Ijumaa, Machi 13, 2020 nje ya gereza la Segerea, Dar es Salaam
Baada ya kulipa faini kwa viongozi saba wa Chadema, alibaki Freeman Mbowe gerezani. Jioni wakati wanachama, wafuasi na viongozi wa Chadema wakimfuata baada ya kulipiwa faini ya Shs. 70 Milioni.
Ulitokea mzozo nje ya lango la gereza la Segerea. Mgogoro ule ulipelekea askari magereza kupiga kipenga kuashiria hali ya hatari.
Watu walichapika sana nje ya gereza hilo la Segerea. Watu walipigwa sana. Wakaitwa askari polisi kutoka kituo cha Stakishari.
Kuongeza nguvu ya mashambulizi. Wakaongezeka kwenye kutoa kipigo kwa wale wadau wa Chadema waliokwenda kumpokea Freeman Mbowe gereza la Segerea.
Bahati mbaya sana, walikuwepo watu wawili ambao hawakua kwenye msafara wa wana Chadema waliokwenda kumpokea Freeman Mbowe.
Majina yao nitayahifadhi. Wameomba hivyo pia. Hawa walikuwa ni marafiki wa TITO MAGOTI na walikwenda kumuona na kumsalimia Tito Magoti na Theodore Gyan gereza la Segerea.
Watu hawa wawili walipigika sana. Waliunganishwa kwenye adhabu za wale wanachama na wafuasi wa Chadema.
Walipewa hadi adhabu ua kujigalagaza kwenye maji na matope yaliyokuwa chini kutokana na kumwagwa maji mengi eneo hilo. Waliunganishwa kwamba walikwenda kufanya fujo.
Wale jamaa waliingizwa katika karandinga la magereza wakalala kifudifudi,
askari wakapanda juu yao, wanaruka na kuwakanyaga kiholela na kwa madaha juu ya migongo na vichwa vyao huku askari hao wakiimba kwa kejeli "people's Power" wakimaanisha salamu ya Chadema ya "Nguvu ya Umma".
Safari ya kutoka gereza la Segerea kwenda kituo cha
Polisi Stakishari ilikuwa ndefu na yenye ghasia nyingi. Askari waliendelea kusimama juu ya migongo na vichwa wakiruka hivyo wakati wote wa safari ile. Ukiguna unapigwa kipigo cha paka aliyekunya kwenye unga
Mmoja kati ya vijana hao akamueleza mkuu msafara wa askari waliotoka
Stakishari kwamba sio wanachama au wafuasi wa Chadema, wapo hapo kumsalimia Tito Magoti, yule bosi akawaeleza maelezo watayatoa kituo cha polisi, wapande karandinga.
Wakazunguka na hilo karandinga na kukamata yoyote ambaye alikuwa jirani na eneo la gereza la Segerea.
Wakazunguka nao sana. Baadae wakarejea gereza la Segerea na kuwavua pingu, wanayo huo kichapo kwa wengine kikiendelea kama dozi.
Kuna askari magereza wa kike ambaye aliwapokea asubuhi ya siku hiyo akawaeleza wenzake kwa sauti "hawa ni ******
wamekuja kumuona mahabusu tangu asubuhi". Wenzake hawakutaka hata kuelewa. Wakaambiwa wachanganyike na wenzao
Mmoja kati ya hao vijana alikuwa amevaa fulana (t-shirt) imeandikwa "SIMAMIA HAKI" na hili liliwakasirisha askari na kusema "hawa wanaharakati ndio wenye vurugu".
Kipigo kikaendelea upya. Na baada ya kipigo ndio wakatupwa kwenye gari za polisi hadi kituo cha polisi, Stakishari.
Hao jamaa walipandishwa gari Moja na hao wanachama, wafuasi na viongozi wa Chadema. Watu walilaliana sana kwa sababu haikuwepo nafasi ya kutosha.
Mmoja kati ya vijana wale alipoteza simu yake, na haijulikani ni wakati huo akiwa kwenye karandinga au wakati akichezea kichapo chini.
Ukiachana na maneno ya kejeli ya "people's power" pia walikuwa wakisema kwa kejeli
"ndio sasa mkome mbwa nyie, tuna siku nyingi hatujapiga watu, Acha tuwachakaze". Kwa kweli watu walichakazwa ipasavyo. Wapo waliovunjika hadi sehemu zao za viungo.
wakagoma, baada ya saa 4 tangu kukamatwa kupita, akafika ndugu yao, akawaeleza sio wanachama wa Chadema, ni ****** walikwenda kumuona Tito Magoti
Lakini wakiwa hapo kituo cha polisi, Stakishari, baada ya askari polisi kubaini kwamba hawa vijana wawili sio wanachama wa Chadema
Hawana uhusiano na vurugu hizo za Segerea na kwamba walikwenda kumuona Tito Magoti, wakalazimishwa kuwa mashahidi wa Jamhuri ili waachiwe huru.
