My Authors
Read all threads
MAAJABU YA MAUAJI YA HARAIKI YA  JONESTOWN
(JONESTOWN Massacre)
#cipherdotseriesandmoviesuzi
#CertifiedThreads
Kabla ya shambulizi la kigaidi la septemba 11, 2001 tukio hili la Jonestown lilikuwa ndo tukio la kwanza kubwa kuchukua roho za wamerekani wengi kwa mara moja
Mauaji ya Haraiki ya jonestown yalitokea  Novemba 18, 1978  waumini kwa kimarekani wapatao 900 wa dhehebu la kidini lililoitwa "Peoples Tample walikufa kifo kilichoelezewa kama mauji ya kujiua ya Umati kufutia agizo la kiongozi askofu wao aliyeitwa Jim Jones aliyeishi
(1931-78) kwenye kijiji kilichofahamika kama Jonestown kusini mwa Amerika kwenye nchi ya Guyana. Stori ipoje ya jambo hili?? Tuambatane tuine nini hasa kulipelekea watu hao wate kujiua?? Je kwa hiari yao walijiua au??
Jones alianzisha dhehebu lake la Peoples Tample huko
Indiana kwenye miaka ya 1950 na baadae kuhamishia dhehebu hilo huko California kwenye miaka ya 1960 kufikia kwenye miaka ya 1970 kutoka na kupata upinzani mkubwa kuhusu mahubiri yake kutoka kwenye vyombo vya habari askofu huyu ambaye tayari alikuwa na nguvu kubwa na
ushawishi mkubwa aliamua kuhamia kwenye msitu uliopo huko Guyana na wafuasi wapatao 1000 ambapo aliwaahidi kuwa wataanzisha kijiji cha kiistarabu.
Sokomoko lilianzia pale saneta wa kimarekani alipoenda kufanya uchunguzi mnamo Novemba 18, 1978 bwana Leo
Ryan na ujumbe wake wakitaka kuthibitisha madhira yaliyokuwa yanawapata waumini hao inaamika kuwa walikuwa wanachapwa fimbo na kufanyishwa kazi ngumu sana, wa mama kubakwa na wengine kuuwawa haya yote yalijulikana kwenye uchunguzi huo
Kabla ya Jones kuhama huko California aliheshimika mno na kufahamika mno, aliweza kuwasaidia viongozi wengi kushika madaraka kwenye kipindi cha uchaguzi, na kuvipa vyombo vya habari misaada mbalimbali, na pia alikuwa anatoa misaada mingi sana kwenye vikundi mbalimbali vya
kusaidia jamii, dhehebu la Peoples Tample lilijihusisha sana kusaidia jamii na kutoa huduma za mahospitali na dawa kwa wenye uhitaji, pia walikuwa wanatoa chakula bure kwenye ukumbi wao wa chakula, kuwasaidia walioathirika na madawa ya kulevya, na kutoa huduma za kisheria bure,
kwa kauli mbiu yake aliyokuwa nayo jones ya usawa kwa watu wote na haki kwa watu weusi hii kauli mbiu yake ilipelekea kupata waumini wengi waliofikia hadi milioni 20 ngoma ikilia sana lazima ipasuke umaruafuu wa Jones ukaanza kuteteleka baada ya taarifa mbaya zilinzoanza
kutoka kwa waumini waliojitoa kutoka kwenye dhehebu hilo zikimweleza mtu huyo ajiitaye Father (mchungaji) kuwa aliwalazimisha na kuwanyang'anya mali waumini pia walilazamishwa kuuza nyumba zao na hela kupewa jones pia baadhi ya wazazi watoto wao walichukuliwa na wazazi
hawakuweza kuwaona mpaka kwa mpango maalum pia alijifanya ni mtu pia awezaje kutibu kansa
Kutokana na kufuatiliwa na vyombo vya habari kwa hali ya juu na uchunguzi wa mara kwa mara akaanza Jones aliyekuwa anavaa miwani meusi wakati wote akaanza
kuingiwa na hofu ilyompelekea kutembea na walinzi (bodyguards) kokote aendako. Baada ya kuona hali imekuwa mbaya kiusalama na kiuendashaji wa dhehebu lake Jones akamua kuhamia huko Guyana na kwenda kufungua mashamba na kuanza kilimo
MAISHA MAGUMU JONESTOWN
