UZI: Dalili za mimba: Ujauzito ni ndoto ya wengi, huku kwa wengine ni jambo wanaloepuka na kuzingatia sana. Wadada wengi wanaonesha kuhitaji watoto tofauti na wanaume. Leo nimekuletea dalili 10 za ujauzito ambazo huashilia uwepo wa ujauzito #BongeLaAfya
1. Kutoona siku zako: Kukosa siku zako ni moja ya dalili za kwanza kabisa ambazo wengi wetu wamezoea. Katika kipindi cha mzunguko kuta ya mfuko wa uzazi huvunjika na kujiengua na kutoka nje katika mfumo wa damu, hudumu kwa siku tatu mpaka saba. Unapopata ujauzito hujishkiza hapo.
2. Misuli ya miguu kubana/cramps: Katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito mwanamke anaweza kuona dalili za miguu kukaza au kubana, Hii inatokana na mabadiliko ya mwili katika kuchakata calcium ambayo huitajika kwa wingi kuunda mifupa ya mtoto, meno na viungo.
3. Uchovu: Wakati mwanamke anakuwa mjamzito, mabadiliko ya homoni yanayotokea yanaweza kumfanya ahisi uchovu muda mwingi. Kuongezeka kwa viwango vya homoni ya estrojeni na progesterone kunaweza kusababisha uchovu mkubwa, haswa wakati wa miezi mitatu ya kwanza.
4. Kichefuchefu : Morning sickness ni neno linalotumiwa mara nyingi wakati wa kuelezea kichefuchefu ambacho wanawake wengine wanapaswa kuhimili wakati wanabeba mtoto. Kichefuchefu huanza wiki sita baada ya mzunguko wa mwisho.
5. Mabadiliko ya mood/mihemuko: Kama nilivyosema mwanzo, mwili wa mwanamke kipindi cha ujauzito huongeza kiwango cha homoni ya oestrogen na progesterone kwenye damu, Hii inaweza kusababisha kubadilika badilika kwa mood. Mara mcheke, mara mnune, mara apende hiki mara achukie.
6. Kukojoa mara kwa mara: Safari za mara kwa mara za chooni huongezeka, Hii ni kwa sababu ya kuongezeka kwa ukubwa wa mfuko wa uzazi na hivyo kubana kibofu cha mkojo, lakini pia kuongezeka kwa mtiririko wa damu kwenye figo,
7. Hyperemesis gravidarum: Najua hujawahi kusikia hili neno, hapa tunaongelea kutapika sana wakati wa ujauzito, Baadhi ya wanawake wameonesha kuendelea kutapika hata kipindi chote cha ujauzito. Kuna tofauti kati ya kichefuchefu na kutapika, kichefuchefu atakiskia tu asitapike.
8. Ladha: Inaeleweka kabisa kuwa wakati wa ujauzito wanawake wengi hupoteza ladha hata kwa vile vitu wanapenda. Ghafla wataanza kupenda baadhi ya vyakula na utaamshwa hata usiku wa manane ufkifate hata kama kiko mbali.
Baadhi ya tafiti pia zimeonesha uwezo wa kunusa huongezeka.
9. Siku zako: Kuna uwezekano wa kuona matone ya damu hata mara moja katika kipindi cha ujauzito. Japo inafahamika kuwa mjamzito hawezi kuona siku zake lakini kuna uwezekano akaona matone kipindi cha upandikizaji. Mara nyingi huwa kipindi mimba inaanza.
10. Maziwa kuuma: Dalili ya mwisho tutakayoongelea leo ni maziwa kuuma au kuonekana kwa mabadiliko mengine tu katika maziwa ya mjamzito kama kuongezeka ukubwa, mishipa ya damu kuonekana n.k.
Kunaweza kuwa na dalili nyingine ambazo sijaziongelea lakini licha ya kuwepo kwa dalili hizi kitu pekee kinachoweza kuthibitisha ni kipimo cha mimba.
UZI: Red eye au bloodshot kwa kitaalamu, hutokea pale ambapo mishipa midogo ya damu inayoonekana kwenye uso wa jicho kupanuka au kujawa na damu. Hali hii hutokea kutokana na uwepo wa kiwango kidogo cha oxygen inayotolewa na tishu zinazofunika jicho au maambukizi. #BongeLaAfya
Hali hii huwa ya kawaida na inaweza kutokea katika jicho moja au macho yote mawili. Hiyo rangi nyekundu inayoonekana ni rangi ya damu katika mishipa yake hapo kwenye jicho, inaweza kuwa sababu ya kupikicha jicho au maambukizi fulani.
