Serikali na Idara zote za Ujasusi ulimwenguni kuna nyaraka ambazo zapaswa kuonwa na watu fulani pekee. Mara zote nyaraka hizi huwa na muhuri wa SIRI.
Pale Marekani kuna nyaraka 2 ambazo ni za siri kubwa zaidi lakini ajabu nyaraka hizi hazina muhuri wa "SIRI" na wala..

THREAD👇👇 Image
mpaka leo nyaraka hizi hazijawahi kuvuja kwa umma au mtandaoni. Nyaraka hizi 2 hazina majina mahususi lakini zinafanana kwa kiasi fulani na nyaraka za Idara yetu ya Usalama wa Taifa hapa nchini ambayo zinaitwa "Site Post Assignment Logs".
Nyaraka ya kwanza inaonyesha maafisa wa..
Idara ya Usalama kitengo cha Ulinzi wa Rais majukumu yao na namna gani watajipanga katika kumlinda Rais kwenye tukio fulani. Lakini pia mbinu ambazo zitatumika kuimarisha ulinzi pamoja na mkakati wa dharura wa kumuokoa Rais kama likitokea shambulio.

Nyaraka ya pili yenyewe ni..
Mahususi kabisa kwa ajili ya ku-track movement za Rais kwa siku nzima. Hii yenyewe inaonyesha mwenendo wa Rais wa siku nzima kabla siku haijaanza. Yaani atakwenda wapi, atapita njia gani, atasalimiana na nani, kama ni jengo basi atapanda lift ipi, kama ni hafla fulani basi lazima Image
ionyeshe atakaa upande gani wa meza, kiti kipi n.k.

Kwa namna ambavyo nyaraka hizi ni sensitive zinapaswa kuwa na mihuri ya siri (CLASSIFIED).

Sababu kuu kwa nini haziwekwi muhuri wa SIRI ni vile kwamba inapaswa kuonwa na watu wengi ndani ya system. Baadhi ya watu hao wanaweza
Wasiwe na 'security clearance'ya kuona nyaraka za level hiyo.
Kwa mfano hapa kwetu kwenye matukio ya hadhara Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wanashirikiana na Jesho la Polisi kwenye ulinzi wa Rais na msafara wake. Pia kule Marekani Secret Services wanashirikiana na...
Local PD kwenye ulinzi wa Rais Kwenye matukio ya Umma.
Sasa hawa Polisi (mfano hapa nyumbani) na wale Local PD wengi wao hawana Clearance ya kuona nyaraka za siri. Hivyo licha ya unyeti wa document hizi inalazimu zisiwekwe muhuri wa siri ili kuleta ufanisi wa kushirikiana kwenye
Kuhakikisha ulinzi wa Rais.
Lakini mkazo mkubwa na umakini wa hali ya juu unawekwa kuhakikisha nyaraka hiyo haivuji kwa jamii, mitandaoni au kuonwa na watu wenye nia ovu.

Siku moja nitawapa kisanga kilichotokea pale Marekani mwaka 2011 mwezi April Rais Obama alipokuwa anapata
Chakula cha jioni na wana habari Hoteli ya Hinckley Hilton (ni hoteli hii ambayo mwaka 1981 Rais Ronald Regan alishambuliwa kwa risasi) Siku hiyo 2011 nyaraka hii ilivuja kwa mtu fulani kwa bahati mbaya.

Nitawapa hicho kisa siku moja

Jioni njema

The Bold
To Infinity and Beyond

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Habibu B. Anga

Habibu B. Anga Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @habibu_anga

5 Apr
Kuna uzi niliandika hapa Mwezi March kuhusu dhana nzima ya Ulinzi wa viongozi wa juu.
Nikasisitiza sana kwamba sula la ulinzi wao sio tu kulinda wasidhuriwe kimwili bali pia kulinda hadhi zao, heshima zao na siri zao.

Kitimbwi ambacho kimetokea leo cha Rais wa nchi

Thread👇👇 Image
Kuteua na kufukuza Mkurugenzi wa TPDC ndani ya masaa machache kabisa... ni failure kubwa ya kitengo cha intelijensia ya nchi ambao wana jukumu la kulinda hadhi na heshima ya Rais.
Mtu yule aliyeteuliwa huku akionekana kwamba hana sifa kabisa ya kushika wadhifa ule, ina reflect..
ombwe la weledi ambalo linaikumba idara hii adhimu ya ujasusi.

Mhe. Rais @SuluhuSamia ambaye watu wametokea kuwa na imani naye sana, tukio la leo kwa kiwango fulani limetia doa hadhi yake na kuzua maswali mengi sana

Kwamba, kosa la dhahiri namna ile limetokeaje?
Intelijensia ya
Read 18 tweets
28 Mar
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

Thread..

Kwa sasa, eneo letu la Afrika Mashariki limeguka kuwa moja ya eneo muhimu sana la kimkakati kiulinzi kwa nchi ya Marekani.

Leo nataka nikusimulie mkasa halisi wa namna gani shirika la Ujasusi la Marekani...
CIA linaendesha shughuli zake kuanzia hapa nchini kwetu Tanzania pamoja na nchi zote zingine za Afrika Mashariki.
Nataka nikusimulie mkasa wa kusisimua ili tuelewe vyema namna gani Afrika Mashariki kwa sasa imegeuka uwanja wa ushushushu wa Kimataifa kati ya Marekani na adui zake.
Ukimaliza kusoma uzi huu, utaelewa kwa nini sio kila "mtalii" umuonae ni mtalii tu kaja kushangaa swala pale Mikumi

Namna hii,

Siku fulani hivi ya tarehe 7 mwezi June mwaka 2011, kuna vijana watatu walikuwa wanasafiri kwa gari binafsi toka pwani ya Somalia kwenye mji unaitwa...
Read 25 tweets
22 Mar
JIHADI JOHN: MCHINJAJI WA ISIS MIKONONI MWA WANAUSALAMA WA TANZANIA

PART 4 (HITIMISHO)

Kwa hiyo wakafanya uchambuzi wote ule kuunda "profile" ya mtu wanayemtafuta.
Kisha wakachukua hii profile na kuoanisha na orodha ya watu ambao kwa muda mrefu MI5 wamekuwa wanawashuku... Image
kujihusisha na mavuguvugu ya kigaidi.
Yaani wanaangalia kwamba kwenye watu ambao siku za nyuma wamekuwa wakiwalia rada pale London, ni nani ambaye ana-fit kwenye hii profile waliyotengeneza kuhusu yule mchinjaji wa ISIS anayeitikisa dunia.

Baada ya kufanya uoanishaji huu..
wakafikia conclusion kwamba mchinjaji wa ISIS ambaye alikuwa anaitikisa dunia alikuwa ni mtu anayeitwa Abdel Bary
Huyu Abdel alikuwa ni maarufu sana hapo London, kwa sababu alikuwa ni mwanamuziki wa Hip-hop anayechipukia kwa kasi sana akitumia jinan kisanii "L Jinny"

Hata kwenye
Read 20 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!