Kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja nimekuwa nikiugua na kutibiwa ugonjwa wa #COVID19 unaotokana na virusi vya #Corona (SARS-CoV-2). Ni jinsi gani niliweza kuambukizwa ugonjwa huu kijijini kwetu Lufilyo, Busokelo, Mbeya, pamoja na kuzingatia tahadhari zote dhidi ya (1/7)
maradhi haya ni kitendawili. Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai, zawadi ya Pasaka. Nawashukuru pia mke wangu Lucy Akiiki, watoto na wajukuu, familia za Kahigwa na Mwandosya, Madaktari na Wauguzi wangu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, na (2/7)
Hospitali ya Nairobi (Nairobi Hospital), @AMREFFlyingDocs, Uongozi wa @StanbicBankTZ na @StanbicKE ,Balozi Chirau na Rose Mwakwere wa Nairobi, Mheshimiwa Jaji Paul na Grace Mugamba wa Uganda, na ndugu na marafiki wote wanaoendelea kunitakia heri na afya njema. Asanteni sana.(3/7)
Huu ni ushuhuda wangu kwamba Corona/Covid 19 ipo #Tanzania .
Tumebahatika kuvuka kipindi cha mpito salama na kumpata Rais mpya Mheshimiwa @SuluhuSamia . Mwenyezi Mungu amjalie neema na baraka tele. Mheshimiwa @DrPhilipMpango , Makamu wa Rais, ambaye nampongeza kwa uteuzi, (4/7)
amepitia hayo yaliyonisibu.
Nawaomba, tena kwa unyenyekevu mkubwa, Mhe.@SuluhuSamia , Mhe.@DrPhilipMpango na Mhe,@DrHmwinyi , Rais wa #zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwamba, tuongozwe na sayansi, na tuungane na tushirikiane na wenzetu duniani kote katika (5/7)
kupambana na ugonjwa huu kama tunavyofanya katika milipuko ya magonjwa mengine. Kwani katika mlipuko wowote, hakuna anayeweza kuwa salama mpaka wote duniani tumekuwa salama.
Maombi yangu kwa Mwenyezi Mungu ni kwamba, ikiwezekana, Mtanzania mwingine awaye yote aepushwe na (6/7)
mateso na taabu za kukabiliana na maradhi haya.
Hakika siwezi kumtakia mtu mwingine yeyote, hata aliye adui yangu mkubwa namna gani, kama yupo, apate ugonjwa huu.
Tutakiane Pasaka njema. Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania. Pro Deo et patrina. (7/7)
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh