NANI ALIYEMUUA SOKOINE?

#UZI

🔲Mnamo April 12, 1984 ilikuwa ni siku mbaya sana ktk Taifa letu na haitosahaulika kwa Watanzania. Siku hiyo tulimpoteza kijana makini aliyekuwa Waziri Mkuu EDWARD MORINGE SOKOINE, aliyefariki kwa ajali mbaya ya gari eneo la Wami-Dakawa (Morogoro). ImageImageImage
🔲SOKOINE mmoja wa viongozi bora nchini amefariki miaka 37 iliyopita akiwa na miaka 46. Ikiwa ulizaliwa kpnd hicho sasahv ushakuwa na watoto na pengine unaelekea wajukuu.

🔲Ingawa historia tumesoma ndio, ILA #chanzo cha kifo chake bado kuna utata kuna maswali YasiYo na majibu. Image
🎤Nimeamua tufukue makaburi najua hukuambiwa haya💣⤵️

🔲Hv NANI HASA ALIYEMUUA SOKOINE?

🔲ILIKUWAJE AKAGONGWA NA GARI La "Private" #KATIKATI Ya MSAFARA na kupelekea kifo chake (Tujuavyo msafara wa VIP unakuwaga na ulinzi wa usalama, hakuna gari linaruhusiwa kutembea hadi upite) Image
↗️ HISTORIA YAKE.!!↖️

(Kabla hatujaendelea)

🔲Alizaliwa mnamo Agosti 01, 1938, huko Kilasho kijiji cha Emairete wilayani Monduli (Arusha). Wazazi wake ni SOKOINE OLE SEVERE (Baba) na NAPELEL SINYATI NOOMAYAKI (mama)

💨Mnaotokea Monduli Juu mnaweza kuwa mnaifahamu familia hiyo. Image
🔲Alianza Shule ya Msingi Monduli (1949-1953) na kisha akajiunga na Monduli Middle School (1953-1956). Baada ya kufaulu alichaguliwa Umbwe sekondari, ambapo alipata elimu ya upili na mnamo Januari 01,1961 alijiunga na TANU na ni miongoni mwa vijana waliopigania Uhuru wa nchi hii.
🔲Mnamo 1962, SOKOINE alienda nchini Ujerumani Magharibi kusomea mambo ya utawala na kurejea mwaka 1963. Baada ya kurejea alipangiwa kazi kama District Executive Officer (DEO) wilaya ya Maasai. Aliendelea kufanya kazi kwa weledi mkubwa na utendaji wake ulisifika sana.
🔲Mnamo Septemba 30, 1965 akiwa kijana mdogo miaka 27 na smart, aliamua kugombea ubunge jimbo la Maasai, mpinzani wake akiwa EDWARD CARLO BONIFACE OLE MBARNOTE aliyekuwa Chifu wa kabila la Wamasai. SOKOINE aliibuka mshindi kwa kura 6,977 dhidi ya kura 871 alizopata Chifu MBARNOTE
🔲Mnamo 1967, SOKOINE aliteuliwa na Mwl Nyerere, kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Usafirishaji na Kazi na ilipofika 1970 alipandishwa hadhi akateuliwa kuwa Waziri wa Nchi. Alijulikana sana kutokana na uchapakazi wake tangu akiwa Naibu Waziri kila kona ya nchi sifa zake zilipenya
🔲Mnamo 1971, ktk kikao cha NEC ya TANU EDWARD SOKOINE alizikonga nyoyo za wajumbe kwa hotuba nzito aliyotoa kuhusu nchi kujilinda. Baada ya hotuba hiyo Mwl. NYERERE alimuita chemba KINGUNGE NGOMBARE MWIRU na kumtaka maoni yake kuhusiana anavyomuona kijana huyu
🔲Kufuatia hotuba hiyo mnamo 1972, Mwl. Nyerere alimteua kuwa W/Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

🔲Chama cha Mapinduzi (CCM) kimezaliwa kutoka TANU na ASP, trh 05-02-1977, akawa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na siku chache baadae Feb 13 mwaka huo huo akateuliwa kuwa Waziri Mkuu.
🔲SOKOINE alikuwa kiungo muhimu kwenye Vita Ya Kagera 1979.

🔲Kabla ya vita kuanza, aliwaagiza maRC's wote wakusanye nyenzo zote ili kumtandika Nduli IDDI AMIN DADA. Mnamo Januari 23, 1979, aliingia mwenyewe huko kambi ya Mutukura lilipokuwa jeshi ambapo baadae tulishinda vita.
🔲Kutokana na vita hivyo, SOKOINE alikuwa halali usingizi hali iliyopelekea afya yake kuterereka. Alijaribu kutibiwa nchini lkn hakupona na Nov 1980 aliomba kujiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu akaondoka kwenda kutibiwa Yugoslavia.

💨Leo hii hayupo waziri anayeweza kufanya hivyo.
🔲Nafasi yake ikashikwa na CLEOPA DAVID MSUYA. Baada ya kurejea nchini Mwl Nyerere alimteua tena kuwa Waziri Mkuu mnamo Februari 24, 1983. Ndio mwaka huo SOKOINE alianza kusomea shahada ya sayansi ya siasa (Political Science). Lengo kubwa ni kuongoza nchi ktk weledi mkubwa.
🔲Mnamo huo huo (1983) aliokuwa amerudi shirika la usafiri (UDA) lilipata changamoto ya ongezeko la wasafiri jijini Dar es Salaam mpk ikawa kero. Baada ya kushindwa kutatua changamoto hiyo SOKOINE aliita viongozi wa UDA wamweleze kwanini wameshindwa.
🔲Alipogundua kuwa hakuna njia mbadala ambayo UDA wangeweza kushughulikia suala hilo, aliwaruhusu wamiliki binafsi wa magari ya usafiri kuungana na UDA kutatua changamoto hiyo, lakini walitakiwa kuilipa UDA kiasi kidogo kutumia leseni zao.
↗️Najua wengi hatufahamu asili ya neno "𝐃𝐚𝐥𝐚-𝐝𝐚𝐥𝐚" pia limetokana na SOKOINE.

