UZI: Nadhani umekutana na picha za hii couple zikizunguka mitandaoni, picha hizi zinawaonesha wapenzi wakiwa na tofauti ya kimuonekano.

Hali aliyonayo huyu mwanaume kitaalamu inaitwa "PROGERIA", Ni moja ya hali zinazotokea kwa nadra sana ambapo mtu huonekana mzee. #BongeLaAfya ImageImage
Hali hii huanza kuonekana kwa mtoto miaka miwili baada ya kuzaliwa, Matatizo ya moyo na kiharusi (stroke) huwa sababu kubwa ya kupoteza maisha kwa watu wenye hali hii. Tafiti zinaonesha hali hii humpata mtoto 1 kati ya milioni 4 dunia nzima. Image
Ugonjwa huu hutokana na hitilafu katika jini ambayo hupelekea kutengenezwa kwa aina ya protini (progerin), Progerin ni abnormal mwilini, seli zikitumia protini hii hufa kwa urahisi na hivyo mtu kuzeeka haraka. Mtu harithi ugonjwa (not inherited). Image
Watoto wenye ugonjwa huu huonekana wenye afya njema wakati wa kuzaliwa ila baada ya mwaka mmoja dalili kama;
-Kichwa kikubwa
-Macho makubwa
-Pua nyembamba
-Mishipa kunekana
-Meno kukua taratibu
-Sauti nyembamba
-Nywele kutoka
-Kupungua uzito au kasi ya ukuaji. Image
Kadiri mtoto anavyokua kutokana na ugonjwa huu mtoto huanza kupata magonjwa na matatizo wanayoyapata wazee. Mpaka sasa haijapatikana dawa ya kutibu japo wataalamu wa tafiti bado wanaendelea kutafuta dawa. Kwa sasa kuna aina ya dawa wanayotumia pia wagonjwa wa saratani. Image
Dawa hii husaidia kupunguza na kuchelewesha baadhi ya dalili. Ukiona mtoto ana dalili hizi fika hospitali umuone daktari ambaye akigundua ni tatizo hili atakutuma kwa daktari wa watoto. Image

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Festo D Ngadaya | Bonge La Afya 🇹🇿

Festo D Ngadaya | Bonge La Afya 🇹🇿 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @FestoNgadaya

25 Aug
UZI: Acha leo niwajuze mambo mengine ninayofahamu, Leo nitawapa tips chache kuhusiana na gari yenye mfumo wa kiautomatiki (automatic transmission). Kitaaluma pia niliwahi kuwa mkufunzi wa udereva. Sasa je hizi: P, R, N, D, 2, L Kwenye gari automatic zina maana gani hasa?
Mfumo wa (uwiano wa kiautomatiki) automatic transmission,auto, self shifting au AT ni mfumo wa ubadilishaji gia unaojiendesha wenyewe haihitaji dereva kubadili gia zaidi tu atailekeza gari kwenda mbele au nyuma. Mfumo huu uligunduliwa miaka ya 1900s na ndugu wa-sturtevan, boston.
Ford ni moja ya makampuni ya mwanzo kabisa maarufu kuanza kutumia mfumo huu. Gari hizi huwa na mfumo wa mpangilio wa gia ukipangiliana kutoka P, R, N, D, 2 na L.

1. P - Parking: Hufunga gearbox hivyo kuzuia gari kutembea. Gia/Mfumo huu hutumika pale ambapo mtu ameegesha gari.
Read 8 tweets
24 Aug
UZI: Acne/folliculitis Keloidalis nuchae au kwa kifupi (AKN) ni hali ambayo mtu huonekana kuwa na makovu au uvimbe nyuma ya shingo. Hali hii iligundulika miaka ya 1800s. Kwa mujibu wa taasisi ya @Medscape hali hii unawapata sana watu wenye asili ya Africa emedicine.medscape.com/article/107214…
Mpaka sasa sababu ya ugonjwa huu haijajulikana japo inafikiliwa sababu mbalimbali kama:
1. Kujikata wakati wa kuchonga nywele ukiwa unanyoa ambapo nywele huingia ndani ya ngozi.

