"NILILAMBA JOKERI🃏.."

Nipo kwenye gari nna hasira flani..nafungua whatsapp natafuta convo yetu mwanzoni kabsa..naandika "mnazingua"
Huyu ni rafiki angu wa kike,Ney, tumepanga kwenda premier ya movie flani ilikua inatoka af tuna ka dk 10 ianze,ameomba aje na rafiki zake wawili
Mi nipo na mchizi,ye ndo kamaindi mbaya. Kanimaindi mimi pamoja na huyo rafiki angu.."kubabeki,tunaenda kuanza movie nusu..si bora tukanywe bia tujue moja" 🤔nkawaza sio wazo baya ujue..
Mara nasikia milango inafunguliwa siangalii hata nyuma nawasha gari..
Nasikia sauti ya ney "kelvin,we are sorry" naongeza sauti ya mziki..
Mchzi anageuza shingo anawasalimu..naona kashalegea kuona vimwana,anaanza kuwapigisha stori pale
Njia nzima nipo kimya..hadi tunafika.
Wanashuka na mimi kma dereva nachek kma vitu vipo sawa kabla sijashuka
Ile nashuka..ndo nikamwona

Kidgo niseme ni elizabeth michael ..sema huyu alikua mrefu kidgo..katupia tight jeanz nyeusi..juu kisweta flani cha kishkaji..raba kali na uhakika alizitoa @JustFittz
Sijawah kumwona huyu..
Nikaelewa kwann mwana alianza kua mchangamfu ghafla
Ney akanifata..akanibembeleza flani kidgo atleast aone naongea..nikacheka
Nikaulizia jina nikaambiwa manzi anaitwa Clara..ni friend wao wamesoma wote secondary..
Mtoto tukagongana macho..ila nikapotezea maana kiroho kishaanza dunda..scenario kibao kichwani jinsi ya kumnasa..
So mnyama nipo mwsho mwsho mtoto akasita naona hyu hapa..
"Mambo..am sorry mi ndo nimewachelewesha..sorry" kisauti cha @_KateFrancis 😣🙌 nikajibu haina shida...basi tukala movie letu tulilocheleewa..siku ikaisha kila mtu kwao...
Kama wiki moja ikapita..nilishaanza kama kupotezea..text inaingia,namba ni mpya..sipendi namba mpya so naipotezea maana txt haijielezei vya kutosha..baada ya dk 5..ikapiga.."sipokeii"..kwanza nna madeni kibao😅.
Text ikaingia tena "hey clara hapa"
Nikajisemea "angeanza hivi"
Ananiuliza nipo wap..
Usiku huu nipo ghetoo..
Njoo..
Sehemu yenyewe siijui..najibeba kiuvivu.
Nafika kumbe kisehemu ni ki pub kipo ghorofani mitaa flani ya mbezi
Nampigia..ananyanyua mkono kwenye meza moja wamekaa wasichana kama wanne pamoja na yeye na wana wawili
Nafika meza yao..ananyanyuka..anaonekana kashalewa..ananichekea.
Ananipiga hug afu ghafla nashangaa napigwa kiss..alikua anakunywa safari huyu..

"Guys...huyu ndo baby wangu"

Mwana bado sielewi kinachohappen..
Anakuja muhudumu kashikilia karatasi..
Huku anaenda kuchukua ki handbag kwenye kiti anapaza sauti kwa nguvu kidgo huku wenzake wanasikia..

"Baby lipia bili tukalale zetu"
Muhudumu ananipa karatasi huku akiniangalia kama 'chukua bili unashangaa nini??😅'

Naisoma ile karatasi..118k
Akili inaniambia geuka uende zako
Nanyanyua macho namwona ananiangalia kama 'tatizo ni nini'..
Bahati yangu nilichukua 130k maana ni usiku chochote chatokea ukikutana na manzi...
Roho haijui iume au vipi...naamua nichukue na k vant kubwa maana kilichobaki ni kimoja tu leo,usiku ushaisha huu
Tunasepa gheto..kusema ukweli hapo najutia kweli. Ila najipa moyo kwamba pisi ni kali sana..mataa ya barabarani yanàmpiga huku macho yangu yakijipa shift..nisije gonga mtu..mtoto alivyokaa..mini ilivyopanda mapajani,unywele ulivyoshuka,kaperfume kake ndo kananichanganya kabisa
Nawaza kwamba potelea pote..kwa pisi ile hela ni makaratasi tu😅
Alichonichanganya zaidi ni tumefika ndani hatukusema hata neno moja..mzigoni.

