Baada ya kumaliza shule nilimpata binti niliyeamini atakuwa wa maisha yangu alikuwa anaitwa Mwajuma, hapo ndio kwanza nilikuwa ninaanza kuingia katika ulimwengu wa mapenzi.
Sikuwa ninaelewa kabisa kuhusu maana ya neno penzi, watu waliotabiri mwisho wangu na Mwajuma niliamini kuwa ni wanafiki na walikuwa na malengo mabaya dhidi yetu.
Siku zilivyozidi kusonga penzi letu lilizidi kustawi kama bustani iliyokuwa inasimamiwa vizuri, tulipanga hadi kutambulishana kwa wazazi.
Kila kitu nilijitoa kwa ajili yake. Wenzangu waliniona "Bushoke" ila sikujali. Nilimnunulia hadi zawadi ya pete kama ishara nzuri ya penze letu kuzidi kunawili.
Licha ya upendo wangu wote kwake lakini sikuwahi kufanya nae mapenzi, ninakumbuka niliwahi kuingia nae hadi chumbani lakini alinikatalia kufanya nae kitu chochote aliniambia muda bado nilikubali kwa kuwa niliamini mimi ni wake
Baada ya kwenda chuo ndipo mauza uza yalipoanza.
Siku moja niliamka asubuhi na nikakuta ameweka Dp ya mwanaume. Niliwaza sana kwani haikuwa kawaida yake.
Nilimuuliza kuwa huyu ni nani?. Alinijibu "Aliwazalo mjinga ndilo linalomtokea".
Sikujua alimaanisha nini, ila mawasiliano yetu hayakuwa kama zamani tena.
Nilichunguza na kugundua kuwa alikuwa ni mwanaume wake mpya, mshikaji alikuwa ni handsome na ana hela kuliko mimi. Washikaji zangu walinicheka sana kwa sababu sikuwahi kufanya nae kitu". Baraka. Zanzibar. #WatuNiStory
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
"Tulifanya interview kutafuta mtu wa finance katika kampuni yetu. Tulipokea maombi mengi, watu tano ndio walifanikiwa kupigiwa simu na kuitwa kwa ajili ya usahili.
Wote walifika. Kila mtu alipangiwa muda wake.
Nakumbuka kuna kijana alikuja amependeza, yuko smart na alikuwa na vigezo vyote vya kupata ajira.
Alikuwa na madaha na majivuno ya hapa na pale wakati tunafanya nae interview. Alitaka mshahara wake usishuke si chini ya milioni moja na laki tano.
Alisema bila mshahara huo hawezi kutoka kwenye kampuni anayoifanyia kazi.
Hatukuwa na hiyo hela. Hivyo tulimchagua mtu mwingine ambaye tulielewana nae.
1/10 “Naitwa William Adam Lukoo ,mzaliwa wa mkoa wa Morogoro. Mwaka 2003 familia yetu ilihamia jijini Tanga kwa ajili ya harakati za kimaisha. Haikua rahis kwa sababu ya ugeni lakini wazazi walipambana kuhakikisha napata elimu bora. Licha ya kutoka kwenye familia ya kimaskini...
2/10 ..nilihakikisha nafanya vizuri kwenye masomo kiasi cha kuwavutia walimu na kujizolea umaarufu shuleni. Nilifanikiwa kuhitimu mwaka 2010 shule ya msingi Majani Mapana wilayani Tanga mjini. Mwaka 2011 nilianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Usagara..
3/10 ..lakini kutokana na ugumu wa maisha, wazazi wangu wote hawakuwa na kazi. Ikawalazimu kufikia hatua ya kuuza vitu vya ndani ili kuweza kunilipia ada. Maisha yalikuwa magumu mno nyumbani kiasi cha kufikia hatua ya kushindwa kupata chakula na kodi.
"Kipindi nipo nyumbani Mwanza, nilikuwa napigiwa simu na Kaka mmoja ambaye nilikuwa nafahamiana nae sana. Alikuwa ananiomba nije sana Kahama akiwa na ahadi ya kunipa kazi, kunipangishia nyumba na ahadi nyingine nyingi nzuri.
Siku niliyofika kahama, nilifikia guest house. Yule kaka ndiye aliyenipokea, hivyo nililala nae na mambo mengine ya chumbani yalifanyika.
Alivyoondoka asubuhi ndio ilikuwa mwisho kunipigia simu. Nikawa kila nikimtafuta naambulia matusi tu. Hakunipa chochote kama alivyoniahidi.
Kwa bahati nzuri nilivyotoka nyumbani Mwanza nilikuwa na akiba ya kama elfu 60.
Ilibidi niingie mtaani kutafuta kazi mimi mwenyewe, kwa maana nisingeweza kurudi tena Mwanza, Ningeambia nini watu maana nilikuwa nimeshaaga.
Nimeona bora niongee na kuomba ushauri wenu kwani nimekaa kimya siku nyingi. Hali inazidi kuwa mbaya. Nazidi kudhoofika kisaikolojia na imefikia hatua Kuna mawazo mabaya yananijia kichwani.
Ni hivi, nilikua na biashara zangu kama tatu hivi nilizokua naziendesha zikiwa eneo moja. Kwa kuwa mimi ni mwalimu wa shule binafsi (private school) muda mwingi nashinda kazini, Hivyo msimamizi mkuu wa biashara zangu alikuwa mke wangu.
Mwezi wa 7 wakati wa likizo ya Corona mke wangu alisafiri kwenda nyumbani kusalimia.
Nikawa nasimamia mimi mwenyewe.
Shule zikafunguliwa huku mke wangu akiwa bado hajarudi.
"Nilimpa mimba binti ambaye sikuwa na mpango nae wa kumuoa, licha ya yeye kuwa ananipenda sana.
Hivyo nilimzimia simu na kupotea kabisa machoni mwake. Ilipita kama miaka miwili huku akiwa hajui kabisa nilipo.
Siku moja nikiwa katika harakati zangu, gafla nikakutana nae.
Alinikimbilia na kunikumbatia kwa upendo ule ule, niliona machozi kwa mbali machoni mwake.
Alikuwa amepungua, mwili wake na umbo zuri lote limepotea. Nilivyomuuliza nini shida, akaniambia ile mimba iliharibika kutokana na msongo wa mawazo baada ya mimi kumkimbia.
Mimba iliharibika vibaya, ilipelekea yeye kuumwa sana kwa kipindi kirefu tena bila msaada wangu.
1/5 “Nilisoma chuo UDSM hadi mwaka wa tatu lakini sikuhitimu. Sikuhitimu kwa sababu ukweli ni kwamba, sikuzingatia masomo ipasavyo, nilipata ajira nikashindwa ku-balance kati ya shule na kazi. Nikaishia kufeli mitihani kadhaa. Ilikua nihitimu mwaka 2015. Miaka yote nimeendelea..
2/5 ...kufanya kazi mbalimbali kwa kutegemea kipaji changu tu. Japo kuna nyakati nilikosa kazi zilizohitaji mtu mwenye degree na sikua na hizo sifa. Ni jambo ambalo limekua likiniumiza na kunifanya nijiskie vibaya. Familia yangu pia iliumizwa na hilo sababu walilipa ada miaka..
3/5 ..yote mitatu ya chuo. Na niliumia sana kuiumiza familia yangu. Namshukuru Mungu mwaka huu baba yangu amenipa nafasi tena ya kurudi chuo na kunilipia ada. Nime-apply tayari nangoja majibu. Japo naona kama miaka mingi imeshapita, nina miaka 28 sasa..