulishuhudiwa ukandamizaji mkubwa uliofanywa na jeshi lake.
Mara tu Conté kufariki kiongozi mwingine wa jeshi alichukua madaraka. Ilikuwa masaa 06 baada ya ABOUBACAR SOMPARE (spika) kuapishwa kuwa kiongozi wa mpito Aliyefanya mapinduzi ni Kapteni MOUSSA DADIS CAMARA ambaye awali alikuwa akipinga hadharani unyanyasaji ktk utawala wa Conté.
Uvumi ulipoenea kwamba Kapteni DADIS amepanga kusalia madarakani. Wapinzani walipanga maandamano nchi nzima, ikatangazwa watu wote watakutania ktk uwanja wa
STADE DU 28 SEPTEMBRE uliopo mjini Conakry mnamo Septemba 28. Hii ndio siku watu 155 waliuawa na zaidi ya 1200 kujeruhiwa.
Kapteni DADIS CAMARA aliondolewa madarakani baada ya Jumuiya za kimataifa kuingilia kati.Kwa kushirikishana na Jeshi ilipangwa kufanyika uchaguzi unaotajwa ulikuwa wa kwanza kufanyika kidemokrasia tangia Guinea ipate uhuru. Uchaguzi ulifanyika 2010 na ALPHA CONDÉ alichaguliwa.
Hivyo Rais ALPHA CONDÉ ametawala toka mwaka huo mpk Juzi alivyopinduliwa akiwa ktk muhula wake wa TATU. Nimefanya hivyo ili yule ambaye hakupitia ule #Uzi wa nyuma aelewe ninachozungumzia.

Tuendelee..👇
ULINZI WA RAIS ALPHA CONDÉ

📋Nchi ya GUINEA kama yalivyo mataifa mengine duniani viongozi wa juu kitaifa hupewa ulinzi na kikosi maalum ndani nchi. Hapa kwetu Rais hulindwa na Usalama wa Taifa (TISS). Maafisa wa TISS huogopwa sana na wananchi wengi, na sio hapa Tanzania🇹🇿 pekee.
Idara hii pia, inaruhusiwa kuchunguza viongozi ktk wizara zote serikalini, mamlaka (Polisi, jeshi) yeyote na kadhalika. Ukiachana na kukusanya taarifa za kiintelejensia na kiusalama, kuzichambua na kuzitumia kuzuia vitendo vyovyote vya kiadui vinavyoelekezwa ktk JMT.
Hufanya kazi ya kumshauri Rais kuhusu masuala mbalimbali ya kiusalama ili kuvifahamisha vyombo vingine vya dola kuhusu uwezekano au kuwepo kwa vitendo vya uhalifu au uasi. #vitendo hivyo ni km:UJASUSI, uhujumu, ugaidi, uhaini pamoja na kudhibiti watu wanaopanga kupindua serikali.
#TISS jukumu lake la kwanza ni kulinda viongozi wakubwa wa nchi (VIP).

Hivyo, imepewa mamlaka ya kumchunguza mtu au kikundi cha watu au Taasisi yoyote, endapo inayo sababu ya msingi (reasonable cause) kuwa mtu (watu) fulani ni chanzo au anahatarisha usalama wa kiongozi wa JMT!
Na SUALA la kutambua kinachohatarisha usalama (identified threats & vulnerabilities) na kuwalinda viongozi ni kwa masaa 24 BILA kukoma!!

#MFANO; Rais wa JMT hulindwa na watu 40 wanaoonekana na wengine 48 wasioonekana, ILA kukiwa na hali ya hatari kiwango cha ulinzi huongezeka.
#VicePresident hulindwa na watu 15 wanaoonekana na wengine 10 wasioonekana, zingatia kukiwa na hatari ulinzi huongezeka. PM MAJILIWA mnavyomuona hulindwa na watu 15 wanaoonekana na 8 wasionekana na huongezeka ktk hatari.

#Inshort:Viongozi wa nchi huwa wanao ulinzi mkali
Idara hii ktk nchi nyingi hutuhumiwa kwa mauaji ya kimya kimya.

#MFANO:TISS🇹🇿 imewahi kuhusishwa na vifo vya Katibu Mkuu wa CCM, marehemu HORACE KOLIMBA, Prof. KIGOMA ALI MALIMA (babaake Adam Malima) aliyekuwa Waziri wa Uchumi serikali ya awamu ya pili na kifo cha Mzee MAHIMBO.
Muundo wa utendaji kazi wa Usalama wa Taifa (TISS) umegawanyika ktk Idara 6:
📡Idara ya vita,
📡Idara ya siasa,
📡Idara ya uchumi,
📡Idara ya mambo ya nje,
📡Idara ya mambo ya ndani
📡Idara ya ukusanyaji na uchakataji TAARIFA!!

Idara zote huripoti kwa Mkurugenzi Usalama Taifa.
Tangu TISS ianzishwe imewahi kuongozwa na wakurugenzi takribani 09. Wa kwanza ni mzee EMILIO MZENA (1961-1975), aliyeaminiwa sana na Mwalimu Nyerere baada ya kuzima majaribio kadhaa ya kumpindua. Alipata umaarufu mkubwa kwa wananchi kiasi cha kujulikana kwa jina la 'MR SERIKALI'.
#Wengine ni Dr. LAWRENCE GAMA (PhD) 1975/78, Dr. HASSY KITINE (PhD) 1978/80, aliyeshika nafasi hiyo akiwa na miaka 33, akafuatiwa na Dr. AUGUSTINE MAHIGA (PhD) 1980-1983, pia aliteuliwa akiwa na miaka 35

Baadae MAHIGA alipelekwa kukaimu ubalozi Canada (Minister Plenipotentiary)
Kuna siri fulani ipo Dr. MAHIGA kupelekwa Canada.

DR. KITINE anakumbukwa jinsi TISS ilivyoshirikiana na Idara ya Usalama na Utambuzi Jeshini (MI) chini ya Meja Jenerali TUMAINIELI KIWELU wakaiteka ndege ya makomandoo kutoka Libya iliyokuja kumsaidia IDD AMIN ktk vita ya Kagera!!
Baada ya Dr MAHIGA kwenda Canada, Mwalimu alimteua Luteni Jenerali IMRANI KOMBE kuwa Mkurugenzi mkuu wa 5 wa TISS mwaka 1983. Mwl. Nyerere ametoka madarani mwaka 1985 akamuacha Lut. Gen KOMBE ktk Idara hiyo na alidumu hadi 1995

Najua unajiuliza mbona nimechimba hapa! Kuna kisa👇
#Haitosahaulika: Mnamo June 30, 1996, Lut. Gen IMRANI KOMBE, aliuawa na polisi @tanpol kwa madai kuwa walifananisha gari lake (Nissan Patrol) na gari iliyokuwa imeibiwa na mtuhumiwa ERNEST MUSHI maarufu kama "White".

Akiwa anatokea MOSHI kuelekea nyumbani kwake Maili Sita (HAI)
Lt. Gen Kombe alimininiwa risasi 04 kifuani😭 licha ya kushuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu (stretching out his arms after being suspected) km ishara ya kusurrender. Askari waliohusika na mauaji hayo walihukumiwa kunyongwa, lkn Rais Kikwete aliwapunguzia adhabu mwaka 2011.
Bado kifo cha Lut. Jenerali Kombe kina maswali mengi kuliko majibu, ipo siku nitaelezea hili ktk uzi mwingine.

Tuachane na TISS ya Tanzania, Uzi wake upo jikoni unakuja, Turudi nchini Guinea maana wkt mwingine nikikumbuka tukio km hilo huwa naumia sana!!

Ulinzi wa ALPHA CONDÉ👇
Kikosi cha Usalama wa Rais nchini Guinea kinafahamika kama "Bataillon Autonome de la Sécurité Présidentielle" (BASP). Kikosi hiki inaamika kinao walinzi 1170 vitengo mbalimbali km ilivyo nchi nyingi na kipo chini ta Rais. Maofisa usalama wa BASP wengi wao ni wa kabila la "Sousou"
#Usichokijua:Guinea ina makabila takribani 24, lkn yenye watu wengi zaidi ni Peuhl (Fulani) 41%, Malinke (Mandika) 33%, Soussou 12%, Kiss 05% pamoja na Kpelle 05%. Asilimia zilizobaki ndio makabila mengine na idadi yao sio kubwa. Nchi nzima watu 89% ni Waislam na Wakristo ni 07%
#UKIONA nimegusia kitu fahamu kina uhusiano na UZI unachotakiwa kufanya ni kuchukua 1 km @mkomonisti unabaki nayo kichwan Tuendeleee😂👇

Achilia wale wazee wa suti nyeusi, BASP huvalia kofia nyekundu na huchuliwa kutoka Airborne Troop Battalions (BATA) na wengine ni makomando
BASP ilikuwa haina wanajeshi, baada ya mapinduzi ya mwaka 2008, Kapteni MOUSSA DADIS CAMARA alianza kukibadilisha akiwaweka watu anaowaamini. Walinzi wengi wa Rais waliundwa kutoka ktk makabila yanayoishi maeneo ya msituni. ILI likitokea lolote popote awe na ulinzi wa uhakika.
Mlinzi mkuu wa Kapteni CAMARA alikuwa Komando JOSEPH MAKAMBO LOUA, ambaye nimekueleza alivyofariki dunia wkt akinusuru maisha yake.Msaidizi wake alikuwa Luteni ABOUBACAR DIAKITÉ, alifahamika "TOUMBA" na ndiye aliyeamrisha wanajeshi kuua waandamanaji ktk tukio la Sept28 uwanjani
#TOUMBA aliongoza Kikosi cha BASP, wakawafyatulia risasi waandamanaji pale uwanjani, wakakamata wanawake wakawabaka na kuwaweka vizuizini viongozi wa upinzani, ndio maana uliona Jumuiya za Kimataifa (AU, EU, UN, ECOWAS na ICC) ziliingilia kati mpk CAMARA akaondolewa madarakani.
Aliyeangushiwa lawama kufuatia mauaji yale ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa rais, Kapteni CLAUDE PIVI, aliyejulikana kama "COPLAN", huyu alikuwa kamanda wa ngazi ya juu anayesimamia usalama wa rais, aliwajibishwaa kwa vitendo hivyo ambavyo walinzi wa rais waliwafanyia wananchi.
MFUMO wa ulinzi wa rais ndivyo ulikuwa.Pale Ikulu km unavyoona picha hii hapa chini imezungukwa na UKUTA mrefu.Pia ili uweze kuingia ndani ni mpk upitie jengo la mikutano lililo mbele ya Ikulu ambapo maofisa usalama hukufanyia 'Advanced check-up' kabla ya kuruhusiwa kumuona rais.
Baada ya Kapteni DADIS aka IDD AMIN kuparazwa kichwani ktk shambulio lile lililomuua Makambo, alipoingia ALPHA CONDE madarakan aliweka walinzi wafuatao:

📋Protection Privée Sécurité (PPS)-42

📋Garde du corps personnel (GP)-08

📋Autonome de la Sécurité Présidentielle (ASP)-31
Kati yao hao wanane hawapumziki kabisa kwani ktk masaa 24 ya siku mlimzi mmoja hutumia masaa mawili tu kupumzika huku muda huo hao saba wakimlinda. Walinzi wote huripoti kwa mlinzi mlinzi mkuu (Grand protecteur personnel) wa rais na wote 81 huambatana naye kwenda popote alipo.!!
Hapo nimetaja upande mmoja wa
walinzi tu wanaohakikisha kuwa Rais haguswi kivyovyote vile. Lkn ukichukua wote kutoka vitengo mbalimbali mfn, Intelijensia, Ulinzi binafsi, Uchumi na siasa, pamoja na wanaohusika na ukusanyaji taarifa ndani na nje ya nchi ndio hufika jumla ni 1170.
Jengo la Ikulu lipo nyuma ya Bandari kuu ya Mjini Conakry, moja ya bandari zinazolindwa na vikosi maalum kutoka Navy's Army (Kuondara) wakisaidiana na Gendarmerie Nationale

Ikulu imepakana na ofisi km ifuatavyo:mbele kabisa lipo jengo la kanisa la kale ndio limetizamana na Ikulu
Kulia kuna wizara hizi: Uchumi, mipango, uwekezaji, balozi za Senegal, Ivory Coast na Filipino. Kushoto: wizara ya Elimu, Sheria, Kilimo, Afya, Viwanda, Madini, Nishati, Mambo ya nje, Usafiri, Ubalozi wa Ufaransa, Ujerumani, Malta, Nigeria, Ukraine na Mahakama kuu na usalama.
ILIKUWA RAHISI KUMKAMATA RAIS?

Licha ya ulinzi binafsi pamoja na uwepo wa kambi 03 za kijeshi ktk mjini huo,mapinduzi haya yamefanya watu kujiuliza maswali mengi.#Ilikuwaje rahisi rais CONDÉ kukamatwa?Ht wewe pia unajiuliza

Hebu nifuatilie tujue operation nzima ilikwenda vipi👇
Kesho Lazima iishe

📋Mamady Doumbouya ni nani?
📋Anayo pesa ndefu, ametoa wapi?
📋Ulinzi wa ikulu
📋Kanalo Doumbouya alichora vp plan kumpimdua rahisi
📋Wanajeshi 500 walivyodhibiti jeshi la watu 4,210
📋Full Operation

IKIWA unathamini nachokifanya
RT🔄 Follow me @Eng_Matarra
KANALI DOUMBOUYA NI NANI?

👩‍💻Mamady Doumbouya ni kijana mdogo sana kutoka kabila moja na Rais Alpha Conde na la pili kwa ukubwa nchini Guinea linaloitwa "Malinke au Mandika".Alizaliwa mnamo Machi 04, 1980 huko mkoa KANKAN uliopo mpakan karibu na nchi jirani za Ivory Coast na Mali
📡Akiwa na umri wa miaka 23 alijiunga na Jeshi la Ufaransa (French Legionnaire), ambako alipata mafunzo ya kijeshi na kisha akajiendeleza ktk vyuo mbalimbali vya kijeshi kabla ya kurejea nyumbani kwake Guinea ambapo pia mafunzo mengine amepata akiwa anatumia Jeshi la nchi yake.
Hadi sasa Mamady Doumbouya ktk mafunzo ya kijeshi CV yake ipo km ifuatavyo:
📋Mafunzo ya Kijeshi (Ufaransa)
📋Mafunzo ya Ukomando (Israel) 📋Mafunzo ya Ukufunzi (Senegal)
📋Mafunzo ya Kivita (Ufaransa)
📋Mafunzo ya Usimamizi Maafisa (Gabon)
📋Mafunzo ya Ulinzi na Usalama (France)
Lakini pia anao uzoefu wa kijeshi kwasababu amewahi kishiriki ktk:
📋Operation ya nje (Cote d'Ivoire)
📋Operation Maalum (Afghanistan)
📋Close Protection (UK & Cyprus)
📋Operation nyingine (Mali, Djibouti & Central Africa)
📋Mafunzo ya kupambana na Ugaidi "FLINTLOCK" (Mauritania)
Mwamba shule amepiga ana Master's Degree in Defense & Industrial Dynamics kutoka Pantheon-Assas University (Ufaransa) na tangia ameanza kusomea jeshi ametumia miaka 15

