My Authors
Read all threads
I ONCE EXPERIENCED THE POWER OF LOVE ❤

Nilidhani nguvu ya treni kuvuta behewa ndio nguvu kubwa kuwahi kutokea nikapingana na fikra hizo pale nilipowaza nguvu ya maji kunyanyua meli
Nlipingana na hayo pale nilipokumbana na nguvu iliyopo katika fikra za walopendana
T H R E A D👇
Binafsi sijizuii kupenda inapobidi japo haimaanishi siwezi kuishi bila mpenzi, naamanisha kisu changu kina kata vyoote lakini hakikati tamaa tuu
Nikimuhitaji mtu akaona siendani nae, naachana nae najiandaa kwa "come back " kubwa 😄
Ndio kilichotokea bana enzi hizo nasoma
High school nliwahi kumpenda mtu akahitaji mpaka niwe na funguo tatu " three keys" ya gari, ya nyumba na ya ofisi nkaona nisonge mbele kama injili maana local man ntavitoa wapi vitu ambavyo wengine wanapata wakistaafu 😂

So baada ya mission hiyo kufeli nkapenda tena.Story began
Ilikua ijumaa kwa kawaida shule zetu za serikali masomo huisha mapema sana ili watu wakafanye mambo mengine. Mi nkaamua niende mjini bhana nkabadilishe chakula kwenye ule mji wa Wanyamwezi😄
Ule wakati narudi njiani nikawa nimeongozana na kiumbe cha ajabu maana ule mwendo
Nkahisi ni twiga anafata nyasi za juu ya mti, lile umbo kwa nyuma kama kiboko mnyama anajidai kando ya bwawa na ule urembo wa ngozi,siha na madaha nkajua huyu ni Pundamilia bila shaka kiufupi ningekua na namba za TANAPA ningewapigia waje wanambie kiumbe gani huyu.Alivutia sana ❤
Alikua binti mrembo ambae ilinibidi niwahi niseme nae. Nlivomfikia nkamsalimia lakini akageuka akaniangalia nakuendelea na mwendo 🙄
Nkaendelea kumdadisi mahali anakokaa na story kadhaa kumuhusu yeye maana mi nshajitambulisha jina naitwa Noel ila mwenzangu haongei kitu anashangaa
Mpaka tunafika mahali pakuachania mi naingia shuleni yeye anaendelea na safari hakuwa ameongea chochote nkabaki nimeduwaa tuu.
Nkaachana na mawazo hayo nkaenda bwenini kujilaza kusubiri kande za shule jioni😄

Jumapili jioni nikiwa nimeongozana na wenzangu tunaenda mgahawani kwa
Sister Khadija kula wali wa jero jero maana chakula cha shule si mchezo halafu canteen kwa kishua andazi moja jero akati hiyo jero nakula wali street na nashiba 😎

Nkamuona yule dada anapita kwenda gengeni kumbe alikua anakaa mitaa ileile bhana nkamsimamisha nkamuuliza kama
Ananikumbuka akaanza kutabasamu huku anatikisa kichwa ishara kwamba ananikumbuka 😀

Nkampa vijistory kumuuliza mbona ile ijumaa aliondoka bila kunijibu kitu lakini bado akawa haongei kitu chochote, daah nkaona sasa hizi mikogo ndo toleo jipya au mi ndo sielewi. Nkaona nisipoteze
Muda nkamuambia kama hatojali kesho mida kama ile tukutane pale pale maana hata iyo simu hakua nayo ambayo ningechukua namba
Woiii sisi malegend tokea form one mpaka six tulikua na simu regardless 🙌🏼😂
Wakati na rudi kutoka kula ikabidi niende kwenye lile genge ambalo yule dada
Alienda kununua vitu ili nipate data..Nkauliza nkaambiwa yule binti bhana anaitwa Joan na ni BUBU 😳
Anaishi nyumba ya jirani tuu na shule yetu yani nikiwa darasani mule PCB 6 nikiinua shingo napaona kwao.
Ikabidi niondoke mnyonge kumbe manzi ni bubu asee lakini mbona mzuri vile!
Sasa kesho yake baada ya vipindi nkabaki class kujisomea lakini ulivofika ule muda nilomwambia yule dada tukutane pale ulivofika nkasita kwenda maana ntaongea nin binti mwenye Bubu halafu lugha ya Ishara mi hata sielewi😒

Anyway nkaenda tuu asije fika halafu mi nkawa sipo itakua
Sio poa..Kweli bhana yule dada akaja nkamsalimia ye anaangalia pembeni.
Nkamuita Joan akashangaa maana hakujua jina nimejulia wapi.😄
Guys mapenzi yana nguvu huwezi amini nlijikuta naongea peke angu Joan ye anafanya kucheka tuu maana hata akiongea sitoelewa lakini niliona jinsi
Alivofurahi..Akanipa ishara ya kuondoka nikampungia mkono akaondoka anatizama chini kwa aibu.
Nkabaki pale muda mrefu nawaza, mbona huwa naskia mabubu hawaongei na pia hawaskii huyu yeye vipi au nlichokua naskia niuongo?? Lakini ivi kweli nimempenda huyu au ni hamu zangu tuu😂
Nkarudi zangu Dormitory nkakuta umeme umekata kilichofata nkawa nawapa story roommates kama nimedata kwa manzi bubu wakacheka sana wakaanza kuniita Z-Anto alopenda binti kiziwi😒

