Kuna uzi niliandika hapa Mwezi March kuhusu dhana nzima ya Ulinzi wa viongozi wa juu.
Nikasisitiza sana kwamba sula la ulinzi wao sio tu kulinda wasidhuriwe kimwili bali pia kulinda hadhi zao, heshima zao na siri zao.

Kitimbwi ambacho kimetokea leo cha Rais wa nchi

Thread👇👇 Image
Kuteua na kufukuza Mkurugenzi wa TPDC ndani ya masaa machache kabisa... ni failure kubwa ya kitengo cha intelijensia ya nchi ambao wana jukumu la kulinda hadhi na heshima ya Rais.
Mtu yule aliyeteuliwa huku akionekana kwamba hana sifa kabisa ya kushika wadhifa ule, ina reflect..
ombwe la weledi ambalo linaikumba idara hii adhimu ya ujasusi.

Mhe. Rais @SuluhuSamia ambaye watu wametokea kuwa na imani naye sana, tukio la leo kwa kiwango fulani limetia doa hadhi yake na kuzua maswali mengi sana

Kwamba, kosa la dhahiri namna ile limetokeaje?
Intelijensia ya
nchi imekufa kiasi hiki.?

Makosa mabaya ya namna hii yanatokea kwa sababu ya kutotaka kusikiliza kelele ambazo watu wengi wamekuwa wanapiga kwa miaka mingi sana kwamba kuna mabadiliko makubwa ya lazima yanapaswa kufanywa pale TISS.
Mfumo wake, uendeshwaji wake na majukumu yake..
vyote vyapaswa kubadilishwa.

Ukiitazama TISS namna ilivyo leo na inavyoendeshwa, ni kama ile TISS DGIS Lau Gama miaka ya sabini. Yaani nyakati zimebadilika mno, lakini hii idara bado iko kwenye mkwamo wa kizamani sana

TISS yapaswa mosi, ipunguziwe majukumu, pili ipewe "mamlaka"
na tatu ifumuliwe.

Tusiogope mabadiliko.. hakuna ubora mzuri kwenye maisha kama kuisoma dunia inakwendaje alafu ukanyumbuka nayo.

Kwa mfano, TISS inapaswa kuvunjwa namna ilivyo sasa na badala yake ziundwe Idara tatu zinazojitegemea.

Kwa mfano, kitengo cha Ulinzi wa Viongozi..
Yapaswa kuwa idara inayojitegemea, yenye Mkurugenzi wake, na ofisi zake.
Jukumu hili la ulinzi wa Viongizi limewaelemea sana tiss kwa muda mrefu sana sasa.

Najua wengi kwa mara ya kwanza wale FPU tumewaona JPM aliposhika nchi (wale maafisa wanaovaa sare zenye mabaka -makirikiri)
Jambo ambalo wengi hamlijui ni kwamba kwa sasa hivi wale FPU karibia 80% ni Polisi ambao huwa wanavaa yale magwanda baada ya kuingizwa kitengo cha PSU

Kuna siku "nikiamka vibaya" nitaichambua hii PSU
Wanaofahamu wanajua namna gani jukumu la Ulinzi wa viongozi linapunguza ufanisi
wa tiss na linaingilia kwenye masuala mengine ya ujasusi na ukusanyaji intelijensia ya nchi.

Ni muda muafaka kuundwe idara inayojitegemea ambayo itahusika mahususi na ulinzi wa viongozi pekee. Vijana wawe recruited toka jeshi la Polisi, JKT/JWTZ na huko Tiss kisha iundwe..
idara hiyo mpya ambayo itakuwa na Mkurugenzi wake, ofisi zake (na field offices kwa zones) na training grounds zakwao.
Focus yao pekee iwe ulinzi wa viongozi wa nchi (Rais, VP, PM, Spika, JM, Ministers na Viongozi wa Kigeni).

Hii itaondoa mzigo mkubwa sana pale Oysterbay..
Pia ni muda muafaka, ujasusi wa nje itoke kwenye kuwa 'kitengo' tu ndani ya tiss na badala yake tuwe na idara kamili.

Yaani tuwe na idara ya Ujasusi wa nje ya nchi na nyingine ya ndani ya nchi.

Idara hii mpya ya ujasusi wa ndani ya nchi, sheria ibadilishwe na wapewe uwezo wa...
kukamata na ku-prosecute.

Wajua mara nyingi tiss wanalaumiwa yanapotokea maskandali kama EPA na Escrow. Watu wanauliza tiss walikuwa wapi??
Wanasahau kwamba tiss wakikusanya intelijensia ya masuala kama hayo, kitu pekee wanachoweza kufanya ni kumpelekea Rais mezani. Kisha Rais..
ndio aamue afanyie nini hiyo taarifa. Rais akiamua aikalie tu hiyo taarifa, ndio madhara yake baadae inakuja kutokea maskandali ya ajabu na kisha watu wanauliza tiss walikuwa wapi??

Ndio maana kuna ulazima, tuunde idara mpya itakayohusika na ujasusi wa ndani ya nchi na idara hii
ipewe mamlaka ya kukamata na kushitaki na wawe na field offices kila mkoa.
Idara hii mpya inaweza kuundwa kwa ku-merge na BCI kutoka Jeshi la Polisi (Criminal Intelligence, Analysis and Decemination).

