TATIZO LA MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI VIZURI (HEART FAILURE).
Moyo ni kiungo muhimu ktk mwili kinachotumika kusambaza/kupokea damu sehemu mbalimbali mwilini (mapafu, ubongo, figo, matumbo n.k). Hivyo, moyo kushindwa kufanya kazi hupelekea mwili kukosa hewa na chakula. #Thread
SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA MOYO KUSHINDWA KAZI. 1. Shinikizo la damu lisilothibitiwa barabara 2. Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital) 3. Magonjwa ya mishipa ya moyo (coronary artery d'se/ischemic heart d'se) 4. Magonjwa ya tezi shingo (thyroid dysfunction) n.k
WATU WALIO KTK HATARI YA KUPATA TATIZO HILO NI; 1. Wenye shinikizo la damu 2. Kisukari 3. Wenye uzito mkubwa (obesity) 4. Watumiaji wa pombe na sigara 5. Wenye historia ya matatizo ya moyo kwenye familia yao n.k
DALILI ZA MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI; 1. Kupata shida ya kupumua wakati wa kufanya kazi 2. Kukosa hewa akilala chali 3. Kukohoa hasa usiku 4. Kushtuka usiku kutokana na kukosa hewa 5. Kuvimba mwili kwa kuanzia miguuni 6. Moyo kutanuka (cardiomegally) 7. Ini kukua (hepatomegaly)
MAMBO YA KUEPUKA KWA MGONJWA WA MOYO KUSHINDWA KAZI; 1. Epuka kunywa pombe 2. Epuka kula vyakula vyenye mafuta mafuta 3. Epuka kula nyama nyekundu 4. Epuka unywaji wa maji mengi 5. Epuka matumizi ya chumvi nyingi/chumvi ya kuongeza 6. Tumia dawa ulizopewa hospitali kikamilifu
Ukipata tatizo lolote linalofanana na hili. Fika hospitali iliyo karibu na wewe mara moja.
TATIZO LA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI (KIDNEY FAILURE).
Figo ni kiungo muhimu sana kwenye mwili wa binadamu kwani hutumika kutoa takamwili kama; urea, maji ya ziada, chumvi n.k. Kushindwa kwa figo hupelekea takamwili kubakia mwilini hivyo kumletea shida mgonjwa. #Thread
SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI. 1. Kisukari 2. Shinikizo la damu 3. UKIMWI 4. Matumizi ya muda mrefu ya dawa zinazoweza kuathiri figo mfano; dawa za maumizi (diclofenac, ibiprofen n.k) 5. Matumizi ya miti-shamba 6. Pombe yaliyozidi
7. Ugonjwa wa figo kuwa na vifuko vyenye maji (polycystic kidney disease) 8. Matatizo yanayoweza kupoteza maji mwilini. Mfano; kutapika sana, kuharisha sana n.k 9. Maambukizi kwenye damu (sepsis).
FAIDA ZA KUNYONYESHA KWA MAMA NA MTOTO KIAFYA
Kutokana na utandawazi na harakati za maisha wanawake waliojifungua wamelazimika kutokunyonyesha watoto wao sawa sawa. Kitaalamu mtoto anatakiwa kunyonya miezi sita bila kupewa chakula isipokuwa dawa na chanjo tu #UZI
FAIDA KWA MAMA 1. Kumpunguzia hatari ya kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua 2. Ni njia moja wapo ya kupanga uzazi 3. Kumlinda dhidi ya kansa ya matiti na kansa ya kizazi 4. Kumjengea uhusiano mzuri na mtoto
FAIDA KWA MTOTO 1. Kuimarisha kinga ya mwili na kumlinda magonjwa mfano; magonjwaya upumuaji na magonjwa ya mfumo wa chakula kama vile KUHARISHA 2. Kumjengea uhusiano mzuri na mama yake. Hivyo kumfanya mtoto awe ni mwenye furaha na kuchangamka