🔲Kpnd aliporuhusu gari binafsi kutoa huduma ya usafiri US$ 01 ilikuwa Tshs 05/=. Makondakta walitumia neno "dala 1" walipodai nauli iliyokuwa sawa na sh. 5/= neno daladala likaenea hadi Leo. Image
🔲NI mwaka huo huo Mwl Nyerere alianzisha kampeni ya kupambana na wahujumu uchumi na mnamo Aprili 05 Sheria (The Economic Sabotage Act No. 9 of 1983) ilipitishwa. Na ilikuwa moja ya kazi aliyokabidhiwa EDWARD MORINGE SOKOINE, kuhakikisha wanaohujumu Taifa wanakamatwa.
🔲Sheria hiyo ilimtaka kila mtu bila kujali cheo chake aeleze mali alizokuwa nazo na wapi alizipata. Kwahiyo zilianzishwa Mahakamani Maalum na Mawakili (advocate's) hawakuruhusiwa kuingilia. Watu walitakiwa wajitetee wenyewe baada ya kuona wangeweza kutumia mawakili wakaachiwa.
🔲NI mwaka huo huo Mwl Nyerere alianzisha kampeni ya kupambana na wahujumu uchumi na mnamo Aprili 05 Sheria (The Economic Sabotage Act No. 9 of 1983) ilipitishwa. Na ilikuwa moja ya kazi aliyokabidhiwa EDWARD MORINGE SOKOINE, kuhakikisha wanaohujumu Taifa wanakamatwa.
🔲Sheria hiyo ilimtaka kila mtu bila kujali cheo chake aeleze mali alizokuwa nazo na wapi alizipata. Kwahiyo zilianzishwa Mahakamani Maalum na Mawakili (advocate's) hawakuruhusiwa kuingilia. Watu walitakiwa wajitetee wenyewe baada ya kuona wangeweza kutumia mawakili wakaachiwa.
🔲Ktk zoezi hilo watu walimuogopa sana SOKOINE hasa jijini DAR. Unaambiwa maeneo ya Oysterbay & Upanga, vitu vya thamani na fedha, vilivyokuwa vimeingizwa kinyemela nchini vilitupwa mitaroni. Watu wakajiokotea ikabidi polisi waamrishwe kuokota fedha na kuzirudisha Benki Kuu (BoT)
🔲Vita hii ilimjenga SOKOINE kisiasa, lkn kwa upande mwingine ilimuongezea maadui hasa kwa viongozi waliokuwa wapigaji wakishirikiana na baadhi ya wafanyabiashara. Kutokana na jinsi zoezi lilivyoendeshwa kulitokea malalamiko mengi mpk SALIMN AMOUR, W/Mambo ya Ndani akaomba radhi Image
🔲Chanzo KILICHOPELEKEA kifo cha SOKOINE kilianzia hapa.

🔲Ingawa baada ya kifo chake, Sheria ile ya mwanzo, ilifutwa na ikatungwa nyingine (The Economic & Organized Crimes Control Act, 1984), ambayo mambo mbalimbali, mfn uwepo wa mawakili mahakamani yalirekebishwa.
🔲Mnamo Aprili 1984, ilikuwa ndio vikao vya Bunge la JMT vinaelekea mwishoni, kwahiyo Kiongozi EDWARD MORINGE SOKOINE alikuwa naye mjini Dodoma ili kufunga na kufuatilia ripoti za mwisho wa vikao, taarifa, na maazimio kwa wawakilishi wanapoelekea majimboni.
🔲Mnamo Jumatatu ya tarehe Aprili 9, 1984 SOKOINE alikwenda kusali Kanisa la St. Paul na usiku wa jumanne ya April 10 aliandaa karamu ya chakula cha jioni kwa Mawaziri na Wakuu wa Mikoa ambapo aliongea nao kuwasisitiza mambo mbalimbali ktk utendaji na baadhi wengine aliwakosoa.
🔲Mnamo April 11, 1984, ndio siku vikao vya bunge vilifungwa na Jioni aliandaa chakula kwa Wabunge wote wa mkoa Arusha, ambapo aliwasihi wafanye jitihada kuondoa umaskini kwa wananchi wao. Kabla ya hapo akiwa hajavunja bunge alitamka maneno haya:
"Ndugu Spika, ningependa kumalizia kwa kukubaliana na wabunge wote waliosema na ambao hawakusema lakini wana mawazo haya kwamba, jambo hili la kutumia fedha bila idhini ya bunge lazima tutafute kila njia ya kulikomesha".
🔲SOKOINE alipangiwa kusafiri kwenda Dar kwa ndege lkn akaamua kurudi kutumia gari na sababu ya kufanya hivyo alisema hivi......⤵️

"...Mungu akipenda tutakutana tena kwenye kikao kijacho cha bunge. Mimi nasafiri kwa njia ya barabara ili nijionee hali ya mazao ya wakulima..." Image
🔲Kilichofuata ni kwamba siku ya Alhamis mnamo April 12, 1984 EDWARD SOKOINE akiwa anatokea Dodoma kwa gari lake aina ya Mercedes Benz na msafara mkubwa uliosheheni magari ya usalama, aligongwa na gari (Land Cruiser) mali ya DUMISAN DUBE raia wa A/Kusini na kupelekea kifo chake. ImageImageImage
🔲SOKOINE sio kwamba alikuwa na afya mbovu! Hapana! Lilikuwa jitu la miraba minne.

🔲Pia sio kwamba gari lake lilikuwa mbele kabisa ktk msafara huo! Hapana! Lilikuwa #KATIKATI ya msafara huku tena alikuwa amekaa siti ya nyuma ktk gari. Image
#KINGINE Tujuavyo msafara wa VIP hupishwa na gari zote unapopita ndio huruhusiwa kupita.

🔲SASA NI NINI KILITOKEA!!

🔲ILIKUWAJE AKAGONGWA NA GARI LAKE LIKIWA KATIKATI YA MSAFARA?

🔲KWANINI SERIKALI HAIKUFANYA UCHUNGUZI JUU YA KIFO CHAKE?

🔲KUNA SIRI GANI? Image
🔲Ikumbukwe siku chache zilizopita Mzee Rashid Kawawa (Waziri wa Nchi-OR) ndio alikuwa ameuza meli ya umma kiasi cha 60M kinyemela na ameambiwa!!

↗️Narudia TENA kulikuwa na Siri gani? Na ni NANI aliyehusika mauaji ya EDWARD MORINGE SOKOINE?

Unataka Muendelezo huu? Image
↗️Mimi siuzi Nyuzi, huwa naandika na kushare nanyi bure kabisa. ILI kuendelea naomba urudi tweet ya mwanzo JUU kabisa halafu Retweet #UZI huu at least kuanzia RT🔄400 ndio niumalizie.

