UZI: Zifahamu njia za kuzuia mimba: Wote tunahitaji taarifa sahihi na zinazoeleweka kuhusu matumizi au njia mbalimbali za kuzuia mimba. Jambo la kuzuia mimba sio la mwanamke pekee bali hata mwanaume ana wajibu wa kujifunza mambo yanayotokea wakati wa tendo la ndoa. #BongeLaAfya Image
Mwanamke yeyote ambaye ameanza kupata hedhi ya kila mwezi anaweza kutumia njia za kudhibiti mimba. Njia hizi hutofautiana kutokana na upendeleo wa mtu binafsi au umri pia. Leo nitakusaidia kuwa na uwezo wa kuzuia mimba kwa kukupa taarifa sahihi. Image
1. Kondomu - Kuna kondomu za kike na kiume ambazo hufanya kazi kwa ufanisi kabisa zinapotumika. Kondomu zinapatikana sehemu nyingi na nina hakika wengi tunazifahamu. Kikubwa kondomu ya kike haitumiki wakati mmoja mnapotumia kondom ya kiume. Chagueni mmoja avae. ImageImageImageImage
2. Vizibo vizuizi au kwa kiingereza diaphragm - Vifaa hivi vina uwezo mkubwa wa kuzuia mimba. Vinatumika huziba njia ya uzazi ili kuzuia mbegu kupita, Zaidi hupakwanpia dawa maalumu ambayo mbegu zikigusa zinakufa. ImageImageImageImage
3. Vijiti - Hufanya kazi kwa ufanisi wa miaka 3 hadi 5 kutegemea na aina ya vijiti. Lazima viingizwe na kutolewa na mfanyakazi wa afya ambaye amepitia mafunzo. ImageImageImage
4. Sindano - Huzuia mimba kwa mwezi 1, 2 au 3. Kuna sindano maalumu ambapo mwanamke anachomwa ili kuzuia homoni hivyo kuepuka mimba. ImageImage
5. Vidonge vya majira - Ufanisi wake ni mkubwa zaidi pale mtu anazingatia matumizi na umezaji wa vidonge katika muda aliopangiwa bila kuruka dozi. Image
6. Kitanzi (IUD) - Hufanya kazi kwa muda wa miaka mitano au 12. Hutegeme ana aina ya kitanzi, Kitanzi kinapaswa kuingizwa na mfanyakazi wa afya mwenye mafunzo maalumu. ImageImageImage
7. Vasektomi (Vasectomy) kwa mwanaume na Kufunga kizazi (tubal ligation) kwa wanawake - Huku ndio kufunga kizazi. Hapa mwanamke hataweza kupata mtoto na mwanaume hataweza kuzalisha. Hakuna athari zozote za kupungua kwa uwezo wa kufurahia tendo. ImageImageImageImage
8. Njia ya kuhesabu siku kwa kuzingatia kalenda - Mwanamke anatakiwa kujua lini atakuwa katika siku zake za kuweza kushika mimba hivyo kuepuka kufanya ngono wakati huo. Aidha unaweza kutumia kondom. Image
9. Kumwaga nje (withdrawal) Ni ngumu sana kutumia njia hii kwa mafanikio. Hata kama mwanaume atachomoa uume, majimaji kidogo yenye mbegu za kiume yanaweza kuingia ukeni na kusababisha mimba. ImageImageImageImage
9. Kumwaga nje (withdrawal) Ni ngumu sana kutumia njia hii kwa mafanikio. Hata kama mwanaume atachomoa uume, majimaji kidogo yenye mbegu za kiume yanaweza kuingia ukeni na kusababisha mimba. ImageImageImageImage
10. Ngono bila kugusana/Kuingiliana kimwili - Bila kuingiza hata uume kidogo ndani ya uke. Mnaweza kufanya hivi kwa ku-kiss, kuchuana au nyingine yoyote. Kuna uwezekano mdogo sana hata wa kupata magonjwa ya zinaa. Image

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Bonge La Afya 🇹🇿

Bonge La Afya 🇹🇿 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @FestoNgadaya

2 Dec
UZI: Kwenye utafutaji, tabia kama za wanyama hawa zinaweza kuua kundi.

Bata: Kujivuta vuta, kufanya kazi polepole na kuendekeza uvivu mapaka mambo ya kikundi yanazorota au kufa kabisa.

Bundi: Mtu anayefikiria ana akili kuliko wote kwenye kikundi- hutumia lugha ngumu kueleweka.
Chura:Rudia rudia kitu kile kile mapaka anawachosha wenzake kundini

Kenge:Hatumii akili sawasawa, ujinga mwingi na kufanya maamuzi ya ovyo yenye kuwakatisha tamaa wenzake

Kiboko:Kulala lala na kupiga miayo, wakati wenzake wanachacharika, yeye ni kukaa tu hafanyi kazi.
Kifaru:Yeye hushambulia wengine kwenye kikundi bila sababu

Kinyonga:Kigeugeu, akiwa kwa mwanakikundi huyu anasema hili na akiwa kwa mwingine anasema tofauti