📋FLINTLOCK ni mafunzo aliyopewa na vikosi vya marekani vilivyoko ktk kambi za majeshi ya G5-SAHEL (Mauritania)
Mnamo 2012, Luteni SIDIKI akiwa Mkuu wa Baraza la Ulinzi alimtambulisha Doumbouya kwa AMARA CAMARA, Balozi wa Guinea nchini Ufaransa. Baadae 2017 alimjulisha Balozi huyo kuwa anataka kuitumikia nchi yake na alirejea nyumbani mnamo 2018 akiwa bado kijana baada ya kuitwa na Rais!!
Kipindi hicho alikuwa na cheo cha "KOPLO" tu, si unajua alikuwa nje ya nchi wazungu ni ngumu kupandisha cheo kikubwa mtu mweusi. Alivyorudi nchini Rais ALPHA CONDE alimteua kuwa In-Charge wa Special Force Group (SFG), kikosi kipya ambacho rais alikuwa ameanzisha ndani ya Jeshi.
Mamady alijulikana kwa mara ya kwanza mnamo 2018 alipojitokeza kwenye gwaride la kijeshi mjini Conakry ktk sherehe za maadhimisho ya miaka 60 tangia taifa hilo kupata Uhuru. Ktk sharehe hizo ndipo alipata umaruufu mkubwa akapandishwa cheo mpk anafanya mapinduzi alikuwa KANALI.
#Inshort: Huyo ndio Kanali Mamady Doumbouya aliyepindua nchi.

Nitamalizia mwishoni kumuelezea
📡 Utajiri wake
📡Familia yake na
📡Mengine kumhusu. Hebu kwanza tuangalie jinsi alivyompindua rais.

