My Authors
Read all threads
ELON MUSK

Alizaliwa South Africa akiwa na miaka 17 alihamia Canada na baadae America, ni mfanyabiashara na mwanzilishi wa makampumi makubwa kama SpaceX, PayPal, Tesla Motors

Leo nimekuletea kila kitu kuhusu Elon Musk

✴️ Historia yake na familia yake

✴️ Biashara zake

Uzi Image
ELON MUSK NI NANI

Ni mzaliwa wa South Africa lakini sasa ana uraia wa Marekani na Canada, ni mfanyabiashara na mwanzilishi wa makampumi ya PayPal, SpaceX na Tesla Motors, alipata pesa akiwa na umri mdogo (20's) baada ya kuuza kampuni yake ya kwanza (Zip2) kwa Compaq computers Image
MAISHA YAKE YA UTOTONI

Elon Musk alizaliwa June 28, 1971 huko Pretoria-South Africa, Musk alizaliwa na tatizo la kusikia ila madaktari waliweza kumtibu akiwa mdogo.

Akiwa na miaka 10 wazazi wake walitengana na aliendelea kuishi na mama yake na ndugu zake wawili Image
alionyesha kupenda computer na akiwa na miaka 10 alijifunza kutengeneza program za computer, akiwa na miaka 12 Elon aliuza program yake ya kwanza (game) iliyoitwa "Blaster"

Mama yake anaitwa Maye Musk ( Canadian model) na baba yake anaitwa Errol Musk ( South African Engineer )
ELIMU YAKE

Akiwa na miaka 17, mwaka 1989 Elon alitoka South Africa kwenda Canada kujiunga na Queens University akikimbia sheria ya lazima ya SA kujiunga na jeshi, mwaka 1992 alitoka Canada kwenda Marekani kujiunga na Pennsylvania university akisomea business and physics Image
Baada ya kumaliza chuo alibaki hapo Penny kuchukua Degree yake ya pili

Alitoka Penny kujiunga na Stanford University kusoma PhD ya energy physics lakini cha ajabu aliacha chuo siku mbili tu baada ya kujiunga Stanford University na kurudi kuanzisha kampuni ya Zip2 mwaka 1995 Image
UMILIKI WA MAKAMPUNI

◾️Zip2 Corporation

Mwaka 1995 Elon na kaka yake Kimbal Musk walianzisha kampuni iitwayo Zip2 Corporation, ( An online city guide) baadae Zip2 ikaanza kuuza maudhui yake kwa kampuni za "The New York Times" na "Chicago Tribune"

Mwaka 1999 kampuni ya Compaq
Computers ilinunua Zip2 Corporation kwa $307 million cash

◾️PayPal

Mwaka 1999 Elon na kaka yake Kimbal walitumia pesa walizopata kutoka kwenye mauzo ya Zip2 na kuanzisha X.com ambayo baadae iliitwa PayPal, kampuni ya malipo kwa njia ya mtandao Image
October 2002, PayPal ilinunuliwa na Amazon kwa gharama ya $1.5 billion ambapo Elon anamiliki 11% ya stock za PayPal

◾️ SpaceX

Mwaka 2002 Elon alianzisha kampuni ya utafiti na utangenazaji wa vifaa vya anga iitwayo "Space Exploration Technologies" ( SpaceX) Image
Mwaka 2008 kampuni ya SpaceX ilipewa tenda kutoka NASA, tenda ya kusafirisha mizigo kwenda kwenye anga za kimataifa

May 22, 2012 SpaceX walitengeneza historia baada ya kuachia rocket "Falcon 9" kwenda kwenye anga za juu zaidi, ikiwa ni kampuni binafsi ya kwanza kufanya hivyo Image
December 2013 Falcon 9 ilifanikiwa kupeleka Satellite kwenye anga za juu zaidi sehemu satellite zinalock kwendana na mzunguko wa dunia ( geosynchronous orbit)

Mwaka 2015 SpaceX waliachia rocket ikibeba vyombo maalumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa mionzi itolewayo na jua Image
March 2018 SpaceX walipewa kibali na serikali ya Marekani kurusha satellites zao kwenda anga za juu kwa lengo la kutoa huduma ya internet kwa gharama nafuu, satellite hizo ziliitwa "Starlink " ambapo May 2019 walifanikiwa kurusha satellites 60 na December 2019 walirusha Image
Satellites zingine 60, na kufika jumla ya satellites 120 za Starlink zikimilikiwa na SpaceX

SpaceX wameonyesha mafaniko makubwa mwaka huu (2020) kushirikiana na NASA baada ya kurusha Rockets kwenda mwezini na sayari zingine kama Mars kwa ajili ya utafiti Image
◾️ Tesla Motors

Mwaka 2003 Elon Musk alianzisha kampuni la kutengeneza Solar, Batteries na magari yanayotumia umeme.