🔲Lengo Langu nataka uwafikie wengi wajifunze, pia usisahau kulike na kunifollow @Eng_Matarra. Image
↗️TURUDI NYUMA:

🔲Ktk yale mapambano ya wahujumu uchumi, moja ya watu waliopitia wkt mgumu ni EDWARD BARUGIRA BARONGO, aliyekuwa RC mkoa Kilimanjaro aliliwa kichwa na kuwekwa detention kwa kpnd cha miezi 04 hadi alipoachiliwa na Mwalimu.

🎤Najaribu kukumbushia Tu. Tuendelee..⤵️ Image
🔲Wiki chache baada ya uteuzi wake wa pili na kuwa tena Waziri Mkuu mnamo Februari 1983, ktk kikao cha Bunge mjini Dodoma, SOKIONE alitangaza kwamba, serikali inaruhusu uingizaji wa magari aina ya trekta, malori na double cabins sababu yataongeza ushuru kuliko magari ya kifahari. Image
🔲Baada ya kumalizika kikao hicho, alianza ziara ktk mikoa ya Dodoma, Singida na Kagera. Unaambiwa alipokuwa Singida mmoja wa viongozi mkoani humo alimfuata ACCADOGA CHILEDI aliyekuwa Press Secretary (PS) wake akamwambia,

"Mzee tumeisha mtayarishia blanketi chapa ya mtu".
#Blanketi akimaanisha "kimada" cha kujivinjari usiku. Bila shaka ni system ya viongozi wengi

🔲CHILEDI alimuuliza..

"Brother, Mhe. SOKOINE unamjua vizuri au unamsikia? Hilo blanketi lako ondoka nalo haraka na utoweke kabisa maana nikimjulisha ujue unapoteza kazi yako sasa hivi"
🔲Baada ya ziara ya Dodoma kish Singida, safari ilianza kwenda Kagera ktk ziara ya siku 03. Baada ya siku 02, alifika mkoani humo na alipanga aanzie Kambi ya kijeshi ya Kaboya iliyopo wilayani Muleba, kukagua makaburi zaidi ya 600 ambayo ni ya askari mashujaa wa Vita vya Kagera. ImageImageImage
🔲Alipokelewa na Kanali wa Jeshi akampeleka yalipo makaburi. Baada ya kufunga bendi nyeusi mkono wa kushoto, alizuru kaburi moja baada ya lingine kwa kutoa heshima. Kulikuwa na ukimya km Dkk 40, kiasi ht pini idondoke chini utaisikia na makaburi zaidi 70% yalikuwa ktk hali mbaya. ImageImage
🔲Kabla ya kuondoka, SOKOINE alimuuliza Afisa Mwandamizi wa Jeshi kwamba mifuko mingapi ya saruji inahitajika kujenga upya makaburi. Baada ya hapo aliondoka kwenda kupumzika yalipo makazi ya mkuu wa mkoa.

💨Najaribu kukupa historia ya nyuma ili twende sawa. ImageImageImage
🔲Safari ya kutoka Kaboya kwenda Bukoba mjini ilikuwa ngumu sana, ikizingatiwa kulikuwa na mvua nyingi, barabara za kizamani no Lami na usafiri iliokuwepo ni gari za LandRover achana na hizi za 8cylinder (LandCruiser), walihangaika hivyo hivyo wakafika Saa 10 Jioni wakiwa hoi ImageImage
🔲Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali KABENGA NSA KAISI, alimwalika Waziri Mkuu EDWARD SOKOINE, kula naye chakula cha jioni na baada ya msosi aliwambia wasaidizi wake wampigie Waziri wa Biashara na Viwanda, ambaye wkt huo alikuwa CLEOPA MSUYA. Muda mfupi simu iliita MSUYA akapokea. ImageImage
🔲SOKOINE alimwagiza CLEOPA MSUYA, mbele ya masikio ya watu wote pale kuwa, ahakikisha anachukua mifuko ya cement ya kutosha kujaza ndege 02 kutoka pale WAZO HILL, inapatikana kabla ya saa 04 asubuhi siku inayofuata na aipeleke uwanja wa ndege (JKNIA). Image
🔲Mara tu alipomaliza na kuongea na MSUYA alimwambia mkuu wa mkoa ampigie Mkuu wa Majeshi, Jenerali DAVID MSUGURI. Simu iliita akapokea na kumuagiza kuwa ahakikishe kabla ya kufika Saa 04 asubuhi ndege mbili za mizigo ziwe zimepatikana ili kubeba cement na kuipeleka Bukoba. ImageImage
🔲Siku iliyofuata, ambayo ndiyo alikuwa anamaliza ziara yake ya wiki Tatu, ilitakiwa wasafiri mida saa 10 jioni, kwa ndege ya Jeshi kutoka Bukoba kwenda Dar es Salaam. Ndege ya mwisho iliyopeleka shehena ya saruji Bukoba iliondoka na ujumbe wa waziri mkuu kurudi Dar es Salaam. Image
🔲Ktk ziara hiyo aliowachagua kumbatana naye walikuwa ni vijana wenzake wawili, MATERN LUMBANGA (kwao Morogoro) na PHILEMON LUHANJO (Iringa) waliokuwa chini ya Katibu Mkuu Kiongozi na LUHANJO alikuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri Ofisi ya Rais. Wkt huo wakiwa na miaka 40 hivi. ImageImage
🔲Wawili hao baadae walikuja kuwa Makatibu Wakuu Viongozi

🔲Huyu Dr. MATERN LUMBANGA alikuja kuwa Katibu Mkuu Kiongozi (1995-2006) ktk kipindi cha B.W Mkapa na PHILEMON LUHANJO alikuwa pia KMK (2006-2015) kipindi cha Kikwete. LUHANJO amewahi kutuhumiwa na ufisadi bungeni (2011). ImageImageImageImage
🔲Kpnd hicho marehemu HORACE KOLIMBA, ndiye aliyekuwa Katibu wa Kudumu wa SOKOINE, ambaye baadae aliwahi kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM kabla hajaondolewa na A.H. Mwinyi. Inasemekana TISS ndio waliomuua KOLIMBA (1997), nafuatilia vyanzo vyangu ili ktk Uzi wa TISS nichomekee. ImageImage
🔲Mwaka 1984 ulikuwa mwaka mgumu sana wenye matukio mengi ktk historia ya Tanzania. Njaa ilikuwa imetaabisha nchi na ndio kpnd ambacho mahindi yale ya rangi ya njano (yanga) yalinusuru kaya nyingi baada ya Marekani @usembassytz kutupatia msaada. Wengine ilikuwa hamjazaliwa bado. ImageImage
🔲Mwaka huu pia ndio kulikuwa na uhaba mkubwa wa mahitaji Muhimu ya nyumbani kama vile sukari, sabuni na chumvi. Mavazi na viatu vilikuwa vichache sana kiasi kwamba watu walilazimika kuvaa hata matambara ilimradi usitembee uchi.