Kabla ya kupewa dhamana hapo Stakishari, OC-CID alipokea simu akasema "kuna Ndugu zake Tito pia kwa hawa waliofanya fujo
Gereza la Segerea, ila wao wameonewa, akapewa maelekezo kuwa hao ndio watakua mashahidi wa Jamhuri, ikiwa hawataki basi tutawajumuisha kwenye kesi ya msingi ya hawa wengine. IMAGINE!
Huyu ndugu yao alikwenda nao Segerea. Akabaki nje ya gereza,
wakati yote hayo yanatokea aliona, akafuatilia hadi Stakishari na kuwakuta. Akaeleza muktadha wote. Wakatakiwa kuandika maelezo ambayo polisi walitoa muundo wake. Ndio wakapewa dhamana.
Masharti ya dhamana yalikuwa ni mengi ikiwa ni pamoja na kufika kituo cha polisi (kuripoti)
kila baada ya siku tatu na baadae wakaekezwa wanatakiwa kuwa mashahidi upande wa Jamhuri. Yaani wakatoe ushahidi dhidi ya wana Chadema kwamba ni kweli walitaka kuvamia gereza la Segerea.
Mmoja kati ya vijana hao waliokwenda kumuona Tito Magoti alivunjwa mbavu na mguu.
Mwingine alivunjwa mkono na mguu. Pia majeraha mengine mengi katika mwili wao. Lakini hawakuwahi kwenda mahakamani kutoa ushahidi huo wa uongo. Walikataa.
Waliishi kwa mwaka mzima tangu Machi 2020 hadi sasa Mei 2021 wakijificha na kuwakimbia askari
ambao walikuwa wakiwatafuta ili wafikishwe mahakamani kutoa ushahidi (ushahidi wa uongo). Askari Magereza pia walishindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi wao. Mahakama imeifuta kesi hiyo kutoka kwenye orodha za Mahakama.
Unaweza kudhani ni hadithi ya kutunga.
Ni ukweli mtupu. Wahusika hawa wanasema wamesumbuliwa sana kwenda kituo cha polisi kuripoti na hata kwenda mahakamani kutoa ushahidi wa uongo. Waligoma. Tunahifadhi majina yao, kwa usalama wao.
Nchi yetu ilifikishwa huko wakati wa utawala wa shujaa.
HATUPENDI kuona masuala haya yakiendelea kwenye ardhi yetu. Baada ya mwaka mmoja kupita na Jamhuri kutokupeleka mashahidi, kesi inefutwa na Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu na hakimu amesema washtakiwa wasibughudhiwe kamwe.
Kamwe, kamwe tusirudi katika zama hizo tena. Zama za utawala wa mkono wa chuma. Watu kulazimishwa kuwa mashahidi wa upande wa Jamhuri hata pasi na kuridhia wao wenyewe, wakatoe ushuhuda wa uongo mbele ya mahakama kwa kiapo mbele ya vitabu vitakatifu. Tusirudishwe huko.
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
MAKOSA 10 TUNAYOFANYA WAKATI TUNATEKWA NA WASIOJULIKANA.
Njia pekee ni kuwa na Machale, tumia muda kidogo sana katika kikao au mikutano yako kila sehemu unayokwenda na unapoondoka eneo hilo. Usiuweke sana na kuwapa nafasi ya wao kukuchora na kujipanga.
>Acha kinywaji mezani wajue unarudi
>Ondoka kwa style ya kujifanya unaongea na simu pembeni
>Ondokea njia ya kwenda chooni, wajue unarudi
>Jifanye unampokea mtu parking kwa haraka
>Omba wenzako wakusindikize mpaka kwenye gari
>uwepo wa wenzako utawasubirisha kwa dakika kadhaa
>Acha kulipa billi hadharani, acha pesa mezani, wasikadirie tendo lako linalofuata..
9. Kushindwa kuishi mazingira sawa na hadhi ya kazi anayofanya
Hapa naongelea tena wale wote walengwa wa kundi la utekwaji sio tu Tanzania bali Duniani, makundi yafuatayo;
MAKOSA 10 TUNAYOFANYA WAKATI TUNATEKWA NA WASIOJULIKANA.