Miaka mitano ya mafaniko ya Tesla March 2008, walifanikiwa kutengeneza gari ya mashindano "Roadster" mwaka huo kampuni ya Toyota iliwekeza Tesla Motors Image
August 2012 walitengeneza gari aina ya "Model 3 sedan" car ambayo ilipiku mauzo ya BMW 5 na mwaka 2013 ilitangazwa kuwa gari bora ya mwaka kupitia gazeti la Motor Trend

Mwaka 2017 Tesla Motors ilitangazwa kuwa kampuni bora ya utangenazaji wa magari ikiipiku General Motors ImageImage
Tesla Motors wanakamilisha utengenezaji wa gari aina ya Roadster Model Y ikikamilika itakuwa gari yenye speed kubwa kuwahi kutengenezwa

◾️SolarCity

Mwaka 2016, Elon Musk alinunua kampuni ya urutubishaji na utangenazaji wa nishati mbadala iitwayo "SolarCity" kwa $2.6 billion Image
Inasemekana kampuni ya SolarCity Corp ilianzishwa na binamu yake mnamo 2006, lengo la kununua SolarCity ni kupanua wigo wa nishati mbadala itakayorahisisha utengenezaji wa magari yanayotumia umeme

◾️The Boring Company

January 2017 Musk alianzisha kampuni ya
Kutengeneza njia za chini kwa chini ( underground) lengo ni kupunguza foleni kwenye baadhi ya sehemu zenye msongamano wa magari,

Mwaka 2019 alipata contract ya kujenga njia za chini kwa chini huko Las Vegas kupunguza foleni kwenye maeneo kuzunguka Las Vegas convection center
◾️ UKARIBU NA DONALD TRUMP

Mwaka 2016 Elon Musk alianza kuwa karibu na Trump kama mshauri mipango ( strategies), Mwaka 2017 akaingia rasmi kwenye mpango wa Trump's manufacturing job initiative, Elon amekuwa karibu sana na Trump kama mshauri wa miundombinu na mambo ya Anga Image
◾️ MAISHA BINAFSI
(Mke na Watoto)

Elon Musk alimuoa Justine Wilson mwaka 2000, walibahatika kupata watoto sita na wote wakiume lakini mwaka 2002 mtoto wao wa kwanza alifariki, watoto waliobaki ni Griffin, Xavier mapacha walizaliwa 2004, wengine ni Triplets, Kai, Saxon na Damian Image
Elon na Justine walitengana mwaka 2008

Mwaka 2010 Elon alimuoa mwigizaji Talulah Riley, walitengana mwaka 2012 na baadae 2013 walioana kwa mara ya pili na mahusiano yao yalivunjika mwaka 2016

Mwaka 2016 Musk akawa na mahusiano na mwigizaji Amber Heard lakini kutokana Image
na ubize wao wa kazi, mahusiano yao yalivunjika August 2017, wakarudiana tena January 2018 lakini mwezi mmoja baade waliachana tena

May 2018, Musk alianza mahusiano na mwanamziki Grimes, na kwenye mahojiano na vyombo vya habari Grimes alisema hivi
"Look, I love him, he’s great...I mean, he’s a super-interesting goddamn person"

May 4, 2020 Walipata mtoto wa kiume wakamuita jina "X Æ A-12" lakini Jimbo la California walikataa hilo jina maana lina namba ikabidi wabadili jina la mtoto na kumuita "X Æ A-Xii" Image
◾️Musk Foundation

Mbali na utajiri wake Musk ana program iitwayo Musk Foundation kwaajili ya kusaidia jamii

October 2019 Musk alitoa $1 million kwa #TeamTrees kusaidia upandaji wa miti million 20 Duniani kwa mwaka 2020 kukabiliana na Mabadiliko ya tabia ya nchi
Sources

◾️ Forbes
◾️ Business Insider
◾️ Wired
◾️ The Verge
◾️ Biography

Retweet

Uzi chini ya @chawanyu

Cc: @Mkuruzenzi @chapo255 @razaqdm01 @asatayo @abdoolkhery @WizaraUUM @njiwaflow
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with #TOTTechs 🇹🇿

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!