Mjadala uliofanyika leo katika mkutano mkuu wa MEWATA kuhusu afya ya akili baada ya kujifungua, umenikumbusha mbali.
Siku moja napita round wodi ya watoto wachanga nawahimiza kina mama kunyonyesha watoto, mama mmoja aliniita “dokta ukimaliza njoo” #UZI #MEWATA2023
Nilipoenda akamchukua mwanae akanikabidhi mkononi akasema, “shogaangu hebu niangalizie mwanangu, maana mie sijielewi”
Nikamuuliza, “unajiskiaje” nikidhani labda ana shida ya mwili ili tuwaite watu wa wodi ya kina mama waje kumhudumia. Akasema, “yani nikimbeba hivi mtoto kumpa
maziwa, kuna sauti zinaniambia kabisa nimnyonge. Yani nawaza nimzibe pumzi afe. Sasa mi sitaki kumdhuru mwanangu, naomba unilelee tu”

Unajua hivi vitu ukivisoma kwenye vitabu vinaonekanaga kama utani fulani hivi hadi siku unakutana navyo. Nikawasiliana na in charge tukatoa
taarifa kwa kitengo cha magonjwa ya akili, tukampeleka akapata msaada. Baada ya muda akaruhusiwa na mwanae yupo vizuri kabisa hana shida huku akiendelea kuhudhuria kliniki.

Lakini huyu sio mwanamke pekee aliyepitia hali hii au inayofanana na hiyo. Kuna wengine wanawachukia
kabisa watoto wao hawataki hata kuwagusa.

Magonjwa ya akili kwa kina mama waliojifungua ni hatari sana kwani yanahatarisha afya yake na ya mtoto wake. Juzi hapa kulikuwa na yule mama aliyewanyonga watoto wake WATATU. Ni vile alikosa huduma za afya ya akili. Lakini kuna yule
mama aliwazamisha watoto wake watano kwenye maji bafuni kwasababu alikuwa anasikia sauti zinamwambia na alishatafuta msaada akakataliwa.

Kwanza suala hili linatukumbusha umuhimu wa kujifungulia hospitalini lakini pia umuhimu wa kuongeza juhudi za huduma za kliniki BAADA ya
kujifungua. Kuna video moja tiktok wanaonyesha ukiwa mjamzito namna unavyojaliwa na ukishajifungua yani macho yote kwa mtoto. Mara nyingi utaulizwa maziwa yanatoka, mtoto anashiba, kidonda kimepona, bado unatokwa uchafu na vitu kama hivyo. Tena kiukweli sehemu nyingine wataulizia
ishu za mtoto tu, zako labda utaulizwa uzazi wa mpango.

Pili, unyanyapaa unaokuja na masuala ya afya ya akili. Mara nyingi mawazo ya kujiua au kumuua mtoto wamama hawa hawasemi kwasababu hebu pata picha unamwambia mfano baba watoto au mama yako kitu kama hicho? Cha kwanza
utaambiwa una mapepo kama sio umepandisha majini. Jamii bado haina elimu ya kutosha kuhusu haya mambo. Utaambiwa mchawi kabisa.

Lakini pia uwaambie huna raha yani hutaki hata kumgusa mwanao, utaambiwa huna shukrani mtoto ni baraka, utaambiwa wewe sio mama bora na maneno mengi.
Kwahiyo mtu anajua kabisa nikisema vile najisikia nitaishia kuonekana mbaya anamezea tu mwisho inakuwa balaa. Inasikitisha. Inasikitisha mno.

Hali hii inaweza kumkuta mtu hata kama anasapoti kubwa kiasi gani kutoka kwa mwenza na familia yake. Naamini @mewata_tanzania wamefungua
njia ya mjadala muhimu sana. Huduma za afya ya akili ziingizwe kwenye huduma za mama na mtoto.

Maana ukuaji wa kimwili na kiakili wa mtoto unaathiriwa na afya ya akili ya mama kwani mara nyingi yeye ndio mlezi mkuu wa mtoto. Saa nyingine unakuta mtoto mchanga mama anafoka na
hata wakati mwingine anapiga kidogo aue. Wakati mwingine shida ipo kwenye akili.

Naamini matokeo ya mjadala huu yataleta mabadiliko chanya katika utoaji wa huduma za mama na mtoto. #DaktariMwandishi
@threadreaderapp unroll please

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Kuduishe Kisowile

Kuduishe Kisowile Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Kudu_ze_Kudu