Kobe:Hujitoa akiudhiwa, hana uvumilivu kwenye changamoto zinazoikabili kikundi.
Read 9 tweets
27 Nov
UZI: Red eye au bloodshot kwa kitaalamu, hutokea pale ambapo mishipa midogo ya damu inayoonekana kwenye uso wa jicho kupanuka au kujawa na damu. Hali hii hutokea kutokana na uwepo wa kiwango kidogo cha oxygen inayotolewa na tishu zinazofunika jicho au maambukizi. #BongeLaAfya Image
Hali hii huwa ya kawaida na inaweza kutokea katika jicho moja au macho yote mawili. Hiyo rangi nyekundu inayoonekana ni rangi ya damu katika mishipa yake hapo kwenye jicho, inaweza kuwa sababu ya kupikicha jicho au maambukizi fulani. Image
Red eye kwa ujumla isikupe wasiwasi saana, lakini hali hii ikiambatana na maumivu ya macho, au kupungua kwa uwezo wako wa kuona nakushauri umuona daktari kwani inaweza kuwa dalili ya magonjwa kama pinkeye (conjuctivitis au kwa kiswahili Kiwambo), Corneal ulcer, Dry eye syndrome. Image
Read 8 tweets
18 Oct
UZI: Dalili za mimba: Ujauzito ni ndoto ya wengi, huku kwa wengine ni jambo wanaloepuka na kuzingatia sana. Wadada wengi wanaonesha kuhitaji watoto tofauti na wanaume. Leo nimekuletea dalili 10 za ujauzito ambazo huashilia uwepo wa ujauzito #BongeLaAfya Image
1. Kutoona siku zako: Kukosa siku zako ni moja ya dalili za kwanza kabisa ambazo wengi wetu wamezoea. Katika kipindi cha mzunguko kuta ya mfuko wa uzazi huvunjika na kujiengua na kutoka nje katika mfumo wa damu, hudumu kwa siku tatu mpaka saba. Unapopata ujauzito hujishkiza hapo. Image
2. Misuli ya miguu kubana/cramps: Katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito mwanamke anaweza kuona dalili za miguu kukaza au kubana, Hii inatokana na mabadiliko ya mwili katika kuchakata calcium ambayo huitajika kwa wingi kuunda mifupa ya mtoto, meno na viungo. Image
Read 13 tweets
7 Oct
UZI: Kwa nini mnapaswa kuaminiana mnapoenda kupima UKIMWI: Miaka mitatu sasa nikifanya kazi hospitali na taasisi za tafiti kuna mambo nimekuwa nikikumbana nayo ambayo leo acha niyaweke mbele yenu ili wote tupate kujifunza. Nitaongelea tukio la upimaji wa UKIMWI. #BongeLaAfya Image
Kwa hii kadhaa nikiwa nafanya kazi za upimaji maabara, Upande wa upimaji UKIMWI kuna changamoto nyingi sana ambazo zinawakumba watu wanaokuja/wanaoleta rafiki/wapenzi wao kupima virusi vya ukimwi. Changamoto hizi nyingi zinatokana na kukosa uaminifu lakini pia udanganyifu. Image
Siku moja walikuja kupima UKIMWI mwanaume na mwanamke ambao kwa kuwaangalia tu unajua ni wapenzi. Baada ya ushauri na kuchukua sampuli ilibidi waende nje wakasubiri majibu. Sasa wakati naendelea kupima ghafla alirudi yule mwanamke na kutaka kuongea na mimi. Image
Read 8 tweets
21 Sep
1/7: Jamii inaweka msukumo mkubwa sana kwa dada zetu "KUOLEWA", Msukumo unaoambatana na kikomo cha miaka kwamba akifika miaka fulani awe ameolewa.

Kama kuolewa ni jambo muhimu kiasi hiki, kwa nini hatuwaandai kuoa/kuolewa tangu mashuleni?
2/7: Mbaya zaidi mategemeo ya wanajamii wengi ni kuwa binti huyu atakua "MKE BORA". Binafsi naona sio sawa, sio sawa kwa maana kama jamii tunajisahau sana. Unawekaje mategemeo makubwa kama haya wakati hufanyi juhudi zozote kuhakikisha mtoto huyu anakua katika njia bora.
3/7: Napongeza taasisi nyingi zilizoweka nguvu katika kumnyanyua mtoto wa kike kutoka katika mkandamizo wa haki zao katika jamii, Swali langu kwenu kama tunavyopambana na hedhi salama lini tutaongelea NDOA? Hatuoni kama ni muhimu kuliwekea nguvu swala hili?
Read 7 tweets
10 Sep
UZI: Nadhani umekutana na picha za hii couple zikizunguka mitandaoni, picha hizi zinawaonesha wapenzi wakiwa na tofauti ya kimuonekano.

Hali aliyonayo huyu mwanaume kitaalamu inaitwa "PROGERIA", Ni moja ya hali zinazotokea kwa nadra sana ambapo mtu huonekana mzee. #BongeLaAfya ImageImage
Hali hii huanza kuonekana kwa mtoto miaka miwili baada ya kuzaliwa, Matatizo ya moyo na kiharusi (stroke) huwa sababu kubwa ya kupoteza maisha kwa watu wenye hali hii. Tafiti zinaonesha hali hii humpata mtoto 1 kati ya milioni 4 dunia nzima. Image
Ugonjwa huu hutokana na hitilafu katika jini ambayo hupelekea kutengenezwa kwa aina ya protini (progerin), Progerin ni abnormal mwilini, seli zikitumia protini hii hufa kwa urahisi na hivyo mtu kuzeeka haraka. Mtu harithi ugonjwa (not inherited). Image
Read 7 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!