▶️FAHAMU BAADHI YA REKODI ZA KUSHANGAZA ZILIZOPO KWENYE KITABU CHA REKODI ZA DUNIA CHA GUINESS.
#uzi
#vitukuntu

01. Msichana mwenye miguu mirefu zaidi duniani.

👉Naam huyu ni "Maci Currin", binti wa miaka 17 tu akitokea kwenye nchini Marekani. Maci ameweka rekodi hii....

📸👇
....mwaka huu huu wa 2021. Maci ana urefu wa futi sita na inchi kumi, lakini miguu yake tuu imechukua karibu asilimia 60 ya urefu wake wote.

(Unaweza ukaangalia picha zake zaidi Instagram kwenye account yake ya @ _maci.currin_)

📸👇
02. Familia yenye nywele nyingi.

👉Familia ya Ramos Gomez iliweka rekodi ya ulimwengu kuwa familia kubwa zaidi yenye nywele nyingi za mwilini mnamo mwaka 2000. Ndugu wanne wa familia ya watu 19 kutoka Mexico walioitwa Victor Larry Gomez, Gabriel Danny Ramos Gomez,......

📸👇
....Luisa Lilia De Lira Aceves na Jesus Manuel Farajado Aceves walizaliwa na tatizo linaloitwa "hypertrichosis" (kuwa na nywele nyingi kwenye uso na kiwiliwili), hivyo kuwafanya kuwa watu wa tofauti na hiyo ilipelekea wao kuweza kuweka rekodi hii ya dunia ya Guiness.

📸👇
03. Mwanamke mwenye kucha za vidole vya mikono ndefu zaidi.

👉Lee Redmond kutoka Amerika aliweka rekodi ya kuwa na kucha ndefu zaidi ulimwenguni mnamo 2008. Alianza kukuza kucha zake tangu 1979. Kucha zake zina urefu wa futi 28 na inchi 4 ambayo ni urefu wa kucha zake.....
....zote kwa jumla. Kucha za Lee kwa bahati mbaya zilikatika alipopata ajali mbaya ya gari mnamo 2009. Hivyo kwa sasa Bi. Lee Redmond amepoteza kucha zake japo kwenye kitabu cha rekodi za Guiness rekodi yake bado ipo.

(📸👇 Hivi ndivyo alivyo kwa sasa)
👉Baada ya kucha za Lee kukatika kwenye ajali rekodi ya mwanamke mwenye kucha ndefu zaidi za vidole vya mikono ilikuja kuwekwa tena na mwanadada "Ayanna Williams" kutoka nchini marekani. Kucha za Ayanna kwa ujumla zina futi 24 na inchi saba. Hata hivyo Ayanna naye.....

📸👇
....amezikata kucha zake baada ya kuzifuga kwa muda wa takribani miaka thelathini.

(📸👇 Ayanna Williams akizikata kucha zake)
04. Mtu mwenye ulimi mrefu zaidi.

👉Nick Stoeberl ambaye amepewa jina la utani "The Lick" kutoka Monterey, California anashikilia Rekodi ya Ulimwengu ya Guinness kwa kuwa na ulimi mrefu zaidi tangu 2012. Ulimi wake una urefu wa sentimeta 10.10.

📸👇
05. Binaadamu mwenye ngozi ya kuvutika zaidi.

👉Garry Turner anashikilia rekodi ya kuwa na ngozi ya kuvutika zaidi ulimwenguni. Anaweza kuivuta ngozi yake ya tumbo lake hadi inchi 6.25 bila ya kusikia maumivu yoyote wakati akifanya hivyo. Hii inaletwa na Ehlers-Danlos..

📸👇
.....syndrome ambayo ni ugonjwa unaosababisha "collagen" kuwa na kasoro na hivyo hupelekea kulegea kwa ngozi ya mwili.

📸👇
06. Mwanadamu aliyeweza kushikilia idadi kubwa ya vijiko kwa kutumia ngozi yake ya mwili.

👉Dalibor Jablanovic kutoka Serbia aliweka rekodi ya kuvishikilia vijiko (teaspoons) 79 kwenye mwili wake mnamo mwaka 2016. Watu wengi hupendelea kumuita "Magnetic Man" (Mtu-sumaku).

📸👇
07. Mtu aliyetengeneza kofia "Hat" ndefu zaidi duniani.

👉Odilon Ozare kutoka USA, alitengeneza kofia ambayo ina urefu wa futi 15 na inchi 9 mnamo mwaka 2018. Ili awe mmiliki halali wa rekodi hiyo Odilon alitakiwa kutembea umbali wa mita 10 akiwa ameivaa kofia hiyo....

📸👇
....na Odilon alifanya hivyo.

📸👇
08. Farasi mfupi zaidi Duniani.

👉Farasi inayojulikana kwa jina la "Bombel" kutoka nchini Poland inashikilia rekodi ya dunia ya kuwa farasi mfupi zaidi duniani ikiwa na urefu wa inchi 22.36 tuu. Rekodi hii ni ya tangu mwaka 2018.

📸👇
09. Msichana mwenye nywele ndefu za kichwani.

👉Nilanshi patel kutoka India aliweka rekodi ya kuwa kijana mwenye nywele ndefu zaidi mnamo mwaka 2018. Nywele zake zina urefu wa jumla ya futi 5 na inchi 7.

📸👇
@threadreaderapp compile it

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Tony Sanga 🎃

Tony Sanga 🎃 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @sangasaimon_

24 Apr
▶️WAFAHAMU WATU MASHUHURI WALIOUWAWA KWA KUPIGWA RISASI.
#uzi
#vitukuntu

01. ABRAHAM LINCOLN
👉Alikuwa raisi wa 16 wa marekani na ndiye raisi wa kwanza wa marekani kuuawa akiwa madarakani. Aliuwawa mwaka 1865 na John Wilkes Booth aliyeudhiwa na maamuzi ya Lincoln ya kutambua....
....haki za watu weusi. Lincoln alipigwa risasi na John Wilkes Booth alipohudhuria kwenye maonyesho ya muziki. Booth nae aliuawa siku mbili baadae baada ya jaribio la kutoroka kushindikana.

(📸👇 John Wilkes Booth)
02. BENAZIR BHUTTO
👉Alikuwa waziri mkuu wa 11 wa Pakistani na kiongozi wa chama chenye ushawishi mkubwa cha PPP. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa la kiarabu akichagizwa na siasa zake safi za kidemokrasia. Aliuwawa disemba 27 mwaka 2007 akiwa kwenye gari yake aina ya....
Read 24 tweets
18 Jan
▶️LEO NIMEKULETEA HAPA BAADHI YA PICHA ZA "BEHIND THE SCENES" ZA FILAMU MAARUFU YA "APOCALYPTO" 🎥
#uzi
#vitukuntu
📸👇🏾 Image
▶️Filamu hii maarufu kutoka kiwanda cha kutengeneza filamu cha nchini Marekani (Hollywood) inayokwenda kwa jina la "Apocalypto" imekuwa ni mojawapo ya filamu nyingi zenye mafanikio na pia mvuto mkubwa kwa watamazaji.

👉🏾Filamu hii iliachiwa mnamo mwaka 2006.

Tuendelee..

👇🏾 👇🏾
▶️Filamu hii ilikuwa na lengo la dhati la kuelezea maisha ya kale ya wanadamu waliokuwa wakipatikana kwenye maeneo ya Amerika ya Kusini hususani wakazi waliokuwa wakiishi kwenye msitu mkubwa wa Amazon.
👉🏾Muongozaji mkuu wa filamu hii anajulikana kwa jina la "Mel Gibson"
Read 10 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!