Sikujali maana hisia zangu zilikua za kweli kwa Joan.Kesho yake baada ya kusoma jioni nkakaa nje
Ya darasa khee yule binti nkamuona kwa mbali maeneo yaleyale ya jana nkamfata nkajua lazima kanisubiri mimi.
Nkamfata tukakaa kwenye mawe flani nampigisha story yeye pia anachangia kwa kucheka na kuonesha ishara nyingi ambazo sikuelewa lakini moyoni nilihisi zinaashiria furaha❤
Bhana ikawa kama mazoea kila jioni lazima nikaonane na Joan kwenye eneo lile la kukutania. Aibu zikaanza kumuisha haniogopi tena mpaka akiwa anacheka ananipiga kikofi mahaba begani 😚
Siku moja nkamuambia ya moyoni jinsi nampenda. Akabaki kimya muda mrefu nlijua anachowaza
Either nataka nichukulie kigezo cha yeye kuwa bubu nimtumie niende au namtania.
Nkaona anaondoka lakini alivofika mbele kidogo nkasika "Oeee " akanionesha busu la mbali kwa kiganja kutoka mdomoni, kwa ububu wake aliishia kuniita "Oee" badala ya Noe..Nlifurahi sana 😄
Sasa kuna
Siku nimeenda kukutana nae nkaona kaja na mfuko ndani kuna hotpot kaniwekea wali mwingi na pande za kuku.
Daah nilijiskia huruma iliyochanganyikana na mapenzi mengi maana kumbe ububu ni hali tuu lakini mapenzi hayachagui..Nkajikuta nampenda sana Joan.Nkabeba nkaenda kula na wana
Sasa kesho yake akaja amevimba uso kweli na mkononi kaunguzwa nkamuuliza ye hasemi anakataa kwa kutikisa kichwa.
Moyoni nkajua huyu kile chakula cha jana aliiba kwao kwa ajili yangu ndo sababu wamemfanya hivi 💔
Nkamuuliza pale anakoishi ni kwa nani akanipa ishara nyingi hata
Sikuelewa, nkapiga nae story kadhaa ili nimfurahishe Joan kweli bana alikua tajiri wa tabasamu na meno yalopangika vizuri.
Tulivoachana pale nkaenda kuuliza watoto walokua wanacheza nyumba ya jirani na anapokaa Joan. Kwa bahati nzuri mtoto mmoja alikua ni ndugu yake. Akasema yule
Joan pale kama yupo kwa Uncle wake tuu.
Nlirudi bwenini naumia sana kuwa sababu ya binti wa watu kuteseka.Kesho yake tulivokutana nkaona kile kidonda alichoumia baada ya kupigwa kinazidi kuharibika nkampeleka dispensary ya pale karibu wakamsafisha. AkaniKiss mdomoni tulivokua
Tunarudi. Nachokumbuka zaidi niliwahi kumfundisha hata namna ya kufanya deep kiss coz alikua hajui kitu mwisho akazoea kunishinda mimi😁
Tulivofika pale mahali pakuachania nkamwambia " Joan mi naona uendelee na maisha yako na mimi nisome maana nimeshakua kikwazo mpaka unapigwa "
Aisee hakutaka kusikia maana alining'ang'ania mkono ananisihi kwa ishara nisifanye hivo. Ile picha mpaka leo naikumbuka, huruma ilinijia pale machozi yalivoanza kumtoka 💔
Nkajipa moyo mgumu nkamtoa mkono wake nkasepa. Iliniumiza sana hata mimi ule usiku niliwaza mno
Kesho yake ikafika mi nkawa bize nasoma hata ule wakati ambao ilitakiwa nkakutane nae nkamuona ye kafika lakini mi sikwenda. Alifanya hivo kama siku nne anakuja mi siendi ilizidi kuniuma mpaka washkaji wakawa wananambia nakosea..Siku moja jamaa yangu mmoja akaja na barua akasema
Alipewa na dogo mmoja aniletee jana yake..Kuisoma naona mwandiko siujui lakini yaloandikwa nliyaelewa, alikua ni Joan nadhani alimpa mdogo wake atafsiri ishara zake aziweke katika maandishi " Noel, nakupenda niache niteseke kwa ajili yako naomba unipende pia sipo tayari kukupotez
Yalikua ni baadhi ya maneno kwenye barua ninayo yakumbuka 💔
Ikabidi niend moja kwa moja kwao nkakuta yupo dogo tuu akanambia Joan kalazwa hospitali ya Mkoa anaumwa sana tumbo 😨
Duuh nkaenda chapu nkapitia chips matunda na maji moja kwa moja mpaka Hospital ya Kitete pale
Nlivofika ile wodi alimolazwa alivoniona hakuamini akaanza kulia mbele ya wale walokua wanamuhudumia.. Nlikaa nae muda kidogo nkakabidhi nlivopelekea nkarudi kula msuli shule.
Kesho yake akaruhusiwa kutoka hospitali. Nlivoenda kumuangalia nkamkuta na mdogo wake yule Akasema kesho
Joan anarudi kwao Shinyanga na hatorejea tena..Asee niliumia moyo sana maana Joan alikua muda wote kainama chini nkamfata nkamsimamisha nkamkumbatia nkampa moyo kwamba kuna siku tutaonana.
Kesho yake ilibidi niende tuu nikamsindikize asubuhi nkaua vipindi shule nkamfata mchumba
Nkampa namba zangu za simu japo nlijua hata akinipigia tutaongeaje wakati anatumia ishara 💔
Ndio mpaka leo sijawasiliana na Joan..But Love has huge power.
#End
#MyMindSpeak
#NohTalk ☕️
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Noe_Wenc 💊

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!