Mnisamehe🙏 nimeenda slow kutokana na network.
Endelea RT🔄 nifollow @Eng_Matarra
#Kimsingi, Ikulu ya Rais wa Guinea alimaarufu SÉKHOUTOURÉYA iliyopo ktk peninsula ya Kaloum imezungukwa na kambi 03 ya usalama zenye na walinzi hodari kutoka Idara ya usalama wa rais Bataillon Autonome de Sécurité Présidentiel (BASP), ambazo makao makuu yao ni kambi ya Makambo.
Kambi ya Makambo camp ipo 2.37Km kutoka Ikulu na walinzi wa hiki Kikosi cha BASP ni walinzi waaminifu (royal) kwa rais. Baadhi yao wamechukuliwa kutoka kwenye kikosi cha walinzi wa Chama tawala Rassemblement du Peuple de Guinée (RPG) na wana mafunzo na mbinu za hali ya juu.
Unaweza kudhani kwamba hawakuwa na silaha. Loh ulinzi wa rais bila shaka unafahamika, hata hapa kwenu mnamuona SSH alivyo na ulinzi mzito. Utaona ni mijitu yenye silaha (strong armed men) na ukicheza kidogo ktk ulinzi huo ooohh utajikuta ukisalimiana na uncle Magu huko ughaibuni.
Lkn asubuhi mapema ya Sept 05, Kikosi kidogo Maalum cha Jeshi kinachojulikana Special Force Group (SFG),wazee wa Red Beret walichezea kambi hizi 03 mchezo ambao ulifanikiwa kufunga barabara kuu inayoingia Ikulu ktk makazi ya ALPHA CONDÉ.Unaweza kufikiri walinzi walikuwa wamelala!
Hata Gen. BRUNO CLÉMENT-BOLLÉE, (Mfaransa), ambaye kwa miaka mingi amekuwa akifanya kazi ya kuliunda na kulisuka Jeshi la Guinea baada ya kuombwa na ALPHA CONDÉ, alipohojiwa na French24.com alithibitisha kuwa Ikulu hiyo ina ulinzi mkali kuliko ht Ikulu ya Ivory Coast!!
"𝑆𝑒́𝑘𝒉𝑜𝑢𝑡𝑜𝑢𝑟𝑒́𝑦𝑎 𝑤𝑎𝑠 𝑜𝑛𝑒 𝑜𝑓 𝑡𝒉𝑒 𝑤𝑜𝑟𝑠𝑡 𝑔𝑢𝑎𝑟𝑑𝑒𝑑 𝑝𝑎𝑙𝑎𝑐𝑒𝑠 𝑖𝑛 𝑊𝑒𝑠𝑡 𝐴𝑓𝑟𝑖𝑐𝑎, 𝑐𝑜𝑚𝑝𝑎𝑟𝑒𝑑 𝑡𝑜 𝒉𝑜𝑤 𝑤𝑒𝑙𝑙 𝑝𝑟𝑜𝑡𝑒𝑐𝑡𝑒𝑑 𝑡𝒉𝑒 𝑃𝑙𝑎𝑡𝑒𝑎𝑢 𝑃𝑎𝑙𝑎𝑐𝑒 𝑖𝑛 𝐴𝑏𝑖𝑑𝑗𝑎𝑛 𝑖𝑠, 𝑖𝑡’𝑠 𝑛𝑖𝑔𝒉𝑡 𝑎𝑛𝑑 𝑑𝑎𝑦".
Kanali Doumbouya alitoka na kikosi chake (SFG) kutoka kambi ya Kaleya iliyopo FORÉCARIAH umbali wa 85km kutoka mjini. Aliongozana na msafara wa magari 50 yakiwa na wanajeshi wenye silaha nzito (armed with machine guns), akaenda kuziba njia ya kuingia Ikulu mida ya saa 02 asubuhi.
Kanali Doumbouya aliondoka na kikosi kizima cha Special Force (SFG) kilichokuwa na wanajeshi wanaokadiriwa 500 na kwenda nao ktk Mission hii. Inasemekana mapinduzi haya aliyapanga ktk mwezi uliopita akisoma position za kujilindia ikiwa atakumbana na vizuizi vya kuingia Ikulu.
Alipofika mjini aligawanya vikosi vyake, kingine kilienda mpk yalipo makao makuu ya usalama wa taifa Makambo Camp, ambapo wakuu wote wa usalama, polisi na jeshi hukutana. Wakaiweka kambi chini ya ulinzi kuzuia walinzi wa rais (Presidential Guards) wasiweze kutoka nje kushambulia.
Kambi kubwa ya kijeshi ya ALMAMY SOMORY TOURÉ iliwekewa vizuizi na vifaru vikaelekezwa ktk kambi hiyo. Upande wa kambi ya wanajeshi wa kikosi cha wanamaji cha Koundara nao vifaru 3 vilitumwa vikaelekezwa langoni. Sauti: "Yeyote atakayejaribu kutuzuia jeshi, tutaanza kushambulia."
Wakati huo, wanajeshi wengine kikosi No. 8602 (Special Unit-8602), ambao wamepewa mafunzo ya kijeshi kutoka nchini Ufaransa na Israeli, wakaelekea Ikulu ya SÉKHOUTOURÉYA yalipo makazi ya Rais ALPHA CONDE, wakiwa silaha nzito, mabomu pamoja na vifaru na magari makubwa ya kivita.
Kikosi 8602 kimeingia maeneo ya Ikulu, ALPHA CONDE akiwa ktk usingizi fofofo (fallen asleep at the first light of dawn). Kumbuka ilikuwa Jumapili (mapumziko) na amekuwa akisumbuliwa na tatizo la Insomnia kwa muda mrefu na karibuni alitoka huko SARDINIA (Italy) kwenye matibabu.
Akiwa huko Sardinia alimtembelea rafiki yake wa kipindi kirefu mfanyabiashara mkubwa mwenye asili ya Italy na Eritrea, MAKONNEN ASMARON, ambaye alikuwa akijiandaa kutembelea mji wa Conakry wkt wa ziara ya Rais ISAIAS AFWERKI wa Eritrea, iliyopangwa kufanyika Septemba 09, 2021.
Hivyo, Rais CONDE mzee mwenye umri wa miaka 83, anayeishi pekea yake ktk kasiri kubwa lililojengwa na Wachina kipindi cha Rais LANSANA CONTÉ, alikuwa kapumzika. Mke wake mkubwa DJENE KABA, anakaa mahali pengine na mtoto wake wa pekee MOHAMED CONDÉ anaishi San José huko Costa Rica
Makabiliano baina ya vikosi vya serikali na wakiongozwa na walinzi wa BASP yaliendelea japo kwa muda mfupi. Kulingana na habari walinzi 20 wa rais waliuawa, akiwemo Kanali YEMOIBA CAMARA, mkuu wa walinzi wa viongozi wa serikali. Pia wanajeshi 02 wawili wa SFG nao waliuawa.
Unaambiwa majibizano yalichukua karibu Dkk 73. Kikosi cha SFG kililenga risasi za moto mpk wakapasua madirisha ya vioo. Walinzi wakakimbilia ghorofa ya kwanza juu lkn walikuwa wameshachelewa haikuchukua muda wote wakadakwa na waliokuwa wamebaki wakasalimu amri kisha wakafungwa.
Lt. Kanali MAMADOU ALPHA KALOKO, ambaye ndiye Mkuu wa Kitengo cha BASP, akapata taarifa kuwa imesikika milio ya risasi ktk kambi ya Makambo zilipo Ofisi za Usalama.Akakimbiza gari spidi kwenda Ikulu kujua hali kiongozi wa nchi, akiwa na walinzi kadhaa, ile kufika tu naye akadakwa
Rais Conde, ametoka chumbani kuja sebuleni akakutana na majamaa yamesimama wakimsubili. Akataka kurudi ndani akaambiwa “If you move, we’ll shoot!” akawa mpole, lkn hajui hili wala lile. Kuangalia huku na kule hakumuona mlinzi wake hata mmoja. Ndipo akafahamu hali si hali shwari!!
Achana na walinzi wa nje, ktk Ikulu hii kuna walinzi kuanzia 06 ambao hawavai uniform kitaalam huitwa "Plainclothes Bodyguards" (PBG), ambao hukaa upande wa chini (ground floor) na lango la kuingia ndani. Na wengine juu ghorofani zilipo Ofisi yake na chumba ambacho huwa analala.
Kisha wakampeleka chini kwenye chumba cha kupumzika. Amefika anakutana na kijana wake aliyemwamini na kumpa cheo kikubwa ndio kuingozi wa uasi ule. Col. MAMADY DOUMBOUYA akamwambia akakae kwenye kiti. Alipokaa akaambiwa tena "stand up again and sit down".Hakuamini alichosikia😂😂
Naam hivyo ndivyo alivyokamatwa Rais ALPHA CONDÉ wa Jamhuri ya Guinea. Kuna chanzo kimoja kilisema ktk tukio hilo wanajeshi wa Kanali Doumbouya, walionekana wakizunguka ndani ya Ikulu, BILA shaka huenda walichukua pesa kwani viongozi wengi wamekuwa wakitunza pesa ndani ofisi zao.
Baada ya picha kusambaa mitandaoni, maeneo ambayo upinzani unakubalika sana, watu walianza kushangilia mitaani. Makao Makuu ya Wizara ya Mawasiliano Redio Rurale na Gazeti la serikali liitwalo HOROYA Na yalipo makao makuu ya chama tawala (RPG) na Tume ya Uchaguzi zilishambuliwa!!
Mwanzoni baada ya kambi za kijeshi kuzingirwa na vikosi vya Kanali DOUMBOUYA huku mapambano yakiendelea, Waziri wa Ulinzi, MOHAMED DIANÉ ambaye ni mtu wa karibu sana wa ALPHA CONDÉ, aliamini kuwa itawezekana kuzima jaribio hilo akisaidiana na wanajeshi waaminifu na polisi wa mji
Baada ya Rais kukamatwa na picha zake kusambaa ktk mitandao ya kijamii, mkakati aliokuwa amepanga kufanya ulikufa GHAFLA.

Moja baada ya nyingine, kambi zote za kijeshi Conakry pamoja na kambi za mikoa pembezoni mwa mji huo ziliungana na Kikosi cha Doumbouya ktk mapinduzi hayo.
#Sababu rahisi kwanini ziliungana ni MOJA, Mamady Doumbouya ni mzaliwa wa kabila Malike kutoka mkoa wa Kankan, kabila ambalo Rais ALPHA CONDÉ, Waziri wa Ulinzi pamoja na Maafisa Wakuu wa Jeshi wote ni wazawa wa kabila hilo. Hivyo Doumbouya kuwa dini tofauti haikuzingatiwa sana.
Rais ALPHA CONDÉ amekuwa akiamini sana jeshi lake kwasababu amelipigania kwa karibu miaka 25, tena akihatarisha maisha yake kipindi akiwa mpinzani nchini humo, hivyo alikuwa na hakika kwamba jeshi alilolijenga kwa mikono yake haliwezi kumuasi wkt kwa mihula 02 amelifanyia makubwa
📋PART C:

📡Doumbouya alipata wapi nguvu?
📡Familia & UTAJIRI kapata wapi?
📡Baada ya mapinduzi tutegemee nn?
📡Tofauti na @KagutaMuseveni hakuna kiongozi mwingine Afrika aliyepinga mapinduzi haya, #why?

Nilikuwa safarini...!!

Kupata muendelezo huu👇
RT🔄FOLLOW ME @Eng_Matarra
Rais CONDE wa Guinea alijiamini sana. Alikabiliana maafisa walionyesha kutofautiana na swahiba wake MOHAMED DIANÉ, waziri wa ulinzi..