💨Tuachane na hayo turudi ktk Uzi (ktk siasa)...⤵️ Image
🔲#Kisiasa;ktk miezi ya mwanzoni kabisa mwa 1984 ilikuwa muhimu sana nchini Tanzania, kilikuwa kpnd ambacho kila Mtanzania alifuatilia kujua ni nani atakuwa mrithi wa kiti cha Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere, aliyekuwa ameonesha dalili zote za kuachia madaraka na kustaafu.
🔲Tangu 1980 Mwl. Nyerere alikuwa akiwaambia mara kwa mara wasaidizi wake wa karibu na wanadiplomasia kwamba anafikiria kustaafu. Kwahiyo mwanzoni mwa 1983, ilikuwa wazi ndani ya CCM kwamba muda wake ulikuwa umekwisha. Na hii ilipelekea kuanza kwa siasa kali kutafuta mrithi wake. Image
🔲Swali ni nani anayemfuata lilikuwa suala la kubashiri.

🔲Kama ujuavyo Watanzania tunavyopenda mada km hizi za kisiasa ilikuwa gumzo. Sio vijiwe vya kahawa, vilabuni na ktk vimbweta huko vyuoni kila ulipokatiza mada ilikuwa kujadili nani anakwenda kumrithi Mwalimu.
🔲Serikalini ilikuwa ndio mwanzo wa fitina, chuki na magenge yameanza sasa na ndio wkt ambao SOKIONE alikuwa amerudi kutoka Yugoslavia kutibiwa na kuteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu.

🔲Pia ndio kpnd sheria ya Uhujumu Uchumi iliyokuwa imetungwa imeanza patashika kila kona ya nchi.
🔲Mpk mwishoni mwa 1983, watu wenye haiba fulani walikuwa wakitajwa tajwa.

🔲Ndio kpnd marehemu AUGUSTINE MAHIGA (mzaliwa wa Iringa) aliondolewa nafasi ya Mkurugenzi wa Usalama kutokana na kula njama na MSUYA ambazo zilibaki siri, akapelekwa mbali kabisa (Canada) kuwa N/Balozi Image
🔲Majina yaliyokuwa yanang'aa sana na kuonekana wanaaminika ktk uongozi yalikuwa 03: Waziri Mkuu EDWARD MORINGE SOKOINE, Katibu Mkuu CCM (wkt huo) Mzee RASHID KAWAWA na Rais wa Zanzibar (wkt huo), ABOUD JUMBE MWINYI ambaye pia kwa mujibu wa Katiba kpnd hicho alikuwa ni M/Rais JMT ImageImageImage
🔲Ingawa pia ktk Baraza la Mawaziri kulikuwa na mawaziri wengine mashuhuri waliotajwa na kufikiriwa kwamba wanaweza kushika nafasi ya Urais. Hawa si wengine bali ni CLEOPA MSUYA na Dkt SALIM AHMED SALIM. ImageImage
🔲Baada ya kumuondoa MAHIGA alimteua kiongozi wa jeshi, Gen. IMRAN KOMBE.

🔲Fitina zilianza mapema kabisa Januari 1984, ambapo JUMBE alilazimishwa kujiuzulu nyadhifa zake zote za chama na serikalini. Watu walisema JUMBE kulazimishwa kujiuzulu ilikuwa ni siasa za mrithi wa rais. Image
🔲Kujiuzulu kwa JUMBE kuliwaacha watu 02; SOKOINE na Mzee KAWAWA waliotizamwa sana kuwa mmoja wao atakuwa mrithi.

🔲SOKOINE akiwa W/M na Mzee KAWAWA akiwa W/Nchi-OR. Lkn ilionekana wazi anayefit zaidi ni SOKOINE aliyekuwa na miaka 46 pia misimamo yake ktk vita rushwa na ufisadi ImageImage
🔲Mtindo wake wa uongozi na sura yake ya ujana na nguvu alionekana kuwa kipenzi cha watu wengi. Hata Wananchi pia walionekana kupendelea SOKOINE kuliko Mzee KAWAWA. Fitina ikazaa chuki, chuki za kutafuta madaraka zikaanzisha mipango ya kumuua SOKOINE. Waliohusika wanaonekana hapo Image
🔲Najua mnasoma Uzi na mnaweza kuniita kunihoji, pia familia ya hawa ninaowataja wapo, lkn ukweli ni kwamba aliyepanga mipango hii alikuwa si mwingine bali swahiba wake mwalimu, Mzee Rashid Kawawa na CLEOPA DAVID MSUYA.