1. Wanaokuja kututeka mara nyingi, tunawaona hawapo katika utaratibu rasmi wa ukamataji.
>Hawavai uniforms (sare)
>huja na magari ya kiraia
>hawaonyeshi vitambulisho
>hutumia nguvu badala ya mashauriano au maelewano
KOSA: Ni kukubali kutoa ushirikiano kwa watu hao, kuogopa watakudhuru au kukuumiza wakati wa mvutano
Ukweli ungepiga kelele au kuburuzwa au kujaza watu ungepata msaada. Ikibidi kama wakuue Mwenge tuokote Maiti,kuliko kudhani bunduki zile haziwezi kukudhuru huko unakokwenda.
2. KUKUBALI KUCHUKULIWA BILA KUACHA TAHARUKI NA KUWAJULISHA RAIA ENEO HILO KUWA UNAKAMATWA NA WATU WASIO SAHIHI.
Hii inatokea mara nyingi, mtekwaji anachukuliwa kwa kuaminishwa na watekaji kuwa ni maofisa sahihi kwa kuonyeshwa vitambulisho. Vitambulisho bandia mara nyingi.
MAMA FATMA KARUME; anasema mzee ABEID KARUME alimueleza, endapo atakutwa na mauti katika mapinduzi ya kumuondoa SULTAN katika ardhi ya Zanzibar, basi mkewe abakie kwa furaha na amani kwa sababu mumewe ni shujaa na akamtaka asomeshe watoto wao (endapo atakutwa na mauti). UZI 👇
PAULINE OPANGO LUMUMBA; mke wa mwanamapinduzi wa Zaire (sasa DR Congo) Patrice Emery Lumumba, alishuhudia kukamatwa kwa mumewe mjini Ilebo jimboni Kassai-Occidental kabla ya kuuwawa jimboni Katanga Januari 17, 1961. Alichofanikiwa kubaki nacho Pauline ni Barua ya Lumumba
Ambayo Patrice aliita “risala yangu ya mwisho kwa Pauline” Kwenye risala Patrice Lumumba alisema "sihofii maisha yangu mwenyewe, ikiwa itahitajika kumwaga damu yangu ili wakongo wapate uhuru wa kweli, kamwe siwezi kusita kuwa sehemu ya sadaka hiyo kwa taifa langu"
●Kambona ni shuhuda wa utiaji saini hati za Muungano 22/4/1964
●Tume ya Kawawa ilipendekeza mfumo wa chama kimoja Kambona akagoma
●Kambona akagoma kutia saini akaanda taarifa nyingine
●Akagoma kukubaliana na Nyerere kwenye kuleta mfumo wa kikomunisti
Nyerere aliporejea kutoka China 1965 alitamani muundo wa siasa za China
●Ndio msingi wa kuundwa tume hiyo iliyopendekeza “muundo wa chama kimoja”
●Msimamo wa Kambona haukumpendeza Nyerere. akamkunjia.
●1966 Nyerere akampiga ‘madongo’ Kambona jukwaa la sherehe za Sabasaba
●siku 2 baadae Kambona akatangaza kujiuzulu ukatibu mkuu wa TANU na uwaziri wa serikali za mitaa
●Baada ya kubaini mpango wa kukamatwa na kuwekwa kizuizini mwezi huo alitoroka nchini
●Alitoroka na familia yake yote, Mkewe, wanae, mtumishi wao kuelekea nchini Kenya
@Matiko_Esther_ aliyekuwa Mgombea Ubunge katika Tarime Mjini, amenieleza habari za kupotezwa kwa ndugu Damas Wilson mmoja ya vijana wa hamasa wa CHADEMA Tarime Mjini ambaye 'alipotea katika mazingira ya kutatanisha' tangu usiku wa 26/10/2020 👇
Imeelezwa kuwa kijana Damas Wilson alipotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa na mwenzake anaitwa Richard Kayanda Tongoli walipokuwa wakitokea nyumbani kwa @Matiko_Esther_ aliyekuwa Mgombea Ubunge Tarime Mjini baada ya kumalizika Kampeni na kwenda kutawanyikia nyumbani
Damas Wilson na Kayanda Tongori ni Vijana wa Hamasa wa CHADEMA Jimbo la Tarime Mjini tangu kuanza kwa Kampeni mpaka kupotea kwao huku Damas Wilson akiwa mkazi wa Mtaa wa Byambwi Kata ya Bomani na Richard Kayanda Tongoli akiwa mkazi wa Mtaa wa Byambwi Kata ya Nyandoto.
On Monday @TunduALissu, Chadema’s candidate in the presidential election, was arrested by Tanzanian police outside the German embassy.
Knowing that they were coming for him, he had sought diplomatic protection. He was first turned away by a political officer at the US Embassy
He then went to Umoja House – where the EU, UK, German and Dutch missions are located – where he waited for several hours while the bureaucrats inside deliberated on whether or not to let him in.
Shortly before he was picked up by the cops he sent a WhatsApp message: “They’re all in dread of this petty tyrant it’s unbelievable.”