MANDARA

Hii ndio ilikuwa point yangu ya kwanza baada ya kutoka getini. Nilikuwa na personal porter anaitwa Fredy. Mwenyewe alinipokea bag (back pack) na kujitambulisha kwangu.

Ukiwa na personal guide ina maana yeye atakua na wewe bega kwa bega, achana na wale guide wa group..
Tulianza kwa story akanielezea safari zake milimani. Yeye keshapanda mara 6 hadi Uhuru Peak. I was excited!

Mwanzo story zilikolea baadae zikakata ule uchovu.

Tunavyopanda tulikuwa tunakutana na makundi ya watu wanarudi na wengi walikua wanatuambia “pole pole”..
..nadhani huu ndio msemo maarufu ukifuatiwa na “Jambo”.

Nilianza kuchoka jinsi masaa yanavyokwenda. Nikawa kama siwezi kupumua vizuri. Muda mwingi Fred alikuwa ananisitiza kunywa maji.

Kuna muda wenzangu walikuwa mbele..
Baada ya kupumzika nikasema hebu nikae hili kundi sitaki kubaki nyuma..

Enhee bana kumbe kasi yao haiendani na mimi. Ile kutembea hata dakika 5 nyingi nikaona kama roho inataka kutoka, mapigo ya moyo yanaenda mbio hatari roho kama yataka kuchomoka.. Joto likanipanda 😟😟
Fred as usual akaniambia pumzika. Nikakaa chini, vua sweta nikanywa maji. Baada ya muda ndio nikarudi hali ya kawaida.

Nilishaanza kupanick kuwa nakufa sasa, maana hapo si tulishaambiwa watu wanakufa huko sana na kila mtu unamwambia unaenda kupanda Mlima anakuwa na doubt..
..mimi nikajua mama yangu hapa na mimi ndio bye bye!

Freddy akanishauri kuwa kila mtu ana speed yake so I should keep same speed maana tunazidi kupanda juu, hali ya hewa ni ya mgandamizo..
Tuliingia Mandara saa 2/3 usiku.

I was excited kwamba after a long walk kuna sehem tumefika tupumzike.

Kitu cha kwanza ni kuregister majina.. Kulikuwa na baridi hatari, mikono ilikuwa na ganzi hata kuandika nilishindwa waliniandikia jina nikaweka signature tu 😃😃
Usingizi ukanipitia. Baada ya muda kidogo mtu akaja kuniamsha kwa ajili ya dinner.

Yaani nilichukia. Nikaona sijawahi kukutana na mtu mbaya na katili duniani kama huyo aliyeniamsha kula. Na hapo tunasisitizwa kwamba ni lazima ule kama unataka kufika juu.
Kufika kileleni nataka ila kama hali ndio hii NO WAY!

Nikaanza kulia ndani ya sleeping bag... lia kishenzi.. Makamasi na machozi yanatiririka tu ila nalia kimya kimya watu wasinisikie.

Mtu unaweza kushangaa kama ni the same person niliyekuwa nashangilia muda mchache uliopita..
Nikawa najiuliza hivi nimekuja kufanya nini huku? Baridi lote hili tena nikale huko nje!

Nikaja kuamshwa tena. Hapo wenzangu hawawezi kula hadi watu wote watimie.

Nimefika dinning sijataka kuongea na mtu. Wakinichekesha najilazimisha kucheka. Huo muda akili inawaza mambo kibao.
Tukaonyeshwa dormitories. Nikatafuta kitanda changu cha chini hicho hapo pichani.

Yaani kuna baridi hatari. Nikajifunika sleeping bag nikajilaza.

Hapo nina hasira kishenzi, ukiuliza hasira za nini sijui 😬😬
Chakula chenyewe nakutana na vegetable soup, macaroni (ndio siyapendi kudadeki), mikate, chai.

Chakula ni kizuri ila hamu ya kula sikuwa nayo hata kidogo. Nakula then straight in bed sisemeshani na mtu.