“𝑰 𝒄𝒂𝒏 𝒃𝒆 𝒌𝒊𝒍𝒍𝒆𝒅 𝒃𝒚 𝒕𝒉𝒆 𝒂𝒓𝒎𝒚, 𝒐𝒓 𝒐𝒖𝒕𝒔𝒊𝒅𝒆 𝒕𝒉𝒆 𝒄𝒐𝒖𝒏𝒕𝒓𝒚 𝒃𝒖𝒕 𝒊𝒕 𝒄𝒂𝒏𝒏𝒐𝒕 𝒐𝒗𝒆𝒓𝒕𝒉𝒓𝒐𝒘 𝒎𝒆,”
Alipoingia madarakani alihakikisha baadhi ya watu wenye ushawishi mkubwa ktk Jeshi na waliotaka kupindua serikali ilizopita anawasafirisha nje ya nchi #Mfn;Jenerali EDOUARD THÉA alimpeleka nchini Angola na mtu mbadi IDDI AMIN Luteni ABOUBACAR SIDIKI CAMARA akampeleka Cuba.
Hivyo, Lawama za kupinduliwa kwake zinarudi kwake mwenyewe ALPHA CONDÉ.

Upofu wake dhidi ya Doumbouya ndio umemfikisha hapa. Hata Luteni ABOUBACAR SIDIKI CAMARA, alionekana kufurahia ujio wa Doumbouya na ghafla walikuwa marafiki utafikiri walikuwa wanafahamiana toka zamani.
Kumbuka nimekwambia 2012, Luteni SIDIKI akiwa Mkuu wa Baraza la Ulinzi ndiye aliyemtambulisha Doumbouya kwa Balozi AMARA CAMARA (Ufaransa). Baadae Doumbouya mwenyewe akaenda kumjulisha Balozi huyo kuwa anataka kuitumikia nchi yake. na alipokelewa na Rais Conde uwanja wa ndege.
Kanali Doumbouya alirejea Guinea, CV yake ikiwa hv👇
📋Mafunzo ya jeshi (Ufaransa)
📋Operation za nje (Afghanistan) 📋Operation nje (Cote d'Ivoire)
📋Mafunzo ya makomando (Israeli) 📋Mafunzo ya ukufunzi Gabon, akamshawishi Rais. Isitoshe kijana wa kabila lake kwanini asimwanini?
Kipindi hicho RAIS alikuwa akijivunia uwezo wa vijana wapya ktk jeshi lake.

Hivyo ujio wake aliufurahia sana na mara moja akamtuma Doumbouya nje masomoni ktk Chuo cha Mafunzo ya Kivita cha ÉCOLE DE GUERRE nchini Ufaransa ili akirudi akiongoze Kikosi cha Special Force Group (SFG)
Awali mpango wa Rais Conde juu ya kikosi hiki, ilikuwa baada ya mafunzo kipelekwe ktk mipaka ya nchi hiyo maeneo ya kaskazini ili kupambana makundi hatari ya "Jihad" yaliyokuwa yameanza kuibuka, lakini pia yalikuwa yameshakuwa tishio la amani ktk nchi jirani za Mali na Senegal.
Alivyorudi kutoka mafunzoni, kijana akaanza kupandishwa vyeo haraka haraka kutoka KOPLO kisha KAPTENI, mdogo mdogo akawa LUTENI KANALI ndani ya kipindi cha miaka 02 Tu. Mnamo 2 Oktoba 2018, akiwa na kikosi cha Special Force akatambulishwa na CONDE ktk maadhimisho ya miaka 60.
Alivutia sana umati wa watu hasa ktk onyesho ambalo walikuwa wanaruka hatua 28 kwa dakika moja.

Onyesho lililokuwa moto na mbwembwe sana mpk Rais DENIS SASSOU NGUESSO wa Kongo-Brazaville, ambaye zamani amewahi kuwa mtaalam mafunzo ya kuruka na parachuti kutoka akashangaa.
DENIS SASSOU NGUESSO alikuwa amealikwa ktk sherehe hizo, alipoona Kikosi cha Special Force Group kinavyofanya manuva pale uwanjani, aliinama akamuuliza ALPHA CONDÉ;
“You have all this??" swali hili lilimjaza Rais na raia wengi waliohudhuria walifurahia sana umahiri wa kikosi hiki
Rais Condé akawa amejazwa amejazika. Baadae alishare na marafiki picha zilizochukuliwa kwenye hafla ile. Kesho ktk kituo cha Television cha Guinea wakaendelea kumpaisha Kanali Mamady Doumbouya. Ktk kipindi Fulani kuna swali mtangazaji aliuliza “Did you see them?"

"Mmewaona?"😂
Wanawake wengi walipiga simu wakimsifia na kusema wametokea kumpenda wanatamani angekuwa mme wao. Kwa bahati mbaya kwao, tayari Kanali Doumbouya alikuwa ameoa!! Hata zilipovuma TAARIFA kuhusu Kanali huyu maarufu kuwa anataka kumpindua, Rais Condé alizipuuza, akasema ni wivu Tu.
Baadhi ya taarifa alizopokea:

📸Siku moja aliambiwa Doumbouya alikuwa akilalamikia maduka kuwa na bidhaa zisizo na ubora. Pia aliwahi kuambiwa kuna MTU kutoka MINUSMA (Mali) anatembelea majeshi halafu anaondoka. Achilia hizo na nyingine alizofikishiwa juu yake zote alizipuuza.
Lakini pia DOUMBOUYA akiwa km Mkuu wa vikosi maalum alionyesha kudharau uwezo wa jeshi la kawaida. Matukio haya yote yaliashiria ushirika wake na IDD AMIN (Gen. SIDIKI) ambaye yuko uhamishoni kidiplomasia (Cuba) na alishikiliwa kwa mashaka makubwa tu ya uasi dhidi ya serikali.
Kuanzia Aprili 2020, alianza kutofautiana na Waziri wa ulinzi MOHAMED DIANÉ, mzozo ambao ulizungumzwa sana ktk vyombo vya habari nchini humo.

Pia kipindi cha uchaguzi wa rais uliofanyika mwaka jana, Kanali Doumbouya aligoma kupeleka kikosi cha SFG kufanya ulinzi mjini Conakry.
SIO eti kisa kambi yake ipo mbali na mjini HAPANA!

Kutoka Kaleya, FORÉCARIAH mpk CONAKRY pana umbali sawa kutoka Chalinze mpk DSM.
#Inshort mwamba aligoma na ikaisha na hakufanywa kitu!!

Madai yake alisema ht angepeleka SFG hakiwezi kuzuia shida yoyote inayohusiana na uchaguzi.
Waziri DIANÉ alipopeleka tuhuma hizo kwa Rais ili aamue. ALPHA CONDÉ alichomjibu, kikosi kingine kichaguliwe na kile cha Doumbouya kibaki ili wajiandae kwa ajili ya uapisho wake.

Mamady Doumbouya akaendelea kuvimba kama BASHITE na Mwendazake na siku anaapishwa hakuhudhuria.!!
Baada ya kuona hivyo, ALPHA CONDÉ akafikiria ni wkt wa kutomuamini TENA mtu Yeyote akahitaji kuimarisha ulinzi wake sasa.

Mwanzoni kabisa mwaka huu (2021) vijana takribani 100 walichukuliwa na kupelekwa kwenye mafunzo ktk Kambi ya Soronkoni iliyopo mkoani Kankan.
Vijana hao walipelekwa kwa amri ya Rais Alpha Conde na wakufunzi walitumwa nchini humo kutoka kwa rafiki yake Rais ERDOGAN wa Uturuki. Lakini bado hakumfukuza Doumbouya. BILA shaka bado alikuwa hadhanii kuwa huenda ipo siku atakuja kumsaliti, ukizingatia pia ni kijana aliyemlea.
Rafiki yake na mtu ambaye kwa kipindi chote amekuwa akimshauri kuhusu masuala ya ulinzi na amekuwa pia akifunza jeshi la Guinea, Jenerali CLÉMENT-BOLLÉ alipokuwa nchini Guinea miezi miwili iliyopita alizungumzia juu ya hali ya kuhatarisha amani kati ya Jeshi na serikali.
“I had never seen the political climate so calm, so atonic. But at the same time, all the insiders were wondering about the special forces and their leader’s intentions.”
👩‍💻Kwanini kuanguka kwa CONDÉ kunaonesha watu wake wa karibu hawajajali?

