UZI: Jana tumesikia Tanzania imejiunga kwenye mpango wa COVAX.

COVAX = Covid Vaccine (chanjo ya corona)

Je COVAX ni nini? ๐Ÿ‘‡
#BongeLaAfya @BongeLaAfya
COVAX ni mpango wa mapatano (partnership) kati ya shirika la afya la dunia (WHO) na mashirika mawili ya kimataifa โ€“ Gavi vaccine alliance na Coalition for Epidemic Preparedness Innovation (CEPI), mapatano haya yanalenga kusambaza chanjo kwenye mataifa yanayoendelea.
COVAX inakusudia kutoa dozi za chanjo bilioni mbili kwa watu katika mataifa 190 kwa mwaka huu, hii ni kuhakikisha angalau asilimia 20 ya watu imepata chanjo (vaccinated). Zaidi pia, inalenga kusambaza chanjo kwa mataifa 92 yenye kipato cha chini bure kabisa.
Pichani, kwa mujibu wa Gavi.org, Tanzania pia ni moja ya nchi zilizowekwa kwenye kundi la lower income, kwa maana sisi pia tutapokea kiasi Fulani cha chanjo hii bure.
Mataifa yaliyo kundi la uchumi wa kati, watapata pia chanjo hii, lakini kwa gharama zao. COVAX inatumia mfumo ambao mataifa yenye pesa watanunua chanjo kwa gharama ambayo itawezesha mataifa yasiyo na pesa kupata chanjo pasipo kutumia gharama (richer pay to subsidize poorer).
COVAX mpaka sasa ina makubaliano na makampuni makubwa ya kutengeneza chanjo kama Pfzer na Johnson & Johnson, japo chanjo zilizosambazwa karibuni zilitengenezwa na AstraZeneca, hawa hutengeneza chanjo ambazo haziitaji kutunzwa katika baridi kali kama ambavyo chanjo zingine zilivyo
Moja ya changamoto waliyokumbana nayo COVAX ni ukusanyaji wa dozi za chanjo za kutosha kwa ajili ya mataifa ya kipato cha chini kwani mataifa tajiri yaliingia mikataba ya moja kwa moja na makampuni yanayotengeneza chanjo na hivyo chanjo nyingi kwenda kwenye mataifa hayo.
Natoa pongezi kwa serikali, kitaalamu ili kufikia โ€œherd immunityโ€, kinga ya jamii au kinga ya wote inapaswa mambo mawili yafanyike, 1. Tuache watu waugue ugonjwa, watengeneze kinga wenyewe na 2. Kugawa chanjo (kinga) kwa wananchi.
Hii njia ya kwanza ingeleta ukakasi kidogo hasa kwa watu wenye magonjwa mbalimbali, miili yao isingeweza kuhimili virusi hivi n ahata kusababisha vifo.

โ€ข โ€ข โ€ข

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
ใ€€

Keep Current with Bonge La Afya ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Bonge La Afya ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @FestoNgadaya

2 Dec 20
UZI: Kwenye utafutaji, tabia kama za wanyama hawa zinaweza kuua kundi.

Bata: Kujivuta vuta, kufanya kazi polepole na kuendekeza uvivu mapaka mambo ya kikundi yanazorota au kufa kabisa.

Bundi: Mtu anayefikiria ana akili kuliko wote kwenye kikundi- hutumia lugha ngumu kueleweka.
Chura:Rudia rudia kitu kile kile mapaka anawachosha wenzake kundini

Kenge:Hatumii akili sawasawa, ujinga mwingi na kufanya maamuzi ya ovyo yenye kuwakatisha tamaa wenzake

Kiboko:Kulala lala na kupiga miayo, wakati wenzake wanachacharika, yeye ni kukaa tu hafanyi kazi.
Kifaru:Yeye hushambulia wengine kwenye kikundi bila sababu

Kinyonga:Kigeugeu, akiwa kwa mwanakikundi huyu anasema hili na akiwa kwa mwingine anasema tofauti