Maisha ndani ya mji wa Jonestown yalikuwa magumu sana waumini walifanyishwa kazi kama watumwa adhabu kali zikitolewa kuhakikisha hawatoroki Jones aliwanyanganya hati za kusafiria (passports) zao zote na dawa kwa wale
waliokuwa wanatumia dawa kwa maradhi mbalimbali, kwa kuwa ilikuwa msituni mbu walikuwa wengi mno na watu wakaanza kuugua magonjwa ya ukanda tropiki, wakati hayo yote yakiwa yanaendelea msitu huo ulikuwa unalimdwa na askari wenye bunduki kama vile uonavyo misitu ya wauza
madawa kwenye filamu yanavyolindwa, walilazimishwa kuhudhuria vikao virefu vya usiku huku wakiwa wamechoka sana na ukisinzia unachezea fimbo, simu zilikuwa zikisikilizwa kuona nini unaongea, kwa kipindi hicho afya ya jones kiakili ilianza kupata mgogoro akaanza kuwa mlevi
kwenye dawa na huku akijifanya kama Yesu,
Muda wote aliwatazama watu wa vyombo vya habari na serikali kama watu anaotaka kumharibia
MASHAMBULIZI KWENYE KIWANJA KIDOGO CHA NDEGE
Seneta Ryan baada ya kusikia kuwa kuna wapiga kura wake
kutoka kwenye jimbo lake ambao wanashikiliwa kinyume na matakwa yao akaamua kwenda kuchunguza ujumbe huu ulikuwa na waandishi na wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari, mnamo Novemba 17, 1978 ujumbe
wa bwana Ryan ulipokelewa na kwa mshangao wao waliandaliwa chakula na sherehe fupi baadae na kuwashangaza zaidi akakubali mpaka kuongea na waandishi wa habari lakini pia kulikuwepo watu waliomuomba Ryan awasadie kurudi nyumbani.
Ilipofika Novemba 18, 1978 seneta Ryan na msafara wake na baadhi ya wale waliomsaliti Jones wakirudi nyumbani
Siku zote ogopa ukiona mtu aliyekuwa mtata ghafla anakuwa mpole na kukubali lolote utakalo jua kuna jambo
anapika, basi msafara wa bwana Ryan ukiwa unasubiri ndege ulivamiwa na watu wenye bunduki na kuwaua wote waliokuwa kwenye msafara huo

VIFO VYA WATU 900
Siku hiyohiyo wakati mauaji yanatokea kwenye kiwanja cha
ndege Jones aliwakusanya waumini wote kwenye bwalo na kuwaambia kuwa wanajeshi watakuja kuwatesa sana hivyo ni bora kufa kifo cha kimapinduzi, watoto wadogo walikuwa wakwanza kufa wakiingizwa kwenye koromeo sumu ya cyanide hii sumu ni kali sana inasemekana hakuna
aliyewahi kujua radha ya hii sumu na kuweza kuelezea habari zisizo rasmi zinasema kuna wakati mtu alipewa hela nyingi ili alambe hii sumu halafu aelezee radha yake huyu bwana alifanikiwa kulamba na kuweza kuongea herufi "S" haieleweki hadi leo alimaanisha sour?or Salt? Au nini?
maana alikufa baada ya kutamka herufi hiyo.
Kwenye picha nyingi za kipelelezi umeshawahi kuona spy wanatafuna kidonge wakiona wapo hatarini utakachoshuhudia ni povu mdomoni na mtu kishakufa. Baada ya watoto wote kufariki watu wazima walijipanga
foleni kwenda kunywa sumu hiyo huku wakiwa wanalindwa ili mtu asitoroke wale walionyesha nia ya kutaka kutoroka walipigwa risasi au na mishale ya sumu
Maofisa wa serikali walivyofika kwenye eneo hilo siku ya pili walikuta maiti zimezagaa eneo lote na wengi walikufa
wakiwa wameshikana mikono au wakiwa wamekumbatiana
Jones alikutwa akiwa amekaa kwenye kiti akiwa amejipiga risasi kwenye paji la uso na kufa watu 909 walikufa siku hiyo watu 33 tu ndio waliopona kwa kuwa walikuwa eneo lingine kwa siku hiyo
Cipherdot Series na Movies Dodoma
Please RETWEET
Please Follow
@cipherdotM
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Cipherdot Series And Movies✍️

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!