Na mtandao ni hakuna so no WhatsApp, Instagram, Twitter wala @JamiiForums
Pichani ni asubuhi tukijiandaa kwenda HOROMBO..

Hakuna sehemu niliyoipenda katika safari hii kama Horombo. Palinifuta machozi yote na kunirejeshea ari yangu ya kwenda kileleni 💪🏾

Naweka kituo hapa kwa sasa!

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Habiba Mtanzania 🇹🇿

Habiba Mtanzania 🇹🇿 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @habibamtanzania

13 Apr
SAFARI YA MOSHI

Tunaingia Moshi usiku saa 2 na kupokelewa na wenyeji wetu wakarimu kishenzi. Wale ma-guide sijui walidhani tumetoka nchi gani hatujui Kiswahili, kumbe ni wabongo tu😅😅

Nadhani walishazoea wanaoenda kupanda Mlima ni foreigners tu. Hii kidogo ilinisikitisha..
Hoteli tuliyofikia kulikuwa na wazungu kibao. Wengi wametoka mlimani wakipongezana kwa dinner, wines na kupeana vyeti..

Nikawa nawatizama kwamba can I do this? Unaona watu wanachechemea miguu, sura hazitamaniki wamebabuka, wengi wako hoi.

Nikaguna, mambo yenyewe ndio hivi!!!
Basi, ule usiku tukafanyiwa training na rescue team ya ile kampuni.

Tukapewa maelekezo yote muhimu yaliyohitajika. Asubuhi safari ya Mlimani.

Nilikuwa na shauku na hofu kwa wakati mmoja. Nikasali na kuamua liwalo na liwe. Kesho ndio kesho!
Read 7 tweets
12 Apr
Leo tunaendelea na experience yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro ambapo machozi, jasho na damu ni sehemu ya safari hii inayohitaji ujasiri na moyo wa chuma kweli kweli..

Mfululizo wa matukio niliyopitia unaweza kukufundisha na kukuandaa vyema ewe Mtalii mtarajiwa 😅😅

UZI 👇🏾
Kituo 1: MLIMA URUGURU

Urefu wa Mlima Uluguru ni kama 8600ft. Na huu ulikuwa ni moja ya mlima wa majaribio kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

Kiukweli hili lilikuwa ndio jaribio rahisi kuliko yote hadi tukaona kumbe mambo ni mepesi hivi! Tungejua 😃😃
Nakumbuka tulienda siku ya Ijumaa. Jumamosi tukapanda Mlima. Jumapili tukarudi Dar.

Mandhari ya Uluguru ni bomba sana. Kuna memories nyingi nzuri ila mojawapo ni kuoga alfajiri katika water falls 🤩🤩

Waluguru mmebarikiwa ndugu zetu. Hii ni moja ya kumbukumbu yangu bora pale!
Read 9 tweets
10 Apr
Miaka kadhaa iliyopita nilipata mzuka wa kwenda kutimiza moja ya ndoto zangu kubwa - kupanda Mlima Kilimanjaro.

Siku zote nilitamani kufika juu kabisa ya "Paa la Afrika". Nikasema ipo siku tu!

Hatimaye siku zikawadia za kuitimiza ndoto yangu hii kongwe.

Ilikuwaje?

THREAD👇🏾
Kampuni niliyotumia inaitwa Origin Trails. Sikusafiri peke yangu, kundi letu tulikua 21. Njia tuliyotumia ni Marangu.

Gharama ilikuwa ni USD 560 kwa kila mmoja na hii ilihusisha kila kitu kuanzia usafiri Dar-Moshi, chakula, hoteli, vifaa, ada za getini, personal guides n.k.
MAANDALIZI YA SAFARI

Baada ya kuthibitisha ushiriki wangu kupanda Mlima Kilimanjaro, jambo la kwanza nilifanya medical checkup. Nikawa 100% fit kupanda mlima na hadi kufika kileleni.

Basi, nikaanza mazoezi. Nakimbia uwanja huki nazunguka mara 7-10 kila siku kuuandaa mwili..
Read 8 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!