Kobe:Hujitoa akiudhiwa, hana uvumilivu kwenye changamoto zinazoikabili kikundi.
Read 9 tweets
27 Nov 20
UZI: Red eye au bloodshot kwa kitaalamu, hutokea pale ambapo mishipa midogo ya damu inayoonekana kwenye uso wa jicho kupanuka au kujawa na damu. Hali hii hutokea kutokana na uwepo wa kiwango kidogo cha oxygen inayotolewa na tishu zinazofunika jicho au maambukizi. #BongeLaAfya Image
Hali hii huwa ya kawaida na inaweza kutokea katika jicho moja au macho yote mawili. Hiyo rangi nyekundu inayoonekana ni rangi ya damu katika mishipa yake hapo kwenye jicho, inaweza kuwa sababu ya kupikicha jicho au maambukizi fulani. Image
Red eye kwa ujumla isikupe wasiwasi saana, lakini hali hii ikiambatana na maumivu ya macho, au kupungua kwa uwezo wako wa kuona nakushauri umuona daktari kwani inaweza kuwa dalili ya magonjwa kama pinkeye (conjuctivitis au kwa kiswahili Kiwambo), Corneal ulcer, Dry eye syndrome. Image
Read 8 tweets
4 Nov 20
UZI: Zifahamu njia za kuzuia mimba: Wote tunahitaji taarifa sahihi na zinazoeleweka kuhusu matumizi au njia mbalimbali za kuzuia mimba. Jambo la kuzuia mimba sio la mwanamke pekee bali hata mwanaume ana wajibu wa kujifunza mambo yanayotokea wakati wa tendo la ndoa. #BongeLaAfya Image
Mwanamke yeyote ambaye ameanza kupata hedhi ya kila mwezi anaweza kutumia njia za kudhibiti mimba. Njia hizi hutofautiana kutokana na upendeleo wa mtu binafsi au umri pia. Leo nitakusaidia kuwa na uwezo wa kuzuia mimba kwa kukupa taarifa sahihi. Image
1. Kondomu - Kuna kondomu za kike na kiume ambazo hufanya kazi kwa ufanisi kabisa zinapotumika. Kondomu zinapatikana sehemu nyingi na nina hakika wengi tunazifahamu. Kikubwa kondomu ya kike haitumiki wakati mmoja mnapotumia kondom ya kiume. Chagueni mmoja avae. ImageImageImageImage
Read 14 tweets
18 Oct 20
UZI: Dalili za mimba: Ujauzito ni ndoto ya wengi, huku kwa wengine ni jambo wanaloepuka na kuzingatia sana. Wadada wengi wanaonesha kuhitaji watoto tofauti na wanaume. Leo nimekuletea dalili 10 za ujauzito ambazo huashilia uwepo wa ujauzito #BongeLaAfya Image
1. Kutoona siku zako: Kukosa siku zako ni moja ya dalili za kwanza kabisa ambazo wengi wetu wamezoea. Katika kipindi cha mzunguko kuta ya mfuko wa uzazi huvunjika na kujiengua na kutoka nje katika mfumo wa damu, hudumu kwa siku tatu mpaka saba. Unapopata ujauzito hujishkiza hapo. Image
2. Misuli ya miguu kubana/cramps: Katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito mwanamke anaweza kuona dalili za miguu kukaza au kubana, Hii inatokana na mabadiliko ya mwili katika kuchakata calcium ambayo huitajika kwa wingi kuunda mifupa ya mtoto, meno na viungo. Image
Read 13 tweets
7 Oct 20
UZI: Kwa nini mnapaswa kuaminiana mnapoenda kupima UKIMWI: Miaka mitatu sasa nikifanya kazi hospitali na taasisi za tafiti kuna mambo nimekuwa nikikumbana nayo ambayo leo acha niyaweke mbele yenu ili wote tupate kujifunza. Nitaongelea tukio la upimaji wa UKIMWI. #BongeLaAfya Image
Kwa hii kadhaa nikiwa nafanya kazi za upimaji maabara, Upande wa upimaji UKIMWI kuna changamoto nyingi sana ambazo zinawakumba watu wanaokuja/wanaoleta rafiki/wapenzi wao kupima virusi vya ukimwi. Changamoto hizi nyingi zinatokana na kukosa uaminifu lakini pia udanganyifu. Image
Siku moja walikuja kupima UKIMWI mwanaume na mwanamke ambao kwa kuwaangalia tu unajua ni wapenzi. Baada ya ushauri na kuchukua sampuli ilibidi waende nje wakasubiri majibu. Sasa wakati naendelea kupima ghafla alirudi yule mwanamke na kutaka kuongea na mimi. Image
Read 8 tweets
21 Sep 20
1/7: Jamii inaweka msukumo mkubwa sana kwa dada zetu "KUOLEWA", Msukumo unaoambatana na kikomo cha miaka kwamba akifika miaka fulani awe ameolewa.

Kama kuolewa ni jambo muhimu kiasi hiki, kwa nini hatuwaandai kuoa/kuolewa tangu mashuleni?
2/7: Mbaya zaidi mategemeo ya wanajamii wengi ni kuwa binti huyu atakua "MKE BORA". Binafsi naona sio sawa, sio sawa kwa maana kama jamii tunajisahau sana. Unawekaje mategemeo makubwa kama haya wakati hufanyi juhudi zozote kuhakikisha mtoto huyu anakua katika njia bora.
3/7: Napongeza taasisi nyingi zilizoweka nguvu katika kumnyanyua mtoto wa kike kutoka katika mkandamizo wa haki zao katika jamii, Swali langu kwenu kama tunavyopambana na hedhi salama lini tutaongelea NDOA? Hatuoni kama ni muhimu kuliwekea nguvu swala hili?
Read 7 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(