🔲KAWAWA alikuwa mtu mzima hata Mwl alikuwa ni mdogo kwake. ImageImage
🔲Kila mahali SOKOINE alipokwenda usalama wake ulilindwa na Jenerali IMRAN KOMBE kwa kuhakikisha wabaya hawa hawafikii kwasababu alipenda tu uchapakazi wake. Kuna siku alimuita nyumbani kwake akamweleza haya. Na kuanzia siku hiyo alianza kuwa makini.
🔲Kipindi hicho ndio SOKOINE alikuwa mkali sana kwa mawaziri wake. Mwalimu Nyerere alifanya safari ya ghafla na kwenda Msumbiji kwa Rais SAMORA MACHEL kuomba ushauri juu ya kasi ya utendaji wa waziri wake mkuu, kasi ambayo ilitishia usalama wake kuelekea urithi wake. Image
🔲Inasemekana ilivyoonekana ni ngumu kumfikia SOKOINE, ndipo njama za kutumia mbinu zingine za kumuua zilipopangwa. Pengine ndege iangushwe ama ktk gari. Hata siku ile aliyofariki ilikuwa afe kwa ajali ya ndege. Taarifa za kiintelijensia zilimfikia akabadili usafiri wa kurudi Dar
🔲Tatizo ni kwamba, SOKOINE alikuwa akitembea na wauaji Bila ya kutambua. Msafara wake walikuwa wamejaa. Taarifa hizi pia mdogo wake Mwl (Joseph Nyerere) alikuwa nazo ndio maana siku ile alipoenda kuona mwili wake alimuuliza Mwl kwnn hana ulinzi mpk Waziri Mkuu anafia barabarani.
🔲Nyerere alivyoona uvumi huo utasambaa, redioni alisisitiza Watanzania waamini kwamba SOKOINE alifariki kwa ajali ya gari na sio vinginevyo. Aliamuua kubeba mzigo wa rafiki yake ukizingatia miezi michache iliyopita alikuwa na tuhuma za kuuza meli ya umma kiasi cha Tshs Mil 60. Image
🔲Wengi walipata ugumu kukubali kwamba SOKOINE alifariki kwa ajali Tu. Kifo chake cha ghafla kilizua mada nyingi mitaani. Wapo waliosema ni njama za Urais. Wengine DUBE alipangwa kwa7bu alikuwa wa A/Kusini mipango isingejulikane na aliahidiwa pesa kirefu na kutofungwa miaka mingi
🔲Wandishi wameandika akiwemo MOHAMMED ALI BAKARI kitabu "The Democratisation Process in Zanzibar:A Retarded Transition", akifananisha na mauaji ya MAHATMA GANDHI (India) na YITZHAK RABIN (Israel) ImageImageImage
🔲LUDOVICK MWIJAGE pia anadai ktk kitabu chake cha "The Dark Side of Nyerere's Legacy" kwamba SOKOINE aligongwa kwa sababu za ustawi wa kisiasa. Anaongezea kuwa raia wa Mwafrika Kusini aliajiriwa ili kuepukana na kumtumia Mtanzania ambaye angejulikana kirahisi. Image
🔲Mwanadada DOROTHY HODGSON pia anasema ktk kitabu chake "Once Intrepid Warriors:Gender, Ethnicity and the Cultural Politics of Maasai Development", kwamba Sokoine aliuawa katika ajali ya gari ya kupangwa. Image
🔲Sio Tanzania Tu ajali ya Sokoine ilishawangaza watu. Nchini Zimbabwe wkt mke wa MORGAN TSVANGIRAI W/Mkuu wa zamani alipofariki kwa ajali ya gari mnamo 2009, rafiki yake THERESA MOKONE aliyekuwa W/Kazi aliomba uchunguzi ufanyike na kusema kifo chake ni sawa na cha SOKOINE 1984. Image
🔲Siku moja kabla ya kifo chake, SOKOINE alihutubia Bunge la Dodoma na kuibua masuala kadhaa ambayo alitaka maafisa wa serikali na mawaziri kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo. Pia alihita ufafanuzi. Taarifa ya kuonesha tahadhari ilianza alipohutubia na kusema "Tutakutana Dar." Image
🔲Siku ya tukio, SOKOINE aliondoka na msafara wake kutoka mjini Dodoma muda wa saa 4.30 asubuhi, akiwa ndani ya Mercedes Benz yake na msafara uliongozwa na msafara wa polisi. Magari yote yaliyokuwa yakikutana na msafara huo yalikuwa yakipaki pembeni kuupisha msafara wake upite.. Image
🔲Msafara wa SOKOINE ulikuwa na mwendo wa kasi (speed); kama "Minutes" za CC ya CCM ya April 17, 1984 ilivyoeleza-:

"... Msafara wa Sokoine uliondoka Dodoma majira ya saa nne na nusu asubuhi na ulikuwa ukienda kwa spidi ya kilomita 154 kwa saa". Image
🔲Baada ya gari hilo kufika eneo la Dakawa, ghafla kilisikika kishindo kikubwa. Gari la Mh. SOKOINE lilikuwa limegongana na gari aina ya Toyota Land cruiser lililokuwa likiendeshwa na Bw. DUMISAN DUBE (23), mpigania uhuru wa chama cha ANC, aliyekuwa akiishi Mazimbu, Morogoro. Image
🔲Licha ya DUBE kusimamishwa na hakusimama sbb nae alikuwa ktk mission na alikuwa kawapakia abiria 02 ambao ni BOYCE MOYE na PERCE GEORGE.

🔲SOKOINE jitu la miraba 4 alikuwa amekaa siti ya nyuma akiwa hajafunga mkanda na alirushwa kutoka nyuma hadi akagonga kioo cha mbele. Image
🔲SOKOINE alifanikiwa kutoka ktk gari akiwa mzima na wauaji ndio waliomkimbiza Hospitali ya mkoa Morogoro eti kunusuru maisha yake. Lkn kabla hawajafika walimalizia kumuua. Baada ya kufariki taarifa haikutumwa Ikulu haraka iwezekanavyo, kwanza walihakikisha wanaclear evidence. Image
🔲Hakuna bodigadi hata mmoja wa SOKOINE aliyeumia sana.

🔲SOKOINE pekeyake ndiye aliyepoteza maisha wengine wote walipata majeraha. YUSTO CHUMA, aliyekuwa bodigadi #1 wake alikaa kiti cha mbele kulia na ALLY ABDALLAH aliyekuwa dereva wake alikaa kushoto na walijeruhiwa kiasi. Image
🔲Ht kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi (Postmortem Report) juu ya chanzo cha kifo chake iliyowasilishwa mbele ya CC ya CCM, mbavu na mifupa ya mikononi na miguuni vilivunjika. Mbavu zilizovunjika zilipelekea kuchoma mapafu yake! Lkn kwa mujibu wa Dr SHABA aliyemfanyia postmortem
🔲Alisema alikuta risasi ktk mwili wake. Ingawa maneno yake yalipuuzwa wakasema alikuwa amelewa kwa7bu aliyasema akiwa Bar jijini Dar es Salaam.