Red eye kwa ujumla isikupe wasiwasi saana, lakini hali hii ikiambatana na maumivu ya macho, au kupungua kwa uwezo wako wa kuona nakushauri umuona daktari kwani inaweza kuwa dalili ya magonjwa kama pinkeye (conjuctivitis au kwa kiswahili Kiwambo), Corneal ulcer, Dry eye syndrome.
UZI: Zifahamu njia za kuzuia mimba: Wote tunahitaji taarifa sahihi na zinazoeleweka kuhusu matumizi au njia mbalimbali za kuzuia mimba. Jambo la kuzuia mimba sio la mwanamke pekee bali hata mwanaume ana wajibu wa kujifunza mambo yanayotokea wakati wa tendo la ndoa. #BongeLaAfya
Mwanamke yeyote ambaye ameanza kupata hedhi ya kila mwezi anaweza kutumia njia za kudhibiti mimba. Njia hizi hutofautiana kutokana na upendeleo wa mtu binafsi au umri pia. Leo nitakusaidia kuwa na uwezo wa kuzuia mimba kwa kukupa taarifa sahihi.
1. Kondomu - Kuna kondomu za kike na kiume ambazo hufanya kazi kwa ufanisi kabisa zinapotumika. Kondomu zinapatikana sehemu nyingi na nina hakika wengi tunazifahamu. Kikubwa kondomu ya kike haitumiki wakati mmoja mnapotumia kondom ya kiume. Chagueni mmoja avae.
UZI: Kwa nini mnapaswa kuaminiana mnapoenda kupima UKIMWI: Miaka mitatu sasa nikifanya kazi hospitali na taasisi za tafiti kuna mambo nimekuwa nikikumbana nayo ambayo leo acha niyaweke mbele yenu ili wote tupate kujifunza. Nitaongelea tukio la upimaji wa UKIMWI. #BongeLaAfya
Kwa hii kadhaa nikiwa nafanya kazi za upimaji maabara, Upande wa upimaji UKIMWI kuna changamoto nyingi sana ambazo zinawakumba watu wanaokuja/wanaoleta rafiki/wapenzi wao kupima virusi vya ukimwi. Changamoto hizi nyingi zinatokana na kukosa uaminifu lakini pia udanganyifu.
Siku moja walikuja kupima UKIMWI mwanaume na mwanamke ambao kwa kuwaangalia tu unajua ni wapenzi. Baada ya ushauri na kuchukua sampuli ilibidi waende nje wakasubiri majibu. Sasa wakati naendelea kupima ghafla alirudi yule mwanamke na kutaka kuongea na mimi.
1/7: Jamii inaweka msukumo mkubwa sana kwa dada zetu "KUOLEWA", Msukumo unaoambatana na kikomo cha miaka kwamba akifika miaka fulani awe ameolewa.
Kama kuolewa ni jambo muhimu kiasi hiki, kwa nini hatuwaandai kuoa/kuolewa tangu mashuleni?
2/7: Mbaya zaidi mategemeo ya wanajamii wengi ni kuwa binti huyu atakua "MKE BORA". Binafsi naona sio sawa, sio sawa kwa maana kama jamii tunajisahau sana. Unawekaje mategemeo makubwa kama haya wakati hufanyi juhudi zozote kuhakikisha mtoto huyu anakua katika njia bora.
3/7: Napongeza taasisi nyingi zilizoweka nguvu katika kumnyanyua mtoto wa kike kutoka katika mkandamizo wa haki zao katika jamii, Swali langu kwenu kama tunavyopambana na hedhi salama lini tutaongelea NDOA? Hatuoni kama ni muhimu kuliwekea nguvu swala hili?
UZI: Nadhani umekutana na picha za hii couple zikizunguka mitandaoni, picha hizi zinawaonesha wapenzi wakiwa na tofauti ya kimuonekano.
Hali aliyonayo huyu mwanaume kitaalamu inaitwa "PROGERIA", Ni moja ya hali zinazotokea kwa nadra sana ambapo mtu huonekana mzee. #BongeLaAfya
Hali hii huanza kuonekana kwa mtoto miaka miwili baada ya kuzaliwa, Matatizo ya moyo na kiharusi (stroke) huwa sababu kubwa ya kupoteza maisha kwa watu wenye hali hii. Tafiti zinaonesha hali hii humpata mtoto 1 kati ya milioni 4 dunia nzima.
Ugonjwa huu hutokana na hitilafu katika jini ambayo hupelekea kutengenezwa kwa aina ya protini (progerin), Progerin ni abnormal mwilini, seli zikitumia protini hii hufa kwa urahisi na hivyo mtu kuzeeka haraka. Mtu harithi ugonjwa (not inherited).