Haki Ngowi Profile picture
🌍 Official X(Twitter) Page Of Haki Ngowi ® 💻📱 Post(Tweets) From Haki Ngowi are signed hn+
Dec 4, 2021 4 tweets 1 min read
🔴Sababu za UTENGUZI

Rais Samia Suluhu Hassan amevunja bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL) na kuagiza wizara kuichukulia hatua bodi ya mamunuzi kwa kutoa tenda ya ujenzi wa meli 5 kwa kampuni ‘HEWA’. 🔷Maamuzi ya Rais Samia leo Dis. 4 yamefuatia uchunguzi wa kina uliofanywa na timu maalumu aliyoiunda kuchunguza uhalali wa kampuni ya Uturuki, YÜTEK iliyoshinda tenda kujenga meli tano za abiria na mizigo za kampuni ya Meli nchini.
Dec 2, 2021 6 tweets 1 min read
🔴UFAFANUZI

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Profesa Riziki Shemdoe ametoa ufafanuzi wa Agizo lililotolewa na Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu kupiga marufuku utaratibu wa Shule za Msingi na Sekondari kuwazuia wanafunzi kwenda Likizo na kusoma hadi usiku katika Muda wa Ziada. Image Prof Shemdoe amesema Kupitia Marekebisho ya Sheria ya Elimu ya Mwaka 1978,zilitungwa kanuni za Elimu za mwaka 2002.
Jun 23, 2020 6 tweets 2 min read
🔵MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia mashtaka Mfanyabiashara Mussa Mohamed aliyefikishwa mahakamani hapo leo Juni 23, 2020 akikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine. ImageImage Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali,Sylvia Mitanto kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Yusto Ruboroga kuwa upande wa mashtaka hauna nia ya kuendelea kumshitaki Mohamed kwa kosa hilo.
Apr 30, 2020 7 tweets 3 min read
🛑MKAZI wa Chanika jijini Dar es Salaam Seleman Mwamsumbwe ameomba kukutana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto @umwalimu kwa lengo la kumueleza habari njema ya kwamba amegundua dawa inayoweza kutibu ugonjwa wa #Covid19 unaotokana na virusi vya #corona Akizungumza na waandishi wa habari leo nyumbani Chanika huku akiwa na furaha na tabasabu tele Mwamsumbwe amesema kuwa dawa hiyo ambayo ameigundua hawezi kuitaja hadharani kwa sasa hadi pale atakapoona na Waziri Ummy Mwalimu.
Apr 2, 2020 4 tweets 2 min read
Mkurugenzi Msaidizi, Kitengo na Udhibiti wa Magonjwa ya mlipuko, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Janneth Mghamba (kushoto) kizungumza baada ya kumalizika mdahalo wa kimataifa kwa njia ya video kuhusu kukabiliana na virusi vya corona #COVID19 🦠 na athari za kuenea kwake. Mkutano huo uliandaliwa na Kituo Cha Mafunzo cha Kimataifa (TaGLC) kwa kushirikiana na GDLN, Korea leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo.Bw. Brown Hasunga