🔲Mwl. alipopata taarifa hizi, hakuamini mpk madaktari walipothibitisha kifo chake. Unaambiwa aliingiwa na hofu kubwa iisivyo kawaida. Image
🔲Majira ya alasiri saa kumi (16:00pm) ya siku hiyo Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ilisitisha ghafla matangazo yake na kuanza kupiga "Wimbo wa Taifa". Baada tu ya kumalizika wimbo huo na kwa uchungu mkubwa, Mwl. Nyerere alitangazia Taifa msiba huo wa kihistoria huku akilia. Image
"Ndugu wananchi, leo hii ndugu yetu, kijana wetu, EDWARD MORINGE SOKOINE, Waziri Mkuu wa Tanzania, alipokuwa akirejea Dar es Salaam kutoka Dodoma, gari lake lilipata ajali na amefariki. Ndugu zangu Watanzania naomba muamini EDWARD amefariki kwa ajali ya gari na si kitu kingine". Image
🔲Baada tu ya Mwl. Nyerere kutoa taarifa hiyo alibubujikwa na machozi kutokana na uchungu mkubwa. Sio yetu bali vilio na simanzi kubwa vilitamalaki nchi nzima. Sio maofisini, vyuoni, mashuleni, hadi kwenye mabaa, mabarabarani, kote huko wananchi walionekana dhahiri wamevurugwa!. Image
🔲Kikao cha UWT kilichokuwa kikifanyika Ofisi za Lumumba, kilisambaratika ghafla bila hata Mwenyekiti wake, mama SOPHIA KAWAWA, kuahirisha kwani mara tu baada ya taarifa hiyo iliyoleta huzuni, jakamoyo na jitimai kubwa, wakinamama waliangua vilio kwa sauti za juu sana!. Image
🔲Serikali ilitangaza wiki mbili za maombolezo na kuamuru bendera nchi nzima kupeperushwa nusu mlingoti. Mwili wa marehemu EDWARD MORINGE SOKOINE uliwasili Magogoni Ikulu jijini DSM kutoka Morogoro mida ya saa 11 jioni siku hiyohiyo ukiwa umefunikwa kwa bendera ya Taifa🇹🇿. Image
🔲Mwl. Nyerere akiongozana na mkewe Mama MARIA waliusogelea mwili wake, kisha Mwl akaifunua ile bendera na kuweka mikono yake miwili ktk paji la uso wa SOKOINE. Kilichofuata yeye na Mama Maria aliyekuwa na kitambaa cheupe walilia sana kwa uchungu hadi wakaondolewa na walinzi wao. Image
🔲Hata mwandishi ATILIO TAGALILE wa "Daily News" ambaye wakati huo alikuwepo Ikulu aliandika-:

"Mwalimu Nyerere burst into tears and was whisked away by his bodyguards". Image
🔲Mdogo wa mwalimu anayeitwa JOSEPH NYERERE, ambaye aliyejulikana kwa kuongea ukweli bila kumung'unya maneno, alikwenda kwa kasi ulipokuwepo mwili huku akiwa na huzuni kubwa na akasema-:

"Mwalimu huna ulinzi. Waziri Mkuu anafia barabarani?!!!" . Image
🔲Pia Prof. ISSA SHIVJI aliwahi kufafanua jinsi Joseph Nyerere alivyoondolewa pale na walinzi baada ya kutamka maneno hayo na alitolewa nje kabisa.

"Security guards quickly whisked Joseph Nyerere away from the casket and he was driven away from the State house".
🔲Mwili wa marehemu SOKOINE ulipelekwa Hospitali ya kijeshi Lugalo kuhifadhiwa. Shughuli ya kutengeneza jeneza alipewa GEORGE CHRISTOS aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari aliyekuwa ni chotara. Baba yake alikuwa ni Mgiriki na mama yake Msukuma (mmoja wa mabinti wa ChIFU KIDAHA). Image
🔲Majira Saa 12 jioni ya siku hiyo, CHRISTOS na mkewe ELIZABETH WALKER pamoja na PAUL MKANGA Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, walienda hospitali kuchukua vipimo vya mwili wa SOKOINE. Kisha wakaelekea Chang'ombe kilipo kiwanda cha HEM-SINGH na bahati nzuri kilikuwa hakijafungwa.
🔲Kazi ya kutengeneza jeneza ikaanza mara moja na kumalizika usiku wa manane. Kisha ELIZABETH WALKER akalipamba jeneza hilo na kupelekwa kule hospitalini (Lugalo). Mipango ya kumuaga SOKOINE ikapangwa na watanzania hasa DSM na mikoa karibu walitaarifiwa ratiba ya kumuaga. Image
🔲Siku ya Ijumaa Aprili 13, maelfu ya wakazi wa Dsm na mikoa ya jirani walifurika ktk ukumbi WA "Karimjee Hall" kumuaga mpendwa wao marehemu SOKOINE. Kwa hakika umati uliokuwepo uliweka rekodi iliyovunjwa, ukiachana na umati uliojitokeza Octoba 21, 1999 kufuatia kifo cha Mwalimu. Image
🔲Mnamo Aprili 14, siku ya Jumamosi, mwili wa marehemu SOKOINE ulipelekwa airport kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Arusha kwenye mazishi. Unaambiwa daladala zote za Dar zilipeleka abiria bure airport kumuaga mpendwa wao kw7bu ndiye aliyeziasisi nimeelezea hapo Juu. Image
🔲Kaburi lake lilijengwa na MJ JOHN BUTLER WARDEN almaarufu "Black mamba", Mtanzania chotara akishirikiana na askari wa jeshi. Unaambiwa Black Mamba alifanya kazi nzuri kiasi cha kupewa mchongo wa kujenga kaburi la SAMORA MACHEL Rais wa Mchumbiji baada ya kufariki Octoba 19,1986. Image
🔲Kaburi lake SOKOINE halikujazwa mchanga lote, bali lilijengwa ktk muundo fulani hivi. Upande wa Juu kuliwekwa maji katikati ndipo lilikaa jeneza, halafu upande wa chini pia pakawekwa maji. Huyu MJ WARDEN alikuja kufariki miaka 09 iliyopita mnamo 2002 na kuzikwa jijini Mbeya. Image
🔲Mazishi ya marehemu SOKOINE yalipewa heshima zote na yalihudhuriwa na umati wa watu wakiongozwa na Baba wa Taifa. Mojawapo ya waliohudhuria OLIVER TAMBO aliyekuwa Rais wa ANC na Katibu wake ALFRED NZO. Walisikitishwa na kifo hicho kilichosababishwa na raia mwenzao wa A/Kusini. ImageImage
🔲Marehemu EDWARD SOKOINE aliacha wajane wawili ambao ni NAPONO na NAKITETO pamoja na watoto 11. Baadae mnamo Mei 17, 1984, aliyesababisha kifo chake, DUMISAN DUBE alifikishwa kwa mara ya kwanza ktk Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, ambapo kesi yake iliahirishwa. Image
🔲Mnamo Juni 12, 1984, upande wa mashaka ukiongozwa na JOHNSON MWANYIKA (SSA), ulitinga mahakamani na mashahidi 21. Na DUBE alisomewa mashtaka 07, ambayo yote alikiri kutenda makosa hayo na mhemimiwa SIMON KAJI (PRM) akamhumukumu kwenda jela kwa kifungo cha miaka mitatu...!!!🤔 Image
🔲Kingine, moja ya sababu ya kukataa chanzo cha kifo chake kwamba ni ajali Tu, kwanini hakufanyika uchunguzi juu ya ajali ya SOKOINE halafu taarifa itolewe kwa umma ukiacha ripoti ya Daktari iliyosomwa ktk kikao cha CC ya CCM Julai 1984 kule Dodoma na yenyewe haileti maana. Image
🔲Barabara hulindwa waziri mkuu anaposafiri kwa gari hapa nchini hilo sote tunajua. Magari mengine, ambayo sio sehemu ya msafara, yanawezaje kuingia kwenye msafara wkt kuna usalama? Ni wazi itifaki ilishindwa upande wa usindikizaji msafara na kupelekea waovu kupata nafasi. Image
🔲Halafu ktk hali km hiyo, iliyokuwa na maswali mengi hivyo, ilikuwaje UCHUNGUZI usifanyike?

