Kwenye gazeti la Sauti ya TANU la Tar. 7 Mei 1958, Nyerere alitumia maneno kama 'washenzi', 'maharamia' na 'magava wa mistuni' kuwaelezea ma-DC wakikoloni, DC Weeks wa Geita na DC Scott wa Songea.
Nyerere alihojiwa na ofisi za TANU kupekuliwa. Tarehe 9 Juni 1959 alisomewa mashtaka rasmi.
Kwa hali ya kisiasa wakati huo, endapo angelazimishwa kifungo, mapambano ya uhuru wa Tanganyika yangehamia kwenye silaha na vita.
Ulipo uwanja wa taifa sasa ulikua uwanja wa ndege. Nyerere alianza kuutumia baada ya mnazi mmoja kujaa mno.
Baraza la machifu wa Tanganyika wakati wa mkoloni lilikua linakutania Mzumbe, Morogoro (niliposoma sekondari lakini hili nilikua silijui).