Oct 3, 2022
When I saw a stream of blood down my leg, I knew right there and then; it’s happening! My worst nightmare was coming true and I couldn’t believe it because it was already days after delivery. I have NEVER been that terrified ALL MY LIFE.
This is my story: SURVIVING PPH #Thread 🧵
I tried to be calm, but I could hear my heart pounding in my ears. It felt like someone ripped out my heart and put it in speaker right next to my ears. I felt dizzy, so I sat down. I can’t tell if I was dizzy because of blood loss or the fear of becoming a statistic.
As we prepared to go back to the hospital, I tried so hard to appear calm; a big smile on my face but in my heart I was terrified. I knew it very well, PostPartum Hemorrhage is no joke. In a matter of seconds EVERYTHING COULD GO WRONG.
I asked for ONE thing: my rozary ring.
Read 24 tweets
Sep 26, 2022
Kuna safari hata ziwe fupi vipi, hazisahauliki. Hazisahauliki kwa mengi; watu uliosafiri nao, watu uliokutana nao, experience ya safari na mengine mengi.
Mimi safari hii pichani sitaisahau.
Nilipata wasaa wa kushare na @buguzi @NormanJonasMD @DrArabiFrank na @JuliethSebbaMD #UZI Image
Ilianza kama utani hivi, nikafahamishwa nimepata nafasi ya kufanya mafunzo Morogoro ambayo yaliandaliwa na @sikika1 na @tacaidsinfo
Na mimi mpenda safari na mpenda afya, naanzaje kukosa? Nikafungasha kibegi changu uelekeo mji kasoro bahari.
Moro bwana! Moro PAZURI NYIE! Basi tu. ImageImageImageImage
Katika mengi nilojifunza siku hizo mbili, kuna kitu kimoja kilichonivutia zaidi ya mandhari nzuri ya Morogoro, maana mara ya mwisho nilikuwa hapa ilikuwa ni trip ya Udzungwa na Mto Mawe.
Kitu hicho ni Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI Tanzania (ATF). Leo naomba niwashirikishe Image
Read 16 tweets
Jul 28, 2021
SEHEMU YA PILI #IjueChanjoNaDaktariMwandishi
Leo, saa 3 asubuhi, Rais SSH atazindua chanjo pale ikulu kwa kupata chanjo hiyo.
Wakati huo, tuendelee kujifunza kuhusu chanjo za COVID19 haswa aina ya Johnson&Johnson ambayo ndio imepokelewa. #UZI FUATILIA
#DaktariMwandishi
3. JE, NIKIPATA CHANJO YA COVID19 KUTANIFANYA NIWE NA SUMAKU (MAGENTIC)?

Hapana. Chanjo za COVID19 hazina uwezo wa kutengeneza "electromagnetic field" (uwezo wa wewe kuwa sumaku) na chanjo zote hazina metals.
Unaweza kuangalia nini kimo kwenye chanjo katika ukurasa wa CDC.
4. KWANINI BAADHI YA TAARIFA ZINASEMA TUMEPOKEA CHANJO YA JOHNSON&JOHNSON NA NYINGINE ZINASEMA "JANSSEN"?
Jina kamili la chanjo iliyopokelewa Tanzania kupitia mpango wa COVAX ni "Johnson&Johnson's Janssen(J&J/Janssen) COVID19 Vaccine" kwahiyo ni kitu kimoja wala si chanjo tofauti
Read 18 tweets
Jul 28, 2021
#IjueChanjoNaDaktariMwandishi
Bado naikumbuka siku ile ilipotangazwa chanjo ya kwanza ya COVID19, nilikuwa twitter, sikuwahi kufurahia matunda ya sayansi kama siku hiyo.
Wakati huo, tayari janga la COVID19 na upotoshwaji ulikuwa juu ...#UZI (SEHEMU YA KWANZA)
#DaktariMwandishi
kitu ambacho sikutegemea, ni upotoshwaji mkubwa zaidi uliokuja na chanjo.
Lakini, siwalaumu wenye maswali dhidi ya chanjo. Yapo maswali muhimu mno ambayo, hatuwezi kuyasukumia uvunguni kwa kigezo cha upotoshaji.
Ni lazima yajibiwe hata kidogo.
Nitajitahidi kutoa majibu machache.
Kabla sijajibu, naomba niseme kuwa ni sawa kuwa na maswali juu ya kile unachokipokea, lakini si sawa kusambaza taarifa za uongo na zisizo na ushahidi wowote.
Kufanya hivyo ni ugaidi. Ni uhalifu dhidi ya binadamu.
Kwanza niseme, mimi NAAMINI KATIKA CHANJO.
NAAMINI KATIKA SAYANSI.
Read 24 tweets
Apr 1, 2021
Just laying on bed, my body aching and my head is literally on fire.
Scrolling through same 3 apps, seeing excitements of a "long weekend" ahead.
Ooh! It dawns on me. It's Easter weekend.
My bad. I haven't been oriented to days of the week, only dates for some time because, you
know..work!
My work wants me to know date and time, I can barely differentiate a weekday and a weekend/holiday until I get on the road and wonder why the jam ain't like usual.
But, I love it here. I love this work. Maybe a lil' too much. Idk.
It's the one thing I've dreamt of all
my life, and worked for it all my life and it turned out not-so-perfect but absolutely how I wanted it to be. Idk if that makes sense lol.
But I love it here.

So, anyways. It's a bit rainy here. (well, it was). And that moment really brought a flash of memories in my head.
Read 18 tweets
Apr 1, 2021
I have to disagree with him.
These changes are NOT going to happen over a year, or decade maybe not even century.
Suffragettes fought for votes over 100yrs ago.
Yet even today, studies have shown that in some areas, women don't really have the freedom to vote for who they want.
I mean, there were cases the other year of divorces and DV because the wives voted for someone that their husbands didn't like. Actually, statistics show that DOMSTIC VIOLENCE cases go up during elections because of these incidents.
There are countries that allowed their women to
vote just few years ago.
But should we say the suffragettes of all countries work was just superficial because we still have issues in women voting? It is very ridiculous to do that.
The suffragettes and all other women movements are under the umbrella of feminism and have done
Read 21 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(