💨Km walishindwa kampuni ya Mercedes Benz, ilitaka kufanya uchunguzi juu ya kifo cha SOKOINE kwasababu ilisema inaharibiwa soko lake lkn Mwalimu hakuwaruhusu? Bila shaka majibu mnayo.
🔲Baada ya kifo cha SOKOINE Mwl Nyerere aliogopa ilichukua takribani mwezi mzima hayuko sawa. Ni dhahiri alikuwa amechoka. Aliangalia Baraza la mawaziri asipate jibu, lkn mwishowe alimteua Dr. SALIM A. SALIM kuwa W/Mkuu na alikaa mpk Mwinyi alipoingia madarakani 1985 akamuondoa. ImageImage
🔲SOKOINE hakupenda utajiri. Maisha yake yalielezewa kwa ufasaha na mwalimu ktk msiba wake. Mshahara wa W/Mkuu kpnd hicho ulikuwa Tshs 3,000/=

"Edward hakuwa na mali yoyote ukiachilia ng'ombe wa urithi. Alikuwa na suti tatu na viatu pea mbili tu"- Mwl Nyerere siku ya mazishi. Image
🔲Mwanae JOSEPH EDWARD SOKOINE aliwahi kuwa Balozi na Naibu Katibu Mkuu. Lakini pia kitu ambacho huwa hakisahauliki ni kwamba, Gari aina ya LandCruiser ambalo lilimgonga SOKOINE, tokea kpnd hicho wati waliziita DUBE. ImageImage
🔲Marehemu EDWARD SOKOINE, mmoja wa viongozi bora kabisa kuwahi kutokea nchini. Mimi nasema alikuwa mzalendo wa kweli aliyewapenda wananchi wenzake kwa dhati kabisa ya moyo wake na aliyejitolea kwa hali na mali kuwasaidia ht alivyopambana na wezi wa mali za umma wala rushwa. Image
🔲Moja ya nukuu zake...⤵️

"Vijana wengi siku hizi wana mali kuliko wazazi wao waliofanya kazi kwa miaka zaidi ya 40 lakini wazee hao wanataka Serikali ndio iwaulize watoto hao wamepata wapi mali hizo. Mzazi unashindwa nini kumuuliza mwanao?"- Edward Moringe Sokoine Image
"Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi kuwa chombo cha kulinda haki na maslahi ya wengi. Kamwe hayaruhusiwi kuwa chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao".- Edward Moringe Sokoine Image
"Viongozi wanaoteuliwa lazma wawe wazalendo wa hali ya juu. Nasikia huko mikoani kuna viongozi wanagombania magari na nyumba. Mambo hayo si ya muhimu. Viongozi wanatakiwa kugombania maendeleo ya wanavijiji. Huu ndio ugomvi mtakatifu".- Edward Moringe Sokoine. Image
#RIP SOKOINE..

🔲Vita uliipiga mwendo wako uliumaliza. Bado Watanzania tunakukumbuka.

Mwisho___&&

Kuendelea kupata Nyuzi kama hizi

💨Easy, Do It........⤵️

💨Follow @Eng_Matarra 🙏🙏 Image
@threadreaderapp compile this

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with JAPHET MATARRA

JAPHET MATARRA Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Eng_Matarra

26 Sep
PUTIN ANAVYOPINDUA VIONGOZI WA AFRIKA KUJIIMARISHA

#UZI:

💨Rais Alpha Conde (Guinea) alipinduliwa kwa msaada wa USA & Ufaransa, lkn kwa ASSIMI GOÏTA (Mali) alisaidiwa na Urusi.Pia mauaji ya IDRIS DÉBY (Chad) yalifanywa na URUSI
👩‍💻𝐌𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐌𝐚𝐳𝐢𝐭𝐨 𝐓𝐮𝐬𝐢𝐲𝐨𝐲𝐚𝐣𝐮𝐚👇
Mnamo Aprili 20, 2021 majira ya jioni zilianza sherehe huko La Brasserie Kiss, umbali wa 100M kutoka ktkt ya mji wa Bangui (Afrika ya Kati). Kila aliyepita huo mtaa aliona magari kadhaa yamepaki mbele ya nyumba moja ya Ghorofa 3, jumba ambalo ni kivutio kikubwa sana ktk jiji hilo
Jengo hili lipo nje kidogo ya mtaa maarufu wa DU COLONEL CONUS na ikifika usiku hupendeza sana kutokana na mng'ao wa taa ulioizunguka. Kulingana na saa kule ilikuwa mida ya saa 2 usiku hivi na kwa wenyeji wa mji huo, ni muda ambao amri ya kutotembea usiku huanza kutumika.
Read 17 tweets
18 Sep
𝐂𝐈𝐀 ILIVYOTUMIA MWANAMUZIKI ARMSTRONG KUMUUA PATRICE LUMUMBA (Congo)

#Thread

Mnamo Sept 19, 1960, Mkuu wa CIA huko Leopoldville (sasa Kinshasa) alipokea SMS kupitia chombo cha siri kutoka wakuu wake huko Washington. Mtu aliyejiita 'Joe from Paris' ndiye aliyepiga simu na ..
kumwambia angefika Congo kwa ajili ya Operation maalum.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa. Baadae mkuu huyo alionywa kutozungumzia ujumbe huo na mtu yeyote. Wiki 01 baadae 'Joe' aliwasili nchini humo.