Alafu ile Idara nyingine wao wabakie na Ujasusi wa nje ya nchi. Wasiruhusiwe..
kukamata wala kufanya operations ndan ya nchi isipokuwa kwa kibali maalumu cha Rais, Waziri wa Ulinzi au Waziri wa mambo ya Ndani

Kwa hiyo kutoka kwenye idara moja ya TISS tufumue na kuunda Idara tatu zinazojitegemea (Ulinzi wa Viongozi, Internal Sec Agency, External Sec Agency)
Alafu kisha tuunde ofisi ya Mkurugenzi wa Intelijensia ya Nchi (Director of National Intelligence).

Huyu awe ni cabinet level official ambaye atafanyakazi kama Kiongozi wa Inteligence Community ya nchi (idara zote za intelijensia na ushushushu za nchi.. External Agency, Internal
Agency, Millitary Intelligence). Ambaye kazi yake itakuwa ni kuratibu mtiririko wa intelijensia yote ya nchi na pia kutoa briefing za kijausi kwa Rais wa nchi.

Anyway, haya ni mawazo yangu tu, nataka kuchochea mjadala wa namna gani twaweza kuboresha our intelligence machinery...
Hili kosa mbalo limetokea leo ni la aibu kubwa sana kwa jumuiya yetu ya intelijensia. Kosa hili linasema vitu vingi sana.
Intelligence machinery iko hijacked na vyama vya siasa na pia imepitwa na wakati mno kimfumo na kiutendaji.

Tusiogope mabadiliko na kujisahihisha.

- Habib

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Habibu B. Anga

Habibu B. Anga Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @habibu_anga

28 Mar
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

Thread..

Kwa sasa, eneo letu la Afrika Mashariki limeguka kuwa moja ya eneo muhimu sana la kimkakati kiulinzi kwa nchi ya Marekani.

Leo nataka nikusimulie mkasa halisi wa namna gani shirika la Ujasusi la Marekani...
CIA linaendesha shughuli zake kuanzia hapa nchini kwetu Tanzania pamoja na nchi zote zingine za Afrika Mashariki.
Nataka nikusimulie mkasa wa kusisimua ili tuelewe vyema namna gani Afrika Mashariki kwa sasa imegeuka uwanja wa ushushushu wa Kimataifa kati ya Marekani na adui zake.
Ukimaliza kusoma uzi huu, utaelewa kwa nini sio kila "mtalii" umuonae ni mtalii tu kaja kushangaa swala pale Mikumi

Namna hii,

Siku fulani hivi ya tarehe 7 mwezi June mwaka 2011, kuna vijana watatu walikuwa wanasafiri kwa gari binafsi toka pwani ya Somalia kwenye mji unaitwa...
Read 25 tweets
22 Mar
JIHADI JOHN: MCHINJAJI WA ISIS MIKONONI MWA WANAUSALAMA WA TANZANIA

PART 4 (HITIMISHO)

Kwa hiyo wakafanya uchambuzi wote ule kuunda "profile" ya mtu wanayemtafuta.
Kisha wakachukua hii profile na kuoanisha na orodha ya watu ambao kwa muda mrefu MI5 wamekuwa wanawashuku... Image
kujihusisha na mavuguvugu ya kigaidi.
Yaani wanaangalia kwamba kwenye watu ambao siku za nyuma wamekuwa wakiwalia rada pale London, ni nani ambaye ana-fit kwenye hii profile waliyotengeneza kuhusu yule mchinjaji wa ISIS anayeitikisa dunia.

Baada ya kufanya uoanishaji huu..
wakafikia conclusion kwamba mchinjaji wa ISIS ambaye alikuwa anaitikisa dunia alikuwa ni mtu anayeitwa Abdel Bary
Huyu Abdel alikuwa ni maarufu sana hapo London, kwa sababu alikuwa ni mwanamuziki wa Hip-hop anayechipukia kwa kasi sana akitumia jinan kisanii "L Jinny"

Hata kwenye
Read 20 tweets
13 Apr 20
Serikali na Idara zote za Ujasusi ulimwenguni kuna nyaraka ambazo zapaswa kuonwa na watu fulani pekee. Mara zote nyaraka hizi huwa na muhuri wa SIRI.
Pale Marekani kuna nyaraka 2 ambazo ni za siri kubwa zaidi lakini ajabu nyaraka hizi hazina muhuri wa "SIRI" na wala..

THREAD👇👇 Image
mpaka leo nyaraka hizi hazijawahi kuvuja kwa umma au mtandaoni. Nyaraka hizi 2 hazina majina mahususi lakini zinafanana kwa kiasi fulani na nyaraka za Idara yetu ya Usalama wa Taifa hapa nchini ambayo zinaitwa "Site Post Assignment Logs".
Nyaraka ya kwanza inaonyesha maafisa wa..
Idara ya Usalama kitengo cha Ulinzi wa Rais majukumu yao na namna gani watajipanga katika kumlinda Rais kwenye tukio fulani. Lakini pia mbinu ambazo zitatumika kuimarisha ulinzi pamoja na mkakati wa dharura wa kumuokoa Rais kama likitokea shambulio.

Nyaraka ya pili yenyewe ni..
Read 9 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!