INTERNATIONAL TRANSFER CERTIFICATE (ITC)
Mara ngap umesikia story kuhusu ITC ? Unajua kwa nn khalid Aucho, Mayele, Djuma Shabani hawagusi gozi la ngombe?
Yes mchawi haswaa ni ITC yaan kwa kilugha cha shule za kidumu na fagio cheti cha kimataifa cha uhamisho.
ITC ni cheti ambazo kinatumika kuidhinisha uhamisho wa kimataifa wa mchezaji kutoka shirikisho moja kwenda lingine kwa lugha rahisi ni kuwa mchezaji huyu anahama kutoka nchi moja kwenda nyingine. Mfano usajili wa Prince Dube kutua matajiri wa Chamazi ulikamilika baaada ya ITC .
Kanuni ya 9 ya sheria ya Usajili na hadhi ya wachezaji ya FIFA inasema kuwa ITC inapaswa kutolewa bure bila masharti yoyote. Na endapo kutakua na kanuni yoyoye ambayo itakinzana na hii itakua haramu na batili.
ITC inatakiwa kutolewa kwa ajili ya mechi za kimashindano tu. Ndo maana tunaona wachezaji ambao hawana ITC wanacheza mabonanza .
ITC haitakiw kutolewa kwa mchezaji ambaye yuko chini ya Miaka 10.
Uhalali wa mchezaji wa kucheza mashindano ya Kimataifa ni lazima uwepo wa ITC .
ITC ndo leseni ya kumuwezesha mchezaji kutoka nchi Moja kwenda Nyingine.
Ni muhimu kwa team kuhakikisha zinapush upatikanaji wa ITC kabla ya kuanza kwa mashindano.
Ni vyema Club na Mashirikisho zikafanya kazi pamoja na haraka kuharakisha upatikanaji wa ITC.
KESI MAARUFU
SISTI MARISHAY (N/F OF EMMANUEL DIDAS V THE BOARD OF TRUSTEE (MOI),
PARMANENT SECRETARY MINISTRY OF HEALTHY AND SOCIAL WELFARE AND ATTORNEY GENERAL
Hii ni kesi ya madai ambayo msingi wake ni uzembe wa kitaalamu uliyopelekea kupotea kwa uwezo wa kiakili na kimwili wa
Ndugu Emmanuel Didas.Majira ya 26/10/2007 Didas(mhanga) alipata ajali mbaya ya pikikiki maeneo ya Morocco jijini Dar es Salaam.Mhanga alikua ni fundi an dereva pikipiki,baada ya ajali mhanga alikimbizwa hospitalini na kupokelewa MOI ambapo alilazwa.Madaktari wakaingia kazini
Kupitia X ray wakabaini mhanga amepata majeraha kwenye goti na kuna mfupa imevunjika (patella).Madaktari wakajipanga na ikapangwa tarehe 1/11/2007 bwana Didas afanyiwe upasuaji hapo ndipo songombingo zilipotokea.Siku hyo hyo Bwana Emmanuel Mgaya sio masanja @mkandamizaji alitaki
KESI MAARUFU
"PINGAMIZI LA AWALI"
POINT OF PRELIMINARY OBJECTION
MUKISA BISCUITS MANUFACTURING CO V WEST END DISTRIBUTORS LTD(1969)EA 696
Kama umekua mfuatiliaji wa masuala ya kesi Mahakamani pasi na shaka utakua umekutana na msamiati au neno maarufu la "PINGAMIZI LA AWALI"
PINGAMIZI LA AWALI ni hoja za kisheria ambazo zinawasilishwa na upande mmoja wa kesi mahakamani ambazo zikisikilizwa au kuendeshwa zinamaliza kesi husika. PINGAMIZI LA AWALI AU POINT OF PRELIMINARY OBJECTION al maarufu PO huwasilishwa mahakaman na upande wowote katika kesi
Katika hatua yoyote ya kesi. PO lazima zitokane na hoja za kisheria na blaa blaa . PO lazima ijikite kisheria zaidi na mahakaman ikikabuliana na hoja hzo kesi inaweza kuisha.
PO inaweza kuletwa kwenye hoja mbali mbali kama shauri liko nje ya muda,mahakama haina uwezo kushughul