Leo nikiwa nasoma kitabu cha 𝐖𝐡𝐢𝐭𝐞 𝐌𝐚𝐥𝐢𝐜𝐞 (Author: SUZAN WILLIAMS)
kilichotoka Agosti 20, 2021, nimejikuta nikiumia sana nafsi baada ya kufahamu jinsi Marekani ilivyomuua Waziri Mkuu wa kwanza wa DR-Congo, mzalendo wa kweli, kijana mdogo mrefu, mwembamba miaka 36, kwasababu tu USA iliogopa Umoja wa Kisovieti (USSR) ikaamua kumuua.
Read 120 tweets
13 Sep
FULL OPERATION MAPINDUZI YA RAIS (GUINEA)

#Thread

Baada ya TALIBAN nchin Afghanistan, habari sasa ni MAMADY DOUMBOUYA kiongozi wa kijeshi huko Guinea, kumpindua rais na kuchukua madaraka #Unadhani kikosi kidogo cha SFG kiliwezaje kudhibiti kambi za kijeshi na kumkamata rais?👇
Yes, mwanajeshi wa zamani wa Ufaransa (French Legionnaire) aliyerudi nyumbani miaka 03 iliyopita na kuaminiwa na Rais ALPHA CONDÉ, ndiye aliyemsaliti na kumuondoa madarakani baada ya kutaka kuongoza nchi kwa muhula wa 03

MAMADY DOUMBOUYA ambaye ana cheo cha Kanali alionekana..
kwenye kituo cha Radio-Télévision Guinéenne(RTG), mnamo 5 Septemba majira ya saa 2 usiku, akiwa amevalia kofia nyekundu (Red Beret) ameweka bendera ya taifa hilo begani mwake, na kuzungukwa na wanajeshi wanane, akatangaza kuwa jeshi limechukua madaraka ya nchi.
Read 147 tweets
9 Sep
MAPINDUZI YA GUINEA TZ🇹🇿 YA SAMIA INACHAKUJIFUNZA

#UZI

Ilianza kama utani Mzee Condé hakuamini kijana wake mwenyewe aliyemlea, mwenye masters ya vita na cheo akampatia alipomwambia "simama juu hlf ukae chini" Unadhani ilikuwa rahisi kumpindua? Naam It's #Guinea:1958-Present👇
Sikuweza kuandika Uzi yalipotokea mapinduzi ktk nchi nyingine mbalimbali, lkn kwa yaliyotokea jumapili nchini Guinea nimeona niandike ili Watanzania tuone km kuna lolote la kujifunza. Nitaangazia upande wa kisiasa tu. Nitachambua kila kitu kuanzia uhuru hadi kutokea mapinduzi.
Maswali nayotaka kukujibu km ulijiuliza ni haya:👇

💨Historia ya Guinea ikoje?

💨Kwnn mpk mapinduzi?

💨Col. Doumbouya ana nguvu gani

💨Kwann wananchi wamefurahia?

History repeats itself, 1st as Tragedy, second as Farce.
Just retweet 🔄 huenda siku
Uzi huu ukakukumbusha kitu
Read 211 tweets
18 Aug
WHO is '𝐓𝐀𝐋𝐈𝐁𝐀𝐍'? WANATAKA NINI HASA AFGHANISTAN?

#𝕿𝖍𝖗𝖊𝖆𝖉:
Ifahamike, walikuwa yatima ktk kambi za wakimbizi Pakistan.
Je, wana uhusiano na AL-QAEDA? #Tragedy:UINGEREZA & URUSI kuchezea kipigo cha Mbwakoko.
✴️Chimbuko
📡Walio nyuma yao?
📋Tofauti yao na MUJAHIDINA..
Vita vya Marekani nchini Afghanistan vimedumu kwa takribani miaka 20. Nimeona watu wengi wakitoa maoni juu ya Jeshi la TALIBANI kuchukua nchi Lkn wengi hawana historia juu yake. Wengine wanasema Rais wa Marekani @JoeBiden mefanya 'makosa' kuondoa majeshi yake.
BIG NO __Hapana.
Wengi tusichojua ni kwamba, huu ulikuwa ni uhalifu wa kivita na DICK CHENEY, aliyekuwa Vice President wa G. W BUSH na DONALD RUMSFELD, Kiongozi Mkuu wa Ulinzi kipindi cha Vita ya IRAQ (alishafariki), ndio walioiingiza Marekani kwenye shida hii unaiona Leo, kisa wanamtafuta OSAMA
Read 114 tweets
11 Aug
𝐅𝐀𝐇𝐀𝐌𝐔 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐉𝐈𝐍𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐈𝐊𝐎𝐀🇹🇿

#𝕿𝖍𝖗𝖊𝖆𝖉:
Tanzania ni nchi iliyoko Africa
Jina "𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚" lilipatikana kwa mashindano yaliyotangazwa mwaka 1964 na 𝐌𝐨𝐡𝐚𝐦𝐞𝐝 𝐈𝐪𝐛𝐚𝐥 𝐃𝐚𝐫 ndiye aliyelibun.Hivi unafaham asili ya jina la mkoa wako?
Ktk kipind cha 𝐔𝐤𝐨𝐥𝐨𝐧𝐢 Tanzania ilikuwa na utawala wa majimbo 8, Lkn baada ya #𝐔𝐡𝐮𝐫𝐮 mikoa ilianzishwa kwa miaka tofauti na mpk Leo hii ninavyoandika #Uzi huu 𝐌𝐢𝐤𝐨𝐚 31 imeanzishwa kutoka pande zote Visiwani na Tz Bara.Najua ulishawahi kujiuliza asili ya Mkoa wako
Kila Jina unalosikia lazima kuna chimbuko ambalo ndio Asili ya jina hilo. Aidha, yawezekana limetoholewa ktk lugha za kigeni na kuchukuliwa kutokana na matumizi yake, muonekano, lugha za asili ktk Eneo fulani, tukio ama hata tabia za watu wa eneo fulani na makosa ya kimatamshi
Read 158 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(