📡#Iko hivi, mbali na lawama zilizotolewa dhidi ya Doumbouya na marais wa Ivory Coast, Togo na Kongo-Brazaville, pamoja na Katibu Mkuu wa UN, ANTONIO GUTTERES hakuna aliyesema Rais CONDÉ arudishwe madarakani
Pia kwa ukanda wa Afrika Rais ALPHA CONDÉ alikuwa na marafiki wachache sana. Lakini Je, umesikia chochote kwa viongozi waliokuwa karibu naye Rais LOIRENÇ wa Angola, RAMAPHOSA wa S. Africa au AFWERKI wa Eritrea wamesema nini? baada ya kupinduliwa kwake? Still wapo kimya
Ikiwa hiyo haitoshi tizama maswahiba wake Rais ERDOGAN wa Uturuki, XI JINPING wa China au Rais PUTIN wa Urusi wamefanya lipi? Bila shaka unawaona wapo kimya. Kati ya hao usimuweke EMMANUEL MACRON wa Ufaransa, yeye alipinga mwanzoni kabisa alipotangaza kuwania tena muhula wa Tatu!
Kutengwa huku JAMAA inaonesha hakuwapendeza wengi kutokana na utawala au sera zake, pia kufunga viongozi wa vyama pinzani na kutaka kudhibiti kila mtu.

Unaweza kuona maneno ya Jenerali CLÉMENT-BOLLÉE, ni ishara ukomo wa kubrashiwa viatu na kupigiwa saluti ilikuwa ukingoni.
Pia mgogoro na waziri mkuu IBRAHIMA FOFANA na malalamiko ya wakuu wa majeshi zamani Gen. NAMORY TRAORÉ na IBRAHIMA BALDÉ, kwa kutochukua hatua dhidi ya uasi wa zamani, ilizua maswali na kuonyesha kutoridhishwa kwao anavyotumia pesa kutengeneza jeshi wkt umaskini unakithiri nchini
Rais Condé, alikuwa akifahamu fika juu kutoridhika kwa viongozi hawa na aliahidi kuzungumzia hilo.

#Ile JIONI ya Tarehe 04 Septemba kabla ya kushiriki chakula cha jioni na wageni waliokuwa wamemtembelea Ikulu, alihutubia Taifa kuelezea mpango wake kiuchumi kuelekea mwaka 2030.
Ktk hotuba hiyo ambayo ilirushwa na runinga ya taifa alisema maneno haya;

“I’m going to reduce the army’s budget, there’s no point in creating problems.”

Kitu ambacho hakujua ni kuwa wkt huo wapelelezi wa Doumbouya walikuwa Tyr mjini ktk Hoteli ya KALOUM.
KALOUM HOTELS ni hoteli kubwa nzuri ilijengwa na Wachina yenye hadhi ya nyota 04. Ilizinduliwa mnamo Oktoba 2018 na ipo mita chache tu kutoka kwa kutoka Ikulu. Je, Kanali Doumbouya alifanya haya kwa kuhisi kibano naye kitamshukia? Na alifanya mapinduzi peke yake au alisaidiwa?
#1st: JAMII (makabila) ndani ya Guinea mpk sasa zimeonyesha kukubaliana na mapinduzi haya.

#2nd: Kingine, Yeye anatokea kabila Malinke/Mandika na ktk mahojiano yaliyofanywa na vyombo vya nje ilionyesha kuwa 90% walimlalamikia Rais Condé kwa utawala wake na wengi wamefurahia.
Haya ni mapinduzi ya 03 yaliyofanikiwa nchini Guinea baada ya yaliyoongozwa na LANSANA CONTÉ na MOUSSA DADIS CAMARA. Kawaida baada ya mapinduzi magereza mbalimbali mjini humo zilifunguliwa na wengi walipongeza tukio hilo. Lkn inasalia kujiuliza nini kitafuata baada ya hili
Kitaenda kutokea nn huko mbeleni?

#1st: Kwangu mimi nachokiona pengine taifa hilo sasa linaenda kutulia kwa kigezo kuwa ALPHA CONDÉ anatokea kabila moja na Kanali Doumbouya, hivyo sidhani km kabila moja hilo hilo litaunda UASI kumpinga mtu wao aliyeondoa utawala wa kiimla.
#2nd:Huenda upinzani ukaanza kutoka makabila MENGINE, kwa sababu sote tumeona dhahiri ni kwa namna gani Jeshi nchini humo likichukua madaraka limekuwa likijiangalia lenyewe peke yake badala ya kuwatumikia wananchi, hivyo huenda ikatokea mkwamo wa kisiasa na kiuchumi nchini humo.
#Hatima ya ALPHA CONDÉ, ikumbukwe jeshi limewahi kumkamata zamani miaka 1998, ambapo alikaa gerezani kwa miaka miwili na nusu, so hatma yake haina uhakika wa kuachiliwa. Na ikiwa Kanali Doumbouya hatarajii kumdhuru basi huenda akapelekwa uhamishoni au asipelekwe kabisa.
Kwa kuongezea hata akiachiwa hana pa kwenda zaidi ya Ufaransa, ambapo mali pekee aliyonayo nje ya nchi ni ghorofa iliyopo 'PLACE D'ITALIE aliyoipata wkt bado akiwa mpinzani?
Mtu anaweza kufikiria ni ufahari kuwa na uongozi wa kiimla ILA mwisho wake mbaya.

ALPHA CONDE kiburi chake kimevunjwa na watu wa karibu yake, heshima yake iko wapi? na utawala wa kimabavu aliofanya km dira yake wkt kesho yake haujui?

📸Wakati wa kujikosoa utakuja baadaye...!!
Kijana mwenzangu mwandishi mtaalam wa masuala ya siasa MAMADOU ALIOU BARRY (@alioubarry), ambaye pia anaongoza Kituo cha Utafiti & mipango nchini Guinea, alisema vikosi vya usalama vilitumika kukandamiza maelfu ya waandamanaji waliopinga 'Awamu ya TATU' ya utawala Conde.
"Nadhani yeye (akimaanisha Rais Condé) alitaka chombo cha usalama kwa ajili ya ulinzi wake binafsi na kikosi cha kukandamiza wapinzani wake kisiasa. Bahati mbaya kwake, wakati alipotaka kuviweka vikosi maalum kufuata amri yake pekee na ndipo vimemgeuka." alisema Barry
Kanali Doumbouya ambaye sasa ndiye kiongozi mpya wa Guinea-Conakry, anakuwa kiongozi wa pili mwenye umri mdogo barani Afrika, akimfuata aliyepindua serikali ya Mali, Kanali ASSIMI GOITA, ambaye alizaliwa mnamo 1983.
#Familia: Mamady Doumbouya ameoa mwanamke mzungu raia wa Ufaransa na anao watoto 3 na utajiri wake unakadiriwa US$ 5.5M sawa na Tshs. 12.7B, Fedha za kitanzania. Ukwasi wake unatokana na migodi ya BAUXITE (madini yanayotengeneza aluminium) na Baba mke wake ana kisima cha Mafuta!!
***Baba mkwe
"If the people are crushed their elites, it is on to the army to give the people their freedom" (maneno ya JERRY RAWLINGS, rais wa zamani Ghana) Doumbouya alisema maneno hayo baada ya mapinduzi.