Asubuhi ya jmosi naamka bado kaulaza..nikaona nimwagizie supu af nimwamshe..
Baada ya ka hangover kake kupungua tukaweka movie pale
Baadae akaniaga anasepa..
Jioni hivi text inaingia..muamala wa 200k umesoma kutoka kwa Clara..nataka kumpigia text inaingia.."nilikua nakujaribu kama utaniweza,umejitahidi.kama una mtu husijibu hii text and thanks kwa jana,ila kama hauna then ntakuja saa tatu nitxt nikuletee nini
Na kvant usiimalize,tafuta na series nzuri"

Nilitukana kimoyomoyo,nikascroll group la wana fasta nkaandika "oi wana nyie nendeni tu mi leo siko njema tumbo linazingua"
Nikavuta namba ya ney kumpa stori..akawa haamini amini..akasema
"Kama kweli kevi basi umelamba bingo,ndo maana aliomba namba yako,maana huyo anapendaga kama hatapenda tena..ila jiandae kuzinguliwa na kaka zake mwenzangu maana wakishua kweli huyo"

Wana TUACHAGE UBAHILI na maisha ni kubet siku zote.

Waambieni #fanani✍️ alipita
Gongeni likes
@tweetsrifle @troniofficial @funjojr @Obofficial3 @sonnino123 @Micky_dee_ommy
Wana nisogezeeni Rt kwa uzi weekend iendelee🙏✌

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Urs truly✍️

Urs truly✍️ Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @urztrue

15 Aug
"THUBUTUU...🤧"

Sijui ilikuwaje hadi nkasahau kuandika kuhusu hiki kisa..🤭
Nadhani kwasababu mchizi hakua mtu wangu wa karibu sana..ilikua ni kuonana kwenye vigenge vya stori na kitaa.

Ila siku tulijikuta wawili tu kwenye kota za tanesco anapokaa,chobingo moja yetu pendwa..
Mchizi aliitwa Saleh..
Tulisalimiana kiwana tukiulizana mishe zinaendaje na vijistori vya hapa na pale vya kupoteza muda.
Mchizi alitoa sigara mbili huku akiniuliza kama natumia..nilimjibu situmii hvyo aliiwasha yake akavuta pafu mbili kubwa..alitoa moshi nje af akabaki kaduwaa
Ilibidi nimuite mara mbili,aliposhtuka ilibidi ajicheke..nikamuuliza vipi asee mbona umeniacha peke yangu..
Nakumbuka alinambia
"aahh kmmk,nna kipengele kimoja hicho na sijui itakuaje" nkamwambia "nipange"
Alisita kidogo akaangalia sigara yake kidgo kisha akaanza kunipa stori
Read 26 tweets
27 Jun
"KARMA..🎭"

🌡Kama huna kifua basi usisome uzi huu haukufai maana mi natoa visa vya ukweli kama ifuatavyo...👇

Nipo na mwana ananionesha picha af ananiuliza "unaikumbuka hii"..naichek af nacheka ni picha ya kitambo kidgo,tukiwepo sisi na wasichana watatu..mmoja wao akiwa VERO
Vero mi nilimjua kipindi anatoka na mchizi wangu huyo..baada ya kukutana nae viwanja..tulikula sana bata za hapa na pale na huyu manzi,kipindi hicho anakaa mitaa ya sabasaba na wenzake.. walikua wamoto..kila weekend lazima niulizwe "shem leo wap!!nna rafki yangu nataka nikususie"
Kiukweli mchizi wangu alikua sio mtuliaji so wana tulikua tunajua saa yoyote kinaweza nuka..ila cha kushangaza haikua hvyo kwa muda mrefu..nadhani style za maisha ziliendana kiasi kwamba ilikua haiboi..
Basi hapo kati Vee kama nilivyokua namwita akapata mimba ya mchizi
Read 18 tweets
7 May
"LAANA...."🧞‍♂️

Wiki moja baada ya kuanza darasa la kwanza kutokana na umbo langu kua dogo kidgo kuliko wengne ilinipa ugumu maana nilishindiliwa uonevu wa kila namna..ila siku,mmoja wa wanafunzi alinikingia kifua..na si mwingine bali ni "MUDI" kama wengi tufupishavyo, jembe langu
Sikuwah kuonewa kuanzia siku hiyo na ndipo nilipojifunza ubabe..sikuwah kumwambiaga ila alikua kama kaka angu japo tulikua umri sawa ila kwa mwili wake na udogo wangu tofauti ilikua kubwa,alikua ndo rafiki wangu wa kwanza kishule shule. Alinifunza kujihami,kujilinda na ni yeye
alinifunza utukutu..asee shule nzma ilikua inamtambua. Kwa kila walimu walichomsema basi na mm nilihusika ila kwakua wengi hawakuamini mi kuhusika ivo mudi alichkua adhabu zote na hakuwah kunitaja. Ila nami nilihakikisha hafeli mitihani kwa njia yoyote na hakuwahi kuniangusha
Read 22 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!