2. Michubuko inayotokana na kola ya shati au bidhaa nyingine za shingoni.
3. Maambukizi sugu ya bakteria.
4. Kushuka kwa kinga ya mwili
5. Matumizi ya baadhi ya dawa za antiepileptic au cyclosporine
6. Kuongezeka kwa seli aina ya mast (mast cells)

Baadhi ya tafiti pia zilionesha unaweza kuwa ugonjwa wa kulithi.
Read 6 tweets
16 May
Ifahamu safari ya mbu kuanzia anapokung’ata mpaka anasababisha ugonjwa wa malaria: Kitu cha kwanza unachotakiwa kufahamu ni kuwa, Japo kuna mbu jike na dume, Mbu jike pekee ndiye anayeng’ata. Mbu dume hang’ati.
#ElimikaWikiendi Image
Hii ni sababu mbu jike uhitaji damu ili kutengeneza mayai huku dume hana uhitaji wa damu maana hatengenezi mayai hivyo hupata chakula kutoka kwenye majimaji ya maua (flower nector) na mimea.
Damu anayoivuta mbu haina faida yoyote ya lishe kwake. Damu hutumika kutengeneza mayai pekee ambayo baadae huyaweka kwenye maji ili dume arutubishe ili kuzalisha mbu wengine. Ili kuishi mbu jike hupata chakula chake pia kwenye maua.
Read 8 tweets
11 May
BS/MRDT: Umefika hospitali daktari kakusikiliza kisha kwenye fomu yako kaandika ukapime BS/MRDT unashindwa kuelewa ila kwa sababu unaumwa unaenda kupima. Hii BS/MRDT ni nini? Leo acha nikujuze.
MRDT ni kifupi cha Malaria Rapid Diagnostic Test (kipimo cha haraka cha ugunduzi wa vimelea viambukizavyo Malaria). Kipimo hiki kinausisha utambuzi wa antibodies za Malaria (kinga za mwili zinazotengenezwa baada ya kuugua)
Mwili huchukua mpaka siku saba ndipo hutengeneza kinga (antibodies) ambazo ndio hutambuliwa na kipimo hiki cha MRDT. Hivyo ukienda hospitali kabla kinga hizi hazijatengenezwa utapima na kuonekana huna Malaria.
Read 9 tweets
6 May
Inakuaje mpaka mtu anapata kitambi? Katika kipindi hiki cha kukaa ndani watu wamepunguza mizunguko ambayo inasaidia kama mazoezi madogo madogo. Sasa leo naomba tujifunze ni namna gani mtu anapata kitambi, Kitambi ni nini hasa? Nitatumia njia ya input na output.
Nimechagua mfumo wa input na output maana hiki ndio kinachotokea hata kwenye mwili mpaka mtu anapata kitambi. Input nikiwa na maana "kinachoingia" na output ''kinachotoka". Nikwambie tu hicho kitambi ni store ya mwili ya kutunzia chakula.
Mwili unahitaji nishati (energy) ili kufanya kazi, Nishat kubwa ya mwili ni sukari (glucose) tofauti na sukali tunayokunywa kwenye chai, Chanzo kikuu cha sukari hii ya mwili ni wanga (carbohydrate). Je inakuaje mpaka wanga unakua sukari?
Read 18 tweets
5 May
Nini kinapelekea mimba kuharibika au kupata mtoto mmoja pekee wa kwanza ikiwa baba ana kundi la damu positive (+) yani A+,B+,AB+ au O+ na mama negative (-) yani A-,B-,AB- au O-. Umewahi kujiuliza hili swali? basi leo nina majibu yako hapa kupitia #WapwaNaAfya Image
Kwanza kabisa kila mtu ana kundi moja la damu kati ya haya makundi manne (A,B,AB au O) kundi ambalo umelipata baada ya mchanganyo wa vinasaba kutoka kwa wazazi wako. Makundi ya damu huenda mbele zaidi na kutofautishwa kama negative- au positive+ kitaalamu tunaita rhesus (Rh).
Kabla ya ujauzito wengi tumekuwa hatufatilii makundi yetu ya damu pasipo kujua ni kitu muhimu sana kwa wote iwe mwanaume au mwanamke. Nimewahi kuelezea kwa undani zaidi kuhusu makundi ya damu: Unaweza kupitia hapa kisha tuendelee.
Read 11 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!