"We will learn from the mistake we have committed and all Guineas will appreciate",
Aliongeza👇

"Ubinafsishaji wa maisha ya kisiasa umekwisha. Tutaweka mpango wa mpito ulio wazi na unaojumuisha watu wote. Tutaweka mfumo ambao (sasa) haupo. Hali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ktk nchi, ufisadi, ukiukaji wa haki za wananchi, kutoheshimu kanuni za demokrasia,
"Ubadhirifu wa fedha za Umma, umaskini kukithiri, ukandamizaji wa WaGuinea pamoja na utawala wa kujitengenezea katiba ili kuwamiliki wananchi ndio umesababisha la jeshi kuchukua madaraka."
"Lazima tusaidie watu wa Guinea kutoka katika hali hii kwasababu tunawahitaji. Tunamsihi kila mtu akae katika makazi yake aendelee na shughuli kama kawaida ikiwa pamoja na kulinda mipaka"

"Lengo letu ni kuhakikisha kuwa watu wa Guinea wana umoja na wanapata faida zote za nchi,
"Hatujaja kufanya mzaha na serikali.Tutajifunza kutokana na makosa yote ambayo tumefanya."

Maneno ya DOUMBOUYA baada ya kuchukua madaraka mnamo Sept 05, 2021 usiku. Baada ya hapo aliagiza viongozi wote wa serikali wafike ukumbi wa Bunge kuna kikao na serikali iliyo madarakani.
Mawaziri wa serikali iliyopinduliwa na maafisa wa serikali kutoka majimbo mbalimbali walipokea wito na kwenda makao makuu ya Bunge kwa mkutano, huku wakitahadharishwa wale wote watakaopinga. Mkutano huo ulifanyika ktk viwanja vya bunge na ulirushwa mubashara
Baada ya kufanya mazungumzo na viongozi hao wa utawala uliopita, Kanali Mamady Doumbouya ameahidi kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa na amehakikisha kwamba hakutakuwa na kamata kamata dhidi ya raia au viongozi wa serikali ya zamani au upinzani.
Viongozi waliotikia wito ni pamoja na Waziri Mkuu IBRAHIMA KASSORY FOFANA, Waziri wa Ulinzi MOHAMED DIANÉ, Waziri wa Usalama, Spika AMADOU DAMARO CAMARA, Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano BOUBACAR YASSINE DIALLO, M/kiti wa Tume ya Uchaguzi na Mkuu wa Mahakama ya Katiba nchini humo.
Kwanza ktk mkutano huo alipowasili Kanali MAMADY DOUMBOUYA, alilakiwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa kwenye viwanja vya bunge.

Na kabla ya chochote kuanza aliagiza watu wote mpk waliopo nje kukaa kimya dakika 01 kwa ajili ya kuwakumbuka wahanga wa utawala wa Rais Alpha Condé
Kulingana na msemaji wa jeshi mipaka ya nchi imefunguliwa tena kwa biashara na shughuli zingine za kibinadamu.

Siku ya Jumatano wiki iliyopita aliagiza pia kuwaachiwa huru kwa wapinzani wa Rais ALPHA CONDÉ, waliokuwa wakizuiliwa ktk magereza mbalimbali za kiraia mjini Conakry.
Miongoni walio achiliwa huru ni ABDOULAYE BAH (UFDG), ETIENNE SOROPOGUI (Valeurs Communes), ISMAËL CONDÉ, KÉAMOU BOGOLAN HABA (msemaji wa muungano wa Anad, unaojumuisha vyama zaidi ya hamsini vinavyomuunga mkono mwanasiasa wa upinzani CELLOU DALEIN DIALLO) na FONIKÉ MENGUÉ.
Watu wengi wamemkubali nchini humo. Kila mtaa ukipita ni mabango yake BILA shaka ni ishara njema kwake maana alikuwa kiongozi wa kijeshi, hivyo angekuwa kwamba ni kiongozi wa kisiasa tungesema ni wafuasi wa chama chake ndio wamepokea vizuri mapinduzi haya lkn sio.
📡Haihitaji nikuulize swali kwamba kupitia hili umejifunza nn? Umeona mwenyewe. ALPHA CONDE mtu mwenye ulinzi mzito, ushawishi wa kukusanya watu kiasi hiki wakamsikiliza na akawa Rais lkn AKAJISAHAU!!

📸UONGOZI unapita Tu!

💨Ukimtimzama ktk frame ya mwisho kuna cha kujifunza👩‍💻
Maneno ya Binti Marie Makambo yalimfanya Kanali Doumbouya kuungana na kikosi chake cha makomando kumweka chini ALPHA CONDE. Leo chini ya ulinzi anakula kwa masharti na jua, mikutano na watu mbalimbali pale Ikulu SEKOUTOUREYA Bila shaka ameshamiss ijapo ht mwezi haujaijaisha.!!
Mnamo Dec 02 ,1995, Meya wa Dar es Salaam na mbunge wa zamani Kigamboni, KITWANA KONDO akishirikiana na watu fulani aliamuru askari wa @tanpol & JWTZ, kuharibu ngano zaidi ya Tani 3, 800 mali ya BAKHRESA tena kukiwa zuio la Mahakama ILA leo hii mwanae anafanya kazi kwa Bakhresa📸
Tuachane na hayo...

📋Kanali Mamady Doumbouya, mpk sasa hv ndiye kiongozi wa Guinea na ulinzi wake sio haba zaidi ya walinzi 60 wanahakikisha haguswi. Narudia kusema maneno ya @JMakamba "Uongozi ni koti muda wowote unaweza kuvuliwa" na Tanzania tujifunze_____!!

#Mwisho..🙏🙏🙏
Uongozi ni huduma inayofumbatwa ktk haki na unyenyekevu.Mamlaka huendana na madaraka ILA Utumishi huendana na Heshima. Ukiwa Kiongozi kumbuka kuna MUNU aliyehai & Haki huinua Taifa
-Mithali 14:34

Kuendelea kupata nyuzi kama hizi

💨Easy Do It...👇

RT 🔄 FOLLOW ME @Eng_Matarra

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with JAPHET MATARRA

JAPHET MATARRA Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Eng_Matarra

Oct 19, 2021
NANI ALIYEMUUA SOKOINE?

#UZI

🔲Mnamo April 12, 1984 ilikuwa ni siku mbaya sana ktk Taifa letu na haitosahaulika kwa Watanzania. Siku hiyo tulimpoteza kijana makini aliyekuwa Waziri Mkuu EDWARD MORINGE SOKOINE, aliyefariki kwa ajali mbaya ya gari eneo la Wami-Dakawa (Morogoro). ImageImageImage
🔲SOKOINE mmoja wa viongozi bora nchini amefariki miaka 37 iliyopita akiwa na miaka 46. Ikiwa ulizaliwa kpnd hicho sasahv ushakuwa na watoto na pengine unaelekea wajukuu.

🔲Ingawa historia tumesoma ndio, ILA #chanzo cha kifo chake bado kuna utata kuna maswali YasiYo na majibu. Image
🎤Nimeamua tufukue makaburi najua hukuambiwa haya💣⤵️

🔲Hv NANI HASA ALIYEMUUA SOKOINE?

🔲ILIKUWAJE AKAGONGWA NA GARI La "Private" #KATIKATI Ya MSAFARA na kupelekea kifo chake (Tujuavyo msafara wa VIP unakuwaga na ulinzi wa usalama, hakuna gari linaruhusiwa kutembea hadi upite) Image
Read 111 tweets
Sep 26, 2021
PUTIN ANAVYOPINDUA VIONGOZI WA AFRIKA KUJIIMARISHA

#UZI:

💨Rais Alpha Conde (Guinea) alipinduliwa kwa msaada wa USA & Ufaransa, lkn kwa ASSIMI GOÏTA (Mali) alisaidiwa na Urusi.Pia mauaji ya IDRIS DÉBY (Chad) yalifanywa na URUSI
👩‍💻𝐌𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐌𝐚𝐳𝐢𝐭𝐨 𝐓𝐮𝐬𝐢𝐲𝐨𝐲𝐚𝐣𝐮𝐚👇
Mnamo Aprili 20, 2021 majira ya jioni zilianza sherehe huko La Brasserie Kiss, umbali wa 100M kutoka ktkt ya mji wa Bangui (Afrika ya Kati). Kila aliyepita huo mtaa aliona magari kadhaa yamepaki mbele ya nyumba moja ya Ghorofa 3, jumba ambalo ni kivutio kikubwa sana ktk jiji hilo
Jengo hili lipo nje kidogo ya mtaa maarufu wa DU COLONEL CONUS na ikifika usiku hupendeza sana kutokana na mng'ao wa taa ulioizunguka. Kulingana na saa kule ilikuwa mida ya saa 2 usiku hivi na kwa wenyeji wa mji huo, ni muda ambao amri ya kutotembea usiku huanza kutumika.
Read 17 tweets
Sep 18, 2021
𝐂𝐈𝐀 ILIVYOTUMIA MWANAMUZIKI ARMSTRONG KUMUUA PATRICE LUMUMBA (Congo)

#Thread

Mnamo Sept 19, 1960, Mkuu wa CIA huko Leopoldville (sasa Kinshasa) alipokea SMS kupitia chombo cha siri kutoka wakuu wake huko Washington. Mtu aliyejiita 'Joe from Paris' ndiye aliyepiga simu na ..
kumwambia angefika Congo kwa ajili ya Operation maalum.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa. Baadae mkuu huyo alionywa kutozungumzia ujumbe huo na mtu yeyote. Wiki 01 baadae 'Joe' aliwasili nchini humo.

Leo nikiwa nasoma kitabu cha 𝐖𝐡𝐢𝐭𝐞 𝐌𝐚𝐥𝐢𝐜𝐞 (Author: SUZAN WILLIAMS)
kilichotoka Agosti 20, 2021, nimejikuta nikiumia sana nafsi baada ya kufahamu jinsi Marekani ilivyomuua Waziri Mkuu wa kwanza wa DR-Congo, mzalendo wa kweli, kijana mdogo mrefu, mwembamba miaka 36, kwasababu tu USA iliogopa Umoja wa Kisovieti (USSR) ikaamua kumuua.
Read 120 tweets
Sep 9, 2021
MAPINDUZI YA GUINEA TZ🇹🇿 YA SAMIA INACHAKUJIFUNZA

#UZI

Ilianza kama utani Mzee Condé hakuamini kijana wake mwenyewe aliyemlea, mwenye masters ya vita na cheo akampatia alipomwambia "simama juu hlf ukae chini" Unadhani ilikuwa rahisi kumpindua? Naam It's #Guinea:1958-Present👇
Sikuweza kuandika Uzi yalipotokea mapinduzi ktk nchi nyingine mbalimbali, lkn kwa yaliyotokea jumapili nchini Guinea nimeona niandike ili Watanzania tuone km kuna lolote la kujifunza. Nitaangazia upande wa kisiasa tu. Nitachambua kila kitu kuanzia uhuru hadi kutokea mapinduzi.
Maswali nayotaka kukujibu km ulijiuliza ni haya:👇

💨Historia ya Guinea ikoje?

💨Kwnn mpk mapinduzi?

💨Col. Doumbouya ana nguvu gani

💨Kwann wananchi wamefurahia?

History repeats itself, 1st as Tragedy, second as Farce.
Just retweet 🔄 huenda siku
Uzi huu ukakukumbusha kitu
Read 211 tweets
Aug 18, 2021
WHO is '𝐓𝐀𝐋𝐈𝐁𝐀𝐍'? WANATAKA NINI HASA AFGHANISTAN?

#𝕿𝖍𝖗𝖊𝖆𝖉:
Ifahamike, walikuwa yatima ktk kambi za wakimbizi Pakistan.
Je, wana uhusiano na AL-QAEDA? #Tragedy:UINGEREZA & URUSI kuchezea kipigo cha Mbwakoko.
✴️Chimbuko
📡Walio nyuma yao?
📋Tofauti yao na MUJAHIDINA..
Vita vya Marekani nchini Afghanistan vimedumu kwa takribani miaka 20. Nimeona watu wengi wakitoa maoni juu ya Jeshi la TALIBANI kuchukua nchi Lkn wengi hawana historia juu yake. Wengine wanasema Rais wa Marekani @JoeBiden mefanya 'makosa' kuondoa majeshi yake.
BIG NO __Hapana.
Wengi tusichojua ni kwamba, huu ulikuwa ni uhalifu wa kivita na DICK CHENEY, aliyekuwa Vice President wa G. W BUSH na DONALD RUMSFELD, Kiongozi Mkuu wa Ulinzi kipindi cha Vita ya IRAQ (alishafariki), ndio walioiingiza Marekani kwenye shida hii unaiona Leo, kisa wanamtafuta OSAMA
Read 114 tweets
Aug 11, 2021
𝐅𝐀𝐇𝐀𝐌𝐔 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐉𝐈𝐍𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐈𝐊𝐎𝐀🇹🇿

#𝕿𝖍𝖗𝖊𝖆𝖉:
Tanzania ni nchi iliyoko Africa
Jina "𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚" lilipatikana kwa mashindano yaliyotangazwa mwaka 1964 na 𝐌𝐨𝐡𝐚𝐦𝐞𝐝 𝐈𝐪𝐛𝐚𝐥 𝐃𝐚𝐫 ndiye aliyelibun.Hivi unafaham asili ya jina la mkoa wako?
Ktk kipind cha 𝐔𝐤𝐨𝐥𝐨𝐧𝐢 Tanzania ilikuwa na utawala wa majimbo 8, Lkn baada ya #𝐔𝐡𝐮𝐫𝐮 mikoa ilianzishwa kwa miaka tofauti na mpk Leo hii ninavyoandika #Uzi huu 𝐌𝐢𝐤𝐨𝐚 31 imeanzishwa kutoka pande zote Visiwani na Tz Bara.Najua ulishawahi kujiuliza asili ya Mkoa wako
Kila Jina unalosikia lazima kuna chimbuko ambalo ndio Asili ya jina hilo. Aidha, yawezekana limetoholewa ktk lugha za kigeni na kuchukuliwa kutokana na matumizi yake, muonekano, lugha za asili ktk Eneo fulani, tukio ama hata tabia za watu wa eneo fulani na makosa ya kimatamshi
Read 158 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(